Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Sample Page
  • Home
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

Waziri wa zamani wa Ukraine ataka uchaguzi vitani

By admin
August 19, 2026 3 Min Read
Comments Off on Waziri wa zamani wa Ukraine ataka uchaguzi vitani

Dar es Salaam. Mzozo mpya wa kisiasa umeibuka nchini Ukraine baada ya Waziri wa zamani wa Ulinzi, Mykhailo Fedorov, kuitaka serikali kuandaa utaratibu wa kufanyika kwa uchaguzi wa rais licha ya vita vinavyoendelea kati ya Ukraine na Russia.

Fedorov, aliyeondolewa katika nafasi ya Waziri wa Ulinzi na Rais wa nchi hiyo, Volodymyr Zelensky,  Julai mwaka huu  ametoa msimamo huo katika video iliyowekwa mtandaoni Jumanne, Agosti 18, 2026. Katika video hiyo alisema Ukraine inakabiliwa na kile alichokiita mgogoro wa kimfumo wa utawala.

Kwa mujibu wa Shirika la habari Reuters, kauli hiyo imekuwa changamoto kubwa zaidi ya kisiasa ndani ya Ukraine kwa Zelensky tangu uvamizi kamili wa Russia ulipoanza mwaka 2022.



Fedorov alisema nchi hiyo inapaswa kutafuta njia halali, salama na inayotekelezeka itakayowezesha kurejeshwa kwa mchakato kamili wa kidemokrasia hata kama vita vitaendelea.

Alisisitiza kuwa demokrasia haipaswi kuwa mateka wa Russia, akisema Ukraine inapigana ili ibaki kuwa taifa huru la Ulaya.

Hata hivyo, utekelezaji wa wazo hilo unakabiliwa na vikwazo vikubwa vya kisheria na kiusalama.

Ukraine imekuwa chini ya sheria ya kijeshi tangu Februari 2022, na sheria zake zinazuia kufanyika kwa uchaguzi wakati hali hiyo ikiendelea.

Uchaguzi wa rais uliotarajiwa kufanyika mwaka 2024 haukufanyika kutokana na kuendelea kwa sheria ya kijeshi.

Zelensky amekuwa akitoa msimamo kwamba uchaguzi unaweza kufanyika endapo mazingira yatakuwa salama.

Februari 2026 alisema Ukraine itafanya uchaguzi baada ya kuwepo kwa usitishaji mapigano na dhamana za usalama.

Awali waliwahi kunukuliwa kuwa  alikuwa tayari uchaguzi ufanyike ndani ya siku 60 hadi 90 iwapo Marekani na washirika wa Ulaya wangetoa msaada wa kuhakikisha usalama wakati wa hatua hiyo.

Msimamo wa Zelensky umeungwa mkono kwa kiasi kikubwa na hoja kwamba uchaguzi wakati wa vita unaweza kuwa mgumu kwa mamilioni ya raia waliokimbia nchi, wanajeshi walioko vitani na wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyo karibu na mstari wa mbele wa mapigano au yanayokaliwa na Russia.

Kwa upande mwingine, Fedorov anaona vita haviwezi kutumika kuahirisha demokrasia bila kikomo.

Amesema ikiwa vita vitaendelea mwaka mmoja, miwili au mitatu zaidi, haiwezi kuwa sahihi kwa Russia kuamua ni lini Waukraine watapata tena nafasi ya kuchagua viongozi wao.

Vyombo vya habari vya kimataifa, vikiwamo Associated Press na The Guardian, vimeripoti kuwa hatua ya Fedorov imeibua mjadala mpana kuhusu utawala, uhalali wa kisiasa na mapambano dhidi ya rushwa.

Wakati huohuo, taasisi za kupambana na rushwa nchini Ukraine zimeanzisha uchunguzi unaowahusu baadhi ya maofisa waandamizi katika ofisi ya rais.

Marekani pia imewahi kuingia katika mjadala huo mwaka 2025, Rais Donald Trump alikosoa kutofanyika kwa uchaguzi nchini Ukraine, akisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika mchakato wa kidemokrasia.

Kauli hiyo ilizua mjadala mkubwa mjini Kyiv na Washington.

Wakati mvutano huo ukiendelea, Bunge la Ukraine Jumatano, Agosti 19, 2026 lilimthibitisha Yevhenii Khmara kuwa Waziri mpya wa Ulinzi kwa kura 312, baada ya Zelensky kumteua kuchukua nafasi ya Fedorov.

Hatua hiyo inaashiria kuwa Fedorov sasa yuko nje ya serikali, huku wito wake wa uchaguzi ukimuweka katika nafasi mpya ya kisiasa.

Habari hii imeandikwa na Salma Hamisi,

kwa msaada wa mashirika ya habari ya kimataifa.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Tanzania yaikabidhi DRC vifaa tiba vya Sh220 milioni kukabili Ebola

Next

Makandarasi, kampuni za ujenzi walalamikia faini TRA

Recent Posts

  • Polisi yawashikilia 18 kwa madai ya kuchoma magari
  • ACT yalaani Gazeti la MwanaHALISI kusitishiwa leseni
  • Wasira awataka wana-CCM kuhakiki taarifa za mitandaoni
  • DIT MWANZA YAONESHA NGUVU YA TEKNOLOJIA NA UZALISHAJI WA BIDHAA TANGA
  • Mgambo wazunguka soko la mitumba, wafanyabiashara ‘wafungiwa’ biashara

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme