Global Publishers
September 21, 2026
0 views
0 Comments

Kagera Sugar FC imewatangazia mashabiki na wadau wake kuwa benchi la ufundi pamoja na baadhi ya maafisa wa klabu hiyo wamehitimisha safari yao ndani ya klabu.
Kupitia taarifa iliyotolewa Septemba 21, 2026, Kagera Sugar FC imesema inaenda kuagana na benchi hilo la ufundi pamoja na maafisa hao baada ya kukamilisha majukumu yao ndani ya klabu.
“Kagera Sugar FC inapenda kuwajulisha mashabiki na wapenzi wa klabu yetu kwamba baada ya mashauriano na makubaliano ya pande zote, benchi la ufundi pamoja na maafisa wa klabu yetu tumekubaliana kuhitimisha safari yetu,” imeeleza taarifa hiyo.

Klabu hiyo imetoa shukrani kwa benchi la ufundi na maafisa hao kwa kujitolea muda wao katika mchango wa maendeleo ya timu pamoja na kuwasaidia kufanikisha majukumu yao katika msimu uliopita.
“Klabu inatoa shukrani za dhati kwa kujitolea muda wao katika mchango wa maendeleo ya timu na kuwatakia mafanikio mema katika majukumu yao mapya,” imeongeza taarifa hiyo.
Kagera Sugar FC haikueleza katika taarifa hiyo majina ya makocha na maafisa waliohitimisha safari yao wala haikufafanua kuhusu mipango ya benchi jipya la ufundi.

