Zidane Akutana na Mtihani Mzito, Ufaransa Yakabiliana na Italia

Je unajua kuwa kuna watu wameweza kubadili maisha yao kwa dau dogo kabisa la shilingi mia tano?. Huenda leo ikawa ni nafasi yako na wewe na unachotakiwa kufanya ni kutengeneza jamvi lako na ubeti sasa.

Kundi A, kutakuwa na mechi ya kukata na shoka k

ati ya Ufaransa dhidi ya Italia moja ya mechi kubwa katika hatua ya makundi ya UEFA Nations League. Ufaransa imeanza vyema chini ya kocha mpya Zinedine Zidane, ikiwa imeshinda mechi zake mbili za kwanza dhidi ya Uturuki na Ubelgiji kwa matokeo ya 1-0. Italia nayo imeonyesha dalili za kuimarika, hasa baada ya ushindi wa 4-1 dhidi ya Uturuki.

Bado Ufaransa iaendelea kumkosa nahodha wake Kylian Mbappé, ambaye alipata jeraha baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya Uturuki. Hata hivyo, kikosi cha Zidane kina kina kikubwa cha vipaji, huku Ousmane Dembélé, Michael Olise, Bradley Barcola na Désiré Doué wakiwa na uwezo wa kuleta tofauti katika eneo la mwisho.

Italia, chini ya Roberto Mancini, inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na matumaini baada ya kuifunga Uturuki 4-1. Mancini amefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi, akiwapa nafasi wachezaji wapya kadhaa kama sehemu ya kujenga timu mpya baada ya kipindi kigumu cha kutofuzu Kombe la Dunia.

Pesa ipo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Italia inaweza kujaribu kutumia nguvu na nidhamu ya Sandro Tonali, Davide Frattesi na Niccolò Fagioli, huku Ufaransa ikiwa na uwezo wa kuvunja mistari kupitia kasi na ubunifu wa viungo na mawinga wake.

Kwa ujumla, Ufaransa inaonekana kuwa na faida kutokana na kucheza nyumbani, kina cha kikosi na mwanzo mzuri wa Zidane, lakini Italia imeonyesha kwamba inaweza kufunga mabao mengi ikiwa itaachiwa nafasi. Hivyo, siioni kama mechi rahisi kwa Ufaransa.

Nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi wanapewa Ufaransa kutokana na kiwango chao ambacho wanacho. Je nani unampa nafasi ya kushinda?. Beti hapa.

Kivumbi kitawaka kwenye mechi ya Ubelgiji dhidi ya Uturuki kwenye michuano ya UEFA Nations League huku tofauti yao hadi sasa ni pointi 3 mpaka sasa kwani Uturuki mpaka sasa hawajashinda mechi yoyote kwenye mbili walizocheza.

Ubelgiji wamekusanya pointi 3 baada ya kuifunga Italia huku leo hii pia wanahitaji ushindi ili kuweza kukaa kwenye nafasi nzuri. Uturuki, kwa upande mwingine, imepoteza mechi zote mbili 1-0 dhidi ya Ufaransa na 4-1 dhidi ya Italia hivyo presha ipo zaidi kwa upande wao. Jisajili hapa.

Kama inavyojulikana kila timu huwa ina mchezaji au wachezaji muhimu zaidi ambao huamua matokeo na kwa upande wa Ubelgiji, Kevin De Bruyne bado ni mhimili, huku nguvu yao ikiwa kwenye uwezo wa kutawala mpira na kutengeneza nafasi kupitia safu ya kiungo na pembeni.

Timu hiyo pia inaonekana kuwa na ubora zaidi katika kumalizia nafasi, jambo ambalo linaweza kuwa tatizo kwa Uturuki ambayo imefunga bao moja pekee katika mechi mbili za kwanza za Nations League.

Licha ya kupoteza mechi zote mbili, Uturuki sio timu ya kudharauliwa na Arda Güler ndiye mchezaji anayetarajiwa kuleta ubunifu na kasi katika mashambulizi. Tatizo kubwa kwa Uturuki ni kwamba safu yao ya ulinzi ilionekana dhaifu sana dhidi ya Italia, na dhidi ya Ubelgiji kosa kama hilo linaweza kuigharimu zaidi.

Mara ya mwisho kuonana ilikuwa ni 2011 na hakuna ambaye alikuwa mbabe kati yao. Je leo hii nani kuondoka na ushindi?. Suka jamvi hapa.

Ajali ya Helikopta ya Wicknell Chivayo Mambo Mapya Yafichuliwa

Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Zimbabwe (CAAZ) imetoa taarifa za awali kuhusu ajali ya helikopta iliyosababisha kifo cha mfanyabiashara maarufu wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, mke wake Lucy Muteke ‘Lulu’  pamoja na watu wengine waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, helikopta hiyo iliondoka Gandami, Chikomba, eneo ambalo Chivayo na mke wake walikuwa wakijenga nyumba yao ya kijijini.

Helikopta hiyo ilianguka katika eneo la Kudenga Farm, takribani dakika 40 baada ya kuondoka. Ajali hiyo ilitokea Septemba 30, 2026, majira ya saa 11 jioni kwa saa za Zimbabwe.

CAAZ YAFICHUA KILICHOTOKEA ENEO LA AJALI

Mkurugenzi Mkuu wa CAAZ, George Mashababe, amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa mafuta yalivuja baada ya helikopta kugonga chini, kabla ya moto kuzuka na kuteketeza nyasi katika eneo la ajali.

“Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa mafuta yalivuja wakati wa athari, na kufuatiwa na moto ulioteketeza nyasi katika eneo la ajali,” amesema Mashababe.

Hata hivyo, mamlaka hiyo imesisitiza kuwa bado haijabaini chanzo kilichosababisha helikopta hiyo kuanguka.

MASWALI YAIBUKA MITANDAONI

Taarifa hizo za awali zimeibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii, huku baadhi ya watumiaji wakieleza wasiwasi kuhusu kasi ya kutolewa kwa taarifa za uchunguzi.

Baadhi yao wameibua madai ya uwezekano wa huwa kuna jambo jingine lililosababisha ajali hiyo, lakini hadi sasa hakuna ushahidi rasmi uliotolewa na mamlaka unaothibitisha madai hayo.

CAAZ bado inaendelea na uchunguzi wa ajali hiyo ili kubaini chanzo chake na mazingira yote yaliyosababisha helikopta hiyo kuanguka.

Umeme chachu maendeleo ya kiuchumi – HabariLeo

DAR ES SALAAM: MAKAMU wa Rais, Deogratius Ndejembi, amesema Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Benki ya CRDB, utarahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi wa mijini na vijijini na kuongeza fursa za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akizungumza leo Oktoba 2, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya utiaji saini na uzinduzi wa mpango huo, Ndejembi amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Misheni 300, unaolenga kuhakikisha hadi mwaka 2030 wananchi milioni 300 barani Afrika wanafikiwa na nishati ya umeme.

Amesema kupitia mpango huo, wananchi wanaostahili watanufaika na utaratibu wa kugharamiwa gharama za uunganishaji umeme, hatua inayotarajiwa kuongeza kasi ya kufikisha huduma hiyo kwa kaya takribani milioni 1.7 kwa mwaka, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Nishati (National Energy Compact).

“Ninaipongeza TANESCO na Benki ya CRDB kwa hatua hii muhimu ya kuanzisha ushirikiano unaolenga kumrahisishia mwananchi kupata huduma ya umeme. Ushirikiano huu ni mfano bora wa namna taasisi za umma na sekta binafsi zinavyoweza kuunganisha nguvu na rasilimali ili kutatua changamoto zinazowagusa wananchi moja kwa moja,” amesema Ndejembi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, Dk. Juma Homera, amesema ushirikiano huo kati ya Serikali na sekta binafsi utawezesha wananchi kunufaika zaidi na uwekezaji unaofanywa na Serikali katika kuhakikisha huduma ya umeme inawafikia.

Naye, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Balozi Zuhura Bundala, amesema mpango huo unaakisi juhudi za Serikali katika kuweka mazingira wezeshi ya kukuza fursa za kiuchumi na kijamii kupitia nishati ya umeme.

“Tunatarajia mpango huu uweze kuwafikia wananchi wengi, ambao tunaamini watanufaika na fursa mbalimbali ikiwemo ajira, uzalishaji, biashara na kuwezesha mazingira bora katika sekta ya elimu,” amesema Balozi Bundala.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Lazaro Twange, amesema awamu ya kwanza ya mpango huo inalenga maeneo ya vijijini, ambapo Benki ya CRDB itawezesha Sh27,000 kwa kila kaya inayostahili, fedha ambazo zitalipwa moja kwa moja kwa TANESCO kama gharama za uunganishaji umeme bila mwananchi kuwa na wajibu wa kuzirejesha.

Amesema kwa wananchi wa mijini na pembezoni mwa miji, CRDB itawezesha upatikanaji wa fedha kupitia mikopo nafuu, ambayo italipwa kwa utaratibu utakaowekwa na benki hiyo.

“Mpaka sasa TANESCO ina takribani wateja milioni 6.4, lakini kupitia mpango huu wa ushirikiano tunatarajia idadi ya wateja itaongezeka na kufikia lengo la kuunganisha kaya milioni 1.7 kwa mwaka,” amesema Twange.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Abdulmajid Nsekela, amesema benki hiyo imetenga Sh bilioni moja kila mwaka kwa ajili ya mpango huo na kwa kushirikiana na TANESCO itaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kutumia fursa hiyo katika kukuza shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Kupitia Mpango wa Kitaifa wa Nishati, Tanzania inalenga kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme kutoka asilimia 78.4 hadi asilimia 100, huku kiwango cha wananchi waliounganishwa na umeme kikilenga kuongezeka kutoka asilimia 46 hadi asilimia 75 ifikapo mwaka 2030.

Makamu wa Rais Aitaka TANESCO Kuwezesha Wananchi Kupata Umeme kwa Mkopo

Global Publishers
October 2, 2026
0 views
0 Comments

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameiagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa kushirikiana na sekta binafsi, kuandaa mpango utakaowawezesha wananchi kununua umeme kwa mkopo wakati wanapokuwa hawana fedha.

Makamu wa Rais ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa uzinduzi wa Mpango wa Ufadhili wa Uunganishaji Umeme kwa Wananchi kati ya TANESCO na Benki ya CRDB.

Amesema mpango huo wa ununuzi wa umeme kwa mkopo unaweza kuwa na mfumo unaofanana na huduma za mikopo inayopatikana kwenye mitandao ya simu, ili mwananchi anapohitaji umeme lakini hana fedha aweze kupata huduma hiyo na kulipa baadaye.

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, hatua hiyo itasaidia wananchi kuendelea kutumia umeme kwa shughuli za uzalishaji mali pamoja na mahitaji ya majumbani, hasa pale wanapokabiliwa na changamoto za kifedha.

Aidha, ameitaka Wizara ya Nishati kupitia TANESCO kuendeleza mpango wa kuwaunganisha kwa gharama ya Shilingi 27,000 wananchi wanaoishi katika maeneo yenye mazingira ya kijijini, lakini kutokana na mipaka ya kiutawala wanatambulika kuwa wanaishi mijini.

Amesema kuna maeneo ambayo wananchi wake wanatenganishwa na mipaka ya kiutawala pekee, huku hali zao za maisha zikifanana, hivyo wanapaswa kupata huduma ya umeme kwa gharama inayozingatia mazingira yao ya maisha.

Makamu wa Rais amesema hatua hizo ni sehemu ya juhudi za kufikia malengo ya kitaifa, ikiwemo Mission 300 na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, kwa kuhakikisha Watanzania wanapata huduma ya umeme kwa gharama nafuu.

Katika hafla hiyo, Makamu wa Rais ameipongeza TANESCO na Benki ya CRDB kwa kuingia katika mpango huo, akisema una lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme na hatimaye kuchangia katika kuboresha maisha ya wananchi.

Jihan Awashukuru Watanzania Baada ya Tanzania Kuingia Top 4

Global Publishers
October 2, 2026
6 views
0 Comments

Mlimbwende wa Tanzania katika mashindano ya Miss Grand International 2026, Jihan Mohin Dimack, amewashukuru Watanzania kwa kumpa sapoti kubwa iliyoiwezesha Tanzania kuingia katika Top 4 ya tuzo ya “Country Powerhouse of the Year”.

Jihan amesema mafanikio hayo si yake binafsi, bali ni matokeo ya mshikamano wa Watanzania waliopiga kura, kushiriki machapisho, kuhamasisha wengine na kuendelea kumpa moyo katika safari yake ya kuiwakilisha Tanzania kimataifa.

Akizungumza baada ya Tanzania kufanikiwa kuingia Top 4, Jihan amesema amejawa na furaha na shukrani, akieleza kuwa kila kura na kila juhudi iliyofanywa na Watanzania imekuwa sehemu muhimu ya safari yake.

“Huenda ni mimi ninayesimama hapa leo, lakini mafanikio haya yana sehemu ya kila mmoja wenu,” amesema Jihan.

Mlimbwende huyo ametoa shukrani zake kwa Watanzania kwa maneno mbalimbali, akiwashukuru kwa kumpokea, kumpenda, kumuamini na kumuunga mkono katika safari yake ya Miss Grand International 2026.

Jihan amesema hatua hiyo imeonyesha nguvu ya umoja wa Watanzania, akisisitiza kuwa kutoka Tanzania hadi kwenye jukwaa la kimataifa, wameweza kuonyesha kwamba mshikamano unaweza kuleta matokeo makubwa.

Kwa upande wake, Jihan ameendelea kuhamasisha Watanzania kuendelea kuwa sehemu ya safari yake huku akitambua mchango wa kila mmoja aliyeshiriki kuhakikisha Tanzania inafika katika hatua hiyo.

MAKATIBU WAKUU WAKAGUA AICC MAANDALIZI YA MWISHO MKUTANO WA IPU, ARUSHA

Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefanya ukaguzi wa mwisho wa maandalizi ya mkutano huo leo Oktoba 02, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Ukaguzi huo uliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Bi. Christine Mwakatobe ambapo

walikagua miundombinu muhimu ikiwemo ukumbi mkuu wa mikutano, kumbi za vikao vya pembeni, Ofisi za Viongozi, mifumo ya sauti na tafsiri, eneo la waandishi wa habari, pamoja na maeneo ya mapokezi ya wageni.

Baada ya ukaguzi huo, Makatibu Wakuu waliiagiza Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya mkutano huo kumalizia maandalizi ya baadhi ya sehemu ambazo zinafanyiwa marekebisho na maboresho ya mwisho kabla ya kuanza kwa mkutano huo Oktoba 04 hadi 09, 2026.

Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki 2,000 kutoka Mabunge 183 wanachama wa IPU ambao ni Maspika, Wabunge, Makatibu na Maafisa mbalimbali.

Dunia inakuja Tanzania, Tuipe sababu ya kurudi tena.

 

Rais Mwinyi Kuzungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Zanzibar Kesho

Global Publishers
October 2, 2026
0 views
0 Comments

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kesho, Oktoba 3, 2026, kuanzia saa 5:00 asubuhi katika Ikulu Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu Zanzibar leo, Oktoba 2, 2026, mkutano huo utarushwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari, ikiwemo televisheni na mitandao ya kijamii, ili kuwawezesha wananchi kufuatilia moja kwa moja.

Taarifa hiyo imetolewa na Raqey Mohamed, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu.

VETA, BGC kushirikiana kukuza ujuzi – HabariLeo

GEITA; Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), ipo katika mazungumzo na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Buckreef (BGC) ya Katoro, Geita, kwa lengo la kukuza ushirikiano utakaoandaa nguvu kazi mahiri kwa ajili ya sekta ya madini.
‎
‎Akizungumza katika kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa kampuni hiyo Oktoba 1, 2026, Meneja wa VETA Kanda ya Kaskazini, Monica Mbelle, amesema ushirikiano huo unatarajiwa kutoa fursa za mafunzo kwa vitendo kwa wakufunzi na wanafunzi wa VETA pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi wa kampuni hiyo.
‎
‎”Tumezungumza na uongozi wa Buckreef kuona namna tunavyoweza kushirikiana, ikiwemo kuleta wanafunzi wetu wanaosoma fani mbalimbali ili wapate mafunzo kazini, mafunzo haya yatasaidia kukomaza ujuzi wao katika stadi wanazojifunza,” amesema Mbelle.
‎
‎Ameongeza kuwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia, VETA imeomba nafasi za mafunzo kwa wakufunzi wake ili waweze kupata ujuzi mpya na kutoa mafunzo yanayoendana na mahitaji ya sasa ya soko la ajira.
‎
‎Aidha, Mbelle amesema VETA itashirikiana na Buckreef kuhakikisha wananchi wanaozunguka mgodi huo wanapata mafunzo ya ufundi stadi yatakayofadhiliwa na kampuni hiyo.


‎
‎”Buckreef wameona kuwa sisi VETA tunaweza kutoa ujuzi kwa vijana wa maeneo haya, na sisi tumeona jinsi tutakavyoandaa programu za kuwawezesha vijana wanaozunguka eneo la mgodi kupata ujuzi katika stadi mbalimbali,” amefafanua.
‎
‎Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa mgodi huo, Isaac Bisansaba, amewataka wananchi wanaozunguka mgodi huo kujiandaa kunufaika na fursa zitakazotokana na ushirikiano huo.

 


‎
‎”Tayari tumeanza mchakato wa kuwatambua vijana waliomaliza kidato cha sita, kidato cha nne au hata wale ambao hawakufaulu kwa viwango vya juu, ili tuwasaidie kujiunga na vyuo vya VETA kwa kulipia sehemu ya gharama za mafunzo yao na baadaye kuwapa nafasi za mafunzo kwa vitendo mgodini kwetu,” amesema Bisansaba.

MAWAKALA WA UTALII KUTOKA INDIA WAVUTIWA NA HIFADHI ZA NGORONGORO NA SERENGETI

Mawakala wa utalii kutoka Jamhuri ya India wameelezea kuridhishwa na kuvutiwa na uzuri  wa Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kufuatia ziara ya mafunzo (Fam Trip) iliyoandaliwa na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa kushirikina na Ubalozi wa Tanzania Nchini India

Ziara hiyo yenye lengo la kuitangaza Tanzania katika soko la kimataifa la utalii, imewajumuisha mawakala 13  kutoka majiji mbalimbali ya India.

Wakizungumza mara baada ya ziara katika hifadhi ya  Kreta ya Ngorongoro iliyotangazwa kama Ajabu ya Nane ya Dunia, walisema Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vya utalii vya kipekee duniani.

“Tumetembea nchi nyingi duniani, lakini kile tulichokiona hapa Ngorongoro ni cha tofauti sana. Muunganiko wa mandhari ya kuvutia, wingi wa wanyamapori katika eneo moja na uhifadhi uliotukuka ni jambo linaoonesha upekee wake, Hakika hii ni sehemu ambayo kila Mhindi anatakiwa kuja kuiona angalau mara moja maishani mwake,”

Kwa upande wa Serengeti, mawakala hao walipata fursa ya kushuhudia moja ya maajabu makubwa ya wanyamapori duniani, yakiwemo maelfu ya nyumbu na pundamilia katika harakati za uhamaji, pamoja na wanyama wakubwa watano (Big Five).

Mmoja wa mawakala hao  alisema Serengeti imezidi matarajio yao.

“Tulikuwa tumesikia mengi kuhusu Serengeti kwenye filamu, lakini kuiona kwa macho yetu wenyewe ni hisia tofauti kabisa. Ni mbuga kubwa, ya asili na iliyohifadhiwa vizuri. Tuliona simba, chui na tembo kwa ukaribu. Huduma za malazi na ukarimu wa Watanzania ni wa hali ya juu,” alieleza.

Naye Afisa Masoko wa TTB Bwana  Michael Ndaisaba alisema soko la India ni muhimu na linaendelea kukua kwa kasi, ambapo Ujio wa mawakala hao utachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza idadi ya watalii kutoka Bara la Asia.

Ziara ya mawakala hao inatarajiwa kuhitimishwa jijini Zanzibar kwa kutembelea vivutio vya utalii wa fukwe na utamaduni.

 

Kituo kipya kuongeza huduma za meno – HabariLeo

DAR ES SALAAM: Huduma za afya ya kinywa nchini zinatarajiwa kuimarika baada ya Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam kuzindua kituo maalumu cha huduma za meno na vipandikizi vya meno, katika hatua inayolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kibingwa.

Kituo hicho kimejengwa kwa uwekezaji wa Sh bilioni 1.3 na kina vyumba sita vya kisasa vyenye vifaa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za meno, ikiwemo huduma za vipandikizi.

Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Emmanuel Tayari, amesema uwekezaji huo unaonesha umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuboresha huduma za afya nchini.

Amesema sekta binafsi ina mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za afya, ambapo takribani asilimia 85 ya huduma za afya katika Mkoa wa Dar es Salaam hutolewa na sekta hiyo, huku katika huduma za afya ya kinywa ikifikia asilimia 70.

Tayari amesema Serikali imeendelea kuwekeza katika huduma za afya ya kinywa kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa vya kisasa, radiolojia ya meno kwa njia ya kidijitali pamoja na kuboresha miundombinu ya huduma hizo.

Amesema mkazo pia umewekwa katika kinga, utambuzi wa mapema na matibabu kwa wakati ili kupunguza hali ya wagonjwa kusubiri hadi kung’oa jino kuwa suluhisho pekee.

Aidha, amesema ushirikiano kati ya mifumo ya bima ya afya na hospitali binafsi unaendelea kuimarika, akitolea mfano Hospitali ya Aga Khan ambayo hivi karibuni ilisaini mkataba na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wa kuendelea kutoa huduma kwa wanachama wa mfuko huo.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Profesa Muzdalifat Abeid, amesema uwekezaji huo ni sehemu ya mkakati wa kuongeza huduma maalumu za afya zenye viwango vya juu, kwa lengo la kupunguza idadi ya Watanzania wanaosafiri nje ya nchi kutafuta matibabu.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya, Utafiti wa Kitaifa wa Afya ya Kinywa wa mwaka 2020 ulionesha kuwa asilimia 76 ya Watanzania watu wazima waliathiriwa na tatizo la kuoza kwa meno, huku asilimia 52 wakiwa na ugonjwa wa fizi.

Aidha, hadi Julai 2025, ni asilimia 42 pekee ya vituo vya afya vya umma vilivyokuwa vikitoa huduma za afya ya kinywa, hali inayoonesha umuhimu wa kuongeza uwekezaji na upatikanaji wa huduma hizo.