WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro wamepongeza juhudi za chama hicho kupitia mdau wa maendeleo Best Simba kuamua kuboresha jengo la ofisi ya chama hicho mkoa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachama hao wamedai kuwa kuboreshwa kwa jengo hilo kunarudisha heshima ndani ya chama kwani lilikuwa limechakaa.
Athuman Rashidi mkazi wa Njoro manispaa ya Moshi alisema kuwa, jengo hilo lilikuwa limechakaa na kupoteza hadhi yake kwa muda mrefu sasa.
Rashidi alisema kuwa, uamuzi wa mwanachama Simba kujitolea kulikarabati jengo hilo na kulirudishia hadhi yake ni kitengo cha kiungwana na cha kujitolea ambaapo wanaccm wanapaswa kumpongeza kwa moyo wake huo.
“Kweli lile jengo jinsi lilivokuwa limechakaa lilikuwa linatutia aibu kubwa sisi wanachama wa ccm ambapo ilikuwa ni aibu tunapofika pale ofisi za mkoa na kulitazama jengo lilivochakaa lakini sasa Best Simba ametuheshimisha sisi wanachama” alisema Rashidi.
Naye Rehema Omary mkazi wa kata ya Mawenzi manispaa ya Moshi alitumia nafasi hiyo kumpongeza Simba kwa jinsi ambavyo amekuwa akijitolea katika maeneo mbalimbali hususani katika kukisaidia chama nyakati mbalimbali.
Rehema alisema kuwa, sasa imefika wakati ambapo wadau wengine wa maendeleo kujitolea kuziboresha ofisi za chama ngazi ya kata na wilaya ili kuzirudisha katika hadhi yake.



