Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Sample Page
  • Home
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

Tanzania yaikabidhi DRC vifaa tiba vya Sh220 milioni kukabili Ebola

By admin
August 19, 2026 3 Min Read
Comments Off on Tanzania yaikabidhi DRC vifaa tiba vya Sh220 milioni kukabili Ebola

Dar es Salaam. Tanzania imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya takribani Sh220 milioni kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za nchi hiyo katika kukabiliana na Ebola na magonjwa mengine ya mlipuko.

Msaada huo umetolewa wakati Tanzania ikisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa nchi za Afrika katika kukabiliana na milipuko ya magonjwa ambayo, kwa mujibu wa Serikali hayaheshimu mipaka ya nchi.

Akizungumza leo Jumatano Agosti 19, 2026 jijini Dar es Salaam baada ya kufungwa kwa mkutano wa nne wa Kamati ya Uongozi ya Mawaziri wa Afya wa Ukanda wa Afrika (ReSCO), Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema vifaa hivyo vimetolewa kwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.



Mchengerwa amesema hatua hiyo inalenga kuongeza uwezo wa DRC kukabiliana na Ebola, huku ikiwalinda pia wahudumu wa afya wanaohudumia wagonjwa na wananchi walio katika maeneo yaliyoathiriwa.

Mawaziri wa Afya wa Ukanda wa Afrika (ReSCO), Tanzania imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya takribani Sh220 milioni kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Vifaa hivi vitatumika kusaidia wahudumu wa afya walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Ebola pamoja na wananchi wanaoweza kuathirika kutokana na ugonjwa huo,” amesema.

Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha vifaa hivyo vinafikishwa nchini DRC kwa wakati mara taratibu za upokeaji zitakapokamilika.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi nyingine za Afrika pale inapohitajika, akisisitiza kuwa changamoto ya kiafya inayotokea katika nchi moja inaweza kuathiri nchi nyingine.

“Maradhi hayatambui mipaka ya nchi moja kwenda nyingine, hivyo changamoto ya nchi moja inaweza kuwa changamoto ya nchi nyingine,” amesema.

Mchengerwa pia amesisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika kuendelea kujenga mshikamano na kuchukua hatua za pamoja badala ya kuishia katika kufanya makubaliano na maazimio wakati wa mikutano.

Mawaziri wa Afya wa Ukanda wa Afrika (ReSCO), Tanzania imekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya takribani Sh220 milioni kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Amesema utekelezaji wa makubaliano ya pamoja ndiyo njia muhimu ya kukabiliana na changamoto za afya ya umma barani Afrika.

Mkutano huo wa ReSCO umefanyika ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkuu wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Septemba 9 hadi 11, 2026 jijini Arusha, utakaowakutanisha wakuu wa nchi.

Unatarajiwa kujadili masuala mbalimbali yanayohusu afya, ikiwamo namna ya kuimarisha ushirikiano wa nchi za Afrika katika kukabiliana na changamoto za afya ya umma na magonjwa ya mlipuko.

Hatua ya Tanzania kuisaidia DRC inakuja wakati nchi hiyo ikikabiliwa na changamoto za magonjwa ya mlipuko, hali inayoweka umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji, kinga na mwitikio wa dharura za afya.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

Mjane aporwa ardhi kwa madai hakuzaa na mumewe, RC aingilia kati

Next

Waziri wa zamani wa Ukraine ataka uchaguzi vitani

Recent Posts

  • Wasira awataka wana-CCM kuhakiki taarifa za mitandaoni
  • DIT MWANZA YAONESHA NGUVU YA TEKNOLOJIA NA UZALISHAJI WA BIDHAA TANGA
  • Mgambo wazunguka soko la mitumba, wafanyabiashara ‘wafungiwa’ biashara
  • Polisi Maswa yatoa msaada kwa wagonjwa
  • Pande mbili utekelezaji agizo la Chalamila kuhusu malori

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme