MZEE MPILI WA YANGA AFARIKI DUNIA,YANGA YAMLILIA

UONGOZI wa Young Africans Sports Club (Yanga SC) umetangaza kwa masikitiko kifo cha mwanachama wake, Haji Omari Ramadhani Mpili, maarufu kama Mzee Mpili, kilichotokea usiku wa Septemba 27, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, marehemu Mpili alifariki dunia katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Uongozi umeeleza kuwa maziko yanatarajiwa kufanyika leo, Septemba 28, 2026, majira ya saa 10:00 jioni.

Shughuli za maziko zitafanyika katika Makaburi ya Msikiti Mkubwa yaliyopo Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

“Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa mpira, na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina,” imeeleza taarifa hiyo.

MAGAZETINI LEO JUMATATU SEPT 28/2029:DKT HOMERA AMRITHI NDEJEMBI NISHATI …

 

KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS HAPA

  

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

Rais Samia Afanya Uteuzi wa Viongozi Saba, Masanja Kadogosa Apewa Ujenzi

Global Publishers
September 27, 2026
0 views
0 Comments

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi saba katika nafasi mbalimbali za Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Septemba 27, 2026, uteuzi huo ni kama ifuatavyo:

  1. Mhe. Masanja Kungu Kadogosa (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.
  2. Mhe. Abdallah Hamis Ulega (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Ulega alikuwa Waziri wa Ujenzi.
  3. Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera (Mb.) ameteuliwa kuwa Waziri wa Nishati. Kabla ya uteuzi huo, Mhe. Dkt. Homera alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
  4. Bi. Asha Khamis Abdulla ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, ambapo atashughulikia masuala ya usimamizi wa fedha.
  5. Prof. Bruno Fokas Sunguya ameteuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
  6. Bw. Jabiri Omari Makame ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
  7. Dkt. Idrissa Muslim Hijja ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa Dodoma, Septemba 27, 2026. Uteuzi huo pia unaonekana katika taarifa rasmi ya Ikulu kuhusu viongozi wa Serikali.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa uapisho wa Mawaziri na Naibu Katibu Mkuu walioteuliwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Taarifa hiyo imesainiwa na Bakari S. Machumu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Dodoma — 27 Septemba 2026.

CCM Yateua Kaimu Makatibu 32 wa Mikoa, Yaandaa Semina Elekezi

Global Publishers
September 27, 2026
12 views
0 Comments

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko ya kiutendaji katika ngazi ya Makatibu wa CCM wa mikoa, kwa kuteua Kaimu Makatibu 32 wa mikoa yake yote ya kichama, ambao wanaanza kazi mara moja.

Taarifa hiyo imetolewa Septemba 27, 2026, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa CCM, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Labani Kihongosi. Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa mabadiliko hayo yanafuatia uteuzi wa viongozi wapya watakaosimamia shughuli za chama katika mikoa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Asha-Rose Migiro, ameandaa semina elekezi ya siku mbili kwa Kaimu Makatibu hao, itakayofanyika jijini Dodoma kuanzia Septemba 29 hadi 30, 2026.

Semina hiyo inalenga kuwaandaa viongozi hao kwa majukumu yao ya kiutendaji, huku orodha kamili ya walioteuliwa ikiwa kwenye kurasa zinazofuata za taarifa hiyo.

CCM pia imewapongeza na kuwashukuru Makatibu wa Mikoa waliomaliza muda wao kwa utumishi na mchango wao ndani ya chama, ikieleza kuwa itaendelea kutumia uzoefu na uwezo wao kama sehemu ya hazina ya viongozi na watendaji wake.

Orodha ya Kaimu Makatibu wa CCM wa Mikoa

  1. Arusha — Pilly John Jackson
  2. Dar es Salaam — Stanley Wilson Mkandawire
  3. Dodoma — Pili Augustine Mbanga
  4. Geita — Ramadhani Kapeto
  5. Iringa — James Dan Mgego
  6. Kagera — Rukia Said Mkindu
  7. Kaskazini Pemba — Salum Khamis Haji
  8. Kaskazini Unguja — Haji Machano Juma
  9. Katavi — Hawa Siri Makonyola
  10. Kigoma — Halid Said Mwinyi
  11. Kilimanjaro — Julius Nansongelya Peter
  12. Kusini Pemba — Bilal Hussein Maulid
  13. Kusini Unguja — Himid Lussan Tweve
  14. Lindi — Zuwena Suleiman Mohamed
  15. Mkoa wa Magharibi — Alawi Haidar Foum
  16. Mkoa wa Mjini — Yusuph Mabena
  17. Manyara — Eva Michael Degeleki
  18. Mara — Godfrey R. Kavenga
  19. Mbeya — Ramadhani Samwel Mahanyu
  20. Morogoro — Joseph Robert Mwega
  21. Mtwara — Ahmada Shaha Vuai
  22. Mwanza — Mwanamasudi Msafiri Pazi
  23. Njombe — Waridi Josephat Mgumi
  24. Pwani — Abdul-Rahim Hamad (Dogo)
  25. Rukwa — Rehema Nzunye Ndele
  26. Ruvuma — Mohammed Ali Khalfan
  27. Shinyanga — Sophia Abdallah Kibaba
  28. Simiyu — Kajoro Peter Vyohoroka
  29. Singida — Jonathan Mabihya
  30. Songwe — Aziza Juma Isimbula
  31. Tabora — Salum Suleiman Tate
  32. Tanga — Twalib K. Berege

Pirates Power Yaleta Msisimko Mpya kwa Wapenzi wa Kasino

Bahari imejaa siri, mawimbi yanapiga kwa kasi na jahazi limejiandaa kuanza safari ya kusaka hazina. Hii ndiyo dunia ya Pirates Power kutoka kwenye kasino mtandaoni ya Meridianbet, mchezo unaokuletea mandhari ya uharamia, burudani na msisimko wa kila raundi. Ukiwa ndani ya jahazi hili, kila raundi inakupa nafasi ya kufurahia mchezo huku ukisubiri alama zinazoweza kufungua milango ya ushindi mkubwa. Ni safari ambayo kila mzunguko unaweza kuleta mshangao mpya.

Kinachoongeza hamasa zaidi ni nafasi ya kushinda hadi mara 5,000 ya dau lako. Hii inafanya kila mzunguko kuwa sehemu muhimu ya safari yako, huku macho yakibaki kwenye skrini kusubiri mchanganyiko wa alama unaotafutwa. Kama ilivyo kwa nahodha anayesubiri kuona ardhi baada ya safari ndefu baharini, kila raundi inabeba matumaini ya kukutana na hazina iliyojificha.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Pirates Power pia inakuja na mistari 20 ya ushindi pamoja na njia 6 za kushinda, hivyo mchezo unakuwa na fursa mbalimbali za kupata mchanganyiko wa alama. Alama ya Wild inaweza kuongeza ushindi mara mbili, wakati Scatter inafungua milango ya raundi za bonasi. Hapo ndipo safari inapata ladha nyingine, kwani kila alama inayotua inaweza kubadilisha mwelekeo wa mchezo.

Lakini hazina kubwa zaidi imefichwa kwenye jackpot zinazopatikana ndani ya mchezo. Mini, Major na Grand Jackpot zinasubiri mabaharia wanaoingia kwenye safari hii, na kufanya kila mzunguko kuwa na mvuto wa kipekee. Kadiri safari inavyoendelea, ndivyo hamu ya kuona ni hazina gani itakayojitokeza inavyoongezeka. Pirates Power inakupa mandhari ya bahari huku ikichanganya burudani na msisimko katika kila raundi.

Kwa hiyo, kama uko tayari kuingia kwenye safari ya kipekee ya mabaharia, Pirates Power kupitia Meridianbet inakusubiri. Panda jahazini, zungusha na ufurahie burudani ya mchezo huku ukifuatilia nafasi za ushindi zinazopatikana. Bahari ina hazina zake, na kila safari huanza na hatua moja.

Serbia Kukiwasha Uholanzi Katika Uefa Nations League

Global Publishers
September 27, 2026
42 views
0 Comments

Timu ya Taifa ya Serbia itakuwa mwenyeji wa Uholanzi katika mchezo wa UEFA Nations League 2026/27 utakaochezwa Jumapili, Septemba 27, katika Uwanja wa Rajko Mitić jijini Belgrade.

Mchezo huo wa Kundi A2 utaanza saa 19:00 usiku na ni sehemu ya siku ya pili ya hatua ya ligi ya michuano hiyo.

Serbia na Uholanzi zipo katika Kundi A2 pamoja na Ujerumani na Ugiriki. Katika mfumo wa msimu huu, timu zitapambana kwenye hatua ya ligi huku nafasi mbili za juu katika kila kundi la League A zikifuzu moja kwa moja kwa robo fainali. Hivyo, kila pointi itakuwa muhimu katika kuwania nafasi hizo.

Kwa upande wa Serbia, kucheza mbele ya mashabiki wake kutakuwa sehemu muhimu ya mchezo huo. Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia uwanjani kikiwa na lengo la kupata matokeo dhidi ya Uholanzi, Huku mchezo wao mwingine wa kundi ukiwa dhidi ya Ugiriki kabla ya kukutana na Ujerumani Oktoba 1.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Uholanzi nayo inaingia kwenye kampeni hii ikiwa katika Kundi A2 na itakuwa na ratiba yenye michezo minne ndani ya kipindi kifupi cha kimataifa.

Baada ya kukutana na Ujerumani Septemba 24, itasafiri kwenda Belgrade kuikabili Serbia, kabla ya kucheza na Ugiriki na baadaye kurudiana na Serbia Oktoba 4.

Mchezo wa Serbia dhidi ya Uholanzi unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na historia na ubora wa wachezaji wa timu hizo. Kwa Serbia, lengo litakuwa kutumia uwanja wa nyumbani kupata matokeo, wakati Uholanzi itatafuta pointi ugenini katika hatua ya mwanzo ya mashindano hayo.

Makamu wa Rais Ndejembi Akutana na Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres

Global Publishers
September 27, 2026
6 views
0 Comments

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amekutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, katika hayo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Mhe. Ndejembi alifanya mazungumzo hayo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA 81) uliofanyika New York.

Kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo, Makamu wa Rais alikutana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kusalimiana naye.

Mkutano huo unaendelea kuwa sehemu ya shughuli za Tanzania katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unaowakutanisha viongozi na wawakilishi wa mataifa mbalimbali duniani kujadili masuala ya kimataifa.

SINTOFAHAMU KIGANJA CHA MKONO WA BINADAMU KUKUTWA JIRANI NA OFISI YA KATA YA ISAKALILO

 

SINTOFAHAMU imejitokeza katika mtaa wa Njiapanda kata ya Isakalilo Manispaa ya Iringa baada ya wananchi kukuta box lenye kiganja cha mkono wa binadamu ndani. 

Matukio Daima Media imefika eneo la tukio na kuzungumza na mashuhuda ambao wamedai kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 7 mchana wa leo Jumapili September 27/2026.

walisema kuwa kata hiyo imekuwa ikikumbwa na matukio ya ajabu ajabu na kuwa hawajui mhusika wa tukio hilo ni nani hasa. 

Hata hivyo walisema kutokana na sintofahamu hiyo walilazimika kujulisha uongozi wa serikali ya mtaa na kata pia polisi kata kwa hatua zaidi.

Mwenyeki wa serikali ya mtaa huo Maisha Modestus Kihuko alisema kuwa alipigiwa simu majira ya saa 6 mchana na baada ya kufika alikuta mkono huo ukiwa na ujumbe wenye kurasa sita ambapo moja moja kata ya jumbe hizo kuwa “Mkono huu ufike Iringa”

Alisema tukio hilo kama linahusishwa na Imani za kishirikina ndani yake Ila vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi zaidi. 

TAZAMA VIDEO YA TUKIO BONYEZA HAPA

Hata hivyo askari polisi waliofika eneo la tukio waliomba wananchi kutoa ushirikiano na pindi watakapobaini mtu hana mkono ama mhusika wa tukio hilo basi wasisite kutoa taarifa polisi

WAZIRI MKUU: SEKTA BINAFSI NI MUHIMU KUFIKIA UCHUMI WA DOLA TRILIONI MOJA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema ushirikishwaji wa sekta binafsi ni muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Tanzania, hasa azma ya kufikisha thamani ya uchumi wa Taifa hadi dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050.

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili, Septemba 27, 2026, jijini Doha, Qatar, alipokutana na Makamu wa Kwanza wa Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda cha Qatar (QCCI), Bw. Mohammed bin Ahmed bin Twar Al Kuwari, pamoja na ujumbe wake katika kikao kilichofanyika katika Hoteli ya Kempinski.

Waziri Mkuu amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuwa akisisitiza umuhimu wa kuishirikisha sekta binafsi katika mipango ya maendeleo ya nchi, kupitia Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050.

“Tunaamini kwamba Serikali peke yake haiwezi kufanikiwa katika uwekezaji huo bila kushirikisha wawekezaji wa ndani au wa nje. Ndiyo maana Serikali imeweka vivutio vya kiuwekezaji ili kuvutia mitaji,” amesema Dkt. Mwigulu.

Katika kikao hicho, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya uchumi na uwekezaji, pamoja na kuainisha fursa zilizopo Tanzania na Qatar, pamoja na fursa zinazotokana na ushiriki wa nchi hizo katika jumuiya za kikanda za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Baraza la Ushirikiano la Nchi za Kiarabu za Ghuba (GCC).

Aidha, kikao hicho kimekubaliana kuhusu umuhimu wa kuwakutanisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Qatar kupitia taasisi zao za uwakilishi, zikiwemo QCCI, TPSF na TCCIA, kwa lengo la kujadili kwa kina maeneo ya ushirikiano wa kimkakati, biashara na uwekezaji.

Kikao hicho kiliwashirikisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe; Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji; Wabunge pamoja na watendaji wengine wa Serikali.

ESAMI kuimarisha tafiti kutatua changamoto za jamii – HabariLeo

ARUSHA: KUIMARISHA tafiti za kitaaluma na kutumia matokeo yake kutatua changamoto zinazoikabili jamii ni miongoni mwa malengo ya Taasisi ya Usimamizi ya Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI).

Uimarishaji wa tafiti hizo umeelezwa kupitia programu mpya za shahada za uzamivu katika Usimamizi wa Biashara (DBA) na Uzamivu wa Falsafa (PhD).

Mkurugenzi Mkuu wa ESAMI, Profesa Peter Kiruku, alisema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa programu hizo, akieleza kuwa utafiti wa kitaaluma unapaswa kwenda zaidi ya kuongeza maarifa na kulenga kuboresha maisha ya watu.

Alisema Afrika na dunia kwa ujumla zinahitaji maarifa mapya na ujuzi wa kiwango cha juu kutokana na mabadiliko yanayoendelea katika taasisi, mashirika na sekta mbalimbali.

Kwa mujibu wa Profesa Kiruku, tafiti zinapaswa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi katika mazingira yao na kutoa matokeo yenye tija kwa jamii.

Alisema uzinduzi wa programu hizo ni sehemu ya hatua za ESAMI kukabiliana na mahitaji yanayobadilika ya elimu ya juu na uongozi barani Afrika.

Naye, Mkurugenzi wa Biashara wa ESAMI, Profesa Joseph Mumba, alisema programu hizo zote ni shahada za uzamivu zinazohusisha utafiti, lakini zinatofautiana katika msisitizo wa tafiti zake.

Alisema shahada ya PhD inalenga zaidi utafiti wa kinadharia na kuzalisha maarifa mapya katika maeneo ya kitaaluma, wakati DBA inalenga kutumia utafiti kutatua changamoto halisi za biashara na taasisi.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Global Humanistic University, Profesa Mario Grabner, alisema ushirikiano huo unalenga kuwezesha watu kupata elimu ya juu bila kulazimika kuacha familia na maeneo yao ya kazi.

Alisema mtandao wa kitaaluma wa taasisi hiyo unajumuisha washauri na maprofesa zaidi ya 150 kutoka nchi zaidi ya 37, huku programu hizo zikiwa na mtazamo wa kimataifa unaozingatia mahitaji ya Afrika.

Akizungumza kwa niaba ya uongozi wa ESAMI, Profesa David Kalaba alisema taasisi hiyo inalenga kutumia uzoefu wake wa kikanda na ushirikiano wa kimataifa kuongeza fursa za elimu ya uzamivu kwa wataalamu.

Alisema programu hizo zinaweza kuwawezesha wataalamu kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kusini kuendelea na masomo bila kulazimika kuhama maeneo yao ya kazi.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi, watumishi wa ESAMI, wahitimu, wasomi na wanafunzi watarajiwa wa programu hizo.