NYANYA GEITA ZAFUNGUA FURSA ZA AJIRA NA BIASHARA, AGITF YATOA MIKOPO KWA WAKULIMA

 

Soko la nyanya mkoani Geita limeendelea kuwa na fursa kubwa, huku wafanyabiashara kutoka Rwanda wakifika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kununua zao hilo, hali inayowapa fursa wakulima na vijana kujikita katika kilimo cha kibiashara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitalu cha miche ya mbogamboga cha Raha Farms, Katoro, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, amesema kilimo ni sekta muhimu kwa uchumi na kuwataka vijana kutumia fursa zinazotolewa na Serikali, ikiwemo mikopo ya pembejeo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Udhamini wa Pembejeo za Kilimo, AGITF, Mwanahiba Mzee, amesema mfuko huo umejikita katika kuwawezesha wakulima wadogo kupata pembejeo kwa masharti nafuu, ikiwemo mikopo ya moja kwa moja kwa riba ya asilimia nne kwa mwaka kwa vijana na wanawake.

Naye Mkurugenzi wa Raha Farms, Raha Aloyce, amesema ushirikiano na AGITF umewezesha kampuni hiyo kuongeza uzalishaji pamoja na ajira, kutoka wafanyakazi watano hadi kufikia 125.

Amesema kampuni hiyo sasa imejikita pia katika uzalishaji wa miche bora ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili wakulima katika upatikanaji wa mbegu na miche yenye ubora.

Uzinduzi huo unalenga kuongeza upatikanaji wa miche bora ya mazao ya mbogamboga na kuwapa wakulima, hususan vijana, fursa ya kuongeza uzalishaji na kipato kupitia kilimo cha kibiashara.

Khamenei Azitaka Nchi Za Kiislamu Kuungana Dhidi Ya Marekani Na Israel – Video

Global Publishers
August 30, 2026
12 views
0 Comments

Kiongozi Mkuu wa Iran, Mojtaba Khamenei, amezitaka nchi za Kiislamu kuungana dhidi ya Marekani na Israel, akizitaja nchi hizo mbili kuwa ni maadui wa ulimwengu mzima wa Kiislamu.

Katika ujumbe uliochapishwa na Shirika la Habari la Iran (IRNA), Khamenei ametoa wito kwa mataifa ya Kiislamu kutambua kile alichokiita kuwa ni “adui wao wa kweli” na kuchukua hatua za kuzuia mipango yake.

Kauli hiyo imekuja wakati mvutano kati ya Iran, Marekani na Israel ukiendelea kuwa mkubwa, huku Tehran ikisisitiza umuhimu wa mshikamano miongoni mwa nchi za Kiislamu.

Khamenei hajawa akionekana hadharani tangu alipoteuliwa kuwa Kiongozi Mkuu wa Iran mwezi Machi, na hivyo ujumbe huo kuwa miongoni mwa taarifa zake chache zilizotolewa hadharani tangu achukue nafasi hiyo.

Wakati huo huo, meli ya kivita ya Marekani, USS Abraham Lincoln, imepita nchini Singapore ikiwa njiani kurejea Marekani baada ya kukamilisha operesheni ya muda mrefu katika Mashariki ya Kati.

Meli hiyo inatarajiwa kusimama nchini Thailand kwa mapumziko kabla ya kuendelea na safari yake kuelekea kituo chake cha kijeshi nchini Marekani.

Mashabiki, Wasanii Wamwaga Pongezi Kwa Maua Sama Baada Ya Picha Za Ujauzito

Global Publishers
August 30, 2026
48 views
0 Comments

Msanii wa muziki wa Tanzania, Maua Sama, amezua furaha miongoni mwa mashabiki na mastaa mbalimbali baada ya kushiriki picha na video zinazomuonesha akiwa na ujauzito.

Maua Sama alishiriki picha na video hizo kupitia mitandao yake ya kijamii na kuandika ujumbe mfupi wa shukrani akisema, “I’m Grateful Alhamdulillah ❤️.”

Baada ya chapisho hilo, sehemu ya mastaa mbalimbali waliingia kwenye maoni na kumpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo mpya ya maisha.

Msanii Jux aliandika, “Hongera sana,” huku Chege akisema, “Baraka za kutosha 🙏.”

Kwa upande wake, Dayana Nyange alionesha furaha kubwa na kumuandikia Maua Sama ujumbe wa pongezi akisema:

“Awwwww Kifua nnacho boo 😍😍😍 Anti Nimeweaza👌 Jamaniii hongera sasa Mama kijacho @mauasama Im so Happy for you love🥰❤️🫶.”

Naye Mamama Chanja alionesha mshangao na furaha kupitia ujumbe wake uliosomeka, “WOOOOOOOOOOOOOOOOOOW NIMESHAUTI HAPA JAMANI 🥹🙏🏻🙏🏻🙏🏻.”

Msanii Ammygal pia hakusita kumpongeza Maua Sama kwa kuandika, “Aaaaaaaw😍😍 Congrats Samaaa wangu😍.”

Aidha, Kim Nana alijiunga na mastaa hao kwa kumpongeza Maua Sama na kusema, “Hongera Babe👏👏😍😍.”

Pongezi hizo zimeendelea kuonyesha namna habari hiyo ilivyopokelewa kwa furaha na watu mbalimbali, huku mashabiki wakimtakia Maua Sama safari njema katika hatua hiyo mpya ya maisha.

Chelsea Yaichapa Brighton 4-3 Kwenye Mchezo Wa Kuvutia Stamford Bridge

Chelsea imeendeleza mwanzo wake mzuri katika msimu mpya wa Ligi Kuu England baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Brighton katika mchezo wa kusisimua uliochezwa Uwanja wa Stamford Bridge.

Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa kocha Xabi Alonso mbele ya mashabiki wa Chelsea katika mchezo wa ligi nyumbani, huku Romeo Lavia akiifungia Chelsea bao lake la kwanza tangu alipojiunga na klabu hiyo.

Chelsea ilipata bao la kuongoza ndani ya dakika nne pekee baada ya Brighton kufanya makosa. Mats Wieffer alifanikiwa kuzuia kichwa cha João Pedro kilichotokana na mpira wa kona, lakini kipa Bart Verbruggen akashindwa kuudhibiti mpira na Lavia akautumia mwanya huo kufunga.

Dakika 10 baadaye, Chelsea iliongeza bao la pili. Morgan Rogers alimzidi Luka Vuskovic upande wa kushoto na kupiga krosi iliyomkuta Pedro Neto, ambaye alitangulia mbele ya Ferdi Kadioglu na kuufikisha mpira wavuni.

Chelsea iliendelea kutawala na kupata bao la tatu dakika ya 32. Jorrel Hato alimzidi Wieffer kwa kasi na kumpatia João Pedro, ambaye hakufanya makosa na kuifungia Chelsea bao la tatu dhidi ya klabu yake ya zamani.

Hata hivyo, Brighton haikukata tamaa na ilianza kurejea mchezoni.

Dakika chache kabla ya mapumziko, Brighton ilipata bao la kwanza kupitia Malick Yalcouyé. Kipa wa Chelsea, Emi Martínez, alitoka langoni kujaribu kumzuia Charalampos Kostoulas, lakini mpira uliomrudia Yalcouyé aliupiga kwa vole na kuifanya Brighton kupunguza pengo.

Brighton iliendelea kuisumbua Chelsea mwanzoni mwa kipindi cha pili na dakika ya 63 ikapata bao la pili. Yalcouyé alimpa Pascal Groß pasi, kisha shuti la Groß likagonga mwili wa João Pedro na kubadili mwelekeo na kumshinda Martínez.

Chelsea ilionekana kupata utulivu zaidi dakika ya 74 baada ya Cole Palmer kufunga bao la kuvutia. Palmer alifanya kazi nzuri binafsi kabla ya kupiga shuti lililopinda na kuingia wavuni kutoka nje ya boksi, na kuirudishia Chelsea uongozi wa mabao mawili.

Brighton hata hivyo iliendelea kupambana hadi dakika za mwisho na kupata bao la tatu kupitia Groß, aliyefunga kwa kichwa katika moja ya matukio ya mwisho ya mchezo.

Licha ya presha kubwa ya Brighton katika dakika za mwisho, Chelsea iliweza kulinda ushindi wake na kuondoka na pointi zote tatu baada ya mchezo uliokuwa na mabao saba.

Nafasi za Kazi Wezesha Mzawa Microfinance – Loan Officer, Mwisho wa Maombi Agosti 31, 2026

Global Publishers
August 30, 2026
8,814 views
0 Comments

We are seeking a motivated, experienced Loan officer/ Credit officer to join our growing company. In this position, you will evaluate and approve or deny loan applications. You will act as liaison between financial institutions, individuals, and businesses applying for loans as well as process loan applications, solicit loans, and act as intermediary for creditors and borrowers.

Loan Officer Job Duties:

  • Evaluates loan applications and documentation by confirming credit worthiness.
  • Improves loan applications and documentation by informing applicant of additional requirements.
  • Rejects loans by explaining deficiencies to applicants.
  • Approves loans by issuing checks or forwarding applications to loan committee.
  • Completes loan contracts by explaining provisions to applicant; obtaining signatures and notarizations; collecting fees.
  • Helps customers by answering questions; responding to requests.
  • Maintains customer confidence by keeping loan information confidential.
  • Accomplishes Company mission by completing related results as needed.

Qualification;

  • Bachelor of finance, economics, Marketing, Business, Banking or related field
  • Experience in the relevant field will be an added advantage
  • Proficient computer skills, including Microsoft Office Suite
  • Able to analyze financial records and transfer data

Additional Knowledge, Skills & Abilities

  • Excellent customer service skills, attentiveness, and information retention.
  • Detail oriented, high degree of accuracy.
  • Familiar with banking regulations and responsibilities relating to each including a working.
  • Self-starter, ability to work independently.
  • Strong communication & organizational skills.
  • Competence with computers.
  • Ability to work in a fast-paced environment & under pressure as needed.
  • The ability to make sound decisions. This may include making on-the-spot decisions regarding customer transactions; weighing customer satisfaction issues with the Bank’s exposure to loss or fraud and the ability to think through and rationalize decisions.

All applications should be filed through the following email address or the physical address with necessary certified attachments befor August 31, 2026.

WEZESHA MZAWA MICROFINANCE,

P.O.BOX 7534, SINZA-MORI,

OPPOSITE WANYAMA HOTEL

DAR ES SALAAM, TANZANIA.

EMAIL: [email protected]

Usikose Mechi Za Leo, Dau Dogo Laweza Kukuletea Milioni

Je unajua kuwa ukiwa na dau dogo pia unaweza ukatengeneza jamvi na ukaweza ukajishindia pesa zaidi ya Milioni?. Basi Meridianbet wanasema kuwa nafasi ndio hii, ingia kwenye akaunti yako na ubeti sasa.

Kule Italia, SERIE A itaendelea ambapo Napoli atamenyana dhidi Como 1907 ambao kwenye mechi yao kwanza walitoa sare hivyo huu ni mchezo ambao kwa namna moja au nyingine wanautolea macho sana.

Vijana wa Allegri wao waliondoka na pointi 3 wakiwa ugenini hivyo sasa watarejea pale katika dimba la Armando Maradona kusaka ushindi mwingine mbele ya mashabiki zao ambao wanaamini timu hiyo msimu huu inaweza ikagombea taji la Scudetto.

Takwimu zinaonesha kuwa mara ya mwisho kuonana hawa wawili, hakuna ambaye alikuwa mbabe kati yao na kwenye hizo mechi mbili hakuna ambaye aliweza kuona lango la mwenzake.

Hivyo basi hii mechi ambayo pointi 3 ni muhimu sana kwa wote wawili kwani kama unahitaji uwe kwenye mbio za ubingwa ni vyema ukaanza kupata matokeo mazuri kwenye mechi za mwanzo kabisa. Beti yako unaiweka kwa nani?. Jisajili hapa.

Piga pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

EPL kule ni Manchester United dhidi ya Ipswich Town ambao wamepanda daraja msimu huu kutoka kule ligi daraja la kwaznza wakiwa na matumaini ya kufanya vyema kwenye ligi kuu.

Ikumbukwe kuwa United chini ya Carrick wameanza msimu vibaya sana baada ya kupoteza kwa mabao 2 kwa bili ugenini, hivyo hii mechi yao ya kwanza wakiwa katika dimba la Old Trafford wanahitaji kupata ushindi wao wa kwanza.

Kwa upande wa Ipswich wao walianza vyema ligi kwa kuandikisha ushindi wakiwa nyumbani na sasa watakuwa ugenini kujaribu kupata matokeo chanya mbele ya Mashetani Wekundu. Odds Kubwa zipo mechi hii, hivyo bashiri sasa.

Uwepo wa kikosi kipana cha Man United kinawafanya wapewe nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi huku pia faida ya kuwa nyumbani inapelekea wao kuwa wateule wa ushindi kwenye mchezo wa leo. Je wataweza kujinyakulia pointi 3 siku ya leo?. Tengeneza mkeka wako wa ushindi pale Meridianbet.

Vilevile Meridianbet wanasema mechi nyingine ya pesa ni hii ya Chelsea dhidi ya Brighton ambao walishinda kwa kishindo kwenye mtanange wa kwanza wa ligi, hivyo hii ni mechi ambayo kila timu inahitaji kupata ushindi mnono siku ya leo.

Vijana wa Darajani chini ya kocha mkuu Xabi Alonso watakuwa na kibarua kizito cha kukusanya pointi 3 dhidi ya timu hiyo ambayo inaonekana ni ngumu kukabiliana nayo kwani msimu uliopita The Blues walipigika mechi zote mbili walizokutana kwenye ligi.

Meridianbet wanakwambia kuwa hii ni nafasi ya kupiga pesa kwa kumpatia ushindi Chelsea aweze kulipa kisasi akiwa nyumbani au umpatie Brighton ushindi kuendeleza ubabe dhidi ya timu hiyo. Bashiri hapa.

Lakini pia kule kule kwa wakali waubashiri wanasema kuwa kwa wale ambao hawajajisajili huu ndio wakati wake, usingoje kupitwa na mtanange huu wa moto pale Uingereza. Suka jamvi hapa.

SERIKALI SAME YAWATAKA WAZAZI KUCHANJA WATOTO DHIDI YA POLIO

Serikali wilayani Same imesisitiza wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wenye umri chini ya miaka 10 wanapatiwa chanjo ya Polio ya matone, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwakinga dhidi ya ugonjwa huo hatari. Aidha, wananchi wametakiwa kutosikiliza taarifa zinazopotosha kuhusu usalama wa chanjo, bali kuzingatia elimu na maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya.

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Same, Bi. Mamndolwa Gembe, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Polio Awamu ya Kwanza kwa watoto wenye umri chini ya miaka 10 wilayani humo.

Bi. Mamndolwa amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha watoto wanakuwa salama na wenye afya njema kupitia huduma mbalimbali za afya, ikiwemo chanjo ya Polio, ambayo ni miongoni mwa hatua muhimu za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

Amesema ugonjwa wa Polio ni hatari kwa kuwa hushambulia mfumo wa fahamu na unaweza kusababisha kupooza kwa mwili, ulemavu wa kudumu na hata kifo. Hivyo, amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wenye umri chini ya miaka 10 wanapata chanjo hiyo, akisisitiza kuwa chanjo ya Polio ni salama na ina umuhimu mkubwa katika kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo.

“Ugonjwa wa Polio ni hatari sana kwani unashambulia mfumo wa fahamu na unaweza kusababisha kupooza kwa mwili na hata kifo. Tuhakikishe watoto wetu wenye umri chini ya miaka 10 wanapata chanjo hii ya Polio, kwa sababu chanjo hii ni salama,” amesema Bi. Mamndolwa.

Aidha, amewataka wahudumu wa afya, watendaji wa Serikali, wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na walimu kuongeza juhudi za kutoa elimu na hamasa kwa wananchi katika maeneo yote ili kuhakikisha jamii inapata uelewa sahihi kuhusu umuhimu wa chanjo.

Amesema ushirikiano wa wadau hao ni muhimu katika kuhakikisha wazazi na walezi wanapata taarifa sahihi na kuwapeleka watoto wao kupata chanjo kwa wakati, hatua ambayo itasaidia kuwalinda dhidi ya ugonjwa wa Polio.

Kampeni ya Chanjo ya Polio Awamu ya Kwanza inafanyika katika mikoa minane nchini Tanzania kuanzia Agosti 27 hadi 30, 2026, ikiwa na lengo la kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo kufuatia milipuko iliyotokea katika nchi jirani.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kampeni hiyo inawalenga watoto wote wenye umri chini ya miaka 10, huku Wilaya ya Same ikitarajia kuwafikia jumla ya watoto 85,677 kwa ajili ya kupata chanjo hiyo.

Dkt Mwigulu: Serikali Kuendelea Kushirikiana Na Taasisi Za Dini Katika Maendeleo Ya Taifa – Video

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu taasisi za dini likiwemo kanisa Katoliki katika kuimarisha huduma za kijamii, maendeleo na ustawi wa wananchi, akisisitiza kuwa mchango wa taasisi za dini ni sehemu muhimu ya safari ya maendeleo ya Tanzania.

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo Jumapili, Agosti 30, 2026, katika maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 25 ya Jimbo Katoliki la Mpanda, yaliyofanyika mkoani Katavi, ambapo amesema Serikali inatambua mchango wa Kanisa Katoliki katika maendeleo ya nchi, hususan katika sekta za elimu, afya na huduma za kiroho.

“Serikali inatambua mchango wa Kanisa na baba Askofu. Kila tunapotaja maendeleo ya nchi yetu, kuanzia mwanzo mpaka hapa tulipofika, hatuwezi kuyataja kwa kina maendeleo hayo bila kutaja mchango wa Kanisa.”

Amesema ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa umeendelea kuwa muhimu katika kuhakikisha huduma za kijamii na shughuli za maendeleo zinaimarika, akisisitiza kuwa milango ya Serikali itaendelea kuwa wazi kwa Kanisa na taasisi nyingine za dini katika masuala yanayolenga ustawi wa wananchi.

“Niwahakikishie Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa na popote pale mlipo na jambo msisite, milango yetu iko wazi ili tuweze kuhakikisha kwamba tufanye jambo lolote linalotufurahisha.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa maelekezo kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi na mamlaka husika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya barabara, maji na umeme, akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kupata huduma hizo kwa wakati.

Amesema maandalizi ya kukabiliana na uwezekano wa kutokea kwa El Niño yanapaswa kwenda sambamba na hatua za vitendo, ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa mifereji na madaraja ili kupunguza athari za mafuriko.

Kuhusu huduma za maji, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Maji na wahusika wa mradi wa maji Mpanda kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ifikapo Desemba 2026, huku akisisitiza pia kuharakishwa kwa miradi ya barabara inayounganisha Katavi na mikoa jirani.

*DKT MWIGULU: SERIKALI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA DINI KATIKA MAENDELEO YA TAIFA*

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu taasisi za dini likiwemo kanisa Katoliki katika kuimarisha huduma za kijamii, maendeleo na ustawi wa wananchi, akisisitiza kuwa mchango wa taasisi za dini ni sehemu muhimu ya safari ya maendeleo ya Tanzania.

Dkt. Mwigulu ameyasema hayo leo Jumapili, Agosti 30, 2026, katika maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 25 ya Jimbo Katoliki la Mpanda, yaliyofanyika mkoani Katavi, ambapo amesema Serikali inatambua mchango wa Kanisa Katoliki katika maendeleo ya nchi, hususan katika sekta za elimu, afya na huduma za kiroho.

 “Serikali inatambua mchango wa Kanisa na baba Askofu. Kila tunapotaja maendeleo ya nchi yetu, kuanzia mwanzo mpaka hapa tulipofika, hatuwezi kuyataja kwa kina maendeleo hayo bila kutaja mchango wa Kanisa.”

Amesema ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa umeendelea kuwa muhimu katika kuhakikisha huduma za kijamii na shughuli za maendeleo zinaimarika, akisisitiza kuwa milango ya Serikali itaendelea kuwa wazi kwa Kanisa na taasisi nyingine za dini katika masuala yanayolenga ustawi wa wananchi.

 “Niwahakikishie Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa na popote pale mlipo na jambo msisite, milango yetu iko wazi ili tuweze kuhakikisha kwamba tufanye jambo lolote linalotufurahisha.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa maelekezo kwa viongozi wa Mkoa wa Katavi na mamlaka husika kuharakisha utekelezaji wa miradi ya barabara, maji na umeme, akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kupata huduma hizo kwa wakati.

Amesema maandalizi ya kukabiliana na uwezekano wa kutokea kwa El Niño yanapaswa kwenda sambamba na hatua za vitendo, ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa mifereji na madaraja ili kupunguza athari za mafuriko.

Kuhusu huduma za maji, Waziri Mkuu ameitaka Wizara ya Maji na wahusika wa mradi wa maji Mpanda kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo ifikapo Desemba 2026, huku akisisitiza pia kuharakishwa kwa miradi ya barabara inayounganisha Katavi na mikoa jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya haki kwa wananchi, akitangaza kuwa Serikali inaelekea kufuta sheria inayohusu utaifishaji wa mifugo, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuondoa changamoto za wananchi kunyang’anywa mifugo yao.

 “Katika Bunge hili linaloendelea tunakwenda kufuta sheria ya utaifishaji wa mifugo… kumekuwepo na majeraha makubwa ya watu kunyang’anywa katika baadhi ya maeneo. Tunataka tuondoe hayo ili kuhakikisha kwamba wananchi wetu wanaepukana na hayo.”

Pia ametoa maelekezo kwa wasimamizi wa sheria kuacha kukamata vitendea kazi vya wananchi kama pikipiki, bajaji na magari katika utekelezaji wa sheria za makosa mbalimbali, akisisitiza umuhimu wa kutumia utaratibu wa kisheria wa adhabu na faini.

Kwa upande wake, Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Mhashamu Baba Askofu Eusebius Nzigilwa, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda na kushiriki katika maadhimisho hayo, akisema uwepo wake umeonesha heshima na kuthaminiwa kwa Jimbo la Mpanda na Kanisa Katoliki Tanzania.

 “Ninakushukuru sana. Tunaona hiyo ni heshima kwa Jimbo letu na kwa Kanisa Katoliki Tanzania, na hivyo tunaomba Mwenyezi Mungu azidi kuwaongoza na kuwajalia neema na hekima katika kutuongoza sisi raia na wananchi wenu.”

Naye Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania anayemaliza muda wake, Mhashamu Askofu Mkuu Angelo Accattino, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa Katoliki, akisema ushiriki wa viongozi wa Serikali na viongozi wa dini mbalimbali katika maadhimisho hayo ni ishara ya mahusiano mema kwa ajili ya ustawi wa jamii.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Jimbo Katoliki la Mpanda mwaka 2001, huku viongozi wa Kanisa wakieleza kuwa katika kipindi hicho Jimbo limepiga hatua katika huduma za kichungaji, elimu, afya na ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya jamii.

Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa Kanisa, waamini na wananchi wa Jimbo Katoliki la Mpanda kwa kufanikisha Jubilee hiyo, akiwataka kuendelea kushirikiana na Serikali katika kujenga jamii yenye amani, mshikamano na maendeleo.

Makamu wa Rais Ndejembi Ashiriki Misa Takatifu Kanisa Katoliki Dodoma

Global Publishers
August 30, 2026
882 views
0 Comments


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Deogratius Ndejembi, pamoja na familia yake wameungana na waumini mbalimbali katika kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Jumapili, katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Paulo wa Msalaba Jimbo Kuu Katoliki Dodoma. Tarehe 30 Agosti 2026.