π™ˆπ˜Όπ™†π˜Όπ™ˆπ™ π™’π˜Ό π™π˜Όπ™„π™Ž π˜Όπ™Žπ™ƒπ™π™ƒπ™π˜Ώπ™„π˜Ό π™π™π™„π˜Όπ™…π™„ π™Žπ˜Όπ™„π™‰π™„, π™ˆπ™‹π˜Όπ™‰π™‚π™Š π™’π˜Ό π™π™Žπ™ƒπ™„π™π™„π™†π™„π˜Όπ™‰π™Š π™’π˜Ό π™π˜Όπ™‰π™€π™Žπ˜Ύπ™Š π™‰π˜Ό π˜Ύπ™π˜Ώπ˜½ π™†π™π™’π˜Όπ™’π™€π™•π™€π™Žπ™ƒπ˜Ό π™’π˜Όπ™‰π˜Όπ™‰π˜Ύπ™ƒπ™„ π™†π™π™‹π˜Όπ™π˜Ό π™π™ˆπ™€π™ˆπ™€.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kushirikiana na wadau husika wa sekta binafsi kuandaa mpango utakaowawezesha wananchi kununua umeme kwa mkopo kama ilivyo mikopo katika mitandao ya simu ili kuwasaidia wananchi wanapokuwa na uhitaji wa umeme lakini hawana fedha.
 
Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa hafla ya utiaji Saini Mkataba wa Uzinduzi wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Amesema hatua hiyo itaweza kusaidia wananchi kuendelea kutumia huduma ya umeme na kufanya uzalishaji mali au mahitaji ya nyumbani hata pale wanapokuwa na changamoto ya fedha ya kununua umeme huo.
 
Aidha, Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuendeleza mradi ulioanzishwa chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuhakikisha wananchi wanaoishi mazingira yanayofanana na kijijini lakini mipaka ya kiutawala inawatambua wapo mjini wanaunganishiwa huduma ya umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 kama ya wananchi wa vijijini. Amesema yapo maeneo ambayo ni mipaka ya kiutawala inawatenganisha wananchi kati ya mijini na vijijini lakini wananchi hao maisha yao yanafanana.
Makamu wa Rais, amesema azma hiyo, inalenga kufikia lengo la kitaifa, malengo ya β€œmission 300” pamoja na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, kuhakikisha huduma ya umeme inamfikia mtanzania kwa gharama nafuu.
 
Makamu wa Rais ameipongeza TANESCO na Benki ya CRDB kwa hatua hiyo muhimu inayolenga kuimarisha na kuboresha maisha ya wananchi kwa kupata huduma ya umeme.  Amesema ushirikiano huo ni mfano bora wa namna ya Taasisi za Umma na Sekta Binafsi zinavyoweza kuwaunganisha watanzania na kuwekeza nguvu na rasilimali ili kutatua changamoto zinazowagusa wananchi moja kwa moja.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Abdulmajid Nsekela amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono na uwepo wa Dira ya Maendeleo 2050. Amesema Serikali na Sekta binafsi kupitia ubunifu itawezesha kutekelezwa na kufanikiwa kwa Dira 2050 inayolenga kujenga uchumi mkubwa, yenye kuzalisha ajira, wenye ushindaji, unaotumia teknolojia na kuboresha maendeleo ya wananchi.
 
Amesema Benki ya CRDB imedhamiria kuwa mshirika wa maendeleo yan chi kwa kutumia uwezo wa kifedha, teknolojia iliyopo, rasilimali ya wataalamu waliopo, mtandao uliopo na ubunifu katika kusaidia kutatua changamoto ya maendeleo ya Taifa.
Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Razaro Twange amesema upatikaji wa umeme umeendelea kuongezeka nchini na ujenzi wa miundombinu ya kusafirisha umeme na kusambaza umeme ikiendelea kujengwa. Amesema Tanzania inafikia megawati 4500-4600 hivi sasa huku kukiwa na mtandao wa kiliometa 9000 za kusafirisha umeme, na mtandao wa zaidi ya kilometa 220,000 wa njia za kusambaza umeme.
 
Utiaji wa Saini wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi, kati ya Benki ya CRDB na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), utawezesha wananchi wa maeneo ya vijiji kuunganishwa bure huduma ya umeme kutokana na ruzuku kutoka Benki ya CRDB, na kwa wananchi maeneo ya mijini watapewa huduma hiyo kwa mkopo wa riba nafuu ambao wataweza kuunganishwa umeme na kufanya shughuli za uzalishaji mali.

DC SHAKA: MIILI YENU ISIWE KITEGA UCHUMI

Na Matukio Daima Media, Kilosa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amewataka wakulima na wananchi wa Kata ya Magole kuacha kutumia madhara wanayopata katika migogoro ya wakulima na wafugaji kama njia ya kujipatia fedha.
Shaka amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakipokea malipo kutoka kwa watuhumiwa na baadaye kuacha kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya vitendo hivyo.
Amesema hali hiyo inaweza kudhoofisha kesi na kuacha mazingira ya matukio ya ukatili kujirudia, hivyo amewataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola hadi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.
Lakini wakati Shaka akitoa tahadhari hiyo, wakazi wa Magole wameibua changamoto nyingine inayohusiana na maisha yao ya kila siku ikiwemo upatikanaji wa ardhi ya kilimo na zahanati isiyo na huduma Rafiki.
Wananchi hao wameiomba Serikali kuwawezesha kupata maeneo ya kulima, hususan mashamba yaliyofutwa, wakisema ongezeko la watu limeongeza mahitaji ya ardhi kwa shughuli za kilimo.
Omary Saidi na Elia Chisongela ni miongoni mwa wakazi walioeleza hitaji hilo huku pia wakibainisha changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya kuwa ni changamoto katika maeneo yao.
Kwa upande wake, Shaka amesema Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya mtu yeyote anayechangia migogoro hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia vyombo vya dola katika kushughulikia vitendo vya ukatili.
Mwisho

 

DC SHAKA: MIILI YENU ISIWE KITEGA UCHUMI

Na Matukio Daima Media, Kilosa.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amewataka wakulima na wananchi wa Kata ya Magole kuacha kutumia madhara wanayopata katika migogoro ya wakulima na wafugaji kama njia ya kujipatia fedha.

Shaka amesema baadhi ya wananchi wamekuwa wakipokea malipo kutoka kwa watuhumiwa na baadaye kuacha kutoa ushahidi mahakamani dhidi ya vitendo hivyo.

Amesema hali hiyo inaweza kudhoofisha kesi na kuacha mazingira ya matukio ya ukatili kujirudia, hivyo amewataka wananchi kushirikiana na vyombo vya dola hadi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya watuhumiwa.

Lakini wakati Shaka akitoa tahadhari hiyo, wakazi wa Magole wameibua changamoto nyingine inayohusiana na maisha yao ya kila siku ikiwemo upatikanaji wa ardhi ya kilimo na zahanati isiyo na huduma Rafiki.

Wananchi hao wameiomba Serikali kuwawezesha kupata maeneo ya kulima, hususan mashamba yaliyofutwa, wakisema ongezeko la watu limeongeza mahitaji ya ardhi kwa shughuli za kilimo.

Omary Saidi na Elia Chisongela ni miongoni mwa wakazi walioeleza hitaji hilo huku pia wakibainisha changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya kuwa ni changamoto katika maeneo yao.

Kwa upande wake, Shaka amesema Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya mtu yeyote anayechangia migogoro hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kutumia vyombo vya dola katika kushughulikia vitendo vya ukatili.

Mwisho

SERIKALI YAWEKA MITAJI KUKUZA KAMPUNI CHANGA ZA TEHAMA

SERIKALI imezindua programu ya uwezeshaji mitaji ya Sh bilioni tano kwa kampuni changa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kwa lengo la kuzisaidia kukuza biashara, kuongeza ajira na kutengeneza suluhisho za kidijitali zinazochochea maendeleo ya uchumi.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amesema hayo wakati wa uzinduzi wa programu ya uwezeshaji mitaji kwa kampuni changa za TEHAMA (STARS-UPS), akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wabunifu kutumia teknolojia kutatua changamoto katika sekta mbalimbali.

Amesema katika zama hizi za maendeleo ya teknolojia, ubunifu ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi, hivyo Serikali kupitia Tume ya TEHAMA imeendelea kuweka mazingira yanayowezesha kampuni changa kuanzisha, kuimarisha na kupanua biashara zao.

Kairuki amesema programu hiyo inalenga kuwapatia wajasiriamali wa TEHAMA mitaji itakayowawezesha kubadilisha mawazo bunifu kuwa bidhaa na huduma zenye thamani ya kiuchumi, huku utekelezaji wake ukifanyika kwa kushirikiana na Benki ya Azania.

Amefafanua kuwa mikopo hiyo itatolewa katika madaraja matatu, kuanzia Sh milioni moja hadi milioni 25, zaidi ya Sh milioni 25 hadi milioni 50, na zaidi ya Sh milioni 50 hadi milioni 100, kwa kuzingatia vigezo na masharti yatakayowekwa.Β 

Amesema programu hiyo inalenga kampuni zinazotengeneza suluhisho za kidijitali katika sekta za fedha, kilimo, utalii, elimu, bima, usafirishaji na ugavi, pamoja na biashara mtandao, ili kuongeza matumizi ya teknolojia katika shughuli za kiuchumi.

Waziri huyo amesema mafanikio ya programu hayatapimwa kwa kiasi cha fedha kilichotolewa pekee, bali pia ukuaji wa kampuni zitakazonufaika, ajira zitakazozalishwa, ongezeko la mauzo na mapato, bidhaa na huduma mpya zitakazoingia sokoni, upanuzi wa masoko na urejeshaji wa mikopo.

Amesisitiza kuwa fedha hizo zinapaswa kutumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa ili kuwezesha kampuni kuongeza uzalishaji, kuimarisha biashara na kutafuta masoko ndani na nje ya Tanzania.

β€œFedha hizi ni moto, hivyo mkazifanyie kazi kwa malengo mliyokusudia, mjenge biashara zenu, mtafute masoko na muimarishe nidhamu ya fedha,” amesema.

Kairuki aliwataka wabunifu na kampuni changa za TEHAMA kujisajili katika mifumo inayotambuliwa na Serikali ili kurahisisha upatikanaji wa huduma na fursa zinazotolewa kwa sekta hiyo.

Aidha, ameitaka Tume ya TEHAMA kukamilisha mwongozo wa utekelezaji wa programu hiyo na kuweka mfumo wa kufuatilia na kupima ukuaji wa kampuni zitakazonufaika, ili kuhakikisha uwezeshaji huo unaleta matokeo yanayopimika.Β 

Amesema pia ni muhimu kwa wabunifu wa TEHAMA kuanzisha umoja rasmi utakaowawezesha kuwa na sauti ya pamoja na kurahisisha ushirikiano wao na Serikali pamoja na wadau wengine.

β€œMpango huu ni muhimu kwa umma. Wale watakaopata mikopo wahakikishe wanaitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa ili wengine nao waweze kunufaika,” amesema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mohammed Khamis Abdulla, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono na msukumo wake katika kuendeleza sekta ya mawasiliano na TEHAMA nchini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya TEHAMA, Dkt. Henry Mwanyika, amesema kampuni changa zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa mitaji, huku baadhi ya benki zikisita kufadhili biashara hizo kutokana na hatari zinazohusishwa na uwekezaji katika kampuni changa.

Amewataka wanufaika kurejesha mikopo kwa wakati ili fedha hizo ziendelee kutumika kuwawezesha vijana wengine wenye mawazo bunifu kukuza biashara zao.

” Fedha hizo si ruzuku wala sadaka, bali ni mikopo inayopaswa kurejeshwa ili kuhakikisha programu hiyo inaendelea kutoa fursa kwa kampuni nyingine zinazohitaji mitaji, ” Amesema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Startup Association (TSA), Zahoro Muhaji, amesema programu hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuendeleza kampuni changa na kukuza sekta ya ubunifu nchini.

Alisema Sh bilioni tano zilizotengwa ni mwanzo muhimu katika kupanua wigo wa uwezeshaji wa kampuni changa, akibainisha kuwa awali fursa za ushindani wa ubunifu zilikuwa zikitoa zawadi zilizofikia Sh milioni 50.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC), Dkt. Godwill Wanga, alisema uwekezaji huo unalenga kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijitali kupitia utengenezaji wa bidhaa, viwanda vya kidijitali na maendeleo ya sekta mahiri.

Aliwataka wabunifu kuelekeza matumizi ya teknolojia katika sekta zote 21 za uchumi ili kuongeza mchango wa ubunifu katika uzalishaji, uundaji wa ajira na maendeleo ya Taifa.

SERIKALI KUKAGUA UMILIKI WA KAMPUNI ZA HUDUMA MIGODINI

_Waziri Mavunde awataka Watanzania kuchangamkia fursa za huduma na bidhaa kwenye migodi_

πŸ“GEITA

Serikali kupitia Tume ya Madini inatarajia kuanza kuhakiki umiliki halali wa kampuni zinazotoa huduma kwenye migodi ya madini nchini, ili kuhakikisha fursa za ajira, huduma na biashara zinawanufaisha Watanzania wenye sifa na uwezo unaohitajika.

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti utaratibu unaodaiwa kuwepo wa kampuni za kigeni kuingia ubia na Watanzania wasio na sifa stahiki kwa ajili ya kutimiza matakwa ya ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini.

Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo mapema leo Oktoba 2, 2026, wakati akifungua Siku ya Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya Kitaifa ya Tisa ya Teknolojia na Uwekezaji katika Sekta ya Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bomba Mbili, Geita.

Amesema katika utekelezaji wa Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, imebainika kuwepo kwa kampuni za kigeni zinazoingia ubia na Watanzania kwa lengo la kutimiza matakwa ya umiliki wa hisa, wakati kiuhalisia kampuni hizo zinamilikiwa na wageni.

β€œNimebaini kumekuwepo na kampuni za kigeni ambazo zimekuwa zikiingia ubia na Watanzania ambao wanatakiwa kuwa na asilimia 20 ya hisa kimaandishi, lakini ukija kiuhalisia unabaini kampuni inamilikiwa na wageni pekee,” amesema.

Amesema Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini, kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali ikiwemo BRELA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), itahakiki umiliki wa kampuni hizo pamoja na miamala inayofanyika ili kubaini umiliki halali wa kampuni husika.

Waziri Mavunde pia amewataka Watanzania kujiandaa kuchangamkia fursa za kutoa huduma na bidhaa kwenye migodi, akisema kampuni 14 zinatarajiwa kuanza shughuli za uchimbaji wa madini, huku leseni nyingine 28 zikiwa katika hatua za kutolewa.

Amesema ongezeko hilo linatarajiwa kuongeza mahitaji ya huduma na bidhaa mbalimbali migodini, hivyo kuwataka watoa huduma wa ndani kujiandaa na, pale inapowezekana, kuungana ili kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji makubwa ya kampuni za uchimbaji.

Katika hatua nyingine, Waziri Mavunde amesema Serikali imeanza kutekeleza mkakati wa kutumia asilimia 10 ya makusanyo ya maduhuli yatokanayo na Sekta ya Madini kwa ajili ya shughuli za utafiti wa madini.

Amesema katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka wa fedha 2026/2027, kuanzia Julai hadi Septemba, Wizara kupitia Tume ya Madini ilikusanya shilingi bilioni 411, sawa na asilimia 117 ya lengo la shilingi bilioni 351.

β€œKatika makusanyo hayo, kiasi cha shilingi bilioni 40, sawa na asilimia 10, kitaanza kutumika katika shughuli za utafiti wa madini,” amesema.

Ameongeza kuwa Serikali pia imetenga eneo lililokuwa likitumika na Mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vitakavyozalisha bidhaa zinazohitajika katika shughuli za migodini, hatua inayolenga kuongeza ushiriki wa Watanzania katika mnyororo wa thamani wa Sekta ya Madini.

Aidha, amesema Serikali inalenga kuhakikisha asilimia 90 ya manunuzi ya kampuni za madini, yenye thamani ya takribani shilingi trilioni 5.1 kwa mwaka, yanafanywa na Watanzania ili kuongeza mchango wa Sekta ya Madini katika kukuza uchumi wa nchi.

Waziri Mavunde pia amewapongeza wachimbaji wadogo kwa mchango wao unaofikia asilimia 40 katika Sekta ya Madini, akisema katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali ilikusanya shilingi trilioni 1.393 kutokana na shughuli za sekta hiyo.

Amesema utekelezaji wa Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini umeendelea kuleta matokeo, ikiwemo kuongezeka kwa ajira rasmi 19,000, huku raia wa kigeni wakichangia asilimia nne ya ajira katika sekta hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, amewataka Watanzania kuacha kulalamika kuhusu fursa zilizopo na badala yake kuwa wabunifu na kuzichangamkia ili kuongeza ushiriki wao katika Sekta ya Madini.

Mbunge wa Geita, Chacha Wambura, ameiomba Wizara ya Madini kuendelea kusimamia kwa nguvu utekelezaji wa Kanuni za Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, huku ikiendelea kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo nchini.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), John Bina, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wachimbaji wadogo, pamoja na kufanya maboresho ya Sheria na Kanuni za Madini.

Awali, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet Lekashingo, amesema mkutano huo uliowakutanisha wamiliki wa leseni za madini na watoa huduma kwenye migodi unalenga kubadilishana uzoefu, kutoa elimu, kuweka mikakati ya ushirikiano na kubuni njia bora za kutatua changamoto zinazowakabili wadau wa Sekta ya Madini.

Wizara ya Elimu Yabadili Tarehe ya Kufunga Shule, Sasa ni Novemba 13

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeagiza shule zote za msingi na sekondari Tanzania Bara kufungwa tarehe 13 Novemba 2026, badala ya tarehe 4 Desemba 2026 kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Uamuzi huo umetangazwa kupitia Waraka wa Elimu Na. 3 wa Mwaka 2026 kuhusu mabadiliko ya tarehe ya kufunga shule za awali, msingi na sekondari Tanzania Bara, uliotolewa na Wizara hiyo tarehe 30 Septemba 2026.

Kwa mujibu wa waraka huo, hatua hiyo imechukuliwa kufuatia taarifa za hali ya hewa zilizotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mvua kubwa zinazohusishwa na El NiΓ±o katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2026.

Wizara imeeleza kuwa mvua hizo zinaweza kusababisha mafuriko na athari nyingine katika baadhi ya maeneo, hivyo hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama na ustawi wa wanafunzi, walimu pamoja na watumishi wengine wa shule.

Awali, kupitia Waraka wa Elimu Na. 6 wa Mwaka 2025 kuhusu kalenda ya mihula ya masomo kwa mwaka 2026 na Waraka wa Elimu Na. 1 wa Mwaka 2026 kuhusu kalenda ya mihula kwa Kidato cha Tano na Sita kwa mwaka wa masomo 2026/2027, shule zilipangwa kufungwa tarehe 4 Desemba 2026.

Hata hivyo, Kamishna wa Elimu, Dkt. Lyabwene M. Mtahabwa, ametangaza kuwa shule zote zifungwe tarehe 13 Novemba 2026, ikiwa ni hatua ya tahadhari kutokana na utabiri wa hali ya hewa.

Waraka huo umeelekeza kuwa uamuzi huo unaanza kutumika rasmi kuanzia Oktoba 1, 2026.

Wizara imetoa waraka huo kwa wadau mbalimbali wa elimu, wakiwemo TAMONGSCO, Christian Social Services Commission (CSSC), BAKWATA, Tanzania Association of Private Investors in Education (TAPIE), Baraza la Sunnar Tanzania (BASUTA), TEN/MET, TAWOSCO pamoja na Umoja wa Wazazi wa CCM.

Muhimbili Yafanya Mapinduzi ya Huduma za Mama na Mtoto – Video

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Delilah Kimambo.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewekeza Sh1.8 bilioni katika ujenzi na uboreshaji wa jengo pamoja na miundombinu ya chumba cha kisasa cha upasuaji wa uzazi (Modular Theatre) kwa ajili ya huduma za mama na mtoto.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Delilah Kimambo, amesema uwekezaji huo umehusisha ujenzi na uboreshaji wa miundombinu pamoja na uwekaji wa vifaa tiba vya kisasa katika vyumba vya upasuaji kwa ajili ya wajawazito na watoto.

Akizungumza na Global TV, Dkt. Kimambo leo Oktoba 2, 2026 amesema uwekezaji huo unalenga kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto, kupunguza muda wa kusubiri huduma pamoja na kusaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga.

Amesema vyumba hivyo vimewekewa vifaa tiba vinavyokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa na ubobezi kwa wajawazito na watoto.

Watangazaji wa Global TV na Global Radio Elvan Sitambuli (kushoto) na Godfrey Nathan (kulia) wakiongea na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Dkt. Delilah Kimambo (katikati).

Mtoto Atatibiwa Akiwa Tumboni
Dkt. Kimambo amesema moja ya huduma mpya zitakazopatikana ni Fetal Maternal Medicine, inayowezesha mtoto kutambuliwa na kufuatiliwa akiwa bado tumboni mwa mama.

Kwa mujibu wa Dkt. Kimambo, huduma hiyo itawezesha wataalamu kubaini mapema matatizo mbalimbali yanayoweza kuhatarisha maisha ya mama na mtoto na kuchukua hatua kabla ya kujifungua.

β€œChumba hiki kinaleta huduma mpya na ya kipekee nchini ambapo mtoto sasa anaweza kutambuliwa kama mgonjwa, kufuatiliwa, na kupata matibabu au upasuaji akiwa bado tumboni mwa mama yake kabla hajazaliwa,” amesema.

Ametaja baadhi ya hali zinazoweza kufuatiliwa kwa karibu kuwa ni pamoja na ujauzito unaohusisha kisukari, selimundu, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha changamoto za kiafya zinagundulika mapema na hatua stahiki zinachukuliwa ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Mfumo Mpya wa Oksijeni
Mbali na huduma hizo, Dkt. Kimambo amesema MNH imeweka pia mfumo wa gesi ya oksijeni ambao utasaidia kupunguza utegemezi wa mitungi ya oksijeni katika baadhi ya maeneo ya hospitali.

Amesema mfumo huo utawezesha oksijeni kufikishwa moja kwa moja kwenye wodi na vyumba vya upasuaji, tofauti na utaratibu wa awali uliotegemea mitungi ya gesi.

Mradi huo ulizinduliwa rasmi Septemba 30, 2026, sambamba na uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ambaye alishiriki katika uzinduzi wa vyumba hivyo vya kisasa.

STORI NA ELVAN SITAMBULI | GPL

Paka na Panya Wapeleka Msisimko Mpya Kwenye Cat ’n’ Rat

Global Publishers
October 2, 2026
48 views
0 Comments

Umeshawahi kuona mchezo ambao paka na panya wanaweza kufanya kila mzunguko uwe ya kusisimua? Sasa hilo limewezekana kupitia Cat ’n’ Rat, mchezo mpya wa sloti kutoka GameArt unaopatikana kwenye Meridianbet. Kuanzia sasa hadi Oktoba 13, 2026, kipindi cha utangulizi kinakupa nafasi ya kuingia kwenye ulimwengu huu wa paka na panya, ambapo kila mzunguko unaweza kufungua mlango wa tukio jipya.

Mchezo huu unaanza kwa urahisi lakini unaendelea kufungua vipengele kadri unavyocheza. Ukipata alama tisa zinazolingana, Card Reveal inafunguka. Ukipata Scatter tatu kwenye gridi ya 3Γ—3, unaingia kwenye mizunguko ya bure yenye nafasi ya hadi mizunguko 25 ya bure. Hapo ndipo safari ya kweli inaanza.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwenye mizunguko ya bure, Dead Cat anaweza kutanuka kwenye reel nzima. Uwezo huo unamruhusu kuchukua nafasi ya alama nyingine na kusaidia kukamilisha mstari wa ushindi. Lakini panya naye ana siri yake. Rancid Rat huleta vizidishi vinavyoweza kuongeza thamani ya mchanganyiko unaoshinda pale anapotokea pamoja na mchanganyiko wenye ushindi.

Na kama Scatter nyingine zitatokea wakati wa mizunguko ya bure, mizunguko inaweza kuongezwa tena. Hii inamaanisha unaweza kuendelea na mizunguko ya bonasi kwa muda mrefu zaidi, huku vizidishi vikiendelea kutoa msisimko kwenye safari.

Kwa hiyo, kama unatafuta burudani mpya ya sloti, Cat ’n’ Rat inakusubiri Meridianbet. Kipindi cha utangulizi kinaendelea hadi Oktoba 13, 2026, na hii ni nafasi ya kumjua Dead Cat na Rancid Rat kabla ya wengine.

Β 

Zidane Akutana na Mtihani Mzito, Ufaransa Yakabiliana na Italia

Je unajua kuwa kuna watu wameweza kubadili maisha yao kwa dau dogo kabisa la shilingi mia tano?. Huenda leo ikawa ni nafasi yako na wewe na unachotakiwa kufanya ni kutengeneza jamvi lako na ubeti sasa.

Kundi A, kutakuwa na mechi ya kukata na shoka k

ati ya Ufaransa dhidi ya Italia moja ya mechi kubwa katika hatua ya makundi ya UEFA Nations League. Ufaransa imeanza vyema chini ya kocha mpya Zinedine Zidane, ikiwa imeshinda mechi zake mbili za kwanza dhidi ya Uturuki na Ubelgiji kwa matokeo ya 1-0. Italia nayo imeonyesha dalili za kuimarika, hasa baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Uturuki.

Bado Ufaransa iaendelea kumkosa nahodha wake Kylian MbappΓ©, ambaye alipata jeraha baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Uturuki. Hata hivyo, kikosi cha Zidane kina kina kikubwa cha vipaji, huku Ousmane DembΓ©lΓ©, Michael Olise, Bradley Barcola na DΓ©sirΓ© DouΓ© wakiwa na uwezo wa kuleta tofauti katika eneo la mwisho.

Italia, chini ya Roberto Mancini, inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na matumaini baada ya kuifunga Uturuki 4-1. Mancini amefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi, akiwapa nafasi wachezaji wapya kadhaa kama sehemu ya kujenga timu mpya baada ya kipindi kigumu cha kutofuzu Kombe la Dunia.

Pesa ipo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Italia inaweza kujaribu kutumia nguvu na nidhamu ya Sandro Tonali, Davide Frattesi na NiccolΓ² Fagioli, huku Ufaransa ikiwa na uwezo wa kuvunja mistari kupitia kasi na ubunifu wa viungo na mawinga wake.

Kwa ujumla, Ufaransa inaonekana kuwa na faida kutokana na kucheza nyumbani, kina cha kikosi na mwanzo mzuri wa Zidane, lakini Italia imeonyesha kwamba inaweza kufunga mabao mengi ikiwa itaachiwa nafasi. Hivyo, siioni kama mechi rahisi kwa Ufaransa.

Nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi wanapewa Ufaransa kutokana na kiwango chao ambacho wanacho. Je nani unampa nafasi ya kushinda?. Beti hapa.

Kivumbi kitawaka kwenye mechi ya Ubelgiji dhidi ya Uturuki kwenye michuano ya UEFA Nations League huku tofauti yao hadi sasa ni pointi 3 mpaka sasa kwani Uturuki mpaka sasa hawajashinda mechi yoyote kwenye mbili walizocheza.

Ubelgiji wamekusanya pointi 3 baada ya kuifunga Italia huku leo hii pia wanahitaji ushindi ili kuweza kukaa kwenye nafasi nzuri. Uturuki, kwa upande mwingine, imepoteza mechi zote mbili 1-0 dhidi ya Ufaransa na 4-1 dhidi ya Italia hivyo presha ipo zaidi kwa upande wao. Jisajili hapa.

Kama inavyojulikana kila timu huwa ina mchezaji au wachezaji muhimu zaidi ambao huamua matokeo na kwa upande wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne bado ni mhimili, huku nguvu yao ikiwa kwenye uwezo wa kutawala mpira na kutengeneza nafasi kupitia safu ya kiungo na pembeni.

Timu hiyo pia inaonekana kuwa na ubora zaidi katika kumalizia nafasi, jambo ambalo linaweza kuwa tatizo kwa Uturuki ambayo imefunga bao moja pekee katika mechi mbili za kwanza za Nations League.

Licha ya kupoteza mechi zote mbili, Uturuki sio timu ya kudharauliwa na Arda GΓΌler ndiye mchezaji anayetarajiwa kuleta ubunifu na kasi katika mashambulizi. Tatizo kubwa kwa Uturuki ni kwamba safu yao ya ulinzi ilionekana dhaifu sana dhidi ya Italia, na dhidi ya Ubelgiji kosa kama hilo linaweza kuigharimu zaidi.

Mara ya mwisho kuonana ilikuwa ni 2011 na hakuna ambaye alikuwa mbabe kati yao. Je leo hii nani kuondoka na ushindi?. Suka jamvi hapa.

Ajali ya Helikopta ya Wicknell Chivayo Mambo Mapya Yafichuliwa

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Zimbabwe (CAAZ) imetoa taarifa za awali kuhusu ajali ya helikopta iliyosababisha kifo cha mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, mke wake Lucy Muteke β€˜Lulu’  pamoja na watu wengine waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, helikopta hiyo iliondoka Gandami, Chikomba, eneo ambalo Chivayo na mke wake walikuwa wakijenga nyumba yao ya kijijini.

Helikopta hiyo ilianguka katika eneo la Kudenga Farm, takribani dakika 40 baada ya kuondoka. Ajali hiyo ilitokea Septemba 30, 2026, majira ya saa 11 jioni kwa saa za Zimbabwe.

CAAZ YAFICHUA KILICHOTOKEA ENEO LA AJALI

Mkurugenzi Mkuu wa CAAZ, George Mashababe, amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mafuta yalivuja baada ya helikopta kugonga chini, kabla ya moto kuzuka na kuteketeza nyasi katika eneo la ajali.

β€œMatokeo ya awali yanaonyesha kuwa mafuta yalivuja wakati wa athari, na kufuatiwa na moto ulioteketeza nyasi katika eneo la ajali,” amesema Mashababe.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imesisitiza kuwa bado haijabaini chanzo kilichosababisha helikopta hiyo kuanguka.

MASWALI YAIBUKA MITANDAONI

Taarifa hizo za awali zimeibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watumiaji wakieleza wasiwasi kuhusu kasi ya kutolewa kwa taarifa za uchunguzi.

Baadhi yao wameibua madai ya uwezekano wa huwa kuna jambo jingine lililosababisha ajali hiyo, lakini hadi sasa hakuna ushahidi rasmi uliotolewa na mamlaka unaothibitisha madai hayo.

CAAZ bado inaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo ili kubaini chanzo chake na mazingira yote yaliyosababisha helikopta hiyo kuanguka.