Mahakama Yaagiza IGP, CDF NA DCI Kutoa Ushahidi Kesi Ya Uhaini Ya Tundu Lissu

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imeagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) pamoja na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuitwa kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Uamuzi huo umetolewa leo, Septemba 10, 2026, na Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, baada ya Lissu kuwasilisha orodha ya mashahidi anaotaka watoe ushahidi katika kesi hiyo.

Miongoni mwa mashahidi waliotajwa na upande wa utetezi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan; aliyekuwa Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango; aliyekuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa; Mkuu wa Majeshi, Jenerali John Jacob Mkunda; IGP; Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa; DCI Ramadhani Kingai; pamoja na John Mnyika, Amani Golugwa, John Heche na Brenda.

Hata hivyo, Mahakama imekataa ombi la kuwaita Rais Samia Suluhu Hassan, Dkt. Philip Mpango, Kassim Majaliwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa kutoa ushahidi.

Mahakama imeeleza kuwa si sahihi kuwaita mashahidi hao kwa madhumuni ya kuthibitisha iwapo walitishika au hawakutishika kutokana na kauli zinazolalamikiwa katika shauri hilo.

Katika uamuzi huo, Mahakama imekumbusha kuwa Agosti 21, 2026, ilitoa uamuzi mdogo kwamba mshtakiwa ana kesi ya kujibu na kumweleza kuwa ana haki ya kuleta mashahidi wake.

Baada ya kuwasilisha orodha hiyo, upande wa utetezi uliiomba Mahakama kutoa wito kwa mashahidi hao ili wafike mahakamani na kutoa ushahidi.

Kwa upande mwingine, Mahakama imekubali kuitwa kwa Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, hatua inayowaruhusu kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Kesi hiyo inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba Amfariji Rais Samia Kizimkazi

Global Publishers
September 10, 2026
0 views
0 Comments

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, pamoja na Mawaziri wengine, wamefika nyumbani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, kutoa pole kufuatia msiba wa mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Dkt. Mwigulu Nchemba na Mawaziri hao walifika Kizimkazi leo, Septemba 10, 2026, ambapo walimfariji Rais Samia na familia yake katika kipindi hiki cha majonzi.

Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Ujio wa Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri ni sehemu ya viongozi mbalimbali wanaoendelea kufika Kizimkazi kutoa pole na kushirikiana na Rais Samia katika kipindi hiki kigumu cha msiba.

Msiba huo umeendelea kuwakutanisha viongozi mbalimbali wa kitaifa, wawakilishi wa taasisi na wananchi, ambao wamekuwa wakifika kutoa salamu za rambirambi kwa Rais Samia na familia yake.

Katika kipindi hiki cha maombolezo, viongozi na Watanzania wameendelea kuungana na Rais Samia, wakitoa pole na faraja kufuatia kuondokewa na mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

 

PSV vs Shakhtar Donetsk: Vita ya Champions League Yaandaliwa Uholanzi

Huu ni mchezo wa kwanza kwa timu hizi katika hatua ya ligi ya Champions League msimu huu, hivyo pointi tatu zitakuwa muhimu katika kuanza safari ya kutafuta nafasi nzuri kwenye msimamo.

PSV inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na hali nzuri baada ya kuanza msimu kwa kiwango cha juu. Katika michezo yake ya mwisho ya Eredivisie, PSV iliifunga Ajax 3-1 ugenini, huku kabla ya hapo ikiwa imepata ushindi mkubwa wa 6-1 dhidi ya Utrecht na 5-1 dhidi ya Groningen. Matokeo hayo yanaonyesha uwezo wao mkubwa katika safu ya ushambuliaji, lakini mchezo wa Champions League utahitaji zaidi ya kufunga mabao; wanapaswa pia kuwa na umakini mkubwa wanapopoteza mpira.

Kwa upande wa Shakhtar Donetsk, timu hiyo inarudi kwenye Champions League ikiwa na historia na uzoefu mkubwa wa mashindano ya Ulaya. Klabu hiyo ya Ukraine, ambayo sasa inaongozwa na Arda Turan, imepitia changamoto kubwa kutokana na hali ya vita nchini Ukraine, lakini imeendelea kujenga kikosi chenye uwezo wa kushindana katika soka la Ulaya. Shakhtar pia imeanza msimu wa ligi ya ndani kwa ushindi, ikiwemo ushindi wa 2-1 dhidi ya Karpaty katika mchezo wake wa mwisho ulioripotiwa.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kimbinu, PSV inaweza kuwa na faida kutokana na kucheza nyumbani na kasi kubwa ya safu yake ya mbele. Shakhtar, chini ya Turan, huenda ikajaribu kuwa na nidhamu kwenye ulinzi huku ikitumia kasi katika mashambulizi ya kushtukiza. Jambo muhimu kwa PSV litakuwa kuvunja safu ya ulinzi ya wageni bila kuacha nafasi nyuma, wakati Shakhtar itahitaji kutumia kila nafasi itakayopata kwa sababu PSV imeonyesha uwezo mkubwa wa kufunga mabao katika wiki za mwanzo za msimu.

Kwa ujumla, huu ni mchezo unaompa PSV nafasi nzuri ya kuanza Champions League kwa ushindi, hasa kutokana na kiwango chake cha hivi karibuni na faida ya uwanja wa nyumbani.

Hata hivyo, Shakhtar si mpinzani wa kupuuzwa na inaweza kuleta changamoto kubwa ikiwa PSV itashindwa kutumia nafasi zake mapema. Kwa mtazamo wa mchezo, PSV inaonekana kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda, lakini Shakhtar inaweza kufanya mchezo kuwa mgumu hadi dakika za mwisho.

 

Mbowe Amfariji Rais Samia Kizimkazi Baada ya Kufiwa na Mumewe

Global Publishers
September 10, 2026
0 views
0 Comments

Mwenyekiti Mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe, amemfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia kifo cha mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Mbowe alifika nyumbani kwa Rais Samia, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 10, 2026, ambapo alitoa pole na kumfariji Rais Samia katika kipindi hiki cha majonzi.

Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar.

Ujio wa Mbowe Kizimkazi ni sehemu ya viongozi na watu mbalimbali wanaofika kutoa pole kwa Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo.

Katika kipindi hiki cha maombolezo, Rais Samia amekuwa akipokea salamu za rambirambi na pole kutoka kwa viongozi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, huku ndugu, marafiki na wananchi wakiendelea kuungana naye katika kipindi hiki kigumu.

Maalim Hafidh Ameir Hassan ataendelea kukumbukwa kwa nafasi yake katika familia na jamii, huku msiba wake ukiwa umewagusa watu mbalimbali waliokuwa karibu na familia hiyo.

Balozi wa China na Viongozi Wengine Wamfariji Rais Samia Kizimkazi Baada ya Kufiwa na Mumewe

Global Publishers
September 10, 2026
0 views
0 Comments

Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, akimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kuwasili nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 10 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.

Viongozi, wanasiasa, mabalozi pamoja na wageni mbalimbali wameendelea kumtembelea na kumfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa Mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan.

Miongoni mwa waliofika kutoa pole ni Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, ambaye amemtembelea Rais Samia nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, leo Septemba 10, 2026.

Aidha, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, pamoja na ujumbe wake, wamefika Kizimkazi kumfariji Rais Samia na familia yake kufuatia msiba huo.

Makatibu Wakuu pamoja na Naibu Makatibu Wakuu nao wamewasili nyumbani kwa Rais Samia kutoa pole na kushiriki katika kipindi hiki cha majonzi.

Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Septemba 7, 2026, katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.

Ziara hizo za viongozi na wageni mbalimbali zimeendelea kuwa sehemu ya utaratibu wa kutoa pole kwa Rais Samia na familia yake katika kipindi hiki cha msiba.

Zelenskyy Aokoka Ajali! Ndege Yake Nusura Igongwe na Drone

Global Publishers
September 10, 2026
6 views
0 Comments

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amekumbwa na tukio la taharuki wakati akisafiri kutoka Moldova kuelekea Oslo, Norway, baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kuripotiwa kuwa karibu kugongwa na drone.

Tukio hilo lilitokea wakati ndege ya Zelenskyy ikiwa inajiandaa kuondoka Moldova, ambako mamlaka ililazimika kufunga kwa muda anga ya nchi hiyo baada ya drone kuingia katika anga yake. Hatua hiyo ilisababisha safari kadhaa za ndege kuchelewa, ikiwemo ndege iliyokuwa imembeba Rais Zelenskyy.

Waziri Mkuu wa Norway, Jonas Gahr Store, alithibitisha tukio hilo na kusema ndege ya Zelenskyy ilikuwa karibu kugongwa na drone wakati ikijiandaa kuruka kutoka Moldova. Hata hivyo, Store hakutoa maelezo kuhusu umbali ambao drone hiyo ilikuwa kutoka kwenye ndege au chanzo cha taarifa hizo.

Kwa upande mwingine, mamlaka za Moldova zilisema droni hiyo iliingia katika anga yao na baadaye ikaanguka katika eneo la Riscani, huku vipande vilivyopatikana vikionyesha sifa zinazofanana na drone aina ya Geran inayotumiwa na Urusi. Hakukuwa na taarifa za majeruhi kutokana na kuanguka kwa drone hiyo.

Zelenskyy alikuwa akielekea Oslo kuhudhuria mazishi ya Mfalme Harald V wa Norway, kabla ya kuendelea na ratiba zake za kidiplomasia. Tukio hilo limeongeza wasiwasi kuhusu usalama wa anga katika eneo hilo wakati vita vya Ukraine vikiendelea.

USHIRIKIANO NI MUHIMU KATIKA MAGEUZI YA KIDIJITALI: KITALI

OWM-TAMISEMI, Arusha

Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Bw. Erick Kitali, amesema mafanikio ya mageuzi ya kidijitali nchini yanahitaji ushirikiano wa taasisi mbalimbali, uongozi wenye maono na kuwashirikisha wataalamu sahihi katika kufanya maamuzi.

Bw. Kitali ameyasema hayo leo  Septemba 10,  2026 jijini Arusha  wakati wa mdahalo kuhusu kuimarisha huduma za afya ya msingi kupitia miundombinu ya umma ya kidijitali na safari ya Tanzania ya kuwalipa wahudumu wa afya ya jamii kwa njia za kidijitali.

Amesema ni muhimu Serikali kuhakikisha mifumo mbalimbali inaunganishwa ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa wakati na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Tunapaswa kuzungumzia ushirikiano na muunganiko wa mifumo. hakikisheni watu sahihi wanakuwepo kwenye meza ya maamuzi,” amesema.

Bw. Kitali amesema Tanzania imejikita pia katika kutumia wataalamu wa ndani kubuni, kuendeleza na kusimamia mifumo ya kidijitali inayotumika katika huduma za afya, ikiwemo usajili, malipo na utoaji wa taarifa.

Amesema Serikali imeandaa Mpango Elekezi (Blueprint) wa matumizi ya teknolojia katika huduma za wahudumu wa afya ya jamii, ukiwemo mpango wa kuanzisha Dashibodi ya Pamoja itakayounganisha taarifa kutoka mifumo mbalimbali.

Kwa mujibu wa Bw. Kitali, amesema dashibodi hiyo itasaidia kufuatilia huduma na malipo kuanzia ngazi ya jamii hadi taifa, pamoja na kubaini kwa haraka changamoto kama ucheleweshaji wa malipo.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kufanya tafiti na ufuatiliaji wa utekelezaji ili kubaini changamoto mapema na kuchukua hatua kwa wakati.

Amesema ushirikiano wa taasisi, matumizi ya wataalamu wa ndani na mifumo iliyounganishwa ni msingi muhimu wa kuboresha huduma za afya ya msingi na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora kwa wakati.

 

Trump Aahidi Tsh Milioni 12.75 Kwa Kila Raia Mtu Mzima Marekani

Global Publishers
September 10, 2026
0 views
0 Comments

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameahidi kutoa “dividend” ya dola 5,000 sawa na TSh 12,750,000 kwa kila raia mtu mzima wa Marekani endapo Chama cha Republican kitafanikiwa kudhibiti tena Baraza la Wawakilishi na Seneti katika uchaguzi wa Novemba.

Trump ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza katika Mkutano wa Republican uliofanyika Dallas, Texas, akisema malipo hayo yanatokana na kile alichodai kuwa ni mafanikio makubwa ya kiuchumi ya Marekani.

Hata hivyo, Trump amesema sharti pekee la fedha hizo ni kwamba zitumike ndani ya Marekani, huku akisema hazipaswi kutumika katika nchi nyingine.

Trump hakutoa maelezo zaidi kuhusu chanzo cha fedha hizo, namna zitakavyotolewa au muda wa utekelezaji wa mpango huo.

Arsenal, Liverpool na Barcelona Zaanza Ligi ya Mabingwa Kwa Ushindi

Global Publishers
September 10, 2026
426 views
0 Comments

Arsenal imeanza vyema kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Napoli, huku nahodha wake Martin Ødegaard akiwa shujaa wa mchezo baada ya kufunga bao pekee dakika ya 75.

Ødegaard alipiga shuti kali kwa mguu wa kushoto lililomshinda kipa Jan Oblak, na kuiwezesha Arsenal kuondoka na alama zote tatu.

Nchini Hispania, Liverpool pia imeanza kampeni hiyo kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Atlético Madrid, huku Alexis Mac Allister akifunga bao la ushindi na kuonyesha umuhimu wake ndani ya kikosi hicho.

Wakati huo huo, Barcelona imeanza kwa kishindo baada ya kuichapa Feyenoord mabao 5-1, huku Paris Saint-Germain ikipata ushindi mkubwa zaidi usiku huo kwa kuifunga Slovan Bratislava mabao 6-1.

Sporting CP nayo imeanza kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Galatasaray, wakati Stuttgart ikiifunga Viking kwa mabao 3-1.

Matokeo hayo yamezifanya Arsenal, Liverpool, Barcelona na PSG kuanza hatua ya ligi kwa ushindi, huku timu hizo zikitoa ishara ya mapema kuhusu nia yao ya kupambania taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Heche Kuendelea Kutoa Utetezi Katika Kesi Ya Uhaaini Ya Lissu Leo

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, leo Septemba 10, 2026 amefika katika Ukumbi wa Mahakama kwa ajili ya kuendelea kutoa utetezi wake katika kesi ya uhaini namba 19605/2025, inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Katika hatua hiyo ya kesi, Lissu alimtaka Heche kuieleza Mahakama kuhusu uzoefu wake na kile alichokiita “matatizo ya chaguzi za nchi.”

Akijibu, Heche amesema amewahi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi mara kadhaa, ikiwemo kuwa Diwani na Mbunge, pamoja na kushiriki katika kampeni mbalimbali za uchaguzi.

Heche pia ameeleza kuwa ameshiriki katika kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Arumeru, Geita, pamoja na kampeni za uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2015 na 2020.

Ushahidi huo ni sehemu ya mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu.

Lissu: Waeleze majaji, nilipokuja jimboni kwako mwaka 2020 nini kilitokea?

Heche: Waheshimiwa majaji, Lissu alikuwa mgombea urais wa CHADEMA mwaka 2020. Alifika jimboni kwetu, tukafanya mikutano maeneo kadhaa. Siku ya kwanza, kesho yake tulitarajia kufanya mikutano katika kata inayoitwa Matongo. Hili eneo linaitwa Kewanja. Polisi walituzuia kwa mabomu katika eneo ambalo mgombea alipaswa kusalimia wananchi. Kukatokea vurugu kubwa sana kati ya raia na polisi. Kulikuwa na maji ya washawasha, risasi na mabomu. Lakini vurugu zilipokuwa kubwa sana na polisi wakazidiwa, walituruhusu kufanya mkutano.

Heche: Lengo lilikuwa kutawanya watu wasije kutusikiliza. Kwa imani yao, tungekosa watu wa kutusikiliza. Bahati nzuri ilikuwa ni Tarime, Waheshimiwa Majaji, ambako si rahisi vitisho hivyo vikawakimbiza watu waliokuwa na hamu ya kumsikiliza mgombea urais.

Heche: Wakati mgombea wetu anafanyiwa hivi, hakuna mgombea wa CCM aliyewahi kufanyiwa hivyo. Si Magufuli wakati ule wala Samia sasa, ambaye mikutano yao imewahi kuharibiwa kwa mabomu, risasi na maji ya washawasha.

Lissu: Waeleze majaji, hili ni swali langu la mwisho kwa leo. Siku ya uchaguzi wa mwaka 2020 katika Jimbo la Rorya kulikuwa na nini?

Heche: Waheshimiwa majaji, siku ya uchaguzi mkuu katika Jimbo la Rorya, ambako alikuwa anagombea Ezekia Biogot Wenje ubunge kupitia CHADEMA, walivamiwa nyumbani kwao na polisi. Katika tukio hilo, ndugu Nyatenda Wenje aliuawa nyumbani kwao pamoja na kuwepo kwa Wenje.

Lissu: Huyu Nyatenda Wenje alikuwa nani?

Heche: Alikuwa ndugu yake wa Ezekia Wenje.

Lissu: Je, Ezekia Wenje kitu gani kilimtokea?

Heche: Katika tukio hilo, Bwana Ezekia Wenje alinusurika kuuawa. Alikimbilia Kenya na baadaye akaenda uhamishoni nchini Canada.

Lissu: Waeleze majaji, hatua zozote zilichukuliwa dhidi ya wauaji wa Nyatenda Wenje?

Heche: Waheshimiwa majaji, sina kumbukumbu yoyote juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi yao.

Lissu: Waheshimiwa majaji, nimemaliza kwa leo.

Lissu: Naomba tuahirishe mpaka kesho ili tuendelee na examination-in-chief, Waheshimiwa Majaji.

Jaji: Upande wa mashitaka mnasemaje?

Nzengeli: Ni sawa, tuahirishe mpaka kesho.

Jaji: Shauri limeahirishwa. Uamuzi utatolewa kesho.

Lissu: Matukio mengine?

Heche: Wakati nagombea ubunge mwaka 2015, nilipokuwa naenda kufanya kampeni Kata ya Nyanungu, Tarime, tulishambuliwa na akauawa Bwana Bokhe Mwita Waitiei.

Lissu: Alishambuliwa na watu gani?

Heche: Alishambuliwa na wafuasi wa CCM. Walikamatwa na baadaye kuachiwa, kisha kesi ikaisha hivyo.

Lissu: Unamaanisha nini unaposema kesi ilifunguliwa?

Heche: Walikamatwa kwa sababu walifahamika, lakini baadaye waliachiwa huru.

Lissu: Nini kilitokea kwenye uchaguzi wa Busanda?

Heche: Aliuawa kiongozi Alphonce Mawazo, ambaye alikuwa mgombea wa Jimbo la Busanda. Hata kumzika ilibidi tuombe amri ya mahakama kwa sababu tulizuiwa kumuaga huku mwili wake ukiwa bado hospitalini.

Lissu: Alphonce Mawazo alikuwa na nafasi gani kwenye chama?

Heche: Alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita na mjumbe wa Baraza Kuu la chama.

Lissu: Kuna hatua zozote zilichukuliwa dhidi ya waliomuua Alphonce Mawazo?

Heche: Sikumbuki vizuri mwisho wa kesi hiyo, hivyo siwezi kueleza kwa uhakika.

Lissu: Waeleze majaji nini kilitokea jimboni kwako Tarime mwaka 2020.

Heche: Mwaka 2020, wakati nafunga kampeni Nyamongo, tulivamiwa kwa risasi. Watu wawili waliuawa na wengine kujeruhiwa. Waliouawa ni Chacha Isangora na Chacha Gabir.

Watu waliowashambulia wanafahamika. Maganda ya risasi yalikutwa eneo la tukio. Baadhi yao walikuwa viongozi wa CCM. Polisi walichukua maganda hayo, waliwashikilia kwa muda, lakini baadaye wakawaachia. Familia zimebaki na yatima na wajane kutokana na matukio yanayohusishwa na uchaguzi.

Lissu: Waeleze majaji kama kuna tukio lingine la wakati wa uchaguzi.

Heche: Kwenye uchaguzi hapana, lakini katika shughuli za siasa zipo nyingine. Polisi walimuua mdogo wangu.

Waheshimiwa majaji, mdogo wangu aliitwa Suguta Heche. Alikamatwa Sirari mwaka 2018, akafungwa pingu mikono nyuma na kuchomwa sindano akiwa katika hali hiyo.

Sirari ipo Tarime Vijijini. Baadaye kulikuwa na madai ya jaribio la kumtupa ili ionekane amepata ajali au ameshambuliwa na watu wasiojulikana. Walinzi wa eneo waliona kilichokuwa kinaendelea, hivyo akarudishwa kituo cha polisi.

RPC wa wakati huo alitoa taarifa kwa umma kwamba mdogo wangu ameuawa kikatili na polisi na kwamba hatua zingechukuliwa. Askari aliyekuwa anahusishwa na tukio hilo aliachiliwa na kuhamishwa kituo, na mpaka sasa ni mtumishi wa Jeshi la Polisi.

Ninaamini mdogo wangu aliuawa kutokana na msimamo wangu wa kisiasa na kupinga maovu ya nchi hii, na kwamba tukio hilo lilikuwa ujumbe kwamba wanaweza kufanya lolote bila hatua za kisheria kuchukuliwa.

Chanzo cha picha, Facebook/Heche

Lissu: Kiswahili cha No Reforms, No Election ni nini?

Heche: Bila mabadiliko hakuna uchaguzi.

Lissu: Ni mabadiliko gani yaliyoazimiwa na Kamati Kuu?

Heche: Kamati Kuu iliazimia mabadiliko ya kikatiba na kisheria ili kuondoa mamlaka makubwa ya Rais ya kuunda Tume ya Uchaguzi, wakati yeye mwenyewe ni mgombea. Ni kama simba anacheza na Yanga halafu Yanga ndiye anachagua refa.

Lissu: Una maana gani unapozungumzia tume?

Heche: Tume Huru ya Uchaguzi ambayo haitakuwa na upendeleo wala kuingiliwa na mgombea ambaye ana maslahi.

Lissu: Usinitangulie, ukinitangulia… anaonesha majaji wa serikali. (Kicheko mahakamani.)

Lissu: Shahidi, nataka uwaeleze majaji uzoefu wako na matatizo ya chaguzi za nchi hii.

Heche: Waheshimiwa majaji, mimi nimegombea mara kadhaa. Nimekuwa diwani na nimekuwa mbunge katika chaguzi za nchi hii. Nimeshiriki maeneo mbalimbali katika kampeni za chama.

Chaguzi zote hizi, waheshimiwa majaji, ziliambatana na maumivu makubwa; kutekwa, kuenguliwa kwa wagombea wetu, kuibiwa kwa fomu za viapo vya mawakala, ratiba zetu kuingiliwa na polisi, kupigwa kwa watu katika mikutano ya kampeni, wagombea wetu kunyimwa fomu za matokeo, kura za uongo kuingizwa kwa maboksi na mabegi na askari polisi ambao walitakiwa kusimamia uchaguzi. Wagombea wetu walienguliwa kwa kuambiwa hawajui kusoma na kuandika.

Naomba nitafafanua jambo moja baada ya jingine.

Nitaanza na mauaji.

Katika uchaguzi wa Arumeru, Katibu wetu wa USA River, Bwana Msafiri Bwambo, aliuawa kwa kuchinjwa kwa chainsaw. Watu waliosadikiwa kuwa wanachama wa CCM walihusishwa na tukio hilo, na mpaka leo hakuna mtu aliyekamatwa au kufungwa kwa mauaji hayo.

Lissu: Tukio lingine, shahidi.

Heche: Hapa Dar es Salaam, Kinondoni, aliuawa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Ananasi, Dani Yona. Vilevile hakuna uchunguzi uliokamilika wala mtu aliyekamatwa, waheshimiwa majaji.

Mwanachama wetu Akwilina Akwilini, ambaye wakati huo Kamanda wa Polisi, Bwana Mambosasa, alithibitisha aliuawa kwa risasi ya polisi. Hakuna askari aliyekamatwa wala kushitakiwa.

Badala yake, nilishtakiwa mimi, John Mnyika, ambaye wakati huo alikuwa Katibu Mkuu; Freeman Mbowe ambaye alikuwa Mwenyekiti; Vincent Mashinji aliyekuwa Katibu Mkuu; Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; na Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Lissu: Waeleze majaji mlishtakiwa kwa kosa gani na kesi iliishia wapi?

Heche: Kwanza nieleze jambo moja. Wote hao walikuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya chama. Walishtakiwa kwa makosa mbalimbali, ikiwemo uchochezi na kushiriki kusanyiko lisilo na kibali.

Lissu: Kabla sijasahau, hiyo kadhia ilinikosaje mimi?

Heche: Waheshimiwa majaji, Mwenyekiti wetu wa sasa alikuwa ameshambuliwa vibaya kwa risasi na alikuwa akipatiwa matibabu nje ya nchi. Wakati huo alikuwa Makamu Mwenyekiti.

Lissu: Uamuzi wa hiyo kesi ulikuwaje?

Heche: Tulihukumiwa kifungo cha miezi sita au kulipa faini. Mimi nililipa faini ya shilingi milioni 40. Kwa ujumla ilikuwa karibu shilingi milioni 300.

Lissu: Ilikuwa katika mahakama gani?

Heche: Ilikuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na ilisikilizwa na hakimu ambaye baadaye alipandishwa cheo na kuwa jaji.

Lissu: Baada ya kuhukumiwa, nini kilifuata?

Heche: Tulikata rufaa Mahakama Kuu, na baadaye hukumu ile ilitupiliwa mbali. Mahakama ikaamuru turejeshewe fedha zetu, lakini mpaka leo sijawahi kurejeshewa, licha ya amri hiyo.

Lissu: Ni jaji gani wa Mahakama Kuu aliyetoa amri hiyo?

Heche: Jaji Mgeta, waheshimiwa.

Lissu: Sasa shahidi, ulisema kulikuwa na mauaji ya Akwilina Akwilini. Hiyo habari iliishia wapi?

Heche: Kama zilivyo habari nyingine za mauaji.

Jaji: Tuambie iliishia wapi.

Heche: Iliishia hapo, na hakuna aliyeshitakiwa wala kufungwa kwa mauaji hayo.

Lissu: Kwa kuwa nimekuita utoe ushahidi katika kesi hii, waeleze majaji mimi ni mtu wa aina gani.

Heche: Namfahamu kama mzalendo, mwanademokrasia, mzalendo wa kweli, mpenda maendeleo ya nchi hii, muadilifu, mtu anayependa kushindanisha mawazo kwa hoja. Amekuwa mbunge, na kabla hata mimi sijaingia bungeni nilikuwa namfuatilia. Ni mtu jasiri asiyeogopa kusema ukweli. Kwa lugha yetu tunasema ni mpiganaji wa kweli.

Kwa sisi watu wa Tarime, nilimfahamu alipokuja kumtetea marehemu Chacha Wangwe na wananchi wa Nyamongo waliodai kunyang’anywa maeneo yao ya asili yaliyokuwa na madini ya dhahabu.

Lissu: Kwa nini umemtaja Mzee Augustino Sasi?

Heche: Mzee Augustino Sasi alikuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kewanja kupitia Chama Cha Mapinduzi na alifungwa kwa kile kilichoelezwa kuwa kesi za uonevu, ikiwemo kupokonywa mali zake.

Baada ya kutoka gerezani alijiunga na chama chetu na akachaguliwa kuwa diwani. Nilifanya naye kazi katika Baraza la Madiwani. Nilimkuta katika kipindi chake cha pili cha uongozi, kwa sababu mimi nilichaguliwa mwaka 2008.

Lissu: Waeleze majaji, kwa kumbukumbu zako, ni watu wangapi niliowatetea katika matatizo yao?

Heche: Ni kundi kubwa. Ninawakumbuka wachache kama kina Wangwe kwa sababu ilikuwa ni jambo kubwa sana Tarime wakati huo kutokana na uonevu uliodaiwa kufanyika.

Lissu: Sasa tuzungumze kuhusu kesi ambayo nimekuita utoe ushahidi wa utetezi. Waeleze majaji, kulikuwa na nini tarehe 3 Aprili mwaka jana?

Heche: Kulikuwa na kikao cha watia nia wa nafasi mbalimbali kupitia chama chetu. Tulikuwa nao katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya chama.

Lissu: Lengo la mkutano huo lilikuwa nini?

Heche: Lengo lilikuwa kuwaeleza kuhusu msimamo wa chama wa “No Reforms, No Election”.

Bila mabadiliko hakuna uchaguzi. Lengo lilikuwa kukutana nao na kuwaelimisha na kuwapa elimu kwa nini chama kimechukua msimamo huo kwenye maamuzi ya vikao vilivyokuwa vimetangulia mwezi wa 12, mwaka uliokuwa umeisha.”

Lissu: Hivyo vikao vilivyotangulia ni vikao gani na tarehe zake kama unakumbuka?

Heche: Nimekuwa mjumbe wa Kamati Kuu kwa muda mrefu, hivyo nilipata nafasi ya kushiriki vikao vya Kamati Kuu baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo kulikuwa na malalamiko kwamba uchaguzi huo umeharibiwa kwa wagombea wa CHADEMA kuenguliwa nchi nzima. Watu waliuawa, ikiwemo Manyoni ambako mgombea wetu aliuawa, na pia Dar es Salaam hapa.