Ajira Mpya Dar: Supervisor – Mshahara Tsh 700,000 Tuma Maombi Yako Sasa!

Global Publishers
September 10, 2026
1,728 views
0 Comments

Location: Dar es Salaam, Tanzania
Salary: TSh 700,000 kwa mwezi

Kampuni inakaribisha maombi kutoka kwa watu wenye uwezo, uwajibikaji na bidii kwa nafasi ya Supervisor. Mwombaji atakayefanikiwa atakuwa na jukumu la kusimamia shughuli za kila siku pamoja na kuhakikisha timu inafanya kazi kwa ufanisi na kufikia malengo yaliyowekwa.

Sifa za Mwombaji

  • Awe na kiwango cha chini cha elimu cha Diploma.
  • Awe anaishi Dar es Salaam kwa sasa.
  • Uzoefu wa kazi katika nafasi ya usimamizi au uongozi utakuwa ni faida.
  • Awe na uwezo mzuri wa mawasiliano na kushirikiana na watu.
  • Awe na uwezo wa kusimamia na kuhamasisha timu.
  • Awe mwaminifu, mwenye nidhamu na anayewajibika.
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi chini ya presha na kufikia malengo.
  • Ujuzi wa msingi wa matumizi ya kompyuta utakuwa ni faida.

Majukumu Makuu

  • Kusimamia na kuratibu shughuli za kila siku.
  • Kusimamia na kufuatilia utendaji wa wafanyakazi.
  • Kuandaa ripoti za kila siku na kila wiki.
  • Kuhakikisha sera na taratibu za kampuni zinafuatwa.
  • Kushughulikia changamoto za wateja na wafanyakazi kwa weledi.
  • Kuhakikisha malengo na shughuli za kila siku zinafikiwa.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wenye sifa wanatakiwa kutuma CV zao kupitia barua pepe:

📧 [email protected]

Waombaji waliochaguliwa pekee ndio watakaowasiliana nao.

📌 Tuma maombi yako sasa!

Matunda 9 Yanayosaidia Kupunguza Mafuta ya Tumbo

Baadhi ya matunda kama zabibu (grapefruit), nanasi, parachichi na kiwi yanaweza kusaidia kupunguza mafuta ya tumbo kutokana na kuwa na nyuzi za lishe (fiber), vimeng’enya (enzymes) na virutubisho vingine muhimu.

Kwa mujibu wa The Times of India, matunda kwa asili yana kalori chache na fiber nyingi, hali inayosaidia kudhibiti njaa kwa kukufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu. Utamu wake wa asili pia husaidia kupunguza hamu ya kula vyakula vyenye sukari nyingi, hivyo kusaidia kuzuia mkusanyiko wa mafuta ya tumbo na kuunga mkono safari ya kupunguza uzito.

Wataalamu wa afya wametaja matunda 9 yafuatayo kuwa na mchango mkubwa katika kupunguza mafuta ya tumbo:

1. Zabibu (Grapefruit)

Utafiti unaonyesha kuwa zabibu zinaweza kusaidia kupunguza kiwango cha insulini, jambo linalochochea upunguzaji wa uzito. Pia zina fiber nyingi na kalori chache, hivyo kusaidia kuchoma mafuta.

Zaidi ya hilo, zabibu husaidia kuimarisha kinga ya mwili, kuzuia kisukari, kuboresha afya ya moyo, kupunguza hatari ya mawe ya figo na kulinda ngozi.

2. Nanasi (Pineapple)

Nanasi lina bromelain, kimeng’enya kinachosaidia usagaji wa chakula na kupunguza tumbo kujaa gesi. Lina maji na fiber nyingi, hivyo ni chaguo bora kwa wanaolenga kupunguza mafuta ya tumbo.

Pia lina vitamini na madini yanayosaidia kuimarisha mifupa, kupambana na maambukizi na kuboresha afya ya uzazi kwa wanaume.

3. Tikiti Maji (Watermelon)

Tikiti maji lina kalori chache sana na maji mengi, hivyo hukufanya ujisikie umeshiba na kubaki na maji ya kutosha mwilini—hali inayosaidia kupunguza mafuta ya tumbo.

Pia husaidia mmeng’enyo wa chakula, afya ya ngozi na mwendo mzuri wa choo.

4. Parachichi (Avocado)

Ingawa lina kalori zaidi, parachichi lina mafuta yenye afya na fiber nyingi zinazosaidia kudhibiti hamu ya kula. Pia husaidia afya ya utumbo na kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

5. Kiwi

Kiwi lina vitamini C na fiber kwa wingi, husaidia mmeng’enyo wa chakula, kudhibiti sukari kwenye damu na kupunguza mafuta ya tumbo. Pia husaidia afya ya moyo na utendaji mzuri wa mfumo wa chakula.

6. Tufaha (Apple)

Tufaha lina maji na fiber nyingi, hivyo hukufanya ujisikie umeshiba kwa muda mrefu. Ni tunda bora kwa kudhibiti uzito.

Kula tufaha mara kwa mara kunahusishwa na kupunguza hatari ya magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo na saratani, pamoja na kuboresha afya ya utumbo na ubongo.

7. Pea (Pear)

Pea lina fiber nyingi na kalori chache, hivyo husaidia kupunguza njaa na mafuta ya tumbo.

Pia husaidia kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, kusaidia mwili kujisafisha (detox), na kupambana na free radicals.

8. Chungwa (Orange)

Chungwa lina vitamini C na fiber, husaidia kupunguza hamu ya kula na kukufanya ujisikie umeshiba.

Pia hulinda seli dhidi ya uharibifu, husaidia utengenezaji wa collagen kwa ngozi laini, huimarisha kinga ya mwili, huongeza ufyonzwaji wa chuma na kupambana na kansa.

9. Papai (Papaya)

Papai lina vimeng’enya vinavyosaidia mmeng’enyo wa chakula, hupunguza tumbo kujaa na kusaidia kupunguza mafuta ya tumbo. Pia husaidia afya ya moyo, hupunguza uvimbe na kulinda ngozi.

Linah Aendelea Kung’ara na EP Yake Mpya ya Love Notes – Video

Global Publishers
September 10, 2026
1,014 views
0 Comments


Msanii wa muziki kutoka Tanzania, Linah, anaendelea kuwafikia mashabiki kupitia EP yake mpya ya LOVE NOTES, inayobeba nyimbo zinazozungumzia mapenzi, hisia na mahusiano.

EP hiyo imekusanya nyimbo zenye ladha ya Bongo Flava na ujumbe wa kimapenzi, huku Linah akitumia sauti yake kuelezea hisia mbalimbali zinazopatikana katika mahusiano.

Wimbo wa kwanza katika EP hiyo, “Raha”, unaelezea hisia za upendo na furaha inayopatikana unapompata mtu wa kipekee katika maisha. Wimbo huo umeambatana na video rasmi ya muziki inayomualika msikilizaji kuingia katika ulimwengu wa LOVE NOTES.

Akifuata ni “Huyu”, wimbo wa pili unaosisitiza mapenzi ya dhati, kujitoa na uhusiano wa karibu kati ya watu wawili. Kupitia wimbo huo, Linah anaeleza hisia za kumpenda mtu ambaye ana nafasi kubwa katika maisha yake.

Wimbo wa tatu, “Nipo”, unaendeleza simulizi hiyo ya mapenzi kwa kuzungumzia uaminifu, uwepo na kusimama pamoja na mtu unayempenda katika nyakati mbalimbali za maisha.

Kwa ujumla, LOVE NOTES ni mkusanyiko wa nyimbo unaomweka Linah katika safari ya kusimulia hadithi tofauti za mapenzi na mahusiano kupitia muziki.

EP hiyo tayari inapatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya kusikiliza muziki, yakiwemo Spotify, Apple Music, Boomplay, Audiomack na YouTube Music.

Mashabiki wanaweza pia kutazama video rasmi za nyimbo hizo kupitia YouTube, kushiriki maoni yao na kusambaza nyimbo hizo kwa watu wao wa karibu.

Kwa LOVE NOTES, Linah anaendelea kuonyesha upande wake wa kimuziki unaogusa hisia, huku mapenzi yakiwa kiini cha safari hii mpya ya muziki.

Taylor Swift Ang’ara Kwenye ‘Date Night’, Avaa Gauni La Tsh Milioni 7.2

Msanii maarufu wa muziki nchini Marekani, Taylor Swift, akiwa na mume wake, Travis Kelce.

Msanii maarufu wa muziki nchini Marekani, Taylor Swift, ameonekana akiwa na mume wake, Travis Kelce, katika ‘date night’ jijini New York, huku akivutia kwa muonekano wake mpya pamoja na gauni lenye thamani ya takribani TSh milioni 7.2.

Wanandoa hao, wote wenye umri wa miaka 36, walitoka Jumapili, Septemba 6, 2026, na kwenda kupata chakula katika mgahawa maarufu wa Kihindi, Ambassadors Clubhouse New York, uliopo eneo la NoMad, Manhattan.

Swift alivaa gauni refu la hariri lenye mistari kutoka kwa mbunifu Stella McCartney, likiwa na thamani ya takribani dola 2,800 (TSh milioni 7.2). Alikamilisha muonekano huo kwa mkoba wa mbunifu huyo pamoja na viatu vya Aquazzura vya rangi ya metali.

Mbali na gauni hilo, Swift pia alionyesha mtindo wake mpya wa nywele fupi, ambao aliutambulisha Agosti 15, 2026, alipohudhuria harusi ya wahandisi wa muziki, Oli Jacobs na Laura Sisk, nchini Uingereza.

Kwa upande wake, Kelce alivaa shati la mikono mifupi la rangi ya krimu lenye mistari, suruali ya kahawia pamoja na viatu vya rangi nyeusi na nyeupe. Alikamilisha muonekano wake kwa miwani myeusi.

Kwa mujibu wa chanzo kilichozungumza na jarida la PEOPLE, Swift na Kelce walikula katika sehemu ya chini ya mgahawa huo wakiwa pamoja na wanaume wengine wawili. Waliagiza aina mbalimbali za vyakula na vinywaji kutoka kwenye menyu.

WAMEFUNGWA NDOA MIEZI MIWILI ILIYOPITA

Kutoka kwao jijini New York kumekuja takribani miezi miwili baada ya Swift na Kelce kufunga ndoa katika Madison Square Garden Julai 3, 2026.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na takribani wageni 1,000, wakiwemo mastaa mbalimbali na watu mashuhuri kutoka tasnia ya burudani. Sherehe hiyo iliendeshwa na rafiki yao, Adam Sandler.

Wanandoa hao walionekana wakiwa wameshikana mikono walipojitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya ndoa, Julai 10, 2026, katika harusi ya aliyekuwa mchezaji mwenzake Kelce, JuJu Smith-Schuster.

Kumbuka: Thamani ya TSh milioni 7.2 ni makadirio kutokana na dola 2,800 na kiwango cha ubadilishaji kilichotumika kwenye uandishi huu.

Rais Samia Awashukuru Wananchi kwa Salamu na Dua Baada ya Kifo cha Mumewe

Global Publishers
September 9, 2026
18 views
0 Comments

Paul Makonda, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akimfariji, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa shukrani kwa wananchi wa ndani na nje ya nchi pamoja na makundi mbalimbali kwa salamu za pole, dua na maombi waliyomfikishia yeye na familia yake kufuatia kifo cha mumewe, Marehemu Hafidh Ameir Hassan, kilichotokea Zanzibar Septemba 7, 2026.

Kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Rais Samia amesema yeye pamoja na familia yake wameguswa sana na upendo, mshikamano, salamu za pole, dua na maombi waliyoyapokea katika kipindi hiki cha majonzi.

Balozi Seif Ali Idd, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akimfariji Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.

Rais Samia amewashukuru Waku wa Nchi na Serikali, viongozi wa kitaifa, wanadiplomasia, jumuiya ya kimataifa, viongozi wa dini pamoja na Watanzania wote kwa salamu, dua na faraja zao katika kipindi chote cha majonzi hadi leo, ambapo wanaendelea kuomboleza kifo cha mpendwa wao.

Marehemu Hafidh Ameir Hassan alifariki dunia Zanzibar tarehe 7 Septemba 2026, na kuacha familia pamoja na ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi cha majonzi.

Baadhi ya Viongozi wa Timu za Yanga na Simba wakimfariji Dkt. Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nyumbani kwake Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Septemba, 2026, kufuatia kufiwa na Mume wake Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan aliyefariki dunia katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena Zanzibar, tarehe 07 Septemba, 2026.
Mke wa Rais wa Msumbiji Gueta Selemane Chapo akimfariji, Dkt. Samia.
Balozi Seif Ali Idd, Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, akimfariji Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

NAIBU WAZIRI DKT MAGHEMBE ASHIRIKI MKUTANO WA KANDA YA AFRIKA WA MPANGO KAZI WA DOHA

Mheshimiwa Dkt. Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameshiriki na kuzungumza kwenye Mkutano wa Kanda ya Afrika wa Mapitio ya Nusu Muhula ya Mpango Kazi wa Doha (Doha Program of Action) uliofanyika tarehe 8 na 9 Septemba 2026, jijini Addis Ababa, Ethiopia. 

Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri na Maafisa waandamizi wa serikali za nchi za Afrika; Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika; na Sekta binafsi kufanya tathmini ya nusu muhula ya nchi zinazoendelea kuhusu changamoto za kimaendeleo zinazokabili nchi hizo, na namna ya kupambana na changamoto hizo kwa ajili ya kuzisaidia nchi zilizo katika kundi la nchi maskini (Least Developed Countries) kuondoka kwenye kundi hilo na kuwa nchi zenye uchumi wa Kati.

Mheshimiwa Dkt. Maghembe amehudhuria mkutano huo akimuwakilisha Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Mheshimiwa Naibu Waziri  ameelezea mafanikio ya Serikali

Dkt. Samia Ashiriki Hitma Ya Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan

Global Publishers
September 9, 2026
6 views
0 Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Septemba 9, 2026, ameshiriki katika Hitma ya kumuombea dua mume wake, Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, iliyofanyika Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Hitma hiyo imefanyika ikiwa sehemu ya taratibu za kumuombea Marehemu Maalim Hafidh Ameir Hassan, huku Dkt. Samia akishiriki pamoja na ndugu, jamaa na wananchi katika dua za kumuombea marehemu.

Maalim Hafidh Ameir Hassan alikuwa mume wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

RAIS SAMIA ATAJWA KINARA AFYA YA MSINGI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametambuliwa kuwa kinara katika kuimarisha huduma za afya ya msingi kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini, hususan katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto. 

Akifungua Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Aya ya Msingi (IPHC) kwa niaba ya Rais Samia katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Jijini Arusha (AICC), Septemba 9, 2026, Waziri Mkuu amesema mafanikio hayo yameiwezesha Tanzania kutambulika kimataifa, ikiwemo Rais Samia kutunukiwa Goalkeeper Award mwaka 2025 na kuteuliwa kuwa kinara wa Umoja wa Afrika wa huduma za afya ya mama na mtoto mwaka 2026.

“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya, na sasa Serikali inaelekeza nguvu zaidi katika kuboresha ubora na ufanisi wa huduma hizo,” amesema Waziri Mkuu. Ameeleza kuwa vifo vitokanavyo na uzazi duniani vimepungua kutoka takribani 328 hadi 197 kwa kila vizazi hai 100,000 kati ya mwaka 2000 na 2023, hali inayoonesha kuwa malengo ya afya yanaweza kufikiwa kwa kuongeza uwekezaji na kutekeleza mipango madhubuti.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuimarisha sekta ya afya kwa kuongeza miundombinu, wataalamu na rasilimali nyingine muhimu, huku zaidi ya watumishi 16,000 wa sekta hiyo wakiajiriwa kati ya Desemba 2025 na mwaka 2026. Aidha, Serikali imejenga nyumba zaidi ya 430 za watumishi wa afya na inapanga kujenga takribani nyumba nyingine 2,000 kuelekea mwaka 2030. Amesisitiza kuwa utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote utawezesha wananchi, wakiwemo wenye kipato duni, kupata huduma bora kwa gharama nafuu na bila ubaguzi wa kipato.

Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu–TAMISEMI, Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, amesema kati ya mahudhurio milioni 32.3 ya wagonjwa wa nje yaliyorekodiwa katika vituo vya afya vya umma, mahudhurio milioni 27.8, sawa na asilimia 86, yalikuwa katika vituo vya afya ya msingi. Aidha, kati ya vituo 8,288 vya afya vya Serikali nchini, vituo 7,946, sawa na asilimia 95.8, ni vya ngazi ya afya ya msingi vinavyomilikiwa na halmashauri. Ameongeza kuwa asilimia 96.6 ya vituo hivyo vimeunganishwa na mfumo wa GoTHOMIS na asilimia 87.6 vimeunganishwa na GePG, hatua inayoongeza ufanisi, uwazi na usimamizi wa mapato na huduma.

upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Makalla, amesema Mkoa huo umepokea zaidi ya Sh bilioni 94 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya ya msingi. Uwekezaji huo umechangia kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za afya kutoka 382 hadi 450, kuajiriwa kwa watumishi wapya 823 wa kada za afya na kupatikana kwa magari 27 ya kuhudumia wananchi, hatua zilizosaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto.

Akizungumza kwa niaba ya asasi za kiraia zinazoshughulikia masuala ya afya nchini, Bw. Amson Mwendamake amependekeza kuimarishwa kwa ushiriki wa jamii katika kupanga, kutekeleza na kufuatilia mipango na bajeti za afya ya msingi. Pia, amesisitiza umuhimu wa kuongeza ufadhili wa ndani, kuwalinda wananchi walio katika mazingira hatarishi dhidi ya gharama kubwa za matibabu na kuimarisha uwajibikaji pamoja na ushirikiano kati ya Serikali na wadau.

Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Afya ya Msingi unafanyika jijini Arusha kuanzia Septemba 9 hadi 11, 2026, ukiwakutanisha wataalamu wa kada mbalimbali za afya kwa ajili ya kujadili na kutathmini masuala ya afya ya msingi. Mkutano huo unaongozwa na kaulimbiu isemayo: “Kuelekea upatikanaji wa huduma za afya kwa wote: Kuimarisha ugharamiaji endelevu wa huduma za afya, ufanisi na uboreshaji wa huduma katika ngazi ya msingi.”

WAZIRI MKUU ASHIRIKI HITMA YA MAREHEMU HAFIDH AMIR HASSAN KIZIMKAZI

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumatano, Septemba 09, 2026, ameshiriki Hitma ya kumuombea marehemu Hafidh Amir Hassan, aliyekuwa mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hitma hiyo imefanyika Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, ikiwakutanisha viongozi mbalimbali, ndugu, jamaa na waombolezaji kwa ajili ya kumuombea marehemu.