Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Sample Page
  • Home
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

Makandarasi, kampuni za ujenzi walalamikia faini TRA

By admin
August 19, 2026 2 Min Read
Comments Off on Makandarasi, kampuni za ujenzi walalamikia faini TRA

Shinyanga. Wafanyabiashara mkoani Shinyanga, wakiwamo makandarasi na kampuni za ujenzi, wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuangalia changamoto zinazowakabili, ikiwamo ya kutozwa faini kutokana na kuchelewa kulipa kodi wakati malipo ya miradi wanayotekeleza yakichelewa.

Wakizungumza leo Jumatano, Agosti 19, 2026, baada ya kupatiwa elimu kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa walipa kodi katika Manispaa ya Shinyanga, baadhi ya wafanyabiashara wamesema changamoto hizo zinawaathiri katika utekelezaji wa majukumu yao.

Mkandarasi wa barabara, Lucy Joseph amehoji namna TRA inavyoweza kuwasaidia makandarasi wanaocheleweshewa malipo ya miradi, huku wakitakiwa kuwasilisha kodi kwa wakati na kutozwa faini wanapochelewa.



“Mnatusaidiaje sisi makandarasi ambao tunacheleweshewa malipo ya ujenzi wa miradi, lakini TRA inataka tulipe kwa wakati na tukichelewa tunapigwa faini? Nilijaribu kufika mamlaka ya mapato na kueleza, pia niliomba hata hati ya uthibitisho wa ulipaji kodi, sikupewa. Mnatusaidiaje?” amehoji Lucy.

Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Lyakare, Christopher Lingo akitoa malalamiko yake juu ya faini ya TRA. Picha na Hellen Mdinda.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya Lyakare, Christopher Lingo amesema makandarasi wanaotekeleza miradi kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), Wakala ya Barabara Tanzania (Tanroads) na halmashauri wanakabiliwa na changamoto zinazohusiana na misamaha ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Amesema baadhi ya miradi ya ujenzi wanayoitekeleza ina msamaha wa VAT, lakini changamoto hujitokeza pale muda wa utekelezaji wa mradi unapoongezwa kutokana na sababu mbalimbali.

“Tunafanya kazi na Tarura, Tanroads pamoja na halmashauri. Walipaswa nao wafike hapa ili waelimishwe pia, kwa sababu kazi tunazofanya za ujenzi zinakuwa na msamaha wa VAT.”

“Ikitokea tumeongezewa muda wa ujenzi kwa sababu mbalimbali, mamlaka inahitaji tupewe barua ya msamaha kwa ule muda ulioongezwa. Lakini waajiri wetu hawako tayari kutoa barua nyingine wakidai kuwa ni mradi mmoja. Hii inapelekea sisi kupigwa faini,” amesema Lingo.

Ofisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania Dodoma, Philipo Eliamini akizungumza na wafanyabiashara wakati wa kutoa elimu ya mabadiliko ya sheria ya mlipa kodi. Picha na Hellen Mdinda.

Kwa upande wake, Ofisa Msimamizi Mkuu wa Kodi kutoka TRA Dodoma, Philipo Eliamini amesema malalamiko hayo yatawasilishwa kwa mamlaka husika ili yafanyiwe kazi.

Aidha, Katibu wa Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC) Mkoa wa Shinyanga, Marcelina Saulo amewataka viongozi wa makandarasi kuandaa taarifa yenye changamoto zinazowakabili na kuiwasilisha katika mabaraza ya biashara ya kimkoa.

Amesema hatua hiyo itasaidia changamoto hizo kufikishwa katika ngazi ya Taifa kwa ajili ya kujadiliwa na kutafutiwa ufumbuzi.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Waziri wa zamani wa Ukraine ataka uchaguzi vitani

Next

Saratani ya mlango wa kizazi yaongoza kwa vifo Tanzania

Recent Posts

  • Wasira awataka wana-CCM kuhakiki taarifa za mitandaoni
  • DIT MWANZA YAONESHA NGUVU YA TEKNOLOJIA NA UZALISHAJI WA BIDHAA TANGA
  • Mgambo wazunguka soko la mitumba, wafanyabiashara ‘wafungiwa’ biashara
  • Polisi Maswa yatoa msaada kwa wagonjwa
  • Pande mbili utekelezaji agizo la Chalamila kuhusu malori

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme