Ligi Zimerudi, Inter, Newcastle na Villarreal wakaziwasha leo

Ligi mbalimbali zimerejea na huu ni msimu wa kutengeneza pesa tuu. Anza safari ya ushindi hapa kwani wengi wametajirika sana. Usisubiri kuhadithiwa kwani mabingwa wote wanapatikana hapa.

ITALIA kule SERIE A kutakuwa na mechi nyingi lakini sisi tutawatazama mabingwa watetezi Inter Milan ambao wao watakuwa nyumbani kukiwasha dhidi ya Udinese ambao wapo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi baada ya kukusanya pointi 4 hadi sasa.

Inter chini ya Chivu imekuwa ni timu ambayo inaendelea kufanya vyema kwani hadi sasa kwenye mechi 3 ambazo wamecheza wamefanikiwa kupata ushindi mechi zote tatu na kukusanya pointi 9.

Timu hiyo inahitaji kuendelea kukusanya kila pointi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea taji lao msimu huu pia huku wakiwa na wachezaji wengi na wenye ubora mkubwa wa kufanya hivyo wakiongozwa na Lautaro Martinez.

Udinese ni moja ya timu ambazo sio rahisi kuzifunga, lakini Inter wanaweza wakatumia uwanja wao wa nyumbani vyema kuhakikisha wanapata ushindi. ODDS KUBWA zipo hapa kwaajili yako hivyo beti sasa.

Mkwanja mnono upo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Ligi kuu ya Uingereza yaani EPL itaendelea kwa mechi moja pekee ambapo Leeds United watakuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Newcastle United, moja ya mchezo ambao unatarajiwa kuwa wa kuvutia kutokana na namna ambavyo timu zote huwa zinacheza.

Leeds United wao wana faida moja ya kutumia mashabiki zao hapo nyumbani ambao kw anamna moja au nyingine wanawapa morali ya kupambana zaidi na kuweka presha kwenye mchezo kwani ushindi huo utakuwa muhimu sana kwa upande wao baada ya kutoa sare kwenye mechi iliyopita. Bashiri mechi hii.

Kwa upande wa Newcastle United, uzoefu na ubora wa kikosi unaweza kuwapa faida katika mchezo huu. Newcastle ina uwezo wa kushambulia kupitia pembeni na pia kutumia mipira ya haraka pale inapopata nafasi. Ikiwa wataweza kutawala eneo la kiungo na kuzuia Leeds kucheza kwa uhuru, wana nafasi nzuri ya kupata matokeo.

Odds kubwa zipo kwenye mechi hii huku wakali wa ubashiri wao wakimpendelea Newcastle kuondoka na ushindi ugenini kutokana na kuwa na wachezaji bora. Lakini je Leeds watakubali?. Jisajili hapa.

Pia kule Hispania LALIGA kutakuwa na mechi moja kati ya Villarreal dhidi ya Real Betis ambapo Nyambizi wa Njano wao wakiwa na faida ya kucheza nyumbani lkaini pia na uwezo wao mkubwa wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi kupitia mashambulizi ya kushtukiza.

Real Betis wao, ni timu yenye uwezo wa kucheza kwa utulivu na kutumia pasi nyingi kujenga mashambulizi. Wakiwa na nafasi, Betis wanaweza kuwa hatari katika eneo la mwisho na kulazimisha Villarreal kurudi nyuma. Hata hivyo, watapaswa kuwa makini dhidi ya mashambulizi ya haraka ya Villarreal.

Tofauti ya pointi kati yao hadi sasa ni 7 pekee ambapo mwenyeji ndio kwanza ana pointi 2 kwenye mechi nne ambazo amecheza hivyo mwenendo wake sio mzuri kwenye ligi hadi sasa, wakati mpinzani wake akiwa na pointi tisa hadi sasa. Beti hapa.

Mara ya mwisho kukutana, yaanai msimu uliopita kwenye mechi mbili walizokutana, Betis alifanikiwa kuondoka na pointi 4 baada ya mechi ya kwanza kutoa sare na ya pili kushinda wakiwa kwao. Je nani kuondoka na ushindi leo?. Jisajili hapa.

 

PGMOL Yakubali VAR Ilikosea Bao la Haaland Dhidi ya Man United

 

 

Chombo cha Waamuzi wa kulipwa nchini Uingereza (PGMOL) kimewasiliana rasmi na klabu ya Manchester United na kuomba radhi baada ya kukiri kuwepo kwa “makosa ya kimaamuzi” katika goli la mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland, lililoamua Dabi ya Manchester iliyochezwa jana usiku.

Mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa ulifikia hatua ya sintofahamu katika dakika ya 60, wakati Haaland alipofunga goli pekee lililoipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester United katika dimba la Old Trafford.

Awali, mwamuzi wa pembeni alinyanyua bendera kuashiria kuwa Haaland alikuwa katika nafasi ya kuotea (offside), hivyo goli hilo likakataliwa.

Hata hivyo, mfumo wa usaidizi wa waamuzi kwa njia ya video (VAR) uliingilia kati na kuufanyia mapitio uamuzi huo. Baada ya kuchora mistari ya offside na kupitia picha za marudio, VAR ilibaini kuwa Haaland hakuwa ameotea, kutokana na nafasi ya beki wa Manchester United, Patrick Dorgu.

Lakini tatizo lilijitokeza katika hatua ya kutathmini ushawishi wa kiungo wa Manchester City, Enzo Fernández, ambaye alikuwa katika nafasi ya kuotea wakati mpira ukipigwa.

Fernández aliruka juu akijaribu kuucheza mpira kwa kichwa huku akiwa anagombea nafasi na beki wa Manchester United, Lisandro Martínez.

Kitendo hicho kinaweza kutafsiriwa kuwa aliingilia mchezo na kuathiri uwezo wa Martínez kucheza au kutetea mpira.

Hata hivyo, VAR ilishindwa kutathmini kikamilifu tukio hilo na kuzingatia tu nafasi ya Haaland, jambo ambalo baadaye lilionekana kuwa sehemu ya kosa la kimaamuzi.

PGMOL imekiri kuwa VAR ilipaswa kuzingatia pia kitendo cha Fernández na ushawishi wake kwa Martínez kabla ya kuthibitisha goli hilo.

Kutokana na hilo, PGMOL imewasiliana na Manchester United na kuomba radhi kwa kosa hilo, huku tukio hilo likiendelea kuibua mjadala kuhusu matumizi ya VAR na namna waamuzi wanavyotathmini matukio ya kuotea.

Na Peter Jinanai



Justin Bieber na Hailey Waadhimisha Miaka Nane ya Ndoa

Shechambo Chris
September 14, 2026
0 views
0 Comments

Staa maarufu wa muziki wa Pop, Justin Bieber, na mke wake Hailey Bieber,  Septemba 13, 2026, wameadhimisha miaka minane tangu walipofunga ndoa.

Justin ameadhimisha siku hiyo kwa kushirikisha picha kadhaa akiwa na Hailey, huku wawili hao wakionekana kufurahia muda wao pamoja, ikiwemo kucheza mchezo wa pool.

Akisindikiza picha hizo, Justin ameandika ujumbe wa kimapenzi kwa Hailey akisema, “8 years until infinity… new beginnings. i love you baby. happy anniversary.”

Ujumbe huo, hususan kauli yake ya “New Beginnings” inayomaanisha “mwanzo mpya,” umeibua mjadala miongoni mwa mashabiki, ambao wameanza kujiuliza ikiwa Justin anazungumzia hatua mpya katika maisha yao ya familia au anadokeza kuhusu kurejea rasmi kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa muda.

Justin na Hailey walifunga ndoa ya kiraia mjini New York mwaka 2018, kabla ya kufanya sherehe kubwa ya harusi huko South Carolina mwaka 2019.

Kwa sasa, wanalea mtoto wao wa kiume, Jack Blues Bieber, aliyezaliwa mwaka 2024.

Hivyo, maadhimisho ya mwaka huu yamekuwa ya kipekee kwa mashabiki, hasa kutokana na ujumbe wa Justin kuhusu “mwanzo mpya,” ambao hadi sasa hajaueleza kwa kina kuhusu maana yake.

Na Razaku Ramadhan.



Mambo yameiva mradi wa uondoshaji majitaka Buguruni

DAR ES SALAAM; Mradi wa uondoshaji majitaka eneo la Buguruni, Wilaya ya Ilala unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) umefikia asilimia 40, huku wakazi takribani 181,440 wakitarajiwa kunufaika na huduma hiyo pindi utakapokamilika.

‎Msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Khalid Upunda, amesema ujenzi wa miundombinu ya kupokea na kusafirisha majitaka unaendelea, huku kilometa 20.2 za mtandao wa mabomba zikiwa zimelazwa kati ya kilometa 25.4 zinazotarajiwa kujengwa katika maeneo ya Magomeni, Ndugumbi na Mzimuni.
‎
‎Amesema mradi huo utahudumia wakazi wa Buguruni na maeneo mengine ya Ilala na Kinondoni, yakiwemo Mivinjeni, Mchikichini, Kariakoo, Jangwani, Gerezani, Kisutu, Mchafukoge, Upanga Mashariki, Upanga Magharibi, Kivukoni, Magomeni, Ndugumbi na Mzimuni.


‎
“Mpaka sasa tumefanikiwa kulaza mtandao wa mabomba ya kusafirisha majitaka ya inchi nane kwa umbali wa kilometa 20.2 kati ya kilometa 25.4 katika kata tatu za Magomeni, Ndugumbi na Mzimuni,” amesema Upunda.

‎Mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Kolon Global Corporation unatarajiwa kukamilika mwaka 2028 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 185.


‎
‎Mhandisi Upunda ametaka wananchi kuwa wavumilivu na kushirikiana katika kulinda miundombinu itakayojengwa, akisema ushirikiano wao ni muhimu kuhakikisha mradi unakamilika na huduma inatumika kwa muda mrefu.
‎
‎Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mivinjeni, Fadiga Mtumwa, amesema mradi huo utasaidia kupunguza changamoto ya majitaka na hatari ya magonjwa yanayohusishwa na mazingira yasiyo safi.

Fahamu Faida na Hasara za Kutumia Gesi Kwenye Gari Kabla Hujafunga Mfumo

Matumizi ya gesi kwenye magari yanaendelea kuongezeka kutokana na gharama nafuu za uendeshaji na jitihada za kupunguza matumizi ya mafuta ya petroli na dizeli. Hata hivyo, kabla ya kufanya uamuzi wa kubadili mfumo wa gari lako kutumia gesi, ni muhimu kufahamu faida na changamoto zake.

Bei ya kufunga mfumo wa gesi (CNG au LPG) kwenye gari hutegemea aina ya mfumo, ukubwa wa injini, idadi ya silinda na ubora wa vifaa vinavyotumika. Kwa Tanzania, makadirio ya bei ni kama yafuatayo:

  • Magari yenye injini ndogo (silinda 3–4): Takribani Sh milioni 1 hadi 3.5.
  • Magari yenye injini za kati (silinda 4–6): Takribani Sh milioni 3 hadi 5.
  • Magari makubwa (V6, V8 au SUV): Takribani Sh milioni 5 hadi 8 au zaidi, kutegemea mfumo unaowekwa.

Bei hiyo mara nyingi hujumuisha:

  • Tanki la gesi.
  • ECU (kompyuta ya mfumo wa gesi).
  • Injectors za gesi.
  • Pressure reducer/regulator.
  • Mabomba na vifaa vya usalama.
  • Ufungaji na majaribio ya mfumo.

Faida za kutumia gesi kwenye gari

1. Gharama nafuu za mafuta
Gesi kwa kawaida huwa na bei ya chini kuliko petroli au dizeli, hivyo hupunguza gharama za uendeshaji kwa madereva wanaosafiri mara kwa mara.

2. Rafiki kwa mazingira
Magari yanayotumia gesi hutoa kiwango kidogo cha hewa chafu, hivyo huchangia kupunguza uchafuzi wa mazingira.

3. Huongeza maisha ya injini
Gesi huungua kwa usafi zaidi kuliko petroli, jambo linalosaidia kupunguza mabaki ya kaboni ndani ya injini na kuongeza maisha ya baadhi ya vipuri.

4. Huongeza chaguo la mafuta
Magari mengi yaliyowekewa mfumo wa gesi yanaweza kutumia gesi au petroli, hivyo dereva ana uhuru wa kuchagua kulingana na upatikanaji wa mafuta.

Hasara za kutumia gesi kwa upande wa injini

1. Kuongeza uchakavu wa valve na valve seats
Gesi huungua kwa joto la juu zaidi kuliko petroli katika baadhi ya mazingira ya uendeshaji. Kwa injini ambazo hazikutengenezwa mahsusi kutumia gesi, hali hii inaweza kuongeza uchakavu wa valve na sehemu zake (valve seats), na kusababisha gharama za matengenezo.

2. Kupungua kwa nguvu ya injini
Baadhi ya magari hupoteza kati ya asilimia 5 hadi 15 ya nguvu ya injini yanapotumia gesi, kutegemea aina ya mfumo na jinsi ulivyowekwa.

3. Hatari ya kuharibika kwa injini ikiwa mfumo umefungwa vibaya
Mfumo usiofungwa au usiotunzwa vizuri unaweza kusababisha mchanganyiko usio sahihi wa hewa na gesi (lean mixture), hali inayoweza kuongeza joto la injini na kusababisha uharibifu wa valve, pistoni au gasket ya kichwa cha injini (head gasket).

4. Kuongezeka kwa mzigo kwenye mfumo wa kuwasha (ignition system)
Matumizi ya gesi yanahitaji mfumo wa kuwasha uwe katika hali bora. Spark plugs, ignition coils na nyaya zake zinaweza kuchakaa haraka zaidi ikiwa hazitafanyiwa matengenezo kwa wakati.

5. Si kila injini inafaa kutumia gesi
Baadhi ya injini, hasa zenye valve seats laini au zilizotengenezwa bila kuzingatia matumizi ya gesi, zinaweza kupata uchakavu wa mapema. Ni muhimu kuhakikisha mtengenezaji wa gari au fundi mwenye uzoefu anathibitisha kuwa injini yako inafaa kufungwa mfumo wa gesi.

6. Gharama za matengenezo zinaweza kuongezeka
Iwapo mfumo wa gesi hautafungwa kwa viwango vinavyotakiwa au hautafanyiwa huduma za mara kwa mara, unaweza kusababisha hitilafu zinazohitaji matengenezo ya gharama kubwa kwenye injini.

Muhimu kufahamu

Hasara hizi si lazima zitokee kwa kila gari. Magari yenye mifumo ya kisasa ya gesi iliyofungwa kitaalamu, kutunzwa vizuri, na yanayotumia vifaa vya ubora mzuri yanaweza kufanya kazi kwa miaka mingi bila kupata uharibifu mkubwa wa injini. Jambo muhimu ni kufunga mfumo katika kituo kinachoaminika, kutumia vifaa vilivyoidhinishwa na kufuata ratiba ya matengenezo iliyopendekezwa.

Ajira Mpya 678 Serikalini, Madaktari na Walimu, Mwisho wa Maombi Sept 17, 2026

Dodoma, Septemba 3, 2026 — Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya

Tangazo hilo lenye Kumb. Na. JA.9/16/01/56, limetolewa Septemba 3, 2026, likiwa na nafasi katika kada mbalimbali kuanzia madaktari, wauguzi, walimu, wataalamu wa mifugo hadi watumishi wa ofisi.

Nafasi zilizotangazwa

1. Daktari Daraja la II – Nafasi 115

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Udaktari kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali, wawe wamekamilisha mafunzo ya Internship na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika.

Majukumu yanahusisha kutoa huduma za matibabu, elimu ya afya, kuzuia milipuko ya magonjwa, kutunza takwimu za afya, kusimamia watumishi na kushiriki katika kuboresha ubora wa huduma za afya.

Mshahara: TGHS E

2. Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II – Nafasi 128

Nafasi hizi ni kwa wenye Stashahada ya Uuguzi ya muda usiopungua miaka miwili kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Mwombaji anatakiwa pia kuwa amesajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

Mshahara: TGHS B3. Afisa Mifugo Daraja la II – Nafasi 39

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Sayansi ya Wanyama (Animal Science) au Shahada ya Sayansi ya Kilimo aliyebobea katika Sayansi ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine au sifa inayolingana kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Majukumu yanahusisha kupanga na kusimamia uzalishaji wa mifugo, kutoa mafunzo kwa wafugaji, kuratibu miradi ya mifugo, kukusanya takwimu na kushiriki katika kudhibiti changamoto zinazohusiana na mifugo na mazingira.

Mshahara: TGS D

4. Tabibu wa Kinywa na Meno Daraja la II – Nafasi 17

Waombaji wanatakiwa kuwa na Stashahada ya Tabibu wa Meno (Diploma in Clinical Dentistry) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Baraza la Madaktari.

Mshahara: TGHS B

5. Mteknolojia Maabara Daraja la II – Nafasi 25

Nafasi hizi ni kwa wenye Stashahada katika Uteknolojia wa Maabara za Afya kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Mwombaji anatakiwa pia kuwa amesajiliwa na Baraza la Wataalamu wa Maabara.

Mshahara: TGHS B

6. Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II – Nafasi 74

Waombaji wanatakiwa kuwa na elimu ya Kidato cha Nne au Kidato cha Sita, pamoja na Stashahada ya Uhazili (NTA Level 6).

Wanapaswa pia kuwa wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa kasi ya maneno 100 kwa dakika moja na kuwa na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi kama Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.

Mshahara: TGS C

7. Mwalimu Daraja la III C – Fizikia – Nafasi 55

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Elimu/Bachelor of Education yenye somo la Fizikia au shahada isiyo ya ualimu yenye Fizikia kama somo la kufundishia pamoja na Stashahada ya Uzamili ya Elimu (PGDE).

Mshahara: TGTS D

8. Mwalimu Daraja la III C – Hisabati – Nafasi 67

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Elimu/Bachelor of Education yenye Hisabati kama somo la kufundishia, au shahada isiyo ya ualimu yenye Hisabati pamoja na PGDE.

Mshahara: TGTS D

9. Mwalimu Daraja la III B – Fizikia – Nafasi 43

Nafasi hizi ni kwa wahitimu wenye Cheti cha Kidato cha Sita waliofaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni na wenye Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili yenye Fizikia kama somo la kufundishia.

Mshahara: TGTS C

10. Mwalimu Daraja la III B – Hisabati – Nafasi 48

Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Sita, wakiwa wamefaulu masomo mawili au zaidi yanayofundishwa shuleni, pamoja na Stashahada ya Ualimu ya miaka miwili yenye Hisabati kama somo la kufundishia.

Mshahara: TGTS C

11. Afisa Misitu Msaidizi Daraja la II – Nafasi 28

Waombaji wanatakiwa kuwa na Stashahada katika fani kama Forestry, Agroforestry, Forest Resources Assessment and Management, Forest Biology, Forest Economics, Forest Engineering au fani inayohusiana.

Majukumu ni pamoja na kusimamia ukusanyaji wa mbegu na bustani za miti, kukusanya takwimu za misitu, kusimamia upandaji na utunzaji wa miti, kupima mazao ya misitu na kufanya doria.

Mshahara: TGS C

12. Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II – Nafasi 26

Waombaji wanatakiwa kuwa na Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wawe wamesajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira.

Majukumu yanahusisha kudhibiti milipuko ya magonjwa, kutoa elimu ya afya ya mazingira, kukagua usalama wa maeneo ya chakula, kusimamia sheria za afya ya mazingira na kuhamasisha jamii kuhusu usafi na afya.

Mshahara: TGHS B

13. Mwalimu Daraja la III C – Fasihi ya Kiingereza – Nafasi 13

Waombaji wanatakiwa kuwa na Shahada ya Elimu/Bachelor of Education yenye Fasihi ya Kiingereza kama somo la kufundishia, au shahada isiyo ya ualimu yenye somo hilo pamoja na PGDE.

Mshahara: TGTS D

Masharti muhimu ya maombi

Waombaji wote wanatakiwa kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wasizidi umri wa miaka 45.

Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha aina ya ulemavu wao kwenye mfumo wa maombi.

Mwombaji anatakiwa kuambatisha cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili, pamoja na vyeti vya elimu na vyeti vya kitaaluma vinavyohitajika kwa nafasi husika.

Sekretarieti ya Ajira imesisitiza kuwa Testimonials, Provisional Results, Statement of Results pamoja na Result Slips za Kidato cha Nne na Kidato cha Sita hazitakubaliwa.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA au NACTVET, kulingana na sifa husika.

Aidha, waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wawe na kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ya nafasi hizi ni Septemba 17, 2026.

Maombi yote yanatakiwa kutumwa kwa njia ya kielektroniki kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira.

Barua ya maombi iliyosainiwa inapaswa kuambatishwa pamoja na vyeti vinavyohitajika na ielekezwe kwa:

KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
Mtaa wa Mahakama, Tambukareli,
S.L.P. 2320,
DODOMA.

Sekretarieti ya Ajira imeonya kuwa maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu uliowekwa hayatafikiriwa.

Aidha, waombaji wamekumbushwa kuwa ni marufuku kutoa au kupokea rushwa kwa lengo la kupata ajira au kupangiwa kituo cha kazi. Mchakato wa ajira unapaswa kuzingatia misingi ya haki, usawa na uwazi.

Limetolewa na:
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Pakistan Yalaani Mashambulizi Dhidi ya Saudi Arabia

Global Publishers
September 14, 2026
24 views
0 Comments

RIYADH, Saudi Arabia — Waziri Mkuu wa Pakistan, Muhammad Shehbaz Sharif, amelaani vikali mashambulizi yanayolenga Saudi Arabia, akieleza kuwa Pakistan inasimama pamoja na Ufalme huo katika kulinda usalama na mamlaka yake.

Sharif alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, Jumapili, Septemba 13, 2026.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Mkuu huyo alilaani mashambulizi yanayohusishwa na waasi wa Houthi dhidi ya Saudi Arabia, akisema yanakiuka waziwazi mamlaka na uadilifu wa eneo la Ufalme huo.

Aidha, Sharif alilaani mashambulizi yaliyolenga miundombinu muhimu ya mafuta ya Saudi Arabia na kusisitiza kuwa Pakistan inaunga mkono juhudi za Saudi Arabia za kulinda usalama wake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Saudi Arabia (SPA), Sharif pia amepongeza msimamo wa Saudi Arabia wa kujizuia katika kipindi hiki cha mvutano wa kikanda.

Waziri Mkuu huyo pia ameunga mkono juhudi za serikali ya Iraq kuhakikisha kuwa ardhi ya nchi hiyo haitumiki kufanikisha mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia au mataifa mengine jirani.

Viongozi hao wawili walijadili pia maendeleo ya hivi karibuni katika eneo hilo pamoja na juhudi za kidiplomasia zinazolenga kupunguza mvutano na kuzuia hali ya usalama katika Mashariki ya Kati kuzidi kuwa mbaya.

Kauli ya Pakistan inaonyesha kuendelea kwa uhusiano wa karibu kati ya Islamabad na Riyadh, huku mataifa ya eneo hilo yakiongeza juhudi za kidiplomasia kukabiliana na ongezeko la mvutano wa kikanda.

Haaland Aichapa United Old Trafford, City Yashinda Derby kwa Bao la Utata

MANCHESTER, England — Erling Haaland amekuwa shujaa wa Manchester City baada ya kufunga bao lenye utata na kuipa timu yake ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa 199 wa Manchester Derby uliochezwa Old Trafford Septemba 13, 2026.

City, iliyokuwa ikicheza ikiwa na wachezaji 10 baada ya Phil Foden kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 23, ilipata ushindi huo kupitia bao la Haaland dakika ya 60.

Awali bao hilo lilikataliwa kwa madai ya Haaland kuwa ameotea, lakini uamuzi huo ulibadilishwa baada ya waamuzi wa VAR kupitia tukio hilo.

Uamuzi huo uliwaibua hasira wachezaji wa Manchester United, ambao walidai kuwa Enzo Fernandez alikuwa katika nafasi ya kuotea wakati wa mchakato wa kutengenezwa kwa bao hilo.

Ligi Kuu ya England ilieleza kuwa bao hilo lilikubalika kwa sababu Fernandez, licha ya kujaribu kuucheza mpira kwa kichwa, hakugusa mpira kabla haujamfikia Haaland aliyekuwa upande wa mbali wa lango.

Hata hivyo, beki wa United, Lisandro Martinez, alieleza kutoridhishwa na uamuzi huo na kuuita “dhuluma.”

Kocha wa United, Michael Carrick, naye alisema hakuelewa sababu iliyofanya bao hilo likubalike.

“Sielewi kabisa. Inatia wasiwasi ikiwa ndivyo mchezo unavyoonekana kwa wale wanaousimamia,” Carrick alisema.

City Yafanikiwa Licha ya Kucheza Watu 10

Manchester City ilipata pigo kubwa katika dakika ya 23 baada ya Phil Foden kupewa kadi nyekundu kwa kumpiga teke Bruno Fernandes.

Wachezaji wa City walipinga uamuzi huo, huku kocha Enzo Maresca akidai kuwa Fernandes pia alistahili kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na tukio hilo.

Licha ya kuwa na mchezaji mmoja zaidi, Manchester United ilishindwa kutumia nafasi hiyo. Marcus Rashford aligonga mwamba kwa mkwaju wa adhabu kabla ya mapumziko, huku Kobbie Mainoo naye akipiga mpira uliogonga mwamba kipindi cha pili.

Ushindi huo umeifanya City kuendelea na mwanzo wake wa asilimia 100 katika msimu huu na kufikisha pointi sawa na mabingwa watetezi Arsenal kileleni mwa msimamo.

Maresca aliwapongeza wachezaji wake kwa kuonyesha mshikamano licha ya kucheza pungufu.

“Ni hali isiyo ya kawaida kushinda mchezo ukiwa na wachezaji 10. Ni jambo la ajabu, na kwa kuwa ni derby, ushindi huu ni bora zaidi,” alisema.

Haaland Aweka Rekodi Mpya

Bao hilo limemfanya Haaland kuwa mfungaji bora wa Manchester Derby katika Premier League, akiwa amefikisha mabao tisa dhidi ya United.

Mshambuliaji huyo wa Norway amempita Wayne Rooney na Sergio Aguero, ambao kila mmoja ana mabao nane katika derby hiyo.

Haaland amefikisha mabao hayo tisa katika mechi nane pekee, wakati Rooney alihitaji michezo 21 na Aguero michezo 13.

Bao hilo pia lilikuwa la sita kwa Haaland katika mashindano yote msimu huu.

United Yabaki Nafasi ya 13

Kwa upande mwingine, Manchester United imeendelea kupata mwanzo mgumu wa msimu ikiwa na ushindi mmoja pekee katika michezo minne.

United iko katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Premier League na sasa italazimika kurejea uwanjani katikati ya wiki dhidi ya Brighton katika mchezo wa League Cup.

Carrick amesema timu yake haina haja ya kuanza upya, bali inapaswa kuendelea kupambana ili kurejea kwenye njia ya ushindi.

“Hatuna pointi nyingi kama tulivyotarajia kufikia hatua hii. Lakini hatuhitaji mapumziko wala kuanza upya. Tunachotakiwa ni kusonga mbele na kuanza kushinda tena,” alisema.

Coventry Yapigwa 5-0 na Brighton

Katika mchezo mwingine wa Premier League, Coventry City iliendelea na mwanzo mbaya wa msimu baada ya kuchapwa 5-0 nyumbani na Brighton.

Coventry, ambayo ilifanya vizuri sana Championship msimu uliopita, sasa imepoteza michezo yote minne ya kwanza tangu kurejea katika ligi ya juu.

Timu hiyo bado haijafunga bao katika michezo hiyo na ina tofauti ya mabao -10.

Charalampos Kostoulas aliipa Brighton uongozi kabla ya mapumziko, huku Malick Yalcouye, Pascal Gross, Lewis Dunk na Yasin Ayari wakiongeza mabao kipindi cha pili na kukamilisha ushindi mkubwa wa Brighton.

Mtendaji Mkuu Singida Black Stars Ajiuzulu, Wamtangaza Tabitha Kidawawa

Global Publishers
September 14, 2026
918 views
0 Comments

Uongozi wa Klabu ya Singida Black Stars umetangaza mabadiliko ya uongozi baada ya Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Kassano Jonathan, kuomba kujiuzulu nafasi yake.

Kupitia taarifa iliyotolewa Septemba 13, 2026, uongozi wa klabu umesema umekubali ombi hilo na kumteua Tabitha Kidawawa kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa Singida Black Stars, akisaidiwa na Naibu wake, Muhibu Kanu.

Aidha, uongozi wa klabu umemshukuru Kassano Jonathan kwa mchango wake mkubwa katika kipindi chote alichohudumu, huku ukimtakia kila la heri katika hatua zake zijazo.

Uongozi umeeleza kuwa unaamini mabadiliko hayo yataisaidia Singida Black Stars kuendelea kuwa nyumbani kwa wanyumbani wake na kufikia malengo yake.