Halmashauri Ya Mbozi Yatangaza Nafasi 10 Za Kazi

Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imetangaza nafasi 10 za kazi kwa Watanzania wenye sifa, zikiwemo nafasi tano za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II na nafasi tano za Dereva Daraja la II.

Tangazo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, kufuatia kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Nafasi za Mwandishi Mwendesha Ofisi

Kwa nafasi tano za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II, majukumu yanajumuisha kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri, kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu husika, kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni na ratiba za kazi.

Majukumu mengine ni kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika, kupokea na kusambaza majalada kwa maofisa husika, kutunza majalada na nyaraka, kuandaa maandalizi ya vikao pamoja na orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

Mwombaji wa nafasi hiyo anatakiwa kuwa na Elimu ya Kidato cha Nne au Sita na Stashahada ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Pia anatakiwa kuwa amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa maneno 100 kwa dakika moja na kuwa na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi, ikiwemo Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.

Nafasi hiyo ina mshahara wa TGS C.

Nafasi za Dereva

Halmashauri pia imetangaza nafasi tano za Dereva Daraja la II.

Majukumu ya dereva ni pamoja na kukagua gari kabla na baada ya safari, kuwapeleka watumishi katika maeneo mbalimbali kwa safari za kikazi, kufanya matengenezo madogo ya gari, kukusanya na kusambaza nyaraka, kutunza taarifa za safari katika daftari la safari na kufanya usafi wa gari.

Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne pamoja na Leseni ya Daraja E au C, akiwa na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Pia anatakiwa kuwa na vyeti vya mafunzo vilivyompatia sifa ya kupata madaraja hayo na kuwa amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari yanayotolewa na VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Nafasi hiyo ina mshahara wa TGS B1.

Masharti kwa waombaji

Tangazo limeeleza kuwa waombaji wote wanapaswa kuwa raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanatakiwa kuainisha ulemavu walionao kwenye mfumo wa kuombea ajira.

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha CV yenye maelezo binafsi, anuani, namba za simu, barua pepe pamoja na majina ya wadhamini watatu, na kuambatanisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.

Aidha, “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of Results” pamoja na hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita hazitakubaliwa. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni Oktoba 1, 2026. Waombaji wanatakiwa kuambatanisha barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Barua hiyo ielekezwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, S.L.P. 3, Mbozi.

Maombi yote yanapaswa kutumwa kielektroniki kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira. Tangazo limeeleza kuwa maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huo hayatafanyiwa kazi.

Vitu 10 Muhimu Unavyotakiwa Kujua Kabla ya Kununua Gari la Speed

Global Publishers
September 23, 2026
5,690 views
0 Comments

Kwa watu wanaopenda gari zenye speed, sio tu kuangalia nguvu ya injini. Kuchagua gari sahihi kunahitaji kuzingatia usalama, udhibiti, na urahisi wa kutumia. Hapa kuna mwongozo wa kina ili kuhakikisha unapata gari linalokidhi matarajio yako.

1. Nguvu ya Injini (Horsepower & Torque)

Kwa gari la speed kubwa, injini za V6, V8, turbocharged au hybrid performance ni bora. Zinaongeza acceleration na kudumisha kasi ya juu kwa urahisi.

2. Aina ya Gari (Body Type)

  • Sports Car – nyepesi, aerodynamic, na zinafika speed haraka.

  • Sedan Performance – inachanganya comfort na speed.

  • SUV Performance – yenye nguvu na stable, lakini mara nyingi si haraka kama sports car.

Chagua aina inayokidhi mtindo wako na mahitaji ya kila siku.

3. Uendeshaji na Transmission

  • Manual – inatoa control zaidi kwenye acceleration, hasa kwenye gari zenye nguvu.

  • Automatic / Dual-clutch – rahisi kutumia, huboresha gear shift na hutoa smooth acceleration.

Transmission yenye ufanisi inaweza kuongeza utendaji wa gari kwenye speed kubwa.

4. Aerodynamics na Uzito

5. Brakes na Safety

6. Tires (Magurudumu)

  • Chagua performance tires zinazoweza kushughulikia acceleration na corners.

  • Angalia speed rating (W, Y, ZR) ikilingana na top speed ya gari.

7. Handling na Suspension

8. Fuel Consumption na Engine Efficiency

9. Electronics na Driving Modes

  • Gari za kisasa zina sport/track mode, traction control, stability assist, na launch control.

  • Hizi zinasaidia kudhibiti gari kwenye speed kubwa na kuongeza usalama.

10. Budget na Insurance

    • Gari za high speed si ghali tu kununua, maintenance na insurance pia ni gharama kubwa.

    • Hakikisha umezingatia gharama za matengenezo na vipuri kabla ya kufanya uamuzi.

Miili ya Askari Watano Waliofariki Katika Ajali Yaagwa Singida (Picha +Video)

Global Publishers
September 22, 2026
474 views
0 Comments

Miili ya askari watano wa Jeshi la Polisi Tanzania waliofariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea Septemba 21, 2026, eneo la Sekenke mkoani Singida, imeagwa leo, Septemba 22, 2026, katika Viwanja vya Shule ya Msingi Shelui, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Zoezi la kuaga miili hiyo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi, Serikali, Taasisi za Kidini, Maafisa wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi wa Mkoa wa Singida.

Viongozi hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego.

Katika zoezi hilo, viongozi mbalimbali wameendelea kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na Jeshi la Polisi Tanzania kufuatia msiba huo, huku wakitambua mchango wa askari hao katika kulinda usalama wa wananchi na mali zao.

Jeshi la Polisi Tanzania limeendelea kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, askari na Watanzania wote walioguswa na msiba huo, huku likiwaombea marehemu wapumzike kwa amani.

Fursa Mpya ya Ajira NEEC, Mwisho wa Maombi Oktoba 1, 2026

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza nafasi moja ya Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika. Tangazo hilo limetolewa Septemba 18, 2026, kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

NEEC limeanzishwa chini ya Sheria ya Uwezeshaji Kiuchumi Na. 16 ya mwaka 2004 na lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Majukumu yake ni pamoja na kusimamia, kuratibu, kuwezesha na kufuatilia shughuli za uwezeshaji kiuchumi nchini.

Sifa za mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uzamili katika mojawapo ya fani zifuatazo:

  • Utawala wa Umma
  • Ujasiriamali
  • Fedha
  • Uhasibu
  • Utawala wa Biashara
  • Biashara, akiwa amebobea katika Ujasiriamali, Masoko au Fedha
  • Uchumi
  • Uchumi wa Kilimo
  • Au sifa zinazolingana kutoka taasisi inayotambuliwa.

Shahada ya Uzamili inapaswa kuhusiana na Shahada ya Kwanza ya mwombaji.

Mwombaji anatakiwa pia kuwa na uzoefu wa kazi wa angalau miaka 12 katika maeneo yanayohusiana, ambapo angalau miaka mitatu iwe katika nafasi ya kiutawala. Uelewa wa masuala ya uwezeshaji kiuchumi umetajwa kuwa ni sifa ya ziada.

Majukumu ya Mtendaji Mkuu

Mtendaji Mkuu atawajibika kusimamia shughuli za kiutawala za Baraza na kuwa msemaji wake. Pia atasimamia utekelezaji wa majukumu ya Baraza, maandalizi ya mipango ya kimkakati na bajeti, taarifa za fedha na maendeleo, pamoja na utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Baraza.

Majukumu mengine ni kusimamia utekelezaji na tathmini ya mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu, kuendesha shughuli za kila siku za Sekretarieti, kuandaa mikakati ya kuongeza ufanisi, kusimamia uundaji na utekelezaji wa sera pamoja na kuongoza juhudi za kutafuta rasilimali za kifedha kwa ajili ya miradi ya Baraza.

Nafasi hiyo ni ya ajira ya kudumu na yenye mafao ya kustaafu, huku mshahara ukiwa kwa mujibu wa kiwango kilichoidhinishwa cha NEECS 13.

Waombaji wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania na kwa ujumla wasizidi umri wa miaka 45, isipokuwa watumishi wa umma. Pia wanapaswa kuambatanisha CV, nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu na taaluma, cheti cha kuzaliwa pamoja na picha ya pasipoti.

Mwisho wa kutuma maombi ni Oktoba 1, 2026. Maombi yanapaswa kutumwa kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Makamu wa Rais Ndejembi Alivyowasili New York Kumwakilisha Rais Samia UNGA81

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasili jijini New York, nchini Marekani, kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81).

Makamu wa Rais amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F. Kennedy, ambako amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Elsie Kanza, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa – New York, Togolani Mavura, pamoja na maafisa mbalimbali.

Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unawakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali pamoja na viongozi mbalimbali kutoka mataifa wanachama, ambapo pamoja na mambo mengine, hujadili masuala ya kiuchumi, kisiasa, mazingira na haki za binadamu.

Mkutano huo unafanyika chini ya kaulimbiu “Kurudisha Imani, Kusimamia Mabadiliko: Umoja wa Mataifa unaohudumia Wote” (Restoring Trust, Managing Transformation: A United Nations That Delivers for All).

Kaulimbiu hiyo inalenga kuhamasisha juhudi za kujenga upya uaminifu na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, sambamba na kusimamia mabadiliko makubwa yanayoendelea duniani, ikiwemo kasi ya maendeleo ya akili unde (AI).

Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, pamoja na kushiriki katika vikao mbalimbali, ikiwemo Mjadala Mkuu (General Debate), mikutano ya pembezoni na mikutano ya pande mbili (Bilateral Meetings).

Fahamu Kwa Nini Wataalamu wa Lishe Wanashauri Kula Korosho Mara kwa Mara

KOROSHO ni muhimu sana katika mwili wa binadamu. Kwa Tanzania zao hili hulimwa kwa wingi katika mikoa ya pwani hasa Mtwara, Lindi na Pwani.  Wengi wetu hatuli korosho na hata pale tunapokula, hula kama kitafunwa cha kuchangamsha mdomo tu, na wala siyo kitu muhimu sana kuliwa. Korosho ina faida nyingi sana kiafya, hasa katika magonjwa yenye uhusiano na magonjwa ya moyo, kama ambavyo tutaweza kuona katika makala ya leo.

Siyo tu kwamba korosho zina kiwango kidogo cha mafuta lakini pia zina aina ya mafuta ambayo hutoa kinga kwenye moyo. Aidha, ndani ya korosho, kuna kirutubisho aina ya Oleic Acid ambacho huimarisha afya njema ya moyo na huwafaa hata wagonjwa wa kisukari.

Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa kwenye jarida la masuala ya virutubisho nchini Uingereza liitwalo British Journal of Nutrition, umeonesha kuwa watu waliopendelea kula korosho na bidhaa zake, kama butter, idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa wa moyo vilipungua kati ya asilimia 11 na 19.

Watu wanaotumia korosho angalau mara nne kwa wiki, walionesha kuondokewa na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo kwa asilimia 37. Inashauriwa kutafuta korosho kiganja kimoja au kijiko kimoja cha chakula kilicho jaa ‘nut butter’, kula hivyo mara nne kwa wiki.

Korosho pia ni chanzo kizuri cha madini aina ya copper ambayo ni muhimu sana katika mwili wa binadamu, korosho pia ina madini yanayoimarisha mifupa na kinga ya mwili. Watu wanaopenda kula korosho, angalau mara mbili kwa wiki, hakuna uwezekano wa kuongezeka uzito na badala yake wanaweza kupungua.

Hivyo inashauriwa kupenda kula korosho au butter kwa afya yako na wala hakuna haja ya kuhofia kuongezeka uzito. Kisayansi inashauriwa kutumia korosho kiasi, kwani ina virutubisho muhimu na adimu, ambapo tafiti zilizofanyika zimebainisha kuwa mtu anayetumia korosho hufaidika kwa kuongeza vitu vifuatavyo mwilini.

Ina miliki calories 155, ni vyakula vinavyohitajika mwilini ili kutengeneza nguvu na kuupa mwili virutubisho vyote vinavyotakiwa katika kujenga mwili, ina miliki gram 9.2 za kabohaidreti, gram 5.2 za Protini na Vitamini E, B6 pamoja na gram 9.5 za vitamini K, gram 10 za madini ya Calcium, mbali na madini hayo ina umiliki mkubwa wa madini ya Zinki, Magneziam, Potasiam, kopa, na Asidi ya Folik.

Hivyo katika mwili wa binadamu korosho husaidia mambo yafuatayo: Inasaidia kunyonya mafuta katika mwili wa binadamu hivyo huulinda mwili dhidi ya magonjwa ya moyo kama tulivyoona hapo juu na kuusaidia moyo kuwa wenye afya njema. Kula korosho mara kwa mara husaidia mwili kuwa na madini ya chuma ambapo ugonjwa wa Anemia hutokana na upungufu wa madini ya chuma hivyo ulaji wa Korosho hukinga mwili na magonjwa ya damu ikiwemo Anemia.

Korosho husaidia uwezo wa macho kuona kama ilivyo kwa karoti. Korosho inamiliki kirutubisho kisayansi kijulikanacho kwa jina la Zea Xanthin ambacho huilinda retina ya jicho dhidi ya miale na uchafu ambao unaweza kudhuru jicho. Korosho ni nzuri kwa kutunza ngozi, kutokana na virutubisho na madini kwa kung’arisha ngozi, kama Zinki, Magnesium, Fosforas na chuma lakini pia uwepo wa madini ya selenium ambayo hulinda ngozi dhidi ya magonjwa ya kansa.

 

TFS YATUMIA MEL 2026 KUONYESHA FURSA ZA UHIFADHI, NYUKI NA UTALII

ARUSHA. Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umetumia Kongamano la Tano la Kitaifa la Wiki ya Ufuatiliaji, Tathmini na Ujifunzaji (MEL) 2026 kuonyesha namna uhifadhi wa misitu na nyuki unavyoweza kuleta fursa za afya, biashara, utalii na ustawi wa jamii, huku huduma ya apitherapy ikiwa miongoni mwa vivutio vinavyowavutia washiriki katika Banda la TFS, Ngurudoto, Arusha.

Mhifadhi wa TFS, Subira Matimbwa, amesema apitherapy ni miongoni mwa huduma zinazohusisha matumizi ya nyuki na bidhaa zitokanazo na nyuki, ambapo katika banda hilo washiriki wanapewa elimu kuhusu huduma hiyo pamoja na matumizi mbalimbali ya bidhaa za nyuki. Huduma hiyo imekuwa kivutio kwa washiriki wanaotaka kufahamu zaidi uhusiano kati ya nyuki, bidhaa zao na matumizi yake katika maisha ya binadamu.

Katika banda hilo, TFS pia inaendelea kutoa elimu kuhusu uhifadhi wa misitu, ufugaji nyuki na utalii ikolojia, sambamba na kuonesha na kuuza bidhaa mbalimbali zitokanazo na nyuki, zikiwamo asali za aina tofauti, honey nuts na bidhaa nyingine zinazotokana na shughuli za ufugaji nyuki.

Afisa Utalii wa TFS, Salome Kivuye, amesema ushiriki wa TFS katika kongamano hilo unalenga pia kuwafahamisha washiriki kuhusu maeneo ya utalii yanayoweza kutembelewa wakati wakiwa Arusha, akitaja Ziwa Duluti pamoja na Maporomoko ya Napuru yaliyopo katika Msitu wa Kupandwa Meru kuwa miongoni mwa maeneo hayo.

Kivuye amesema maeneo hayo yanatoa fursa kwa washiriki kuchanganya shughuli za kongamano na utalii, huku akiwahamasisha kutumia huduma za kidijitali za TFS, ikiwamo e-Misitu, ili kupata taarifa na kurahisisha upatikanaji wa huduma za utalii katika maeneo yanayosimamiwa na TFS.

Kongamano hilo la siku tano linafanyika Arusha kuanzia Septemba 22 hadi 26, 2026, likiwakutanisha zaidi ya washiriki 1,500 kutoka Serikali, taasisi na wadau mbalimbali kujadili matumizi ya ushahidi wa kitafiti na takwimu katika kupima matokeo na kuboresha utekelezaji wa mipango ya maendeleo. Kaulimbiu ya kongamano hilo ni “Kutoka katika Ushahidi hadi Vitendo, Kuimarisha Tathmini kwa Maendeleo Endelevu.”

Akihusisha ushiriki huo na maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani, Kivuye pia amewaalika washiriki kuelekea Kondoa Rock Art Site kushiriki katika tukio litakalojumuisha shughuli mbalimbali za utalii na burudani, zikiwamo Outdoor Movie Night, Night Games, Guide and Tour, Bonfire, Painting, Paintball Game, Bata Pori Fun Run, Live Music Performance, Bata Pori Bike Ride Challenge, Karaoke Night pamoja na ziara za kuongozwa katika eneo hilo la urithi wa dunia.

TFS YAIMARISHA UPATIKANAJI WA MBEGU BORA ZA MITI

Mwandishi Wetu – Iringa

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wahifadhi wa misitu katika ukusanyaji wa mbegu bora za miti, hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa mbegu zenye ubora kwa ajili ya uzalishaji wa miche na upandaji miti nchini.

Mafunzo hayo yameanza leo Septemba 22, 2026 katika Shamba la Miti Sao Hill, mkoani Iringa, yakifunguliwa na Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayesimamia Kurugenzi ya Huduma Saidizi na Utawala TFS, DCC Emmanuel Wilfred Kiboko, aliyesisitiza umuhimu wa kutumia utaalamu na mbinu za kisayansi katika ukusanyaji wa mbegu.

DCC Kiboko amesema upatikanaji wa mbegu bora ni msingi wa kuzalisha miche yenye ubora na hatimaye kuimarisha misitu yenye afya na tija, huku akieleza kuwa TFS itaendelea kuwekeza katika mafunzo ya watumishi ili kuendana na teknolojia za kisasa na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.

“Ujuzi huu mnaoendelea kuupata tuutumie tunapoenda kutekeleza majukumu, kwani malengo ya taasisi ni kuhakikisha tunakuwa na misitu endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho,” amesema DCC Kiboko.

Amewataka wahifadhi hao kuzingatia miongozo, taratibu na kanuni za utumishi wa umma, kutumia ujuzi wanaoupata katika maeneo yao ya kazi na kutunza vifaa watakavyokabidhiwa ili viweze kutumika kwa muda mrefu.

Akitoa taarifa kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi na Meneja wa Sehemu ya Baiolojia ya Mbegu za Miti, SACC Fandey H. Mashimba, amesema kada ya wavunaji mbegu imekuwa ikikabiliwa na upungufu wa watumishi kutokana na kustaafu, hali iliyosababisha TFS kubaki na watumishi watano ambao nao wanakaribia kustaafu.

Mashimba amesema kupitia mradi wa “Enhanced Conservation of 57 Highly Threatened Tanzanian Tree Species”, unaofadhiliwa na Franklinia Foundation, kuratibiwa na Missouri Botanical Garden ya Marekani na kutekelezwa na TFS, seti 10 za vifaa maalumu vya kukwea na kuvunia mbegu zimenunuliwa pamoja na kugharamia mafunzo kwa watumishi wapya 10.

“Mafunzo haya yataimarisha utambuzi, uchaguzi na ukusanyaji wa mbegu kutoka kwenye miti bora kwa kufuata kanuni za kitaalamu, kuongeza wataalamu nchini na kusaidia kukidhi mahitaji ya mbegu bora za miti,” amesema Mashimba.

TANZANIA YASISITIZA MSIMAMO WA UONGEZAJI THAMANI MADINI MKAKATI NDANI YA NCHI

▪️Yazitaka Nchi za Afrika kutolegeza masharti kwa kisingizio cha kuvutia uwekezaji

▪️Uongezaji thamani madini nguzo kuu ya uendelezaji madini mkakati

▪️Tanzania kuanza utekelezaji wa Programu ya Utafiti wa kina wa Madini hivi karibuni

▪️Kituo cha Utafiti cha Jiosayansi-Kunduchi chapigiwa chapuo kwa nchi za Afrika

Newyork, Marekani

Ikishiriki Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu ya Viongozi pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa United Nations General Assembly (UNGA 81), Tanzania yaweka msisitizo juu ya msimamo wake wa kuhakikisha uongezaji thamani wa madini mkakati unafanyika ndani ya nchi yanamochimbwa kabla ya kusafirishwa kwenda nje.

Hayo yamesemwa leo tarehe 21 Septemba, 2026 na Waziri wa Madini, *Mheshimiwa Anthony P. Mavunde (Mb)* alipomwakilisha *Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan* kwenye Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Viongozi kuhusu maendeleo ya madini mkakati Barani Afrika.

“Baadhi ya Nchi za Afrika zinadhani msimamo huu wa kutaka madini mkakati kuongezwa thamani ndani ya nchi kabla ya kusafirishwa nje unachelewesha uwekezaji”

“Niwaombe wenzangu katika Bara la Afrika tusilegeze masharti yetu kwa kisingizio cha kuvutia uwekezaji, kwani uongezaji thamani madini ndani ya Nchi ni nguzo muhimu ya kuendeleza Nchi zetu hususan katika kufikia manufaa tarajiwa kwenye uvunaji wa madini mkakati” alisisitiza Waziri Mavunde.

Aidha, Waziri Mavunde alibainisha kuwa Nchi za Afrika zinapoweka msimamo wa kuongeza thamani madini mkakati ndani ya Nchi zinajiweka katika ramani ya dunia katika uzalishaji wa madini hayo ni kuongeza manufaa kwa wananchi wake kwa kuongeza ajira na mchango wa sekta kwenye uchumi.

Pia, Mhe. Mavunde alieleza kuwa kutokana na umuhimu huo, Tanzania ipo mbioni kuanza utekelezaji wa programu ya utafiti wa kina wa madini yenye lengo la kuongeza eneo lililofanyiwa utafiti wa kina kutoka asilimia 16 hadi kufikia asilimi 50 ifikapo mwaka 2030. 

“Hatua hii ina lengo la kuhakikisha kama Nchi tunapata uwekezaji stahiki kwenye uvunaji wa rasilimali zetu na kuchochea uanzishwaji wa viwanda vya uongezaji thamani ndani ya nchi” aliongeza Mhe. Mavunde.

Katika hatua nyingine, Waziri Mavunde alikitaja Kituo cha Utafiti wa Jiosayansi (African Minerals and Geosciences Centre – AMGC) kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam kuwa ni nyenzo muhimu ambayo Nchi za Afrika zinayo nafasi ya kukitumia ili kuimarisha tafiti na uongezaji thamani wa madini mbalimbali, kwani Kituo hicho ni Mali ya Nchi zote za Afrika.

Mkutano huo uliandaliwa na African Strategic Mineral Group (ASMG), ambapo kwa sasa Serikali ya Shirikisho ya Jamhuri ya Nigeria ndiye Mwenyekiti.

NCHI 22 ZA AFRIKA ZAKUTANA TANZANIA KUBADILISHANA UZOEFU WA MTAALA UNAOZINGATIA UMAHIRI – PROF. SHEMDOE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema nchi 22 za Afrika zimekutana nchini katika Mkutano wa Sita wa Jumuiya ya Taasisi za Mitaala Afrika kwa ajili ya kubadilishana uzoefu kuhusu namna mabadiliko ya mitaala inayozingatia umahiri yanavyotekelezwa katika mataifa yao.

Prof. Shemdoe amesema hayo leo, Septemba 22, 2026, jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, mara baada ya kufungua Mkutano wa Sita wa Jumuiya ya Taasisi za Mitaala Afrika kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ambapo Tanzania ni nchi mwenyeji kwa mwaka huu.

“Mataifa haya ya Afrika yatabadilishana uzoefu wa mitaala inayozingatia stadi na umahiri, hivyo mwanafunzi akihitimu anakuwa amepata ujuzi ambao utamwezesha kuutumia katika fani mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuendesha maisha yake,” amesema Prof. Shemdoe.

Prof. Shemdoe amesema katika mkutano huo pia yanashiriki mataifa kutoka nje ya bara la Afrika kwa ajili ya kujionea namna mataifa ya Afrika yanavyotekeleza mitaala inayozingatia umahiri, ikiwemo Tanzania ambayo imeachana na Mtaala wa mwaka 2014 na sasa inatekeleza Mtaala mpya wa mwaka 2023 unaolenga kumpa mwanafunzi wa shule ya msingi na sekondari ujuzi unaohitajika katika maisha na shughuli mbalimbali.

“Sote ni mashahidi kwamba Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa shule 103 za amali ambazo zimejengwa nchi nzima, na shule hizi ndizo zitakazowezesha utekelezaji wa mtaala huu wa mwaka 2023 unaozingatia umahiri. Hivyo, washiriki wa mkutano huu watapata fursa ya kujionea hatua tuliyoipiga katika utekelezaji wa mtaala huo,” Prof. Shemdoe amesisitiza.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Taaluma, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Bi. Mwanahamis Adam Ameir, amesema mkutano huo ni muhimu sana katika kipindi hiki ambacho mageuzi mbalimbali yanahitajika katika mifumo ya elimu, hivyo Tanzania itapata fursa ya kubadilishana uzoefu na kupata uelewa wa mambo muhimu ya kuzingatia katika utekelezaji wa Mtaala mpya unaozingatia umahiri.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dkt. Aneth Komba, amesema mkutano huo wa siku nne unatarajiwa kuzaa Azimio la Dar es Salaam kuhusu Mitaala ya Afrika, Mwongozo wa Uandaaji wa Mitaala Barani Afrika, pamoja na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha utekelezaji na uandaaji wa mitaala barani Afrika. Ameongeza kuwa, siku ya mwisho, wageni watapelekwa katika shule mbalimbali ili kujionea namna Serikali ya Awamu ya Sita inavyotekeleza Mtaala mpya wa Elimu wa mwaka 2023.

Kupitia mkutano huo, Tanzania inatarajia kupata maarifa, uzoefu na ubunifu wa kimitaala utakaosaidia kuimarisha mfumo wa elimu unaozalisha wananchi wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na maadili, pamoja na uwezo wa kukabiliana na mahitaji ya uchumi wa kisasa. Kwa msingi huo, mkutano huo una umuhimu katika kufanikisha matarajio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kuimarisha elimu inayojenga rasilimali watu yenye ujuzi, umahiri na uwezo wa kutumia maarifa na ubunifu katika kuchochea maendeleo ya Taifa.