Global Publishers
September 22, 2026
0 views
0 Comments

Msanii mkubwa wa Nigeria, Davido, ametangaza kufanya maonyesho maalum ya siku tatu mfululizo katika jiji la Lagos, Nigeria, kuelekea mwisho wa mwaka 2026.
Davido ametangaza show hiyo ya siku tatu katika National Theatre, Lagos, itakayofanyika kuanzia Desemba 17 hadi 19, 2026.
Katika maonyesho hayo, Davido anatarajiwa ku-perform kwa mara ya kwanza album yake mpya, ORIADE, kwa ukamilifu mjini Lagos, pamoja na nyimbo zake nyingine kubwa zilizomjengea jina katika kipindi cha miaka 15 ya safari yake ya muziki.
Tukio hilo pia lina umuhimu mkubwa kwa Davido kwa sababu linakuja wakati anatimiza miaka 15 tangu aanze safari yake ya muziki. Waandaaji pia wametangaza kuwa kutakuwa na wageni maalum watakaoshiriki katika baadhi ya siku hizo tatu.
Tangazo hilo limeambatana na trailer ya residency hiyo pamoja na video mpya ya Davido ya wimbo “On The Road,” ambayo inaonyesha vipande mbalimbali vya safari yake ya kimuziki katika mwaka uliopita.
Na RAZAKU RAMADHAN | GPL- TUDACO
