Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Awasili Roma Kumwakilisha Rais Samia

Global Publishers
September 20, 2026
0 views
0 Comments

 

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili jijini Roma, Italia, leo, Septemba 20, 2026, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo (One Health), utakaofanyika Septemba 21–23, 2026, katika Makao Makuu ya FAO.

Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Leonardo da Vinci (Fiumicino), Waziri Mkuu amepokelewa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.

Rais Dkt. Mwinyi: SMZ Inathamini Mchango Wa Kanisa Katika Maendeleo ya Jamii

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali na taasisi za dini zina wajibu wa kuendelea kushirikiana katika kuimarisha amani, umoja na mshikamano, kukuza maadili mema na kuchangia ustawi wa wananchi.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 20 Septemba 2026, katika hafla ya kuwekwa wakfu na kumketisha kitini Mhashamu Askofu Lameck Paul Ndomba kuwa Askofu wa 11 wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Zanzibar, iliyofanyika  Kanisa Kuu la Kristo, Mkunazini Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amesema Kanisa na taasisi nyingine za dini zina mchango mkubwa katika elimu, afya, malezi, ujenzi wa maadili na maendeleo ya jamii, akisisitiza kuwa tofauti za kiimani zinapaswa kuwa msingi wa kuheshimiana, kuvumiliana na kushirikiana katika kudumisha amani ya Zanzibar.

Rais Dkt. Mwinyi amempongeza Mhashamu Askofu Lameck Paul Ndomba na kumtakia hekima, afya, nguvu na neema ya Mwenyezi Mungu katika kutekeleza majukumu yake ya kuiongoza Dayosisi ya Zanzibar.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Anglikana katika kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya kihistoria kwa lengo la kuhifadhi historia ya Zanzibar, kutoa elimu na kukuza utalii wa kihistoria na kiutamaduni.

Akizungumzia hali ya hewa, Rais Dkt. Mwinyi amewahimiza wananchi kuchukua tahadhari na kuzingatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mvua za Vuli zinazotarajiwa kuathiriwa na hali ya El Niño, huku akizitaka taasisi za dini kushirikiana na Serikali kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa.

Naye , Mhashamu Askofu Lameck Paul Ndomba amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa ushirikiano anaouonesha kwa taasisi za dini na juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi .

G Nako Na Live Band Kutikisa Jukwaa, Wasanii Wengine Kukiwasha

Global Publishers
September 20, 2026
60 views
0 Comments

Nguli wa muziki G Nako (Warawara) anatarajiwa kulipua jukwaa katika kilele cha Gambe Fest 2026 tarehe 03/10/2026, akitumbuiza mubashara na Live Band pamoja na wasanii wengine wakubwa.

Kilele hicho kinatarajiwa kuwa na performance ya hatari kutoka kwa G Nako & Live Band, sambamba na wasanii waalikwa, Guest DJs, Guest Artists, Karaoke Battle, Live Band Experience, Fashion Bonanza, Sip & Shop, Acrobatic & Fire Shows na michezo kibao ya kushirikisha mashabiki.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Masoko wa Mi Casa Lounge, Denis Binamungu, amesema Gambe Fest 2026 linatua rasmi kuanzia tarehe 20/09/2026 hadi 03/10/2026, likiahidi wiki mbili za msisimko wa hali ya juu na burudani isiyo na kikomo katika Mi Casa Lounge, Barabara ya Mandela, Ubungo.

Amesema burudani hizo zitaenda sambamba na Live BBQ, ambapo mashabiki watapata nyama choma na msosi wa mkaa papo hapo muda wote wa tamasha.

Kwa mujibu wa Binamungu, tiketi tayari zimeanza kuuzwa kupitia @otapptz na Mi Casa Lounge, Mandela Road, Ubungo, huku mashabiki wakitarajiwa kupata mchanganyiko wa muziki, burudani, michezo na burudani shirikishi kwa siku zote za Gambe Fest 2026.

Pia Sloti: Mchezo Wenye Mandhari ya Marekani ya Kale na Jackpot

Global Publishers
September 20, 2026
414 views
0 Comments

Katika kasino, wakati mwingine kinachomvutia mchezaji si ushindi pekee, bali pia namna mchezo unavyompeleka kwenye ulimwengu mwingine. Pia Sloti imekuja na dhana hiyo, ikichanganya mandhari ya kuvutia na safari ya kutafuta hazina katika mazingira yenye ladha ya Marekani ya kale. Kupitia Meridianbet, mchezo huu unaendelea kuwa sehemu ya burudani kwa wapenzi wanaopenda kuona kitu kipya kila wanapoanza mzunguko.

Mara tu mchezo unapoanza, simulizi linachukua nafasi. Unajikuta katika mazingira yanayokukumbusha hadithi za wawindaji hazina waliokuwa wakitafuta utajiri uliofichwa. Kila alama inayotokea inaweza kuongeza msisimko wa mzunguko, huku macho yakibaki kwenye mchezo kuona kitakachofuata. Ni safari ambayo kila raundi inakuja na matarajio yake na inaweza kuwa tofauti na iliyopita.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Lakini safari ya Pia Sloti haijaishia kwenye mandhari pekee. Jackpot ya ngazi tatu inaongeza kipengele kingine kinachoweza kufanya kila mzunguko uwe na mvuto zaidi. Wachezaji wanaweza kufuatilia viwango vya jackpot huku wakifurahia mchezo, wakisubiri kuona kama safari yao itafikia mojawapo ya zawadi hizo. Hapo ndipo kila raundi inapopata nafasi ya kuwa sehemu ya simulizi kubwa zaidi.

Kwa upande mwingine, urahisi wa mchezo na muonekano wake wa kuvutia vinafanya Pia Sloti iwe rahisi kuingia na kuifurahia. Kwa wapenzi wa kasino wanaopenda burudani yenye ladha ya safari, mchezo huu unaleta mchanganyiko wa mandhari, uchezaji na matarajio katika sehemu moja. Kila mzunguko unafungua ukurasa mwingine wa simulizi, huku mchezaji akiendelea kufurahia safari hiyo.

Kwa hiyo, kama unataka kubadili mazingira na kuingia kwenye safari yenye ladha ya wawindaji hazina, Pia Sloti ndani ya Meridianbet iko tayari kukupa burudani hiyo. Ingia kwenye mandhari ya Marekani ya kale, furahia kila mzunguko na fuatilia jackpot ya ngazi tatu.

Haaland kuongoza Man City dhidi ya Sunderland EPL leo

Global Publishers
September 20, 2026
84 views
0 Comments

Manchester City itakuwa mwenyeji wa Sunderland jioni ya leo Jumapili, Septemba 20, katika mchezo wa Ligi Kuu England utakaochezwa kwenye Uwanja wa Etihad. Mchezo huo utaanza saa 16:00 jioni, ukiwa ni mchezo wa raundi ya tano ya EPL msimu wa 2026/27.

Manchester City wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na mwanzo mzuri wa msimu, baada ya kushinda michezo yote minne ya kwanza ya EPL na kukusanya pointi 12. Katika mchezo wao uliopita wa ligi, walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester United kwenye dimba la Old Trafford, huku Erling Haaland akifunga bao pekee la mchezo huo.

Kwa upande wa Sunderland, timu hiyo imekusanya pointi nne katika michezo minne ya mwanzo, ikishinda mmoja, sare mmoja na kupoteza miwili. Mchezo wao uliopita wa ligi uliisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya Brentford, kabla ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya AZ Alkmaar katika Europa League katikati ya wiki.

Haaland anatarajiwa kuwa mchezaji wa kuangaliwa zaidi katika mchezo huo kutokana na kuanza msimu akiwa na mabao manne katika mechi nne za ligi.

Taarifa za ratiba, matokeo na takwimu za michezo mbalimbali ya EPL zinapatikana kupitia majukwaa ya taarifa za michezo, ikiwemo Meridianbet, pamoja na vyanzo vingine vya michezo.

Manchester City Pia wana wachezaji wenye uwezo wa kutengeneza nafasi kama Anthonio Semenyo na Rayan Cherki, wakati Sunderland watategemea wachezaji kama Granit Xhaka, Enzo Le Fée na Wilson Isidor katika kujaribu kuvunja  safu ya ulinzi ya Mn city.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, hasa kutokana na Sunderland kuhitaji matokeo mazuri dhidi ya moja ya timu zinazoshika nafasi za juu. Manchester City, kwa upande wao, watajaribu kutumia faida ya kucheza nyumbani na kuendeleza mwenendo wao mzuri katika msimu huu.

Waziri Mkuu Kumwalikisha Rais Dkt. Samia Mkutano wa Afya Moja Nchini Italia

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 19, 2026) kwenda Roma, Italia kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo.

Mkutano huo utakaofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), jijini Roma, Italia kuanzia Septemba 21–23, 2026 unalenga kuimarisha utekelezaji wa dhana ya Afya Moja (One Health) inayotambua uhusiano kati ya afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira, kwa lengo la kuhakikisha mifumo endelevu ya chakula na kilimo

Mkutano huo utahusisha viongozi wa nchi na Serikali, wakiwemo Marais kati ya watano hadi saba, Mawaziri kati ya 30 hadi 50, pamoja na wawakilishi wa taasisi za kikanda na kimataifa, wadau wa maendeleo, sekta binafsi, taasisi za utafiti na mashirika ya kimataifa.

Mambo muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni Ujumuishaji wa dhana ya Afya Moja (One Health) katika sera na uwekezaji wa mifumo ya chakula na kilimo; na uimarishaji wa ushirikiano wa kisekta kati ya sekta za kilimo, mazingira, afya, fedha na mipango ya miji.

Mengine ni ukuzaji wa ubunifu, sayansi na maarifa ya ndani ili kuboresha uzuiaji wa vihatarishi, ufuatiliaji na usimamizi endelevu wa rasilimali na kuhamasisha uwekezaji na ushirikiano ili kutafsiri ahadi kuwa hatua madhubuti zenye matokeo yanayopimika.

RC BABU APIGA MARUFUKU WAFANYABIASHARA WA NJE YA SOKO LA MBUYUNI..

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA, MOSHI.

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewaagiza wafanyabiashara wanaopanga bidhaa zao chini katika barabara za soko la Mbuyuni manispaa ya Moshi kuondoka katika maeneo hayo na kufanya biashara zao ndani ya soko hilo ili kuepuka milipuko ya magonjwa pamoja na uchafuzi wa mazingira.

Babu alitoa kauli hiyo jana wakati wa zoezi la ufanyaji usafi katika soko hilo ambapo alisema kuwa, barabara zimewekwa kwa ajili ya kupita magari na wananchi kupita bila kubugudhiwa.

Alisema kuwa, wafanyabiashara hao ambao wanapanga bidhaa zao chini wanapaswa kwenda kwa viongozi wa soko hilo waweze kuwapangia maeneo ya kufanyia biashara kabla ya serikali haijachukua hatua za kuwaondoa katika maeneo hayo.

“Niwataka muanze kuondoka wenyewe mapema tusije kuja kuwaondoa sisi mkasema tunawaonea serikali imetumia fedha nyingi kujenga masoko haya sasa ni wajibu wenu mkafanye biashara ndani ya masoko haya ambayo yamewekwa miundombinu rafiki ya kuwahudumia” alisema Babu.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa, wafanyabiashara hao wote wakijipanga ndani ya soko hilo wateja watawafuata humo ndani kununua na kuwataka kutekeleza sheria hiyo bila shuruti.

KUPIGA KURA TUZO YA SKA2026 PIGA MATUKIO DAIMA HAPA

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

WAZAZI WASEMA KLABU ZA VIPIMO ZIMEWAFUNGUA MACHO

Wazazi jijini Dodoma wamesema elimu ya vipimo inayotolewa kupitia Klabu za Vipimo katika shule za msingi imeanza kuleta mabadiliko ndani ya familia, baada ya watoto waliopatiwa mafunzo na Wakala wa Vipimo (WMA) kuanza kuwafundisha wazazi wao namna ya kutambua vipimo sahihi na kujilinda dhidi ya upunjaji katika manunuzi.

Wazazi wameyasema hayo  Septemba 18,2026  wakati wa mahafari ya wanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Mtemi Mazengo jijini Dodoma ambapo  wanafunzi wa klabu ya vipimo walikuwa wakitoa elimu ya vipimo kwa wazazi na watu wengine mbalimbali waliohudhuria akiwemo Mgeni Rasmi.

Mzazi wa mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mtemi Mazengo, Bertha Paulo Chipaga, amesema mtoto wake, Gloria Elisha Enock, amekuwa akimsaidia kuelewa matumizi sahihi ya mizani ya chakula, mita ya maji na vipimo vingine, jambo ambalo limempa uelewa na kujiamini zaidi kama mlaji.

Bi.Chipaga amesema awali hakuwa na uelewa mpana kuhusu namna ya kutambua kama kipimo kinachotumika katika biashara ni sahihi, lakini tangu mtoto wake ajiunge na Klabu ya Vipimo amekuwa akipata elimu hiyo nyumbani na sasa anaelewa umuhimu wa kuhakikisha bidhaa anayonunua inalingana na kiasi cha fedha anacholipa.

“Hatua hiyo inaonesha kuwa elimu inayotolewa kwa watoto haiishii shuleni, bali inasambaa hadi kwenye familia na jamii, hivyo akawataka wazazi wengine kutumia fursa hiyo kuwaelimisha watoto wao kuhusu haki za mlaji na matumizi sahihi ya vipimo.”amesema Bi.Chipaga

Akizungumza kuhusu umuhimu wa kuwaandaa watoto na elimu hiyo, mkazi wa Makao Mapya jijini Dodoma, Peter Daudi Mponzi, amesema mafunzo ya vipimo kwa wanafunzi ni uwekezaji muhimu kwa jamii kwa sababu yanawajengea uwezo wa kutambua mizani na vipimo visivyo sahihi wanapokuwa katika mazingira ya biashara.

Amesema mtoto anayeelewa vipimo anaweza kwenda dukani na kuangalia kama mzani unaotumika umehakikiwa, hivyo kupunguza uwezekano wa yeye au familia yake kupunjwa na wakati huo huo kueneza elimu hiyo kwa watu wengine.

Mponzi amesema kuanzia elimu hiyo katika umri mdogo kunaweza kujenga kizazi chenye uelewa mpana wa masuala ya vipimo na haki za walaji, kwa kuwa watoto wanakuwa na nafasi ya kutumia maarifa hayo katika maisha yao ya kila siku.

 “Watoto wanapotoka shuleni na kwenda majumbani, dukani na katika maeneo mengine ya jamii, wanakuwa sehemu ya mnyororo wa elimu unaoweza kuwafikia wazazi, ndugu na wananchi wengine, hivyo kuongeza uelewa wa jamii kuhusu umuhimu wa vipimo sahihi.”amesema

Mwanafunzi wa Klabu ya Vipimo katika Shule ya Msingi Mtemi Mazengo, Gloria Elisha Enock, amesema WMA imewajengea uwezo wa kuelewa maana na umuhimu wa vipimo pamoja na jukumu la Wakala la kumlinda mlaji.

Amesema wamefundishwa kuwa WMA huhakiki vipimo mbalimbali, ikiwemo mizani, mita za maji na umeme, pamoja na bidhaa zilizofungashwa, huku mlaji akitakiwa kuangalia alama ya WMA kwenye mizani ili kuhakikisha kipimo  hicho kimehakikiwa na kinafanya kazi kwa usahihi.

Kwa upande wake, mwanafunzi mwenzake, Venosa Michael Simba, amesema elimu hiyo imemsaidia kubadilika kutoka kuwa mtoto anayekwenda dukani bila kuzingatia usahihi wa vipimo hadi kuwa mfuatiliaji na mtoa elimu kwa jamii.

Amesema baada ya kupata mafunzo hayo aligundua hata nyumbani kwao kuwa mita ya maji ilikuwa haijahakikiwa na akaweza kutoa elimu kwa watu waliokuwa hawajui umuhimu wa kuhakiki vipimo.

 “kabla ya kupata elimu hiyo alikuwa akienda dukani bila kuangalia chochote, lakini sasa anaelewa kuwa mlaji ana wajibu wa kuhakikisha anapata kiasi sahihi cha bidhaa anayolipia.”amesema

Kwa ujumla, Klabu za Vipimo za WMA zimeanza kuwa darasa la vitendo la kuwaandaa watoto kuwa mabalozi wa ulinzi wa mlaji, huku elimu hiyo ikitoka shuleni na kuingia moja kwa moja katika familia na jamii.

Mpango huo unaongeza uelewa wa wananchi kuhusu matumizi ya vipimo sahihi, unasaidia kujenga utamaduni wa kuhoji na kuthibitisha vipimo vinavyotumika katika biashara na, kwa muda mrefu, unaweka msingi wa kizazi kinachothamini uadilifu, usawa na uwazi katika shughuli za kiuchumi.

Fahamu Mambo Muhimu Yasiyotakiwa Kupuuzwa Katika Gari Lako

Global Publishers
September 20, 2026
5,756 views
0 Comments

Kila mmiliki wa gari anapaswa kuwa makini na alama ndogo ndogo zinazoweza kuashiria matatizo makubwa yanayoweza kusababisha ajali au gharama kubwa za matengenezo. Kupuuza tatizo dogo leo inaweza kumaanisha tatizo kubwa kesho. Hapa kuna mambo muhimu yasiyotakiwa kupuuzwa kwenye gari lako:

1️⃣ Breki – Moyo wa Usalama
Breki ni kila kitu barabarani. Kelele zisizo za kawaida, kuvuja kwa majimaji au breki zisizofanya kazi ni ishara ya hatari. Ukipuuzia, unajiwekea maisha yako na ya wengine hatarini.

2️⃣ Mataili
Mataili ni kinga ya gari lako kwenye dhoruba, mvua au barabara yenye changamoto. Angalia mataili mara kwa mara na ubadilishe pale inapohitajika. Usipuuze!

3️⃣ Maji ya Radiator (Rejeta) na Mafuta ya Engine (Oili ya gari)
Engine inahitaji Oili sahihi na maji ya radiator. Ukosefu wa mafuta au maji hupelekea engine kuchemka na kuharibiwa sehemu zingine, jambo linalogharimu pesa.

4️⃣ Taa na Viashiria – Usikose kuangalia
Taa za mbele, brake, na viashiria vya mwelekeo vitaleta usalama. Ukipuuzia tatizo lolote, hasa usiku au mvua, unajiwekea kwenye hatari kubwa ya ajali.

5️⃣ Viashiria vya Dashibodi – Onyo la Haraka
Taa ndogo za onyo kwenye dashibodi si za kupuuziwa. Kila mwanga ni ishara ya tatizo, iwe ni mafuta, betri, au breki. Chukua hatua mara moja.

6️⃣ Belt za Engine – Hatarishi Kuu
Belt zinapoharibika zinaweza kusababisha engine kushindwa kufanya kazi na kuharibu sehemu nyingi za gari. Angalia belt na ubadilishe pale inapohitajika.

7️⃣ Kichungi cha Mafuta na Mafuta
Kichungi kilichoziba au mafuta machache huathiri engine, kupunguza nguvu na kuongeza gharama ya matengenezo. Usisubiri hadi engine ishindwe kufanya kazi.

8️⃣ Mafuta ya Breki na Clutch
Breki na clutch zinahitaji lubrication sahihi. Ukosefu wa fluids huongeza hatari ya ajali na kuharibu mfumo mzima wa gari.