Yanga Yaichapa JKT Tanzania 4-0, Yarudi Kileleni Ligi Kuu Bara

Yanga SC imeendeleza mwanzo wake mzuri katika msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa JKT Tanzania mabao 4-0 katika mchezo uliochezwa jana, Agosti 24, 2026, kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Yanga ilianza kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kwanza dakika ya 29 kupitia Albert Kangwanda, aliyefungua ukurasa wa mabao na kuipa timu yake uongozi wa 1-0.

Dakika tano baadaye, Ibrahim Bacca aliifungia Yanga bao la pili dakika ya 34, akimalizia pasi ya Zoukaine na kuongeza presha kwa JKT Tanzania.

Yanga iliendelea kutawala mchezo na juhudi zake zilizaa matunda tena dakika ya 39, ambapo Chadrack Boka alifunga bao la tatu akitumia pasi ya Kangwanda, na kuifanya Yanga kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili, Yanga iliendelea kutawala mchezo huku JKT Tanzania ikishindwa kupata njia ya kurejea mchezoni.

Dakika ya 64, mshambuliaji Peter Shalulile alikamilisha ushindi wa Yanga kwa kufunga bao la nne, akitumia asisti ya Kangwanda na kuifanya timu hiyo kushinda kwa mabao 4-0.

Kangwanda alikuwa miongoni mwa wachezaji walioangaza zaidi katika mchezo huo, akihusika moja kwa moja katika mabao matatu baada ya kufunga bao moja na kutoa asisti mbili. Kiwango hicho kilimfanya atambuliwe kuwa mchezaji bora wa mechi.

Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha ushindi wa tatu katika michezo mitatu ya Ligi Kuu Bara msimu huu. Katika michezo hiyo, mabingwa hao wamefunga jumla ya mabao 11 na kuruhusu mawili pekee.

Matokeo hayo pia yanaifanya Yanga kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi, huku ikiendelea kuweka presha katika mbio za kuwania ubingwa wa msimu wa 2026/27.

Mwanzo huo wa kuvutia unaendelea kuipa Yanga matumaini ya kutetea taji lake, huku safu yake ya ushambuliaji ikionyesha makali katika michezo ya awali ya msimu.

Stori na Na Haika Urio | GPL – TUDACO

Southampton Yawakaribisha West Ham Katika Pambano la Carabao Cup

Southampton na West Ham United watakutana leo Jumanne, Agosti 25, 2026, katika raundi ya pili ya Carabao Cup (EFL Cup). Mechi hii itachezwa katika uwanja wa St. Mary’s Stadium, na itaanza saa 7:45 jioni kwa saa za Uingereza (BST) sawa na saa 21:45 usiku, Timu zote mbili kwa sasa zinashindana katika ligi ya Championship, hivyo hii ni mechi ya “ndugu” itakayovutia mashabiki wengi.

Kwa upande wa Southampton, msimu huu unafuatia msimu wenye taharuki baada ya kashfa maarufu ya “Spygate” iliyowagharimu nafasi ya fainali ya kuwapandisha daraja msimu uliopita, ambapo walikuwa vipenzi vya kushinda na kurejea Premier League.

Chini ya kocha mpya Tonda Eckert, Saints walianza msimu vizuri kwa kuwafunga Colchester United mabao 2-0 katika raundi ya kwanza ya kombe hili, huku Cyle Larin akifungua bao dakika ya 72 na Romeo Akachukwu, aliyekuwa akikopeshwa Colchester msimu uliopita, akiongeza bao la pili muda wa nyongeza.

Hata hivyo, ushindi huo ulifuatiwa na kushindwa 2-1 dhidi ya Watford katika mchezo wao wa kwanza wa ligi. Baadaye walipata nafuu kidogo baada ya kuwafunga Stoke City kwa msaada wa mabao ya Larin na Divin Mubama, pamoja na penalti ya marehemu ya Ryan Manning, huku Stoke wakichezea watu kumi baada ya Svante Ingelsson kufukuzwa uwanjani.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

West Ham United, ambao msimu huu wanacheza Championship kwa mara ya kwanza baada ya kushuka daraja kutoka Premier League, wanaingia mechini wakiwa na kina kikubwa zaidi cha kikosi ikilinganishwa na wenyeji.

Chini ya kocha Nuno EspĂ­rito Santo, Hammers walionesha nguvu kubwa ya mashambulizi katika raundi ya kwanza walipowaangamiza Portsmouth mabao 3-1, ambapo ValentĂ­n Castellanos alifunga mabao mawili (brace) na Jarrod Bowen naye akiongeza bao.

 

Matokeo hayo yanaonesha kikosi chenye nguvu halisi ya kufunga mabao. Hata hivyo, taarifa zinaonesha kuwa Nuno anaweza kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi baada ya kushindwa hivi karibuni dhidi ya Charlton.

 

Kwa muhtasari, mechi hii inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa kati ya timu mbili za Championship zenye historia ndefu. Southampton watatafuta kutumia nguvu ya uwanjani kwao kujirekebisha baada ya kuanza vibaya ligi, huku West Ham wakitegemea nguvu ya mashambulizi yao na upana wa kikosi kuendelea na msimamo wao mzuri katika kombe hili kuelekea raundi ya tatu.

 

 

Nafasi za Kazi kwa Wanawake – Wahudumu wa Maduka Mlimani City na Posta

Global Publishers
August 25, 2026
1,086 views
0 Comments

Nafasi za kazi zimetangazwa kwa wanawake pekee kwa ajili ya kufanya kazi kama Wahudumu wa Maduka katika maeneo ya Mlimani City na Posta, Dar es Salaam.

Mshahara: TSh 450,000 kwa mwezi.

Sifa za mwombaji:

  • Awe mwanamke.
  • Awe mchapakazi, mwaminifu na mwenye nidhamu.
  • Awe na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wateja.
  • Uzoefu wa kazi ni faida.

Jinsi ya kuomba

Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kupitia WhatsApp: 0747065803.

Kumbuka: Nafasi hizi ni kwa wanawake pekee na nafasi ni chache. Waombaji wanashauriwa kutuma maombi mapema.

Tundu Lissu Afunguka Hadharani; Nimepigania Haki Tangu Nikiwa Shuleni – Video

Ikiwa ni mwendelezo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye sasa anajitetea mwenyewe katika Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Kanda ya Dar es Salaam, Lissu amefunguka namna ambavyo mchakato wa “No Reform, No Election” ulivyoanzia ndani ya chama, akieleza kuwa msimamo huo haukuwa kauli yake binafsi, bali ulikuwa msimamo wa CHADEMA ulioanzia katika maamuzi ya chama kabla ya uchaguzi wa ndani wa uongozi.

Lissu amesema kuwa tarehe 10 Desemba 2024, Mwenyekiti wa wakati huo wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ndiye aliyetamka msimamo huo, huku chama kikisubiri kwanza uchaguzi wake wa ndani uliokuwa umepangwa kufanyika Januari 2025.

Lissu amesema kuwa tarehe 20 Januari 2025, Baraza Kuu la CHADEMA lilifanya kikao chake, ambacho kwa mujibu wa utaratibu wa chama ndicho chombo kinachopokea na kupendekeza ajenda zitakazojadiliwa katika Mkutano Mkuu. Aidha, amesema kuwa Kamati Kuu iliwasilisha mapendekezo kuhusu msimamo wa “No Reform, No Election” kwa Baraza Kuu, na baada ya kukubaliwa, suala hilo likapendekezwa kuwa ajenda ya Mkutano Mkuu wa chama uliofanyika Januari 21, 2025.

Katika Mkutano huo Mkuu, Lissu amesema, pamoja na masuala mengine ya chama, mambo mawili muhimu yalifanyika. Kwanza, ulipitishwa msimamo wa CHADEMA kuhusu “No Reform, No Election”, na pili, uchaguzi wa viongozi wa chama ulifanyika ambapo yeye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Vilevile, Lissu amesema kuwa baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti, alimteua John Mnyika kuwa Katibu Mkuu, huku Golugwa akiteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na kiongozi mwingine akiteuliwa kwa upande wa Zanzibar.

Baada ya uongozi huo mpya kuingia madarakani, Lissu amesema kuwa walianza maandalizi ya mkakati wa “No Reform, No Election”, ambao ulikuwa na lengo la kuhamasisha wananchi nchini kuhusu masuala ya demokrasia na mabadiliko ya kisiasa.

Amesema kuwa mpango huo haukuwa wa kupanga kufanya uhaini, kuchoma nyumba za watu au kuvunja sheria za nchi, bali ulikuwa wa kuhamasisha umma na kuwasisitiza wananchi kudai mabadiliko ya kisiasa kwa njia za kisiasa, ikiwemo mikutano na maandamano.

Aidha, Lissu amesema kuwa katika utekelezaji wa mkakati huo, walipanga kuzungumza na Watanzania kupitia makundi na taasisi mbalimbali katika maeneo yao. Amesema miongoni mwa taasisi walizoanza nazo zilikuwa taasisi za kidini, ambapo walianza na shula za maimamu.

Hata hivyo, amesema hawakuhusika na BAKWATA wala CCM. Pia, amesema waliomba kukutana na Baraza la Maaskofu, lakini hawakufanikiwa kukutana nao, huku wakifanikiwa kukutana na Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya habari na kuzungumza nao kuhusu masuala hayo.

Vilevile, Lissu amesema kuwa kwa kuwa Tanzania ina uhusiano na marafiki katika nchi nyingine, waliamua kwenda Nairobi na kukutana na Raila Odinga, ambaye wakati huo alikuwa hai, pamoja na kwenda kumuona Mzee Warioba ili kuzungumza naye kuhusu “No Reform, No Election” na msimamo wao wa kisiasa.

Aidha, amesema kuwa alialikwa katika Chuo Kikuu cha Makerere kuzungumza kuhusu Mwalimu Julius Nyerere na urithi wake, na katika mazungumzo hayo alizungumzia pia changamoto za mfumo wa kikatiba nchini.
Lissu amesema kuwa baada ya kurejea nchini, majukumu yaligawanywa kwa ajili ya kuanza ziara mbalimbali.

Amesema yeye alipangiwa Kanda ya Nyasa, ambako alipaswa kuzungumza katika mikutano ya hadhara. Lissu amesisitiza kuwa katika ziara hizo hawakuwa wanapanga kufanya uhaini wala kuvunja sheria za nchi.

Amesema ziara yao ya kwanza waliimaliza Iringa tarehe 30 Machi 2025. Baada ya hapo, Naibu Katibu Mkuu Golugwa alimtumia ujumbe mfupi wa simu akimtaka kuandaa watia nia kwa ajili ya uchaguzi mkuu. Pia, amesema alitumiwa ujumbe kwamba tarehe 3 Aprili 2025 alitakiwa kufika Makao Makuu ya chama kwa ajili ya kuzungumza na watia nia hao kuhusu msimamo wa chama.

Lissu amesema tarehe 1 Aprili alirejea Dar es Salaam akiwa pamoja na John Heche kwa ajili ya maandalizi ya mkutano huo. Amesema mkutano huo uliofanyika kwa lengo la kuzungumza na watia nia na kuwaeleza msimamo wa CHADEMA kama chama.

Lissu amesema yeye ndiye alikuwa mzungumzaji katika mkutano huo, na kwamba hilo lilikuwa jukumu lake la kuzungumza baada ya mkutano kuandaliwa na taarifa kutolewa na Katibu Mkuu.
Kwa msingi huo, Lissu amesema anashangaa kusikia kwamba yeye ndiye aliyeandaa mkutano huo. Amesema kama wangeuliza ni nani aliyeuandaa, wangeweza kupata majibu kuhusu mtu aliyekuwa na jukumu hilo.

Aidha, amesema yeye alipewa taarifa na Katibu Mkuu kuhusu jukumu lake la kwenda kuzungumza katika mkutano huo, hivyo kuwa mzungumzaji hakumaanishi kwamba ndiye aliyekuwa mratibu au mwandaaji wa mkutano.

Lissu amesema ushahidi uliowasilishwa mahakamani na mashahidi 17 pia unaibua maswali. Amesema kuna maneno katika ushahidi huo ambayo, ukisoma tu, hayangeweza hata kuchukua dakika moja, wakati mkutano wake ulikuwa mrefu sana. Kuhusu video ambayo anadaiwa kuichapisha kupitia Jambo TV, Lissu amesema hajawahi kuiona hadi leo.

Kwa hiyo, amesema akiulizwa alitumia dakika ngapi kwenye video hiyo, hawezi kutoa jibu kwa sababu hajawahi kuiona.
Lissu amesema siku hiyo ya mkutano aliulizwa maswali mengi na alijibu maswali yote, akisisitiza kuwa mkutano huo ulikuwa wa zaidi ya saa tatu.

Aidha, amesema hakufanikiwa kuiona video hiyo kwa sababu kesho yake, tarehe 4 Aprili 2025, walielekea katika ziara mkoani Ruvuma.

Amesema tarehe 9 Aprili 2025, alipokuwa akielekea kumaliza mkutano wake jioni huko Mbinga, alikamatwa na kupigwa kabla ya kupelekwa katika kituo cha polisi Mbinga. Baadaye, amesema alihamishiwa Songea mjini, katika ofisi ya RPC.

Akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi, Lissu amesema alieleza kuwa alikuwa na njaa na kuwaambia polisi kwamba alikuwa na dada yake katika eneo hilo ambaye angeweza kumletea chakula. Amesema majira ya saa nne usiku chakula kilifika na baadaye usiku alipelekwa Dar es Salaam.
Lissu amesema kwa mtazamo wake, shahidi pekee aliyesema ukweli ni P17, huku akidai mashahidi wengine walitoa maelezo ambayo hayakuwa sahihi.

Amesema P17 ndiye aliyesema kuwa yeye ndiye aliyekuwa amechapisha maudhui hayo mtandaoni, siyo Lissu. Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa, Lissu amesema P17 alipata taarifa kutoka kwa bosi wake, John Marwa, ambaye naye alikuwa amepewa taarifa na Ofisa Habari wa chama, Brenda Rupia.
Hapo ndipo Lissu anapoona mkanganyiko mkubwa katika upande wa mashtaka.

Amesema upande wa mashtaka unamhusisha yeye na uchapishaji wa maudhui hayo mtandaoni, wakati wao wenyewe walimleta P17 kama shahidi na P17 akaeleza kuwa yeye ndiye aliyerusha maudhui hayo mtandaoni.
Vilevile, Lissu amesema upande wa mashtaka unadai kuwa yeye ndiye aliyeandaa mkutano, wakati kwa maelezo yake yeye alikuwa mzungumzaji tu na mkutano uliandaliwa na chama, huku taarifa kuhusu kushiriki kwake akipewa na Katibu Mkuu.

Kwa hiyo, Lissu amesema kama kweli kulikuwa na mtu aliyekuwa na jukumu la kuandaa mkutano huo, ushahidi ulipaswa kuelekeza kwa mhusika aliyekuwa na jukumu hilo, badala ya kumhusisha yeye kwa sababu tu alikuwa mzungumzaji wa mkutano.



Fahamu Kanisa la ajabu Barcelona, Ujenzi wake Wachukua Miaka 140

Global Publishers
August 25, 2026
36 views
0 Comments

Ukiambiwa kuna kanisa ambalo ujenzi wake umechukua zaidi ya miaka 140 na bado haujakamilika, huenda ukashangaa. Lakini hali hiyo ipo katika jiji la Barcelona nchini Hispania, ambako kuna kanisa maarufu la Sagrada FamĂ­lia.

Ujenzi wa kanisa hilo ulianza mwaka 1882, kabla ya mbunifu Antoni GaudĂ­ kuchukua jukumu la kuendeleza usanifu wake. GaudĂ­ alilitumia sehemu kubwa ya maisha yake katika kulibuni na kulisimamia, lakini alifariki mwaka 1926 kabla ya kukamilika.

Baada ya kifo chake, ujenzi uliendelea kwa kutegemea michango na misaada ya watu binafsi. Hata hivyo, safari ya ujenzi haikuwa rahisi.

Mwaka 1936, wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Hispania, sehemu ya nyaraka, michoro na vielelezo vya GaudĂ­ ziliharibiwa, jambo lililosababisha changamoto kubwa kwa waendelezaji wa mradi huo katika kujaribu kufuatilia maono yake ya awali.

Kutokana na ukubwa na ugumu wa usanifu wa jengo hilo, pamoja na mabadiliko yaliyotokea kwa miaka mingi, ujenzi umeendelea kwa hatua tofauti hadi sasa.

Sagrada FamĂ­lia liliwekwa wakfu mwaka 2010 na kutangazwa kuwa basilika ndogo, huku likifunguliwa rasmi kwa umma.

Kinacholifanya kanisa hilo kuwa la kipekee ni kwamba hata baada ya kutumika kwa ibada na kutembelewa na watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani, baadhi ya sehemu zake bado zinaendelea kujengwa.

Kwa hiyo, zaidi ya miaka 140 tangu kuwekwa jiwe la msingi, Sagrada FamĂ­lia bado linaendelea kuwa moja ya miradi mikubwa ya usanifu na ujenzi duniani, likibeba historia ndefu ya maono ya Antoni GaudĂ­ na vizazi vilivyokuja baada yake.

Aishi na Uvimbe Miaka 20 Aomba Msaada wa Matibabu, Afunguka Mazito -Video

Global Publishers
August 25, 2026
996 views
0 Comments

Usemi wa Kiswahili “Kabla hujafa hujaumbika” unaakisi kwa kiasi kikubwa maisha ya Ester Juma, mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Tabata Barakuda jijini Dar es Salaam, ambaye kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa akiishi na uvimbe mkubwa usoni.

Ester anapitia wakati mgumu huku akihangaika kutafuta fedha kwa ajili ya matibabu na upasuaji wa kuondoa uvimbe huo ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa maisha yake ya kila siku.

Akizungumza kuhusu hali yake, Ester amesema amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbali anapokuwa katika maeneo ya umma. Anaeleza kuwa baadhi ya watoto humkimbia wanapomuona, huku wakati mwingine hata mtoto wake mwenyewe akimuogopa kutokana na mabadiliko ya sura yake.

Changamoto hiyo, amesema, imemfanya kuishi maisha yenye maumivu na msongo mkubwa huku akiwa na matumaini ya kupata msaada wa matibabu.

Ester amesema aliwahi kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu, lakini hakufanikiwa kuanza mchakato huo baada ya kushindwa kupata Shilingi 450,000 zinazohitajika kwa ajili ya vipimo.

Kwa sasa, Ester anaendelea kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kupata fedha za vipimo na hatimaye kufanyiwa upasuaji.

Mtu yeyote aliyeguswa na hali ya Ester na angependa kumsaidia anaweza kuchangia kupitia namba 0760 780914, jina Magoli Juma.

Jux na Priscy Waweka Wazi Sura ya Mtoto Wao Kwa Mara ya Kwanza

Global Publishers
August 25, 2026
48 views
0 Comments

Mwanamuziki wa Bongo Flava, Juma Jux, na mke wake Priscilla Ojo, maarufu kama Priscy, wamezua gumzo mitandaoni baada ya kuamua kuonyesha sura ya mtoto wao kwa mara ya kwanza tangu kuzaliwa.

Kwa miezi kadhaa, wawili hao walikuwa wamechagua kutoweka wazi sura ya mtoto wao, jambo lililowaacha mashabiki na wafuasi wao wakisubiri kwa hamu kumuona.

Hata hivyo, Jux na Priscy sasa wamevunja ukimya huo baada ya kushirikisha picha rasmi ya mtoto wao iliyopigwa kwa mtindo wa kitaalamu na kuvutia hisia za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Uamuzi huo umeongeza gumzo miongoni mwa mashabiki, huku wengi wakieleza furaha yao baada ya hatimaye kupata nafasi ya kumuona mtoto huyo ambaye amekuwa akifichwa kwa muda.

Mbali na sura yake, mavazi na muonekano wa mtoto huyo pia yamezua mjadala, huku baadhi ya mashabiki wakigusia maisha ya kifahari yanayoonekana katika familia ya Jux na Priscy.

Priscy, ambaye anatokea nchini Nigeria, amejijengea jina katika mitindo, biashara na ushawishi kupitia mitandao ya kijamii. Yeye ni binti wa mwigizaji maarufu wa Nollywood, Iyabo Ojo.

Licha ya kukulia katika familia yenye umaarufu, Priscy amefanikiwa kujenga chapa yake binafsi katika ulimwengu wa mitindo na burudani, huku uhusiano wake na Jux ukiendelea kuvuta hisia za mashabiki Tanzania na Nigeria.

Netanyahu Aingia Mtegoni, Uturuki Yataka Interpol Imkamate

Global Publishers
August 25, 2026
18 views
0 Comments

Uturuki imetangaza hatua ya kutaka Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, akamatwe kimataifa kufuatia uchunguzi kuhusu shambulio dhidi ya wanaharakati waliokuwa wakipeleka misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.

Waziri wa Sheria wa Uturuki, Akin Gurlek, amesema hati za kukamatwa zimetolewa dhidi ya Netanyahu pamoja na mshukiwa mwingine, kwa tuhuma zinazohusisha mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mateso.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kesi hiyo inawahusisha jumla ya watu 35 na inahusiana na tukio la Israel kuingilia boti za Global Sea Flotilla katika maji ya kimataifa wakati zikiwa njiani kuelekea Gaza kwa ajili ya kupeleka misaada ya kibinadamu.

Uturuki imekuwa mkosoaji mkubwa wa operesheni za kijeshi za Israel nchini Gaza, huku serikali yake ikiendelea kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua dhidi ya kile inachodai kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Hatua hiyo ya Uturuki inatarajiwa kuongeza mvutano wa kisheria na kidiplomasia kati ya nchi hiyo na Israel, huku suala la kukamatwa kwa Netanyahu likiwa sasa likielekezwa kwenye taratibu za kimataifa kupitia Interpol.

Hata hivyo, Israel imeendelea kukataa tuhuma za kufanya ukiukaji wa sheria za kimataifa na haki za binadamu, jambo linalofanya hatua hiyo ya Uturuki kuwa suala linaloweza kuendelea kujadiliwa katika ngazi za kimataifa.

Stori na Ilankize Godfrey | GPL – TUDACO

Rais wa UEFA ÄŚeferin Amtaka Infantino Kujiuzulu Urais wa FIFA

Global Publishers
August 25, 2026
42 views
0 Comments

Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA), Aleksander ÄŚeferin, amemtaka Rais wa FIFA, Gianni Infantino, kujiuzulu nafasi hiyo, huku akisema hana mpango wa kugombea urais wa FIFA dhidi yake.

ÄŚeferin ametoa kauli hiyo wakati Infantino akikabiliwa na shinikizo la kuondoka madarakani kufuatia mpango uliositishwa wa kuuza hisa katika Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi.

Mashirikisho matatu ya soka ya mabara yameupinga mpango huo, yakidai kulikuwa na udanganyifu, huku UEFA ikitishia kususia baadhi ya mashindano yanayoandaliwa na FIFA.

Akizungumza katika mahojiano na podcast nchini Uingereza, ÄŚeferin amesema Infantino amepoteza uungwaji mkono wa baadhi ya wadau muhimu wa soka, wakiwemo mashabiki, wachezaji na makocha.

Hata hivyo, ÄŚeferin amesema hana nia ya kuwania urais wa FIFA, akieleza kuwa anaipenda nafasi yake ndani ya UEFA na pia anataka kupata muda wa kufurahia maisha nje ya majukumu ya uongozi wa soka.

Infantino amekuwa Rais wa FIFA tangu mwaka 2016. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwisho wa kuwasilisha fomu za wagombea katika uchaguzi huo ni Novemba 18.

ÄŚeferin, mwenye umri wa miaka 58, amesisitiza kuwa licha ya kutokuwa tayari kugombea nafasi hiyo, anaamini wakati umefika kwa Infantino kuachia madaraka ya uongozi wa soka duniani.

Stori na Ilankize Godfrey | GPL – TUDACO