IRINGA: WAKULIMA mkoani Iringa wamehimizwa kutumia mbegu bora na zilizoidhinishwa ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao, huku Serikali ikiimarisha mikakati ya kudhibiti mbegu bandia na kuwawezesha wakulima kupata pembejeo zenye ubora kwa wakati.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya jitihada za kuongeza uzalishaji wa kilimo mkoani humo, hasa wakati wakulima wakijiandaa kwa msimu mwingine wa kilimo, kwa kuzingatia umuhimu wa kuanza maandalizi mapema na kutumia mbegu zinazoendana na mazingira ya kilimo ya maeneo yao.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya, Wakala Mkuu wa Mbegu za Serikali (ASA) chini ya Wizara ya Kilimo pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mgongolwa Agrovet and Seeds, Joseph Mgongolwa, ameipongeza serikali kwa kuendelea kuwawezesha wakulima kupata mbegu bora za ruzuku huku ikiimarisha elimu ya kuzitambua na kuzitumia kwa usahihi.
Amesema hatua hiyo inalenga kuwakinga wakulima dhidi ya wafanyabiashara wanaouza mbegu zisizo na ubora, ambazo zinaweza kusababisha hasara kwa wakulima kutokana na kushuka kwa kiwango cha uotaji na uzalishaji.
Aidha Mgongolwa amepongeza mpango wa uwepo wa mawakala katika maeneo mbalimbali akisema utasaidia kurahisisha upatikanaji wa mbegu zilizoidhinishwa na kupunguza mianya ya wafanyabiashara wanaoweza kutumia fursa hiyo kuuza mbegu bandia.
Amesema matumizi ya mbegu bora, yakichanganywa na kanuni bora za kilimo, yana nafasi kubwa katika kuongeza tija kwa mkulima na hatimaye kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao.
Kwa upande wake, Afisa Kilimo wa Kata ya Ilolo Mpya, Oswald Kapungu, amewataka wakulima kutumia ushauri wa wataalamu wa kilimo katika kuchagua mbegu kulingana na aina ya zao, eneo na mazingira ya kilimo.
Amesema wakulima wanapaswa pia kuzingatia maandalizi ya mashamba, muda sahihi wa kupanda na matumizi sahihi ya pembejeo ili kuhakikisha mbegu bora zinatoa matokeo yanayotarajiwa.
Naye Diwani wa Kata hiyo, Patrick Muhegele, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kusikiliza changamoto za wakulima kwa kuhakikisha wanapata mbegu bora kwa gharama nafuu, akiwataka kutumia fursa hiyo kuongeza uzalishaji.
Muhegele amewataka wakulima kuanza maandalizi ya mashamba mapema na kuhakikisha wanapata mbegu kwa wakati ili kuepuka kuchelewa kuanza msimu wa kilimo.
Baadhi ya wakulima wa Kijiji cha Magozi wameishukuru Serikali kwa kuwapatia mbegu bora za ruzuku, wakisema hatua hiyo imeongeza matumaini ya kuongeza uzalishaji na kipato kupitia kilimo.
Hata hivyo, wameiomba Serikali kuendelea kuimarisha upatikanaji wa masoko ya uhakika kwa mazao yao ili ongezeko la uzalishaji liendane na fursa za kuuza mazao kwa bei nzuri.
Ikiwa ni mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye sasa anajitetea mwenyewe katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Kanda ya Dar es Salaam, Lissu amefunguka namna ambavyo mchakato wa “No Reform, No Election” ulivyoanzia ndani ya chama, akieleza kuwa msimamo huo haukuwa kauli yake binafsi, bali ulikuwa msimamo wa CHADEMA ulioanzia katika maamuzi ya chama kabla ya uchaguzi wa ndani wa uongozi.
Lissu amesema kuwa tarehe 10 Desemba 2024, Mwenyekiti wa wakati huo wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ndiye aliyetamka msimamo huo, huku chama kikisubiri kwanza uchaguzi wake wa ndani uliokuwa umepangwa kufanyika Januari 2025.
Lissu amesema kuwa tarehe 20 Januari 2025, Baraza Kuu la CHADEMA lilifanya kikao chake, ambacho kwa mujibu wa utaratibu wa chama ndicho chombo kinachopokea na kupendekeza ajenda zitakazojadiliwa katika Mkutano Mkuu. Aidha, amesema kuwa Kamati Kuu iliwasilisha mapendekezo kuhusu msimamo wa “No Reform, No Election” kwa Baraza Kuu, na baada ya kukubaliwa, suala hilo likapendekezwa kuwa ajenda ya Mkutano Mkuu wa chama uliofanyika Januari 21, 2025.
Katika Mkutano huo Mkuu, Lissu amesema, pamoja na masuala mengine ya chama, mambo mawili muhimu yalifanyika. Kwanza, ulipitishwa msimamo wa CHADEMA kuhusu “No Reform, No Election”, na pili, uchaguzi wa viongozi wa chama ulifanyika ambapo yeye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Vilevile, Lissu amesema kuwa baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti, alimteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu, huku Golugwa akiteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na kiongozi mwingine akiteuliwa kwa upande wa Zanzibar.
Baada ya uongozi huo mpya kuingia madarakani, Lissu amesema kuwa walianza maandalizi ya mkakati wa “No Reform, No Election”, ambao ulikuwa na lengo la kuhamasisha wananchi nchini kuhusu masuala ya demokrasia na mabadiliko ya kisiasa.
Amesema kuwa mpango huo haukuwa wa kupanga kufanya uhaini, kuchoma nyumba za watu au kuvunja sheria za nchi, bali ulikuwa wa kuhamasisha umma na kuwasisitiza wananchi kudai mabadiliko ya kisiasa kwa njia za kisiasa, ikiwemo mikutano na maandamano.
Aidha, Lissu amesema kuwa katika utekelezaji wa mkakati huo, walipanga kuzungumza na Watanzania kupitia makundi na taasisi mbalimbali katika maeneo yao. Amesema miongoni mwa taasisi walizoanza nazo zilikuwa taasisi za kidini, ambapo walianza na shula za maimamu.
Hata hivyo, amesema hawakuhusika na BAKWATA wala CCM. Pia, amesema waliomba kukutana na Baraza la Maaskofu, lakini hawakufanikiwa kukutana nao, huku wakifanikiwa kukutana na Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya habari na kuzungumza nao kuhusu masuala hayo.
Vilevile, Lissu amesema kuwa kwa kuwa Tanzania ina uhusiano na marafiki katika nchi nyingine, waliamua kwenda Nairobi na kukutana na Raila Odinga, ambaye wakati huo alikuwa hai, pamoja na kwenda kumuona Mzee Warioba ili kuzungumza naye kuhusu “No Reform, No Election” na msimamo wao wa kisiasa.
Aidha, amesema kuwa alialikwa katika Chuo Kikuu cha Makerere kuzungumza kuhusu Mwalimu Julius Nyerere na urithi wake, na katika mazungumzo hayo alizungumzia pia changamoto za mfumo wa kikatiba nchini. Lissu amesema kuwa baada ya kurejea nchini, majukumu yaligawanywa kwa ajili ya kuanza ziara mbalimbali.
Amesema yeye alipangiwa Kanda ya Nyasa, ambako alipaswa kuzungumza katika mikutano ya hadhara. Lissu amesisitiza kuwa katika ziara hizo hawakuwa wanapanga kufanya uhaini wala kuvunja sheria za nchi.
Amesema ziara yao ya kwanza waliimaliza Iringa tarehe 30 Machi 2025. Baada ya hapo, Naibu Katibu Mkuu Golugwa alimtumia ujumbe mfupi wa simu akimtaka kuandaa watia nia kwa ajili ya uchaguzi mkuu. Pia, amesema alitumiwa ujumbe kwamba tarehe 3 Aprili 2025 alitakiwa kufika Makao Makuu ya chama kwa ajili ya kuzungumza na watia nia hao kuhusu msimamo wa chama.
Lissu amesema tarehe 1 Aprili alirejea Dar es Salaam akiwa pamoja na John Heche kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo. Amesema mkutano huo uliofanyika kwa lengo la kuzungumza na watia nia na kuwaeleza msimamo wa CHADEMA kama chama.
Lissu amesema yeye ndiye alikuwa mzungumzaji katika mkutano huo, na kwamba hilo lilikuwa jukumu lake la kuzungumza baada ya mkutano kuandaliwa na taarifa kutolewa na Katibu Mkuu. Kwa msingi huo, Lissu amesema anashangaa kusikia kwamba yeye ndiye aliyeandaa mkutano huo. Amesema kama wangeuliza ni nani aliyeuandaa, wangeweza kupata majibu kuhusu mtu aliyekuwa na jukumu hilo.
Aidha, amesema yeye alipewa taarifa na Katibu Mkuu kuhusu jukumu lake la kwenda kuzungumza katika mkutano huo, hivyo kuwa mzungumzaji hakumaanishi kwamba ndiye aliyekuwa mratibu au mwandaaji wa mkutano.
Lissu amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani na mashahidi 17 pia unaibua maswali. Amesema kuna maneno katika ushahidi huo ambayo, ukisoma tu, hayangeweza hata kuchukua dakika moja, wakati mkutano wake ulikuwa mrefu sana. Kuhusu video ambayo anadaiwa kuichapisha kupitia Jambo TV, Lissu amesema hajawahi kuiona hadi leo.
Kwa hiyo, amesema akiulizwa alitumia dakika ngapi kwenye video hiyo, hawezi kutoa jibu kwa sababu hajawahi kuiona. Lissu amesema siku hiyo ya mkutano aliulizwa maswali mengi na alijibu maswali yote, akisisitiza kuwa mkutano huo ulikuwa wa zaidi ya saa tatu.
Aidha, amesema hakufanikiwa kuiona video hiyo kwa sababu kesho yake, tarehe 4 Aprili 2025, walielekea katika ziara mkoani Ruvuma.
Amesema tarehe 9 Aprili 2025, alipokuwa akielekea kumaliza mkutano wake jioni huko Mbinga, alikamatwa na kupigwa kabla ya kupelekwa katika kituo cha polisi Mbinga. Baadaye, amesema alihamishiwa Songea mjini, katika ofisi ya RPC.
Akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi, Lissu amesema alieleza kuwa alikuwa na njaa na kuwaambia polisi kwamba alikuwa na dada yake katika eneo hilo ambaye angeweza kumletea chakula. Amesema majira ya saa nne usiku chakula kilifika na baadaye usiku alipelekwa Dar es Salaam. Lissu amesema kwa mtazamo wake, shahidi pekee aliyesema ukweli ni P17, huku akidai mashahidi wengine walitoa maelezo ambayo hayakuwa sahihi.
Amesema P17 ndiye aliyesema kuwa yeye ndiye aliyekuwa amechapisha maudhui hayo mtandaoni, siyo Lissu. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, Lissu amesema P17 alipata taarifa kutoka kwa bosi wake, John Marwa, ambaye naye alikuwa amepewa taarifa na Ofisa Habari wa chama, Brenda Rupia. Hapo ndipo Lissu anapoona mkanganyiko mkubwa katika upande wa mashtaka.
Amesema upande wa mashtaka unamhusisha yeye na uchapishaji wa maudhui hayo mtandaoni, wakati wao wenyewe walimleta P17 kama shahidi na P17 akaeleza kuwa yeye ndiye aliyerusha maudhui hayo mtandaoni. Vilevile, Lissu amesema upande wa mashtaka unadai kuwa yeye ndiye aliyeandaa mkutano, wakati kwa maelezo yake yeye alikuwa mzungumzaji tu na mkutano uliandaliwa na chama, huku taarifa kuhusu kushiriki kwake akipewa na Katibu Mkuu.
Kwa hiyo, Lissu amesema kama kweli kulikuwa na mtu aliyekuwa na jukumu la kuandaa mkutano huo, ushahidi ulipaswa kuelekeza kwa mhusika aliyekuwa na jukumu hilo, badala ya kumhusisha yeye kwa sababu tu alikuwa mzungumzaji wa mkutano.
TANGA; Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na taasisi zake kuhakikisha bunifu zinazozalishwa na Watanzania haziishii kuoneshwa kwenye maonesho, bali zinaendelezwa, zinalindwa na kupelekwa sokoni, ili zitoe suluhisho kwa changamoto mbalimbali na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Waziri Mkuu ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu, Agosti 24, 2026, jijini Tanga wakati akihitimisha Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu, akisisitiza umuhimu wa kujenga mfumo unaowawezesha wabunifu kubadilisha mawazo yao kuwa bidhaa na huduma zenye tija.
Amesema Tanzania ina wabunifu wenye uwezo mkubwa katika maeneo mbalimbali, hivyo hatua inayohitajika sasa ni kuhakikisha ubunifu huo unavuka hatua ya kuoneshwa kwenye maonesho na kufikia hatua ya kutumika, kuzalishwa kwa wingi na kuuzwa sokoni.
“Ni lazima tuvuke kwenye maonesho, twende kwenye uhalisia wa maisha kwamba hivi vitu ambavyo tunavionyesha kwenye maadhimisho kama haya sasa viende kwenye utaratibu wa kila siku wa maisha, tuvitengeneze vya kutosha, vitumike na viingie sokoni,” amesema Dk Mwigulu.
Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika sayansi, ujuzi na ubunifu kwa lengo la kuyageuza maeneo hayo kuwa nguzo muhimu za uchumi wa Taifa na kuchochea maendeleo kupitia matumizi ya tafiti na teknolojia.
“Hatutaweza kuendelea bila kuwa na sayansi, teknolojia na tafiti na tukatumia matokeo ya tafiti hizo. Hatutapata tija bila kutumia matokeo ya tafiti hizo,” amesema.
Dk Mwigulu pia amesema Serikali haitakubali kushusha viwango vya elimu, akisisitiza umuhimu wa taasisi zinazosimamia ubora wa elimu kuendelea kusimamia misingi ya kitaaluma katika kuandaa wataalamu wenye uwezo unaokubalika.
“Tusitengeneze mazingira yawe rahisi ya kujifunza, yawe na alama kubwa kubwa, lakini kazini kuwe na zero kubwa kubwa. Hiyo hapana. Lazima tusimamie misingi ya elimu,” amesema.
Amesisitiza kuwa katika sekta nyeti kama afya, uhandisi na elimu, ubora wa mafunzo haupaswi kuchezewa.
“Hatuwezi kucheza na afya za Watanzania… Hatuwezi tukaandaa wataalamu kwa namna duni duni hivi, tutaharibu sekta yote. Tunataka walimu walio bora, maengineia walio bora; wakijenga daraja, wakijenga jengo, liwe jengo kweli kweli,” amesema.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameagiza mipango ya maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Tanga iangalie mahitaji ya kiuchumi na kijamii ya mkoa huo kwa kipindi cha miaka 25 ijayo, ili miundombinu inayojengwa sasa iendane na ukuaji wa uchumi, biashara, uwekezaji na ongezeko la matumizi ya usafiri wa anga.
“Lazima tunapojenga tuwaze mbele, tusijenge kwa ajili ya leo. Tuwaze mbele miaka 20 mbele, 25 mbele, kama ambavyo Dira yetu inatuambia,” amesema Dk Mwigulu.
Amesema uwanja huo unapaswa kujengwa kwa hadhi ya Tanga kama lango muhimu la shughuli za kiuchumi kutokana na miradi mikubwa inayotekelezwa katika mkoa huo.
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ProF Adolf Mkenda amesema maonesho hayo yanaakisi jitihada za Serikali katika kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuimarisha elimu inayounganisha nadharia na vitendo, ili kuandaa wahitimu wenye ujuzi wa kujiajiri na kuingia kwa ufanisi katika soko la ajira.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof Caroline Nombo amesema jumla ya taasisi 91 za umma na binafsi zimeshiriki katika maadhimisho hayo, ambayo yamehusisha maonesho ya elimu, sayansi, teknolojia na ubunifu, mashindano ya kitaifa ya ujuzi na ubunifu pamoja na makongamano yaliyolenga kujadili mchango wa elimu, ujuzi na teknolojia katika kufikia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Husna Sekiboko amesema Bunge litaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kuendeleza elimu, ujuzi na ubunifu kupitia bajeti, sera na miongozo inayolenga kuwawezesha watafiti na wabunifu wa ndani kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
Amesema kuna umuhimu wa kuzipa kipaumbele bidhaa na teknolojia zinazozalishwa nchini, zikiwemo katika taasisi za Serikali, ili kuongeza matumizi ya bunifu za Watanzania na kuchochea ukuaji wa wabunifu hao.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilda Buriani amesema uwekezaji wa Serikali katika sekta ya elimu umeendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia mkoani humo, kuongeza miundombinu na kuchochea mafanikio ya wanafunzi, huku akipongeza maonesho hayo kwa kuibua na kuonesha uwezo mkubwa wa Watanzania katika sayansi, teknolojia na ubunifu.
Global Publishers August 24, 2026 18 views 0 Comments
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, amelipongeza Kanisa Katoliki kwa mchango wake katika kuhubiri amani na utulivu nchini Tanzania.
Shigongo ametoa kauli hiyo wakati wa Jubilee ya Miaka 25 ya Upadri ya Padre Cleophace Magesa, iliyofanyika nyumbani kwao katika Kigango cha Itulabusiga, Parokia ya Mwangia ya Mwangika.
Amesema madhehebu mbalimbali ya dini yamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha amani nchini, akisisitiza kuwa amani ni msingi muhimu wa maisha ya jamii.
“Hivyo, tuendelee kuwaombea viongozi wa dini kwa kazi waliyonayo ya kuhubiri amani na utulivu ndani ya nchi yetu,” amesema Shigongo.
Aidha, Shigongo amesema juhudi za viongozi wa dini katika kuhubiri amani zinapaswa kuthaminiwa na kuungwa mkono kutokana na nafasi yao katika kujenga jamii yenye mshikamano na utulivu.
Global Publishers August 24, 2026 414 views 0 Comments
Yanga SC leo Agosti 24, 2026 inatarajiwa kushuka dimbani kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex kuanzia saa 18:00 jioni.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Yanga ikilenga kuendelea na mwenendo mzuri katika msimu huu, wakati JKT Tanzania ikisaka matokeo mazuri dhidi ya mabingwa hao.
Akizungumzia mchezo huo, Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, amesema mashabiki wamekuwa wakisubiri kwa muda kuona timu yao ikicheza katika uwanja huo.
“Mashabiki wameusubiri kwa muda mchezo huo na sasa siku imefika ya kuiona timu yao ikicheza katika Uwanja wa KMC,” amesema Ali Kamwe.
Aidha, Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kukata tiketi kupitia simu zao ili kuepuka usumbufu wakati wa kuingia uwanjani.
Mashabiki wa Yanga wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi KMC Complex kushuhudia mchezo huo, huku klabu ikiwataka kufanya maandalizi mapema kwa kukata tiketi kabla ya kwenda uwanjani.
Mchezo huo unaongeza hamasa katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, huku macho ya mashabiki yakielekezwa KMC Complex kusubiri kuona nani ataibuka na pointi tatu.
Global Publishers August 24, 2026 6 views 0 Comments
Yanga SC leo Agosti 24, 2026 inatarajiwa kushuka dimbani kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex kuanzia saa 18:00 jioni.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Yanga ikilenga kuendelea na mwenendo mzuri katika msimu huu, wakati JKT Tanzania ikisaka matokeo mazuri dhidi ya mabingwa hao.
Akizungumzia mchezo huo, Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, amesema mashabiki wamekuwa wakisubiri kwa muda kuona timu yao ikicheza katika uwanja huo.
“Mashabiki wameusubiri kwa muda mchezo huo na sasa siku imefika ya kuiona timu yao ikicheza katika Uwanja wa KMC,” amesema Ali Kamwe.
Aidha, Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kukata tiketi kupitia simu zao ili kuepuka usumbufu wakati wa kuingia uwanjani.
Mashabiki wa Yanga wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi KMC Complex kushuhudia mchezo huo, huku klabu ikiwataka kufanya maandalizi mapema kwa kukata tiketi kabla ya kwenda uwanjani.
Mchezo huo unaongeza hamasa katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, huku macho ya mashabiki yakielekezwa KMC Complex kusubiri kuona nani ataibuka na pointi tatu.
Klabu ya Simba leo Agosti 24, 2026 imetangaza kurejea kutumia Uwanja wa Meja Isamuhyo kama uwanja wake wa nyumbani katika mechi za Ligi Kuu ya NBC, baada ya awali kutangaza kutumia Uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Semaji wa Simba, Ahmed Ally, amesema uamuzi huo umetokana na mafanikio ambayo timu hiyo ilipata msimu uliopita ilipotumia Meja Isamuhyo, akisema uwanja huo umekuwa sehemu salama kwa Simba.
“Msimu uliopita ambao tulicheza kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo hatukupoteza mchezo hata mmoja, ni sehemu salama kwelikweli kwa upande wetu,” amesema Ahmed Ally.
Amesema Simba itaanza kutumia uwanja huo kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, unaotarajiwa kuchezwa Agosti 27, 2026.
Katika mchezo huo, kiingilio kimewekwa Sh5,000 kwa jukwaa la Mzunguko na Sh10,000 kwa VIP A. Pia Simba imewataka mashabiki wake kujiandaa kutumia mfumo mpya wa ununuzi wa tiketi kwa njia ya simu.
Ahmed amesema mfumo huo unalenga kuwawezesha mashabiki kununua tiketi wakiwa walipo bila kulazimika kwenda vituoni kupanga foleni.
Mbali na Ligi Kuu, Simba imeeleza mipango yake katika mashindano ya kimataifa, ambapo itaanza hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers ya Malawi.
Mchezo wa kwanza utachezwa Septemba 6, 2026 nchini Malawi, huku mechi ya marudiano ikipangwa Septemba 13, 2026 jijini Dar es Salaam. Simba imesema uwanja utakaotumika katika mchezo wa marudiano utatangazwa baadaye.
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka nchini Septemba 4 kuelekea Malawi, ambapo kitafanya mazoezi siku hiyo na Septemba 5 kabla ya kushuka dimbani Septemba 6.
Ahmed Ally amesema Simba imefanya tathmini ya kutosha baada ya kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali msimu uliopita, huku usajili wa wachezaji wenye uzoefu ukitajwa kuwa sehemu ya mkakati wa kurejea kwenye ushindani mkubwa Afrika.
“Ni imani yetu mwaka huu tutavuka hatua ya makundi na kwenda robo fainali. Malengo yetu makubwa ya msimu huu kimataifa ni kucheza hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema.
Simba pia imeandaa safari maalum ya basi kwa mashabiki wake watakaotaka kwenda Malawi kuishangilia timu dhidi ya Mighty Wanderers.
Safari hiyo itaanza Septemba 3, 2026 saa 1 usiku kutoka Ubungo, Dar es Salaam, kuelekea Lilongwe, Malawi.
Klabu hiyo imesema inalenga kuwa na angalau mabasi matatu ya mashabiki, huku wanaotaka kusafiri wakitakiwa kuwa na hati ya kusafiria.
Kwa mujibu wa Ahmed Ally, safari hiyo inalenga kuongeza nguvu ya mashabiki kwa timu na kuvunja rekodi ya idadi ya Wanasimba watakaosafiri kwenda kuishangilia timu yao nje ya nchi.
Global Publishers August 24, 2026 48 views 0 Comments
Burudani ya kasino imepata ladha mpya baada ya Wild 4th Fruits kuwasili Meridianbet ukiwa na muonekano unaovutia na mfumo wa uchezaji uliotengenezwa kwa urahisi. Mchezo huu unawaleta wachezaji katika dunia iliyojaa matunda yenye rangi angavu, mazingira yenye uhai na msisimko unaojengwa kila unapocheza. Kwa wale wanaopenda michezo yenye mguso wa kisasa, Wild 4th Fruits ni moja ya chaguo jipya linaloweza kuongeza ladha kwenye burudani yako.
Kama ilivyo kwenye mchezo wowote wenye mvuto, mwanzo wa safari ndio unaochochea hamu ya kuendelea. Wild 4th Fruits imeundwa kwa mtindo unaorahisisha mchezaji kuingia moja kwa moja kwenye burudani bila kulazimika kupitia mfumo mgumu. Kila raundi inafungua ukurasa mpya, huku alama za matunda zikitoa mandhari inayokumbusha michezo ya kasino ya kizazi cha zamani.
Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Moja ya vitu vinavyoweza kuwavutia wachezaji ni kasi tulivu ya Wild 4th Fruits. Mchezo haujajengwa kukufanya uhisi kama unakimbizana na muda, bali unakupa nafasi ya kufurahia kila raundi na kila tukio linalotokea kwenye skrini. Hii inaufanya uwe rafiki kwa wachezaji wanaotafuta burudani rahisi baada ya siku ndefu au wanaotaka kujaribu mchezo mpya wenye mazingira mepesi.
Tayari mchezo huu umeanza kuvutia umakini kutokana na simulizi za ushindi miongoni mwa wachezaji wa Meridianbet. Kwa hiyo, Wild 4th Fruits inaweza kuwa sehemu ya burudani yako ikiwa utaicheza huku ukifurahia muonekano wake wa kipekee na safari ya kila mzunguko.
Sasa ni wakati wa kufungua mlango wa dunia yenye matunda, rangi na burudani mpya kupitia Wild 4th Fruits. Xpanse imeleta mchezo unaochanganya urahisi wa michezo na mwonekano unaoendana na kizazi cha sasa. Kama unapenda kuona kila raundi ikileta tukio jipya, mchezo huu unakualika kuuchunguza na kufurahia kila sekunde.
DAR ES SALAAM: SHIRIKA la Uvuvi Tanzania (TAFICO), limesaini mkataba wa ujenzi wa meli mbili za uvuvi wa bahari kuu na Kampuni ya Rongcheng Xinyang Ship Industry Limited ya China, ikiwa ni hatua ya kuimarisha na kuongeza tija katika sekta ya uvuvi nchini.
Mkataba huo umesainiwa leo, Agosti 24, 2026,Jijini Dar es Salaam kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) inayofadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD).
Akizungumza wakati wa kushuhudia utiaji saini wa mkataba huo, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk Bashiru Kakurwa, amesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025 pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kwa lengo la kuleta mapinduzi katika sekta ya uvuvi.
Dk Kakurwa ameishukuru IFAD kwa ufadhili wa ujenzi wa meli hizo kupitia AFDP, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi katika kufungua fursa zaidi za uvuvi wa bahari kuu na kukuza uchumi wa Taifa.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dk Jim Yonazi, amesema Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa Mratibu Mkuu wa AFDP, inatambua utiaji saini wa mkataba huo kuwa hatua muhimu katika utekelezaji wa programu hiyo.
Amesema ujenzi wa meli hizo ni hatua itakayochangia ukuzaji wa uchumi kupitia uvuvi wa bahari kuu, pamoja na kuongeza uwezo wa Tanzania kutumia kikamilifu rasilimali zake za bahari.
Naye Mratibu wa AFDP kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Salum Mwinjaka, amesema utiaji saini wa mkataba huo ni hatua muhimu katika kuhakikisha malengo ya programu yanafikiwa kwa wakati na utekelezaji wake unakuwa na mafanikio.
Amesema Serikali inalenga kuhakikisha walengwa wa programu pamoja na Taifa kwa ujumla wananufaika na fursa zinazotokana na utekelezaji wa AFDP.
AFDP inalenga kukuza uzalishaji endelevu wa kibiashara unaozingatia mazingira, hususan katika uzalishaji wa mbegu za mazao ya kilimo kama mahindi, alizeti, maharagwe na jamii ya mikunde, pamoja na uvuvi na ufugaji wa viumbe maji.
Programu hiyo pia inalenga kuwawezesha wanawake na kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za uzalishaji.
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Wahusika, Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shaban Ally Lila.
Dar es Salaam, Agosti 24, 2026 — Tume ya Kuchunguza Wahusika, Ghasia na Ukiukwaji wa Sheria Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 imeanza rasmi kazi, huku Mwenyekiti wake, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Shaban Ally Lila, akieleza kuwa lengo kuu ni kubaini wahusika wa ghasia hizo na namna walivyoshiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jaji Lila amesema Tume hiyo imepewa jukumu la kuchunguza matukio ya ghasia, uvunjifu wa amani na madhara yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi huo.
Amesema Tume itachunguza pia chanzo cha ghasia hizo pamoja na ukiukwaji wa sheria uliojitokeza, ikiwemo kubaini watu waliohusika katika kupanga, kufadhili, kuratibu na kutekeleza matukio hayo.
Kwa mujibu wa Jaji Lila, Tume hiyo ina jukumu tofauti na Tume iliyokuwa chini ya Jaji Mstaafu Othman Chande, ambayo ilichunguza zaidi matukio ya ghasia na madhara yaliyotokea.
Tume mpya imepewa jukumu la kwenda hatua zaidi kwa kuchunguza wahusika wa ghasia hizo, namna walivyoshiriki na kiwango cha nguvu kilichotumika katika kudhibiti vurugu hizo.
Jaji Lila amesema Tume pia itachunguza madhara yaliyotokana na ghasia hizo, yakiwemo vifo, majeruhi na watu waliopotea.
Amesema Tume iliyokuwa chini ya Jaji Chande ilibainisha vifo vya watu 518, huku ikieleza kuwa huenda idadi hiyo ilikuwa kubwa zaidi kwa sababu si waathirika wote waliweza kufikiwa au kutambuliwa.
Katika utekelezaji wa majukumu yake, Tume ya Jaji Lila imepewa hadidu tano za rejea.
Hadidu ya kwanza ni kuchunguza na kubainisha wahusika wa ghasia na namna walivyoshiriki katika kupanga, kufadhili, kuratibu au kutekeleza matukio hayo.
Hadidu ya pili ni kuchunguza matukio mahsusi yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi, ikiwemo madai ya vifo visivyo vya kawaida vya watoto na watu wa makundi maalum.
Hadidu ya tatu ni kuchunguza taarifa za watu waliopotea katika maeneo yaliyokumbwa na ghasia na uvunjifu wa amani.
Hadidu ya nne ni kuchunguza madai ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kubaini iwapo taratibu na miongozo ya matumizi ya nguvu ilizingatiwa.
Hadidu ya tano inalipa Tume nafasi ya kuchunguza suala lolote litakaloonekana kuwa muhimu na linalohusiana na majukumu yake.
Jaji Lila amesema Tume imeundwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuzinduliwa rasmi Agosti 7, 2026.
Tume hiyo inaongozwa na Jaji Mstaafu Shaban Ally Lila na inajumuisha majaji wastaafu wa Mahakama Kuu, akiwemo Jaji Gad Mjemmas, Jaji Awadh Bawazir na Jaji Aishieli Sumari, pamoja na wajumbe kutoka nje ya Tanzania, akiwemo Naibu Jaji Mkuu wa Namibia na Jaji Cheborion Barishaki kutoka Uganda.