VURUGU KILOSA: MTU MMOJA AFARIKI, ASKARI 3 WAJERUHIWA.

 

Na Matukio Daima Media, Kilosa

VURUGU zinazohusishwa na mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, zimesababisha vifo vya watu wawili katika matukio tofauti, kujeruhiwa kwa askari watatu na kuharibiwa kwa mali za Jeshi la Polisi.

Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro inaeleza kuwa tukio linaanzia Septemba 23, 2026, saa 7 mchana katika Mashamba ya Bondeni, Kitongoji cha Legeza Mwendo, Kijiji na Kata ya Tindiga, Tarafa ya Masanze, ambako Festo Selias Chaula maarufu kwa jina la Walter Mkulima alijeruhiwa vibaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Andrew  Kantimbo akasema kuwa Festo alikatwa kichwani kwa kitu chenye makali na kupigwa kwa vitu butu sehemu mbalimbali za mwili wake na kupata majeraha makubwa yanayosababisha kifo chake katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Baada ya tukio hilo, Polisi lilifanya ufuatiliaji na kuwakamata Seletwi Samiji Mdamanya na Paulo Lukas Sumai, likiwatuhumu kuhusika na mauaji hayo. 

Wawili hao wanaelezwa kuwa ni wafugaji na wakazi wa Kijiji cha Malangali, Kata ya Tindiga.

Hata hivyo, wakati askari wakiwa wanawapeleka watuhumiwa Kituo cha Polisi Kilosa, kundi la watu linalodaiwa kuwa wakulima na kukadiriwa kufikia 200 lilidaiwa kufunga barabara na kuanza kuwashambulia askari waliokuwa wamewabeba watuhumiwa hao.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kantimbo, kundi hilo lilikuwa na silaha mbalimbali za jadi  likilenga kuwadhuru watuhumiwa hao jamii ya wafugaji.

Askari Polisi ikadaiwa walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi hao waliokuwa na visu, mapanga, mishale, mikuki, marungu na mawe.

Baada ya kundi hilo kutawanyika, Polisi walifanya ukaguzi na kumkuta mmoja wa wananchi, Kelvin Mhagama, mkulima na mkazi wa Kichangani, akiwa amejeruhiwa kwa kitu chenye makali sehemu mbalimbali za mwili wake.

Majeruhi huyo alipelekwa hospitali ya wilaya ya Kilosa, lakini alifariki Dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Kamanda huyo wa Polisi amethibitisha licha ya kifo hicho, katika vurugu hizo, askari watatu walipata  madhara ikiwemo kujeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili baada ya kushambuliwa kwa silaha za jadi na wanaendelea na matibabu.

Vurugu hizo pia zimesababisha pikipiki ya Polisi yenye namba PT 3131 aina ya SANLG kuteketea kwa moto, huku gari la Polisi PT 5877 Toyota Hilux likiharibiwa baada ya kupigwa kwa mawe.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewataka wakulima, wafugaji na wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na kutumia njia rasmi za kisheria katika kushughulikia migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Polisi pia wanaendelea na msako wa kuwakamata wote waliohusika na vurugu hizo na kujichukulia sheria mkononi katika tukio hilo.

NG’OMBE WAINGIA MIWA MTIBWA, WALINZI WAWILI WASHAMBULIWA

 

Na Matukio Daima, Mvomero.

Kundi la ng’ombe linalodaiwa kuingizwa katika mashamba ya miwa ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa, Mvomero, limeibua vurugu baada ya walinzi wawili wa kiwanda hicho kushambuliwa na kujeruhiwa wakati wakijaribu kuwaondoa mifugo hiyo katika mashamba.

Tukio hilo limetokea Septemba 23, 2026 majira ya saa sita mchana katika eneo la D6, ndani ya mashamba ya miwa ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa, Kata ya Mtibwa, Tarafa ya Turiani, Wilaya ya Mvomero.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Andrew Kantimbo, amesema walinzi hao walifanikiwa kulikata kundi la ng’ombe na kuanza kuwaswaga kuelekea Kambi ya Dumila One inayomilikiwa na kiwanda hicho kwa ajili ya utambuzi na hatua zaidi.

Hata hivyo, amesema zoezi hilo lilikumbana na upinzani kutoka kwa wafugaji waliodaiwa kuzuia walinzi na kuanza kuwashambulia kwa visu aina ya sime, marungu na fimbo.

Mashambulizi hayo yalisababisha walinzi Sayuni Ndika Nemes (25) na Sanula Masaga Msabila (36) kujeruhiwa. Wote ni walinzi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa.

Katika tukio hilo.

Jeshi la Polisi limewakamata Sisone Lugaso Ndabali (20), Taturo Tetetea Shangalima (28) na Likua Kaika Ndikila (21), wote wakazi wa Kijiji cha Kambala, Kata ya Mkindo, Mvomero.

Polisi Mkoa wa Morogoro limewataka wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima na kuacha kujichukulia sheria mkononi, likisisitiza matumizi ya taratibu na sheria katika kudai haki

Mwisho

Watanzania wanaorejea Afrika Kusini kutibiwa bure – HabariLeo

DAR ES SALAAM: HOSPITALI ya Rufaa ya Amana imeanzisha programu maalumu ya kuwasaidia Watanzania wanaorejea nchini kutoka Afrika Kusini kwa kutoa huduma za matibabu ya meno pamoja na ushauri nasaha na msaada wa kisaikolojia.

Daktari Kiongozi wa Hospitali ya Amana, Dk Mafele Ihoyelo, amesema mpango huo umeanzishwa baada ya kubaini baadhi ya Watanzania wanaorejea kutoka Afrika Kusini wakiwa na changamoto za meno, huku wengine wakihitaji msaada wa kisaikolojia ili waweze kuanza maisha mapya nchini.

Amesema huduma hizo zinalenga kurejesha afya ya kinywa kwa wanaokabiliwa na changamoto za meno, huku huduma za kisaikolojia zikilenga kuwasaidia wanaohitaji kurejesha matumaini na kuimarisha afya yao ya akili.

“Programu hiyo itatekelezwa kwa njia ya mtandao na inalenga kuwasaidia watu 100 katika awamu ya kwanza,” amesema.

Hospitali hiyo pia imezihimiza taasisi na wadau mbalimbali kujiunga na programu hiyo na kushirikiana katika kuwafikia watu wengi zaidi.

Kwa upande mwingine, Mohamed Msangi, Mtanzania anayeishi Pretoria/Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema Watanzania wanaorejea nchini wanahitaji kupokelewa vizuri na kusaidiwa kuanza maisha mapya badala ya kukumbana na masimango.

Msangi amesema bado kuna idadi kubwa ya Watanzania waliopo Afrika Kusini wanaohitaji kurejea nchini, lakini baadhi yao wamekuwa na hofu kuhusu namna watakavyopokelewa na kuanza maisha baada ya kukaa huko kwa muda mrefu.

Amesema baadhi ya Watanzania wameishi Afrika Kusini kwa zaidi ya miaka 15 hadi 32, huku wengine wakiwa wamejikita katika biashara na shughuli mbalimbali za kiuchumi, hivyo wanahitaji mazingira yatakayowawezesha kutumia ujuzi na uzoefu wao wanaporejea nchini.

Amesema hadi sasa Watanzania 543 wamekwisharejea nchini kupitia mpango huo, huku wengine 1,500 wakitarajiwa kurejea katika awamu zinazofuata. Wanaorejea wanajumuisha akina mama, watoto, vijana na wazee.

Kwa mujibu wa Msangi, changamoto za meno na afya ya kisaikolojia ni miongoni mwa mahitaji yaliyoonekana kwa baadhi ya wanaorejea, hivyo ushiriki wa Hospitali ya Amana na wadau wengine unaweza kusaidia kuwawezesha kuanza upya maisha yao nchini.

Kaya zaidi ya 40 zaagizwa kuhama Same – HabariLeo

KILIMANJARO: ZAIDI ya kaya 40 katika Kijiji cha Marieni, Kata ya Chome, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, zimeagizwa kuhama makazi yao kutokana na kusogea kwa ardhi na kutokea kwa nyufa kubwa ambazo tayari zimesababisha uharibifu wa nyumba takribani 10 pamoja na kanisa moja.

Serikali imesema hatua hiyo ni ya haraka kutokana na hatari ya kutokea kwa maporomoko ya ardhi na kuporomoka kwa miamba katika eneo hilo lenye milima na miteremko.

Agizo hilo limetolewa baada ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), chini ya Wizara ya Madini, kufanya utafiti na kubaini mabadiliko ya kijiolojia yanayoendelea chini ya ardhi.

Mabadiliko hayo yameongeza hatari kwa usalama wa wananchi wanaoishi katika eneo hilo, hivyo hatua ya kuwahamisha inalenga kuwalinda dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza.

Utafiti huo wa GST umefanyika baada ya kuonekana kwa nyufa kubwa katika eneo hilo, hali ambayo tayari imeanza kusababisha uharibifu wa baadhi ya miundombinu na makazi ya wananchi.

Serikali inatarajiwa kuendelea kufuatilia hali ya eneo hilo na kuchukua hatua stahiki kulingana na matokeo ya utafiti wa kitaalamu, huku wananchi wakitakiwa kuzingatia agizo la kuhama kwa ajili ya usalama wao.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Watangaza Nafasi Nne za Kazi

Kampuni ya Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited imetangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu katika sekta ya bima, mauzo, masoko, biashara, uhasibu na nyanja zinazohusiana.

Nafasi zilizotangazwa ni Business Development Executive, Accountant pamoja na Insurance Sales Executives, huku waombaji wakitakiwa kutimiza vigezo vilivyowekwa kwa kila nafasi.

1. Business Development Executive

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Insurance and Risk Management, Sales and Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima, maendeleo ya biashara, mauzo au masoko.

2. Accountant

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Accounting au Finance, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima. Sifa ya CPA ni nyongeza.

3. Insurance Sales Executives

Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti katika Insurance and Risk Management, Sales, Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana.

Uzoefu katika sekta ya bima na kazi za mauzo ni nyongeza.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na viambatisho muhimu vilivyothibitishwa kupitia barua pepe au kwa anuani ya ofisi ya kampuni kabla ya Septemba 30, 2026.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited
P.O. Box 7534, Sinza Mori
Global Group House/Building, Opposite Wanyama Hotel
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: [email protected]

ACT Wazalendo Yafanya Mabadiliko Baraza Kivuli la Mawaziri

Global Publishers
September 24, 2026
0 views
0 Comments

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Manka Semu.

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Manka Semu, ametangaza mabadiliko katika Baraza Kivuli la Mawaziri la chama hicho, kufuatia mashauriano na Waziri Mkuu Kivuli, Isihaka Mchinjita.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Septemba 24, 2026, mabadiliko hayo yamehusisha uteuzi wa viongozi watatu katika nafasi mbalimbali za Baraza Kivuli.

Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

  1. Emmanuel Lazarus Mvula ameteuliwa kuwa Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mvula ni Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania na amewahi kuhudumu kama Waziri Kivuli wa Fedha, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2022 hadi 2025.
  2. Hussein H. Kalyango ameteuliwa kuwa Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Naibu Waziri Kivuli wa Ulinzi, Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia, huku pia akiwa amewahi kuhudumu kama Naibu Waziri Kivuli wa Utumishi na Utawala Bora mwaka 2025–2026.
  3. Dickson Modestus Kilufi ameteuliwa kuwa Waziri Kivuli wa Kilimo, Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo umeanza rasmi Septemba 24, 2026. Mabadiliko ya Baraza Kivuli ni sehemu ya mfumo wa vyama vya upinzani wa kuainisha wasemaji na viongozi wanaofuatilia sekta mbalimbali za Serikali. ACT Wazalendo pia imekuwa ikitumia mfumo huo katika shughuli zake za kisiasa.

Kichwa mbadala:
ACT Wazalendo Yateua Mawaziri Kivuli Watatu, Mvula, Kalyango na Kilufi Wapewa Nafasi

Lissu Ahoji Kisheria Maneno Yanayodaiwa Kuunda Kosa la Uhaini

DAR ES SALAAM, Septemba 24, 2026 — Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ameendelea kutoa majumuisho yake ya mwisho katika kesi ya uhaini inayomkabili, akisisitiza kuwa Mahakama inapaswa kutathmini kama maneno anayodaiwa kuyasema yanaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda kosa la jinai linalomkabili.

Lissu ametoa hoja hizo mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama Kuu, akiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, katika hatua ya mwisho ya kesi hiyo. Anashtakiwa kwa kosa la uhaini chini ya kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, kuhusiana na madai ya kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Katika majumuisho yake, Lissu amesema hoja yake siyo tu kuhusu iwapo alitamka maneno yanayodaiwa na upande wa mashtaka, bali kama maneno hayo, yakitazamwa pamoja na mazingira yaliyotolewa, yanatimiza vipengele vinavyotakiwa kisheria kuthibitisha kosa la uhaini.

Amesema maneno yanayodaiwa kutamkwa katika mkutano wa Aprili 3, 2025, yakiwemo madai ya “tutazuia uchaguzi”, “tutahamasisha uasi” na “tutakinukisha vibaya”, hayajafafanuliwa na upande wa mashtaka kuhusu namna yanavyounda kosa la jinai.

Kwa mujibu wa Lissu, si wajibu wa mshtakiwa kufafanua kwa niaba ya upande wa mashtaka maana ya maneno hayo au kueleza kwa nini hayakuwa kosa. Amesema jukumu hilo liko kwa upande wa mashtaka kuonyesha kwa ushahidi kwamba maneno hayo yanatimiza masharti ya kosa analoshtakiwa.

Lissu pia amejikita katika hoja ya madai kwamba maneno yake yalilenga kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amehoji ni chombo gani au kiongozi gani wa Serikali anayedaiwa kutishiwa, akitaja kwa mfano Rais, Makamu wa Rais, Serikali yenyewe au taasisi nyingine.

Hoja hiyo inaendana na hoja aliyoiwasilisha katika siku ya kwanza ya majumuisho, ambapo alisema hati ya mashtaka haijaeleza kwa usahihi ni sehemu gani ya Serikali iliyodaiwa kutishiwa.

Lissu pia amesema katika maneno yanayodaiwa kutamkwa hakuna mahali ambapo ametaja Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais, Makamu wa Rais au kiongozi mwingine wa Serikali.

Kwa upande wake, upande wa mashtaka unasema mazingira na maudhui ya kauli hizo yanaonyesha dhamira ya kutishia Serikali na kuzuia uchaguzi.

Katika kuchambua ushahidi, Lissu amesema ushahidi wa baadhi ya mashahidi wa Jamhuri unatofautiana kuhusu maana ya maneno aliyodaiwa kuyasema.

Ametaja PW1, PW2 na PW16 kama mashahidi waliotoa tafsiri kwamba kauli hizo zilihusisha tishio kwa Serikali, huku akisema PW17, ambaye alikuwa katika mkutano huo, hakutoa tafsiri hiyo.

Kwa mujibu wa Lissu, PW17 alikuwepo kwenye mkutano wa Aprili 3, 2025 na alisikiliza yaliyokuwa yakijadiliwa, ikiwemo sera ya CHADEMA ya “No Reform, No Election.”

Lissu amesema ushahidi wa PW17 unaunga mkono hoja ya utetezi kwamba mkutano huo ulihusisha mjadala kuhusu sera ya chama na changamoto za mfumo wa uchaguzi.

“Kesi imejengwa kwenye hisia”
Lissu amesema anachopinga ni tafsiri ya upande wa mashtaka kwamba kauli hizo zilikuwa na nia ya kuitishia Serikali.

Amedai kuwa msingi huo unatokana na hisia au tafsiri ya mashahidi badala ya ushahidi unaoonyesha moja kwa moja nia hiyo.

Amesema ushahidi wa upande wa utetezi unaonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kueleza msimamo wa CHADEMA kuhusu mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi na sera ya “No Reform, No Election”, na kwamba hakulenga kuitishia Serikali wala kuhamasisha vurugu.

Katika hatua hiyo, Lissu pia amesisitiza kuwa Mahakama inapaswa kuzingatia ushahidi uliotolewa na pande zote kabla ya kufikia hitimisho kuhusu nia yake.

Arejea kesi ya Freeman Mbowe
Lissu amerejea pia uamuzi wa Mahakama katika kesi iliyomhusu aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akisema uamuzi huo una umuhimu katika hoja yake kuhusu ulazima wa hati ya mashtaka kueleza kwa uwazi tuhuma zinazomkabili mshtakiwa.

Amesema sheria inapaswa kumpa mtu anayeshtakiwa taarifa ya kutosha kuhusu kosa analodaiwa kutenda ili aweze kuandaa utetezi wake.

The Chanzo imeripoti kuwa Lissu alitumia pia uamuzi wa Isdory Patrice kuunga mkono hoja kwamba mshtakiwa anapaswa kupewa maelezo ya kutosha ya tuhuma ili aweze kujitetea ipasavyo.

Kesi iko hatua ya mwisho
Upande wa Jamhuri ulifunga ushahidi wake Agosti 17, 2026 baada ya kuwaita mashahidi 17 kati ya 30 waliokuwa wameorodheshwa. Mahakama baadaye iliamua kuwa Lissu ana kesi ya kujibu, na upande wa utetezi ukafunga ushahidi wake Septemba 18.

Kwa sasa, pande zote zinaendelea na majumuisho ya mwisho kabla ya jopo la majaji kufanya tathmini ya hoja na ushahidi uliowasilishwa.

Lissu amesema uamuzi wa kesi hiyo hautamhusu yeye pekee, bali unaweza pia kuweka msingi wa kisheria utakaozingatiwa katika kesi zijazo.

Stori na mwandishi Wetu

Haaland Kuongoza Mashambulizi ya Norway dhidi ya Denmark

Je unajua kuwa siku ya leo unaweza ukaondoka na kitita cha mkwanja wa maana ukibashiri mechi zako sasa. Mechi nyingi kupigwa kwenye viwanja mbalimbali huku wewe kwa dau dogo tuu unaibuka bingwa.

Norway atamleta kwake Denmark kwenye michuano hii ya UEFA Nations League ambapo wenyeji wanaingia kwenye mchezo huu wakihitaji kufanya mashambulizi zaidi kwenda kwa mpinzani kwani wana mshambuliaji hatari Duniani Erling Haaland na ni salaha kubwa sana kwenye kikosi hicho.

Ukiachilia kuwa na mshambuiliaji huyo, pia wana wachezaji wenye uwezo wa kuleta kasi pembeni na kusaidia kutengeneza nafasi, huku Martin Ødegaard akiwa muhimu katika kuunganisha kiungo na safu ya ushambuliaji.

Kinachoweza kuwa muhimu ni namna Norway itakavyomtafuta Haaland. Ikiwa Denmark itafanikiwa kumtenga na mipira, Norway inaweza kulazimika kutumia zaidi mashambulizi ya pembeni.

Huku Denmark wao wanaingia kwenye mchezo wakiwa na uzoefu mkubwa wa kucheza mechi za kiwango hiki. Hii si timu inayotegemea mchezaji mmoja pekee; nguvu yake kubwa ipo katika mpangilio wa timu, matumizi mazuri ya mpira na uwezo wa kucheza kwa nidhamu.

Mkwanja mrefu upo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Eneo la kiungo litakuwa muhimu sana. Denmark ikifanikiwa kudhibiti tempo na kuwazuia Ødegaard pamoja na viungo wa Norway kupata nafasi ya kupiga pasi za mwisho, itapunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya Haaland.

Lakini Denmark pia lazima iwe makini inapopoteza mpira. Norway ina uwezo wa kubadilisha mchezo kutoka kujilinda kwenda kushambulia kwa kasi, hasa ikiwa Ødegaard atapata nafasi ya kuanzisha mashambulizi.

Mechi mbili za mwisho kukutana kati yao Denmark aliondoka na ushindi, hivyo hii ni mechi ya kisasi kwa kina Haaland na wenzake. Suka jamvi hapa.

Mechi nyingine ni hii ya Uholanzi dhidi ya Ujerumani huku timu zote mbili zikiwa zimejiandaa vyema kabisa kupata ushindi mnono kwenye hili Kundi lao ambalo wapo.

Timu zote mbili zina makocha wapya hivyo hii inakuwa mara yao ya kwanza kukutana ambapo kocha wa Uholanzi ni Xavi Hernandez ambaye amekabidhiwa kijiti cha kuinoa timu hiyo, huku kwa upande wa Ujerumani wao wana Jurgen Klopp ambaye anahitaji kurejesha matumaini kwa klabu hiyo kubwa Duniani.

Hii ni mechi ya kwanza wa Xavi Hernandez akiwa na Uhalonzi kama tunavyojua ni kocha ambaye anapenda timu icheze kwa kumiliki mpira na kushambulia lango la mpinzani inapopata nafasi hiyo. Lakini pia timu hiyo ina wachezaji wakubwa na wenye uwezo mzuri akiwepo Van Dijk, De Jong, Gakpo Memphis Depay na wengine wengi.

Vilevile kwa upande wa Jurgen Klopp hii ni mechi yake ya kwanza akiwa kama kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ujerumani baada ya kuchukua mikoba ya Nagelsmann huku kocha huyo mwenye mafanikio makubwa akiwa ni tumaini kwenye Taifa hilo.

Ujerumani wakiwa kama washindi wa Kombe la Dunia 2014 wana wachezaji wenye uwezo mkubwa kabisa kama vile Joshua Kimmich, Musiala, Floarian Wirtz, Hevertz na wengine wengi ambao wanaungana kutengeneza kikosi hiki chenye uwezo mkubwa kabisa Duniani.

Uholanzi itataka kumiliki mpira na kujenga mashambulizi kwa utulivu, wakati Ujerumani chini ya Klopp inaweza kutafuta kutumia presha zaidi kwenda kwa mpinzani wao.

Kwa upande mwingine, kama Ujerumani itaruhusu Uholanzi kumiliki mpira kwa muda mrefu bila kuweka presha sahihi, De Jong, Reijnders na Gravenberch wanaweza kuanza kuutawala mchezo. Jisajili hapa.

Timu hizi mbili zimeshakutana sana na mara ya mwisho Ujerumani ndiye ambaye aliibuka mshindi. Je leo hii nani ataibuka na ushindi?. Odds Kubwa zipo kwenye mechi hii, hivyo bashiri sasa.

Video: Makonda Afichua Gharama za Tanzania Kuwa Mwenyeji Wa Afcon 2027

DAR ES SALAAM, Septemba 24, 2026 — Serikali ya Tanzania imelipa Dola za Marekani milioni 32, sawa na takriban Shilingi bilioni 74, kwa ajili ya kupata uenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amesema hayo leo, Septemba 24, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uwekezaji wa Serikali katika sekta ya michezo na usimamizi wa nembo za taifa.

Kwa mujibu wa Makonda, fedha hizo ni sehemu ya gharama za kuipatia Tanzania uhalali wa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo, na si fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanja, barabara au miundombinu mingine.

“Tumelipa sisi taifa kuwa wenyeji wa AFCON milioni 32, sawa na takriban bilioni 74. Hii ni pesa ya kuwa tu mwenyeji,” amesema Makonda.

Makonda amesema Serikali pia ipo katika mazungumzo na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuhusu malipo ya Dola za Marekani milioni 12, sawa na takriban Shilingi bilioni 30, kwa ajili ya kupata haki za matangazo ya televisheni za AFCON 2027.

Amesema uwekezaji huo unaangaliwa kwa mtazamo mpana zaidi ya michezo, ikiwemo kuitangaza Tanzania kimataifa, kukuza utalii na kuvutia wawekezaji.

“Fedha hizi sio za kujenga uwanja, sio za kununua maji, sio za kujenga barabara. Kama nchi tumelipa ili tupate uhalali wa ku-host haya mashindano,” amesema.

Ameongeza kuwa Tanzania inatarajia kutumia fursa ya mashindano hayo kuitangaza nchi na kuonyesha fursa zilizopo kwa wageni na wawekezaji watakaofika nchini.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, uwekezaji huo pia unalenga kuchochea shughuli za kiuchumi na kusaidia kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Akizungumzia suala la jezi ya Taifa Stars, Makonda amesema kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika kuiwakilisha Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa, jezi ya timu hiyo inapaswa kupewa thamani na uzito unaostahili.

Amesema jezi ya Taifa Stars ni miongoni mwa alama zinazotambulisha Tanzania na hivyo suala la uzalishaji, utambulishaji na uuzaji wake linapaswa kufanyika kwa utaratibu rasmi.

Makonda amesisitiza kuwa jezi hiyo haipaswi kuchukuliwa kama bidhaa ya kawaida, bali inapaswa kuangaliwa pia kama sehemu ya nembo ya taifa na fursa ya kuitangaza Tanzania.

Kauli hiyo imekuja wakati Tanzania ikiendelea na maandalizi ya AFCON 2027, ambayo inatarajiwa kuwa moja ya matukio makubwa ya michezo yatakayoiweka nchi katika uangalizi wa kimataifa.

Amsha Nguvu ya Totem na Volcano Inayosubiri Mlipuko wa Mara 6,750

Global Publishers
September 24, 2026
24 views
0 Comments

Usiku unapokuwa kimya, Volcano bado huwa na nguvu zake ndani kabisa. Ndivyo ilivyo kwenye mchezo huu wa kasino kutoka Meridianbet, ambapo Totem Wild anaweza kujitokeza wakati wowote na kuleta kizidishi cha mara 2 au 3. Ni mwanzo wa safari ambayo kila raundi inaweza kuleta mabadiliko na kuongeza msisimko.

Kama Totem mmoja ni mwanzo, wawili au watatu kwenye mstari mmoja ni nguvu nyingine kabisa. Vizidishi vyake ujikusanya kwa pamoja na hii inafanya kiwango cha malipo kuendelea kupanda kadri nguvu hizo zinavyoungana. Hapo mchezo unaanza kupata ladha ya kweli, kwa sababu kila Totem anayefika anaweza kuongeza uzito wa tukio linalofuata.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Lakini kuna hatua ambayo inaweza kubadilisha kabisa mazingira, ni hatua ya kuamsha Volcano. Ikianza kulipuka, bonasi za mizunguko zinaingia na safari inaendelea kwa kasi mpya. Kila raundi inakuwa kama mlango mwingine wa sapraizi, huku Totem zaidi wakitafutwa ili kuongeza nguvu ya mlipuko.

Na mwisho wa safari hiyo kuna namba inayovutia macho, kizidishi cha mara 6,750. Hicho ndiyo kiwango ambacho mchezo unaweza kufikia, huku idadi kubwa ya Totem wanaoitikia wito ikimaanisha mlipuko wenye nguvu zaidi. Hakuna anayejua raundi inayofuata italeta nini, na hapo ndipo burudani inapopata ladha yake.

Sasa ni wakati wa kuamsha Totem na kuacha Volcano ifanye kazi yake. Fungua safari yako ndani ya Meridianbet, fuatilia vizidishi vikijikusanya na mizunguko ya bonasi ikimiminika.