Mpigie Kura Godmuya, Kura Yako Ni Ushindi! – Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026

Global Publishers
September 27, 2026
3,444 views
0 Comments

Mtangazaji wa @globaltvonline na @255globalradio, Godfrey Nathan @godmuya ameteuliwa kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards 2026.

Sasa Godmuya anaomba support yako, mfuatiliaji wa Global TV, kwa kumpigia kura ili kufanikisha ushindi wake.

🗳️ MPIGIE KURA: GODFREY LUHILABAKE NATHAN
🔢 Kodi: 260246

Kura yako ni mchango mkubwa kwa Godmuya katika safari hii ya tuzo.

🙏 Piga kura, share na mwambie mwingine apige kura!

Katibu wa CCM Iringa Afutwa Kazi kwa Tuhuma za Maadili – Video

Global Publishers
September 27, 2026
24 views
0 Comments

Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Uamuzi huo umetangazwa Septemba 26, 2026 wakati Chacha akizungumza katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa uliojadili maandalizi ya

Chacha amesema hatua hiyo haimaanishi Goha ameondolewa kabisa katika majukumu ya chama, bali atapangiwa jukumu jingine ndani ya CCM.

Amesema mchakato wa kumpata Katibu mpya wa CCM Mkoa wa Iringa umeanza, huku chama kikiendelea na utaratibu wa kuhakikisha shughuli za uongozi mkoani humo zinaendelea bila kusimama hadi atakapopatikana atakayeshika nafasi hiyo.

Katika mkutano huo, Chacha amesisitiza umuhimu wa nidhamu miongoni mwa viongozi na wanachama wa CCM, akisema chama hakitafumbia macho mwenendo unaodaiwa kuathiri taswira na heshima yake.

Sifa Gospel Fest 2026 Yamalizika kwa Kishindo Mwanza, Mastaa wa Gospel Wakiwasha – Video

Global Publishers
September 27, 2026
882 views
0 Comments

MWANZA — Septemba 26, 2026: Uwanja wa Furahisha, Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza, ulikuwa kitovu cha ibada na burudani ya muziki wa Injili wakati wa kilele cha Sifa Gospel Fest 2026.

Hafla hiyo iliwakutanisha waumini na mashabiki wa muziki wa Injili katika siku maalum ya kusifu na kuabudu, huku jukwaa likipambwa na huduma mbalimbali za muziki na ibada.

Miongoni mwa wasanii walioifanya siku hiyo kuwa ya kipekee ni Rose Muhando, Obby Alpha na Zabron Singers, ambao walipanda jukwaani na kuwahudumia maelfu ya waliokusanyika katika Uwanja wa Furahisha.

Nyimbo za sifa na kuabudu, ujumbe wa kiroho pamoja na nyimbo zilizobeba hamasa vilitawala uwanja huo, na kufanya kilele cha Sifa Gospel Fest 2026 kuwa sehemu ya kumbukumbu kwa washiriki wa hafla hiyo.

Kwa ujumla, Sifa Gospel Fest 2026 imehitimisha kilele chake Mwanza kwa kuunganisha muziki wa Injili, ibada na ushirika katika jukwaa moja, huku Rose Muhando, Obby Alpha na Zabron Singers wakiwa miongoni mwa waliotoa burudani na huduma katika hafla hiyo.

Fursa Mpya ya Ajira NEEC, Mwisho wa Maombi Oktoba 1, 2026

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza nafasi moja ya Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika. Tangazo hilo limetolewa Septemba 18, 2026, kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

NEEC limeanzishwa chini ya Sheria ya Uwezeshaji Kiuchumi Na. 16 ya mwaka 2004 na lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Majukumu yake ni pamoja na kusimamia, kuratibu, kuwezesha na kufuatilia shughuli za uwezeshaji kiuchumi nchini.

Sifa za mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uzamili katika mojawapo ya fani zifuatazo:

  • Utawala wa Umma
  • Ujasiriamali
  • Fedha
  • Uhasibu
  • Utawala wa Biashara
  • Biashara, akiwa amebobea katika Ujasiriamali, Masoko au Fedha
  • Uchumi
  • Uchumi wa Kilimo
  • Au sifa zinazolingana kutoka taasisi inayotambuliwa.

Shahada ya Uzamili inapaswa kuhusiana na Shahada ya Kwanza ya mwombaji.

Mwombaji anatakiwa pia kuwa na uzoefu wa kazi wa angalau miaka 12 katika maeneo yanayohusiana, ambapo angalau miaka mitatu iwe katika nafasi ya kiutawala. Uelewa wa masuala ya uwezeshaji kiuchumi umetajwa kuwa ni sifa ya ziada.

Majukumu ya Mtendaji Mkuu

Mtendaji Mkuu atawajibika kusimamia shughuli za kiutawala za Baraza na kuwa msemaji wake. Pia atasimamia utekelezaji wa majukumu ya Baraza, maandalizi ya mipango ya kimkakati na bajeti, taarifa za fedha na maendeleo, pamoja na utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Baraza.

Majukumu mengine ni kusimamia utekelezaji na tathmini ya mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu, kuendesha shughuli za kila siku za Sekretarieti, kuandaa mikakati ya kuongeza ufanisi, kusimamia uundaji na utekelezaji wa sera pamoja na kuongoza juhudi za kutafuta rasilimali za kifedha kwa ajili ya miradi ya Baraza.

Nafasi hiyo ni ya ajira ya kudumu na yenye mafao ya kustaafu, huku mshahara ukiwa kwa mujibu wa kiwango kilichoidhinishwa cha NEECS 13.

Waombaji wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania na kwa ujumla wasizidi umri wa miaka 45, isipokuwa watumishi wa umma. Pia wanapaswa kuambatanisha CV, nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu na taaluma, cheti cha kuzaliwa pamoja na picha ya pasipoti.

Mwisho wa kutuma maombi ni Oktoba 1, 2026. Maombi yanapaswa kutumwa kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

China Yaitaka Marekani Kuheshimu Nchi za Ghuba na Kuondoa Vikwazo Cuba

NEW YORK: China imetumia hotuba yake katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupinga baadhi ya sera za Marekani kuhusu Iran na Cuba, ikisisitiza kuheshimiwa kwa mamlaka na usalama wa nchi za Ghuba na kutaka kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Cuba.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa Jumamosi, Septemba 26, 2026, Makamu wa Rais wa China, Han Zheng, hakuitaja Marekani moja kwa moja, lakini alitoa wito kwa nchi zenye nguvu kuheshimu sheria za kimataifa na kutotumia vitisho vya nguvu dhidi ya mataifa mengine.

“China inaamini kwamba mamlaka na usalama wa nchi za Mashariki ya Kati, ikiwemo nchi za Ghuba, vinapaswa kuheshimiwa,” Han alisema.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kukutana na Rais wa China, Xi Jinping, katika mazungumzo yaliyofanyika White House.

China yazungumzia Iran

Han pia alisisitiza kwamba nchi kubwa zina wajibu maalumu katika kulinda amani na usalama wa kimataifa na zinapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuheshimu sheria za kimataifa.

Msimamo huo unakuja wakati mzozo kati ya Marekani, Israel na Iran ukiendelea, huku Washington ikiendelea kuweka shinikizo dhidi ya Tehran.

Balozi wa Marekani nchini China amesema Trump alimuonya Xi kuhusu kutoa msaada kwa Iran wakati wa mazungumzo yao, huku akisema China ilitoa hakikisho kwamba haitafanya hivyo.

Ripoti pia zimeibua madai kwamba Beijing imeisaidia Tehran kukabiliana na vikwazo, ikiwemo katika masuala ya mauzo ya mafuta na vifaa vya ulinzi. Madai hayo yamekuwa sehemu ya mvutano mpana wa kisiasa kati ya Washington na Beijing.

China yataka vikwazo dhidi ya Cuba viondolewe

Katika hotuba hiyo, Han pia aliitaka Marekani kusitisha kile alichokiita vitisho vya kutumia nguvu dhidi ya Cuba na kuondoa vikwazo na zuio la kiuchumi dhidi ya nchi hiyo.

“China inatoa wito kwa nchi husika kusitisha mara moja matumizi ya vitisho vya nguvu dhidi ya Cuba na kuondoa kikamilifu zuio na vikwazo dhidi yake,” Han alisema.

Kauli hiyo imekuja wakati Cuba ikikabiliwa na changamoto kubwa za nishati na miundombinu, huku kukiwa na matatizo ya upatikanaji wa mafuta na kukatika kwa umeme.

Baadaye, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov, pia alitoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Cuba. Lavrov alitaka Washington kuondoa kile alichokiita “kuzingirwa” kwa Cuba na pia kuondoa vikwazo vya biashara.

Han alitumia hotuba yake pia kusisitiza nafasi ya China kama mshirika wa nchi zinazoendelea, akisema mataifa yote, makubwa na madogo, yanapaswa kuwa na usawa katika jumuiya ya kimataifa.

Alisema masuala ya dunia yanapaswa kushughulikiwa kupitia mashauriano ya pamoja badala ya maamuzi ya upande mmoja.

MAGAZETINI LEO JUMAPILI SEPT 27/2026:MNYUKANO MKALI MAJUKWAANI CCM NA CHADEMA

 

 

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

Sifa Gospel Fest 2026: Suma Awaunganisha Vijana na Fursa za Maisha – Video

MWANZA — Mratibu Mkuu wa ibada ya kusifu na kuabudu ya Sifa Gospel Fest 2026, Suma Mwaitenda, amewataka vijana kufikiri nje ya boksi na kutambua uwezo na ujuzi walionao ambao unaweza kuwaongezea thamani katika maisha, mbali na vyeti vya taaluma walivyopata shuleni.

Suma ameyasema hayo jijini Mwanza wakati wa mafunzo katika kliniki ya vijana iliyopewa jina la Sifa Youth Talk, iliyofanyika kwa mara ya kwanza kwa lengo la kuongeza thamani katika maisha ya vijana kupitia elimu kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo maadili, uchumi na jamii.

Akizungumza kuhusu Career Development, yaani ukuzaji wa safari ya kitaaluma na kikazi, Suma amesema vijana wanapaswa kutambua ujuzi wao na namna wanavyoweza kuutumia katika kujenga maisha yao.

“Nje ya vyeti, una ujuzi gani unaouzika? Haijalishi umesoma nini.”



Aidha, leo inafanyika siku ya kilele cha ibada kubwa ya kusifu na kuabudu ya Sifa Gospel Fest 2026, inayofanyika katika Uwanja wa Furahisha, Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza.

Akizungumzia maandalizi ya ibada hiyo, Suma amesema maandalizi yote yamekamilika huku akieleza kuwa mwitikio kutoka kwa wakazi wa Mwanza umekuwa mkubwa.

“Maandalizi yote ya ibada hii yamekamilika, mwitikio wa watu wa Mwanza ni mkubwa na tumebarikiwa kuwa na listi kubwa ya watumishi wa Mungu na waimbaji ambao watahudumu leo,” amesema.

Suma amesema ibada hiyo imeendelea kuwagusa watu mbalimbali, huku akieleza kuwa waandaaji wanaamini kuwa kupitia kusifu na kuabudu, watu wanaweza kupata uponyaji.

“Ibada hii imeendelea kuwagusa watu wengi ambao, na sisi tunaamini kuwa katika kusifu kuna uponaji na watu wengi wameendelea kupona kupitia ibada hii,” amesema.

Katika hatua nyingine, wasanii mbalimbali wanaotarajiwa kuhudumu katika ibada hiyo wameeleza furaha yao kwa tukio hilo kufika jijini Mwanza, huku wakitoa shukrani kwa waandaaji kwa nafasi ya kushiriki katika Sifa Gospel Fest 2026.

Waandaaji Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva Walipa Faini ya Dudu Baya

Global Publishers
September 26, 2026
12 views
0 Comments

Waandaaji wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Fleva wametangaza kutekeleza adhabu iliyotolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), ikiwemo kumlipia msanii Godfrey Tumaini, maarufu kama Dudu Baya, faini ya Sh milioni tatu.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na mmoja wa waratibu wa tamasha hilo, Madee Ali, amesema baada ya kupokea maamuzi ya BASATA, wamekubali kuyatekeleza na kwa haraka wamelipa faini iliyotolewa kwa waandaaji, pamoja na faini iliyotolewa kwa Dudu Baya.

Waandaaji hao wameihakikishia BASATA pamoja na wadau wa sanaa nchini kuwa wanaheshimu maamuzi yaliyotolewa na wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zilizowekwa.

Aidha, wamesema ushirikiano, uwajibikaji na uzingatiaji wa sheria ni miongoni mwa misingi muhimu katika kulinda, kukuza na kuendeleza sekta ya sanaa nchini.

“Tunatoa shukrani kwa BASATA na wadau wote kwa ushirikiano wao, huku tukiahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka husika katika kuhakikisha sekta ya sanaa inakua na kuendelezwa kwa kuzingatia misingi ya kisheria na kitaaluma,” amesema Madee.

Tanzania Yaahidi Kuongeza Juhudi Kutokomeza Sotoka Ifikapo 2040

Global Publishers
September 26, 2026
0 views
0 Comments

Tanzania imesema imejizatiti kushiriki kikamilifu katika juhudi za kimataifa za kutokomeza ugonjwa wa Sotoka ifikapo mwaka 2040, kupitia kuimarisha uwekezaji wa ndani pamoja na ushirikiano wa kikanda na kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa baada ya Tanzania kushiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo uliofanyika jijini Roma, Italia, Septemba 21 hadi 23, 2026.

Katika mkutano huo, mwakilishi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, alishiriki katika majadiliano yaliyolenga kuimarisha mifumo ya chakula na kilimo, usalama wa chakula pamoja na afya ya binadamu na mifugo.

Mkutano huo pia ulisisitiza umuhimu wa uwekezaji endelevu katika sekta ya afya na kilimo, matumizi ya sayansi na tafiti, pamoja na kuimarisha chanjo na mifumo ya kudhibiti magonjwa ya mifugo.

Tanzania imeeleza kuwa udhibiti wa magonjwa ya mifugo ni sehemu muhimu katika kulinda uzalishaji wa mifugo, usalama wa chakula na maisha ya wafugaji.

Katika kutekeleza azma ya kutokomeza Sotoka ifikapo mwaka 2040, Tanzania inalenga kuimarisha umiliki wa kitaifa wa kampeni hiyo, kuongeza uwekezaji wa ndani na kuendeleza ushirikiano na nchi nyingine pamoja na taasisi za kikanda na kimataifa.

Mkutano huo uliwakutanisha wadau kutoka maeneo mbalimbali duniani kujadili namna ya kujenga mifumo ya chakula na kilimo inayoweza kukabiliana na changamoto za afya, magonjwa ya mifugo na usalama wa chakula.

Kwa Tanzania, ushiriki huo unaendelea kuonyesha umuhimu wa kuunganisha afya ya binadamu, wanyama na mazingira katika juhudi za kukabiliana na changamoto zinazohusiana na afya na uzalishaji wa chakula.