Global Publishers September 28, 2026 0 views 0 Comments
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius John Ndejembi, amewasili mkoani Arusha leo Jumatatu, Septemba 28, 2026, kwa ajili ya kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma (C-CEOs Forum).
Makamu wa Rais amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambako amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.
Baada ya kuwasili Arusha, Ndejembi anatarajiwa kuelekea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), ambapo atafungua rasmi kikao hicho kinachowakutanisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma.
C-CEOs Forum inalenga kuwa jukwaa la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uendeshaji, utendaji na mchango wa Taasisi na Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameiomba Mahakama kutotegemea ushahidi uliotolewa na mashahidi wa kificho katika kesi inayomkabili, akidai kuwa baadhi ya ushahidi wao ulikuwa na uongo, mkanganyiko na maslahi.
Lissu ametoa ombi hilo leo, Jumatatu, Septemba 28, 2026, wakati akiendelea kuwasilisha hoja zake za mwisho mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.
Katika hoja zake, Lissu amewataja mashahidi hao kuwa ni PW5, PW7, PW8, PW10, PW11, PW13 na PW14, akidai kuwa ushahidi walioutoa mahakamani una mapungufu mbalimbali.
Lissu amesema ushahidi wa mashahidi hao haupaswi kupewa uzito kutokana na kile alichodai kuwa ni taarifa zisizo za kweli na zenye maslahi.
Kwa upande wa PW5, Lissu amedai kuwa shahidi huyo alitoa taarifa zinazokinzana kuhusu dini yake, akieleza kuwa mahakamani alikula kiapo kama Mkristo, wakati katika maelezo yake yaliyowasilishwa kama kielelezo D4 alijieleza kuwa ni Muislamu.
Pia amedai kuwa PW5 alitoa taarifa zisizo sahihi kuhusu uanachama wake wa CHADEMA.
Akizungumzia PW7, Lissu amedai kuwa shahidi huyo alitoa taarifa za uongo kuhusu kupelekwa katika Kituo cha Polisi Songea pamoja na suala la uanachama wake wa CHADEMA.
Kuhusu PW8, Lissu amesema ushahidi wake ulikuwa na mikanganyiko na taarifa ambazo, kwa mtazamo wake, hazikuwa za kweli.
Aidha, akielezea ushahidi wa PW10, Lissu amedai shahidi huyo alitoa maelezo kwa polisi kwamba mshtakiwa alisema walikuwa wamejipanga kufanya fujo ili kuzuia uchaguzi. Lissu amekanusha kauli hiyo, akisema hakuwahi kutoa kauli kama hiyo.
Kwa upande wa PW11, Lissu amesema ushahidi wake pia ulikuwa na mikanganyiko na kwamba haukuwa wa kweli.
Kuhusu PW13, Lissu amedai shahidi huyo alitoa taarifa zinazokinzana kuhusu uanachama wake wa CHADEMA, akisema katika maelezo yake alijitambulisha kama mwanachama wa chama hicho, jambo ambalo Lissu amepinga.
Lissu pia amepinga ushahidi wa PW14, akidai shahidi huyo alitoa taarifa zinazokinzana kuhusu kazi yake. Kwa mujibu wa Lissu, katika maelezo ya polisi shahidi huyo alijitambulisha kama mkulima wa Kata ya Mwakibete, huku mahakamani akisema yeye ni fundi umeme wa Jiji la Mbeya.
Lissu pia amekanusha madai kwamba PW14 alimsikia akisema “lazima tukichafue,” akisema hakuwahi kutoa kauli hiyo.
Hoja hizo zimewasilishwa na Lissu katika hatua ya hoja za mwisho, huku Mahakama ikiendelea kusikiliza pande zinazohusika kabla ya hatua inayofuata ya kesi.
Global Publishers September 28, 2026 12 views 0 Comments
Sherehe za MTV Video Music Awards (VMAs) 2026 zimefanyika Jumapili, Septemba 27, katika ukumbi wa Peacock Theater jijini Los Angeles, Marekani, huku Snoop Dogg akiwa mwenyeji wa hafla hiyo.
Katika tuzo hizo, Madonna aliongoza kwa kupata tuzo kadhaa, huku BTS, Taylor Swift, Ariana Grande, Bruno Mars, LISA na wasanii wengine wakitajwa miongoni mwa washindi.
Hii hapa ni orodha ya washindi kwa baadhi ya vipengele vikuu:
Best Group: BTS
Best Long Form Video: Madonna – Confessions II – The Film
Best Album: Madonna –Confessions II
Song of Summer: Ariana Grande – hate that i made you love me
Video of the Year: Taylor Swift –The Fate of Ophelia
Artist of the Year: Madonna
Song of the Year: BTS – Swim
Best New Artist: Sienna Spiro
Best Collaboration: Madonna & Sabrina Carpenter – Bring Your Love
Best Pop: LISA –Dream feat. Kentaro Sakaguchi
Best Hip-Hop: Cardi B ft. Kehlani – Safe
Best R&B: Bruno Mars –I Just Might
Best Alternative: Olivia Rodrigo – the cure
Best Dance: Madonna – Confessions II – The Film
Best Latin: Bad Bunny – NUEVAYoL
Best K-Pop: BTS –SWIM
Best Country: Ella Langley – Choosin’ Texas
Best Direction: Taylor Swift – Opalite
Best Art Direction: PinkPantheress –Stateside + Zara Larsson
Best Cinematography: Madonna – Confessions II – The Film
Best Editing: Sabrina Carpenter –House Tour
Best Choreography: Madonna –Confessions II – The Film
Best Visual Effects: Ariana Grande –hate that i made you love me
Mbali na tuzo hizo, Taylor Swift alitunukiwa tuzo mpya ya Artist Director Honors, huku kundi la Nirvana likipewa Video Vanguard Award.
Hafla hiyo pia ilihusisha maonyesho ya wasanii mbalimbali, wakiwemo Madonna, LISA, RAYE, Shaboozey, Gunna, Sienna Spiro, Gener8ion na Yung Lean. RAYE, Sombr na Teddy Swims walishiriki katika heshima maalum kwa George Michael, huku Kacey Musgraves akiongoza heshima kwa Dolly Parton.
IRINGA: Ujenzi wa nyumba ya muhudumu wa afya katika Zahanati ya Usolanga, wilayani Iringa unatarajiwa kupiga hatua baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Arif Abri, kuchangia mabati 30.
Pamoja na msaada huo utakaosaidia kuimarisha mazingira ya utoaji wa huduma kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo ya jirani, kada huyo wa CCM ametoa msaada wa kompyuta moja kwa matumizi ya Zahanati hiyo.
Diwani wa Kata ya Malengamakali, Stephano Mkisi, amesema nyumba hiyo ni sehemu muhimu ya jitihada za wananchi kuhakikisha wahudumu wa afya wanakuwa na mazingira bora ya kuishi karibu na kituo chao cha kazi.
“Mpango huu unalenga kurahisisha upatikanaji wa huduma wakati wowote, hususan kwa wagonjwa wanaohitaji msaada wa haraka nje ya muda wa kawaida wa kazi,” amesema.
Amesema msaada huo wa Abri umeongeza nguvu katika ujenzi wa nyumba hiyo ambayo tayari ilikuwa imefikia hatua ya kuezekwa wakati wananchi walipowasilisha mahitaji yao kwa viongozi na wadau wa maendeleo.
Mkisi, amesema ujenzi wa nyumba hiyo ni miongoni mwa mahitaji muhimu yaliyotambuliwa na wananchi kwa lengo la kuboresha huduma katika zahanati hiyo.
Mabati hnpamoja na kompyuta hiyo yamekabidhiwa kwa niaba ya Abri na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Arnold Mvamba, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho.
Akizungumza katika mkutano huo, Mvamba amesema serikali ndiyo mdau mkuu wa maendeleo, lakini ushiriki wa wananchi, viongozi na wadau wengine ni muhimu katika kuharakisha utekelezaji wa miradi inayogusa maisha ya wananchi.
Mvamba amesema msaada huo unatokana na ahadi iliyotolewa na Abri wakati wa ziara yake Usolanga, ambapo wananchi walieleza changamoto zinazowakabili katika huduma za afya na uhitaji wa vifaa vya teknolojia.
Amesema msaada huo unaonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, wananchi na wadau mbalimbali katika kutatua changamoto za huduma za kijamii.
Licha ya msaada huo kuwa hatua muhimu ya ujenzi huo amesema, bado ushirikiano wa wananchi unahitajika ili kukamilisha nyumba hiyo na kuhakikisha inatumika kwa lengo lililokusudiwa.
Aidha Mvamba amewataka wananchi kuendelea kuzingatia tahadhari zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mvua na kuchukua hatua stahiki kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb.), amewasili jijini Muscat, Oman, Septemba 27, 2026, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Uwili baina ya Tanzania na Oman unaotarajiwa kufanyika Septemba 28, 2026.
Mkutano huo unalenga kuimarisha uhusiano wa kimaendeleo na kiuchumi baina ya Tanzania na Oman, pamoja na kujadili maeneo ya kimkakati ya ushirikiano ikiwemo Siasa, uwekezaji, biashara, Madini, nishati na uchumi wa buluu.
Maeneo mengine yatakayojadiliwa ni pamoja na miundombinu na usafirishaji, Elimu, Maji, kilimo, mifugo, utalii na malikale, yanayogusa pia uhusiano wa kihistoria na kitamaduni unaozihusisha Tanzania na Oman.
Makubaliano yatakayofikiwa katika mkutano huo yanatarajiwa kuweka msingi wa kukuza na kuendeleza ushirikiano Katika Sekta hizo kwa manufaa ya pande zote mbili.
Dar es Salaam – Mambo ya mapenzi yameendelea kuteka mjadala katika ulimwengu wa mastaa wa Bongo, safari hii baada ya Kajala Masanja kufunguka kuhusu uhusiano wake na mwanamuziki Harmonize, huku mastaa wenzake Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na Aunty Ezekiel wakihusika katika mazungumzo hayo.
Kajala ameeleza kuwa changamoto zinazojitokeza mara kwa mara katika uhusiano wake na Harmonize hazimaanishi kwamba hana sehemu nyingine ya kwenda au kwamba hana mtu mwingine anayempenda.
Akizungumza mbele ya marafiki zake, Kajala amesema sababu kubwa inayomfanya aendelee kuwa na Harmonize ni namna anavyojisikia anapokuwa naye, akisisitiza kuwa moyo wake unapata hali ya furaha na utulivu akiwa pamoja na mwanamuziki huyo.
Jambo la kuvutia ni kwamba Harmonize alikuwa akisikiliza maelezo hayo moja kwa moja, hivyo alisikia mwenyewe namna Kajala alivyoeleza hisia zake kuhusu uhusiano wao.
Katika mazungumzo hayo, Irene Uwoya na Aunty Ezekiel walimweleza Harmonize kuwa baadhi ya matendo yake yamekuwa yakimkwaza Kajala, hasa kutokana na kuhusishwa na wanawake wengine kisha kurejea kwenye uhusiano wake.
Walimshauri mwanamuziki huyo kufanya maamuzi yatakayompa Kajala uhakika na usalama katika uhusiano wao, badala ya kuendelea na hali inayoweza kumfanya mwenza wake kuwa na mashaka.
Kwa mujibu wa ushauri huo, Harmonize anatakiwa kutulia na kuweka msimamo katika uhusiano wake ili kujenga mazingira yenye utulivu na kuondoa migogoro inayojitokeza mara kwa mara.
Katika sehemu nyingine ya mazungumzo hayo, Harmonize alionekana kushangazwa na mazingira ya kukaa pamoja na Jacqueline Wolper, ambaye aliwahi kuwa mpenzi wake, huku Wolper akiwa tayari na maisha yake ya sasa.
Harmonize alieleza kuwa si jambo la kawaida kwake kukaa sehemu moja na mtu ambaye waliwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi, hasa wakati kila mmoja ana mwenza wake wa sasa.
Hali hiyo iliongeza mvuto wa mazungumzo hayo, kwa kuwa iliwakutanisha watu wenye historia mbalimbali za kimapenzi katika mazingira moja.
Kwa upande wake, Irene Uwoya alitoa mtazamo wake kuhusu wanaume wanaoingia kwenye mahusiano na wasanii wa kike.
Alisema mwanaume anayekuwa kwenye uhusiano na msanii anapaswa kuwa na uwezo wa kifedha, akisisitiza kuwa katika mahusiano hayo si suala la kutegemea umaarufu wa mwanamke pekee, bali pia mwanaume kuwa na uwezo wa kifedha na kusimama katika majukumu yake.
Mjadala huo umeibua mazungumzo kuhusu changamoto zinazowakabili mastaa katika mahusiano, hasa pale maisha yao binafsi yanapokuwa sehemu ya mijadala ya umma.
Kwa upande wa Kajala na Harmonize, kauli zilizotolewa katika mazungumzo hayo zimeonyesha namna ambavyo hisia, uaminifu na msimamo katika mahusiano vinavyoweza kuwa sehemu muhimu katika kudumisha uhusiano wa watu maarufu.
Masanja Kungu Kadogosa ni Mbunge wa Jimbo la Bariadi Vijijini mkoani Simiyu, kupitia chama cha Chama cha Mapinduzi (CCM) ameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Ujenzi, akichukua nafasi iliyoachwa na Abdallah Hamis Ulega, ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Uteuzi huo umetangazwa Jumapili, Septemba 27, 2026, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka.
Kadogosa anaingia katika nafasi hiyo akiwa na uzoefu wa muda mrefu katika sekta ya miundombinu, hususan kwenye masuala ya reli na usafiri. Kabla ya kuingia katika siasa, aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika sekta ya fedha na reli.
Kwa miaka kadhaa, Kadogosa alihudumu katika uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kipindi ambacho Tanzania ilikuwa ikitekeleza mradi mkubwa wa Reli ya Kisasa (SGR).
Safari yake ya kikazi ilianza katika sekta ya benki, ambako aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Mikopo katika Benki ya Maendeleo ya TIB. Mwaka 2016 aliteuliwa kuongoza kampuni ya Reli Tanzania (TRL).
Kadogosa ana shahada ya uzamili ya Utawala wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Umeå nchini Sweden, huku akiwa na uzoefu katika maeneo ya uhasibu, usimamizi wa fedha na benki.
Kisiasa, mwaka 2025 aliingia kwenye mchakato wa mchujo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuwania nafasi ya ubunge, kabla ya sasa kuingia katika Serikali kama Waziri wa Ujenzi.
Akiwa Waziri wa Ujenzi, Kadogosa atakuwa na jukumu la kusimamia sekta inayohusisha ujenzi na maendeleo ya barabara, madaraja pamoja na miradi mbalimbali mikubwa ya miundombinu nchini.
Uteuzi wake unakuja wakati ambapo miradi ya miundombinu ikiendelea kuwa sehemu muhimu ya ajenda ya maendeleo ya Tanzania, hivyo utekelezaji na usimamizi wa miradi hiyo utakuwa miongoni mwa maeneo yatakayokuwa chini ya wizara hiyo.
Uapisho wa mawaziri walioteuliwa utafanyika katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Timu ya mpira wa wavu wanaume ya Jeshi la Magereza imeendeleza ushindani katika Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026, baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3–1 dhidi ya Timu ya JKT Tanzania, katika mchezo mkali uliofanyika leo Septemba 27, 2026 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mchezo huo uliokuwa wa kusisimua na wenye mashambulizi makali kutoka pande zote mbili, uliwashuhudia wachezaji wa Magereza wakitumia vyema mipango ya ushambuliaji na kuweka ulinzi imara, hali iliyowawezesha kutawala mchezo na hatimaye kupata ushindi wa seti 3–1.
Ushindi huo umeongeza nguvu kwa timu hiyo katika mwendelezo wa mashindano hayo, huku Magereza ikiendelea kuonyesha ushindani mkubwa dhidi ya timu za majeshi na vyombo vya ulinzi na usalama vinavyoshiriki BAMMATA 2026.
Katika mchezo uliotangulia, Timu ya Kanda ya Magereza ilikutana na Timu ya Ngome ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambapo Magereza ilipata ushindi wa seti 3–2 katika mchezo uliokuwa wa ushindani mkubwa.
Matokeo hayo yanaendelea kuonyesha kiwango cha ushindani cha timu ya Magereza katika michuano hiyo, huku wachezaji wakiendelea kuweka nguvu na umakini katika michezo inayofuata.
Global Publishers September 27, 2026 12 views 0 Comments
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya kiutendaji katika ngazi ya Makatibu wa CCM wa mikoa, kwa kuteua Kaimu Makatibu 32 wa mikoa yake yote ya kichama, ambao wanaanza kazi mara moja.
Taarifa hiyo imetolewa Septemba 27, 2026, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Labani Kihongosi. Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa mabadiliko hayo yanafuatia uteuzi wa viongozi wapya watakaosimamia shughuli za chama katika mikoa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha-Rose Migiro, ameandaa semina elekezi ya siku mbili kwa Kaimu Makatibu hao, itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Septemba 29 hadi 30, 2026.
Semina hiyo inalenga kuwaandaa viongozi hao kwa majukumu yao ya kiutendaji, huku orodha kamili ya walioteuliwa ikiwa kwenye kurasa zinazofuata za taarifa hiyo.
CCM pia imewapongeza na kuwashukuru Makatibu wa Mikoa waliomaliza muda wao kwa utumishi na mchango wao ndani ya chama, ikieleza kuwa itaendelea kutumia uzoefu na uwezo wao kama sehemu ya hazina ya viongozi na watendaji wake.
Global Publishers September 27, 2026 24 views 0 Comments
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Uamuzi huo umetangazwa Septemba 26, 2026 wakati Chacha akizungumza katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa uliojadili maandalizi ya
Chacha amesema hatua hiyo haimaanishi Goha ameondolewa kabisa katika majukumu ya chama, bali atapangiwa jukumu jingine ndani ya CCM.
Amesema mchakato wa kumpata Katibu mpya wa CCM Mkoa wa Iringa umeanza, huku chama kikiendelea na utaratibu wa kuhakikisha shughuli za uongozi mkoani humo zinaendelea bila kusimama hadi atakapopatikana atakayeshika nafasi hiyo.
Katika mkutano huo, Chacha amesisitiza umuhimu wa nidhamu miongoni mwa viongozi na wanachama wa CCM, akisema chama hakitafumbia macho mwenendo unaodaiwa kuathiri taswira na heshima yake.