EPL na Serie A Kutamba leo, Chelsea na Roma Kuwania Pointi Tatu

Wakali wa ubashiri Tanzania, Meridianbet wanakwambia kuwa Wikendi hii ipo kwaajaili ya kuhakikisha hawakuachi patupu. ODDS KUBWA zipo kwenye mechi za leo hivyo bashiri sasa.

SERIE A kule Italia itaendelea ambapo AS Roma atakipiga dhidi ya Fiorentina ikiwa huu ni mchezo wa kuvutia sana kwani timu hizi zina historia ya kutoa mechi nzuri na ya kuvutia huku kwa ubora wa Roma ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi.

Timu hiyo chini ya kocha mkuu Gian Gasperini klabu hiyo ya AS Roma wanatarajiwa kuwa na msimu mzuri kwani kocha huyo anajulikana kuwa na mbinu nzuri za kunoa vikosi, huku mechi hii ikiakisi mwanzo mzuri wa ligi kwa wote. Ushindi katika mchezo wa kwanza wa ligi unaweza kutoa msingi mzuri wa kujiamini kwa kikosi katika msimu ambao Roma wanataka kupigania nafasi za juu.

Kwa upande mwingine, Fiorentina wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na kiu ya kubadilisha taswira yao baada ya msimu uliopita ambao haukuwa mzuri. Hata hivyo, maandalizi yao yameonyesha kwamba wana uwezo wa kuwa tishio tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita.

Msimu uliopita, Roma liondoka na ushindi kwenye mechi zote mbili ambazo walikutana hivyo wageni wanaingia uwanjani maalumu kwaajili ya kutaka kulipa kisasi. Odds kubwa na machaguo zaidi ya 1000 yanakusubiri wewe leo. Jisajili hapa.

Piga pesa kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Lakini pia kule EPL ni Fulham dhidi ya Chelsea kutoka pale Stamford Bridge, huku mechi hii ikiwa na matarajio makubwa kwa timu zote mbili kwani ushindi pekee ndio kila timu inahitaji pale Craven Cottage.

Wenyeji wanaingia kwenye msimu huu wakiwa na mabadiliko makubwa baada ya kuahana na aliyekuwa koha wao Marco Silva baada ya kuhudumu kwa miaka mitano na kuhamia Benfica. Nafasi yake imechukuliwa na Álvaro Arbeloa, ambaye aliwahi kuwa kocha wa Real Madrid.

Chelsea nao wako kwenye mabadiliko makubwa kwani wanaanza msimu wakiwa na kocha mpya Xabi Alonso ambaye ameanza kazi kama kocha mpya baada ya klabu kumaliza msimu uliopita katika nafasi ya 10. Lengo lao kuu msimu huu ni kurudi kwenye nafasi 4 za juu yaani Top Four.

The Blues wamefanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi, huku wakisajili wachezaji kama Morgan Rogers kwa £117m, Lacroix, na wachezaji wenye uzoefu mkubwa kama vile Jordan Henderson na Danny Welbeck.

Kwenye maandalizi ya mwisho ya msimu, Chelsea waliifunga Real Sociedad 3-1, jambo linalompa Alonso matumaini kabla ya mchezo huu wa ligi ambao unatarajiwa kuwa mgumu ugenini.

Fulham wanapata faida ya kutumia uwanja wa nyumbani kwani kutakuwa na mashabiki zao lakini hiyo haiwafanyi The Blues washindwe kufanya vizuri, kwani timu ambayo imejipanga vyema ndio inaweza kuondoka na ushindi. Beti sasa.

Quevin Castro Afariki Dunia Baada Ya Kuanguka Uwanjani

Global Publishers
August 24, 2026
36 views
0 Comments

Kiungo wa zamani wa West Bromwich Albion, Quévin Castro, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 25 baada ya kuanguka ghafla wakati akiichezea Real Sport Clube katika mchezo wa kirafiki nchini Ureno.

Tukio hilo lilitokea Jumamosi, Agosti 22, 2026, katika mchezo kati ya Real Sport Clube na Estrela da Amadora. Castro alianguka takribani dakika 10 baada ya mchezo kuanza na kupoteza fahamu.

Madaktari waliokuwa uwanjani walitoa huduma ya dharura na kutumia mashine ya kushtua moyo (defibrillator) kabla Castro hajapelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu zaidi.

Hata hivyo, juhudi za kumuokoa hazikufanikiwa na Castro alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini. Kifo chake kimetikisa soka la Ureno na Uingereza.

Castro alikuwa ameanza maisha yake ya soka nchini Uingereza na baadaye akajiunga na West Bromwich Albion mwaka 2021, ambako alicheza mechi mbili za kikosi cha kwanza. Pia aliwahi kuzichezea klabu kadhaa ikiwemo Burton Albion, Notts County, Gateshead na York City kabla ya kurejea Ureno.

Kifo hicho kimepokelewa kwa huzuni kubwa na klabu alizowahi kuzichezea, huku West Bromwich Albion ikieleza kusikitishwa na kifo cha ghafla cha mchezaji huyo mwenye umri mdogo.

Mchezo ambao Castro alianguka ulisitishwa kufuatia tukio hilo, huku jumuiya ya soka ikiendelea kutoa salamu za pole kwa familia, ndugu, marafiki na klabu yake.

Stori na Haika Urio | GPL – TUDACO

Aishi na Uvimbe Miaka 20 Aomba Msaada wa Matibabu, Afunguka Mazito -Video

Global Publishers
August 24, 2026
90 views
0 Comments

Usemi wa Kiswahili “Kabla hujafa hujaumbika” unaakisi kwa kiasi kikubwa maisha ya Ester Juma, mwenye umri wa miaka 32, mkazi wa Tabata Barakuda jijini Dar es Salaam, ambaye kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa akiishi na uvimbe mkubwa usoni.

Ester anapitia wakati mgumu huku akihangaika kutafuta fedha kwa ajili ya matibabu na upasuaji wa kuondoa uvimbe huo ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa maisha yake ya kila siku.

Akizungumza kuhusu hali yake, Ester amesema amekuwa akikumbana na changamoto mbalimbali anapokuwa katika maeneo ya umma. Anaeleza kuwa baadhi ya watoto humkimbia wanapomuona, huku wakati mwingine hata mtoto wake mwenyewe akimuogopa kutokana na mabadiliko ya sura yake.

Changamoto hiyo, amesema, imemfanya kuishi maisha yenye maumivu na msongo mkubwa huku akiwa na matumaini ya kupata msaada wa matibabu.

Ester amesema aliwahi kufika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kupata matibabu, lakini hakufanikiwa kuanza mchakato huo baada ya kushindwa kupata Shilingi 450,000 zinazohitajika kwa ajili ya vipimo.

Kwa sasa, Ester anaendelea kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kupata fedha za vipimo na hatimaye kufanyiwa upasuaji.

Mtu yeyote aliyeguswa na hali ya Ester na angependa kumsaidia anaweza kuchangia kupitia namba 0760 780914, jina Magoli Juma.

Brighton Yaichakaza Aston Villa 4-0, Liverpool Yaokolewa Na Penalti Ya Dakika Za Mwisho

Brighton imeanza kwa kishindo msimu wa 2026/27 wa Ligi Kuu England baada ya kuichapa Aston Villa mabao 4-0 katika mchezo uliochezwa Jumapili, Agosti 23, 2026, kwenye Uwanja wa Amex.

Brighton ilianza mchezo kwa kasi na kupata bao la kuongoza dakika ya nane baada ya Victor Lindelöf kujifunga mwenyewe.

Dakika 10 baadaye, Maxim De Cuyper aliongeza bao la pili na kuifanya Brighton kuendelea kutawala mchezo.

Jack Hinshelwood aliendelea kuiumiza Aston Villa baada ya kufunga mabao mawili ndani ya dakika mbili, akitikisa nyavu dakika ya 30 na 31 na kuifanya Brighton kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 4-0.

Hali ilizidi kuwa ngumu kwa Aston Villa dakika ya 40 baada ya João Gomes kuonyeshwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea vibaya mchezaji wa Brighton.

Villa hivyo ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa pungufu kwa mchezaji mmoja, huku Brighton ikiwa tayari imeweka msingi wa ushindi mkubwa.

LIVERPOOL YAOKOLEWA DAKIKA ZA MWISHO

Katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu England, Liverpool imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Newcastle United kwenye Uwanja wa St James’ Park.

Newcastle ilianza kwa kasi na kupata bao la kuongoza dakika ya tano kupitia Anthony Elanga.

Liverpool ilirejea kipindi cha pili na kusawazisha kupitia Cody Gakpo dakika ya 55, kabla ya Joe Willock kuirudisha Newcastle kifua mbele dakika mbili baadaye.

Liverpool iliendelea kusaka bao la kusawazisha hadi dakika za mwisho, ambapo ilipata penalti katika muda wa nyongeza.

Dominik Szoboszlai alitulia na kufunga mkwaju huo dakika ya 90+9, akiipa Liverpool pointi moja katika mchezo wake wa kwanza wa msimu.

Matokeo hayo yameifanya Liverpool kuanza kampeni ya msimu wa 2026/27 kwa sare, huku kocha mpya Andoni Iraola akianza rasmi safari yake katika Ligi Kuu England.

Stori na Haika Urio | GPL – TUDACO

Binti wa Museveni Atawazwa Kuwa Askofu wa Kanisa la CNC Uganda

KAMPALA, Uganda — Pastor Patience Rwabwogo, binti wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, ametawazwa kuwa Askofu wa Covenant Nations Church (CNC) katika ibada iliyofanyika Jumapili, Agosti 23, 2026.

Hafla hiyo ilifanyika katika kampasi ya CNC Maya, Kyengera Town Council, Wilaya ya Wakiso, na kuhudhuriwa na Rais Museveni pamoja na Mama Janet Museveni, wazazi wa Patience na viongozi wa Uganda.

Miongoni mwa viongozi wengine waliohudhuria ni Makamu wa Rais Jessica Alupo, Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa NRM Moses Kigongo, mawaziri, viongozi wa vyombo vya usalama akiwemo Inspekta Jenerali wa Polisi Abbas Byakagaba, wanadiplomasia na viongozi mbalimbali wa dini.

Ibada hiyo ilifikia kilele muda mfupi baada ya saa 8:00 mchana, ambapo Askofu maarufu kutoka Marekani, Dk. LaDonna Osborn, alimwita Pastor Patience mbele kwa ajili ya kutawazwa rasmi kuwa Askofu.

Katika mahubiri yake akitumia vifungu vya Luka 4:8-21, Osborn alimtaka Askofu Patience kukubali kikamilifu jukumu la kuhubiri Kristo, kulijenga Kanisa na kuendeleza ufalme wa Mungu.

Kabla ya utawazo huo, wazee wa CNC wakiongozwa na Allen Kagina walitoa uthibitisho wa wito na uwezo wa Patience kuongoza kama Askofu.

Walisema Patience ndiye mwanzilishi na mchungaji mkuu wa CNC, wakieleza kuwa kanisa hilo lilianza takribani miaka 20 iliyopita kama kikundi kidogo cha waumini kilichokuwa kikikutana nyumbani.

Kwa mujibu wa wazee hao, huduma hiyo imekua kupitia maombi, uvumilivu na mafanikio ya kiroho na sasa imejikita katika mafundisho ya Biblia, uanafunzi, maombi, ibada, uongozi, uinjilisti na huduma kwa jamii.

Viongozi hao pia wamepongeza mchango wa Patience kwa vijana, wakiwemo wanafunzi na wataalamu vijana, kupitia mafundisho ya Biblia, ushauri, mikutano ya uongozi na shughuli za uinjilisti.

Wamesema huduma yake imewahamasisha waumini kutumia elimu, vipaji na fursa walizonazo kwa ajili ya utukufu wa Mungu na manufaa ya jamii.

Kutawazwa kwake kuwa Askofu kunatajwa kuwa hatua muhimu katika safari yake ya zaidi ya miongo miwili ya huduma ya kidini.

Stori na Na Ashura Karimu | GPL -TUDACO

 

WAZIRI MKUU AWASILI TANGA, MGENI RASMI KILELE CHA WIKI YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU

WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili leo Jumatatu, Agosti 24, 2026, katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Tanga, ambapo anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, mkoani Tanga.

Amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Batilda Burian, pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda.

Alipowasili katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, Waziri Mkuu ametembelea mabanda mbalimbali ya maonesho na kujionea bunifu, teknolojia na kazi mbalimbali zinazowasilishwa na washiriki katika maadhimisho hayo.

 

Miss Universe kuhamasisha matumizi nishati safi – HabariLeo

DAR ES SALAAM; Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amewapongeza washiriki wa shindano la urembo la Miss Universe Tanzania kwa jitihada zao za kuwa mabalozi wa nishati safi ya Kupikia kwa kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia nishati hiyo nchini.

Naibu Waziri Salome amesema serikali itaendelea kushirikiana na jukwaa hilo muhimu katika kuifikisha ajenda ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi, huku akiwataka washiriki 33 wa shindano hilo kuwa chachu ya kufikisha ujumbe sahihi kwa jamii, hususan katika maeneo ya vijijini.

Ametoa kauli hiyo Agosti 23, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa shindano la Miss Universe Tanzania kwa lengo la kupata warembo 20 watakaoendelea na hatua inayofuata ya mashindano hayo, kuelekea kumpata mwakilishi wa Tanzania katika shindano la Miss Universe duniani.

Amesema ushiriki wa warembo hao katika Kampeni ya Nishati Safi ya Kupikia unatoa fursa muhimu ya kuifikisha ajenda hiyo kwa makundi mbalimbali ya jamii na kuongeza uelewa kuhusu faida za kutumia nishati salama, nafuu na rafiki kwa mazingira.

Ameeleza kuwa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, inayopewa msukumo na Rais wa Tanzania, Dk  Samia Suluhu Hassan, inalenga kuhakikisha angalau asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Ameongeza kuwa matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini yameongezeka kutoka takribani asilimia 6 miaka michache iliyopita hadi asilimia 28.6 kwa sasa.

Amempongeza Mkurugenzi wa Taifa wa Miss Universe Tanzania, Millen Magese, kwa kuunganisha mashindano hayo na Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia, pamoja na kuwashukuru wadhamini wanaounga mkono jitihada hizo.

Pia ametoa wito kwa kampuni na wadau wengine kujitokeza kuunga mkono mashindano hayo ili yaweze kuwafikia wanawake wengi zaidi na kupanua wigo wa uhamasishaji.

Kwa upande wake, Magese amesema Miss Universe Tanzania imeamua kubeba ujumbe wa Nishati Safi ya Kupikia mwaka 2026 ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na serikali katika kuongeza uelewa na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Amesisitiza kuwa Miss Universe Tanzania itaendelea kushirikiana na serikali pamoja na wadau wa maendeleo kuhakikisha ujumbe wa Nishati Safi ya Kupikia unaendelea kuwa sehemu ya mashindano hayo kila mwaka, hivyo kuwapa washiriki nafasi ya kuwa mabalozi wa mabadiliko katika jamii.

Katika shindano hilo, washiriki walipata nafasi ya kutoa ujumbe mbalimbali kuhusu Nishati Safi ya Kupikia, wakieleza umuhimu wa Watanzania kuhamia katika matumizi ya nishati salama, nafuu na rafiki kwa mazingira.

 

WANAFUNZI 95 WAENDA INDIA KUSOMEA AI, UHANDISI

 

Na Mwandishi Wetu

Zaidi ya wanafunzi 95 wa Kitanzania wameondoka nchini kuelekea India kuanza masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, ikiwa ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi 198 wanaotarajiwa kwenda kusoma nchini humo kupitia Global Education Link katika mwaka 2026.

Wanafunzi hao walioondoka kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Terminal 3, jijini Dar es Salaam, wengi wao wamechagua programu zinazohusiana na sayansi, teknolojia na taaluma zinazohitajika katika dunia ya sasa, zikiwemo Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence, Civil Engineering, programu mbalimbali za afya, sheria na biashara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, amesema kuondoka kwa wanafunzi hao ni sehemu ya mpango mpana wa kuwaunganisha vijana wa Tanzania na fursa za elimu ya kimataifa.

“Zaidi ya wanafunzi 95 wanaondoka katika kundi hili la kwanza kuelekea India, lakini kwa mwaka huu tunatarajia wanafunzi 198 kwenda kusoma nchini India. Hili si kundi la mwisho kwa sababu bado tuna wanafunzi wengine wanaoendelea kukamilisha taratibu zao,” amesema Musa.

Amesema mbali na India, Global Education Link inaendelea kuwaandaa wanafunzi wengine wapatao 185 wanaotarajiwa kuelekea nchini China, huku wengine wakiwa katika hatua mbalimbali za maandalizi ya kwenda kusoma Malaysia, Marekani na Uingereza.

“Kadiri muda unavyokwenda Watanzania wataendelea kuona makundi mengine ya wanafunzi yakiondoka. Tunawaomba vijana wenye ndoto ya kusoma nje ya nchi wafike katika ofisi zetu zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Arusha. Muda bado upo. Njoo na matokeo yako, nasi Global Education Link tupo tayari kukusaidia kuifanya ndoto yako kuwa uhalisia,” amesema.

Musa pia amewataka wazazi na walezi wenye vijana wanaotamani kupata elimu nje ya nchi kutumia ofisi za Global Education Link kupata ushauri kuhusu uchaguzi wa vyuo, programu za masomo, udahili, visa na maandalizi ya safari.

Miongoni mwa wanafunzi walioondoka ni vijana wanaokwenda kusomea Computer Science Engineering, Artificial Intelligence na Cyber Security, wakisema wamechagua taaluma hizo kutokana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia na umuhimu wake katika maendeleo ya uchumi wa kisasa.

Alvin Andrew Munda, mwenye umri wa miaka 17, anayeelekea Lovely Professional University nchini India, amesema amechagua Computer Science kwa sababu anataka kujenga ujuzi wa vitendo katika teknolojia na baadaye kujikita zaidi katika Cyber Security.

Amesema mfumo wa masomo wenye nafasi kubwa ya mafunzo ya vitendo na matumizi ya maabara ulimvutia kuchagua chuo hicho.

“Napenda mfumo wenye practical zaidi kuliko kusoma theory na kuandika mitihani pekee. Nataka nitumie elimu nitakayoipata kutengeneza suluhisho na baadaye nijikite katika Cyber Security kwa sababu usalama wa mtandao ni muhimu sana katika dunia ya sasa,” amesema.

Akimshukuru Global Education Link, Munda amesema taasisi hiyo imeisaidia familia yake katika mchakato mzima, kuanzia kupata chuo hadi kukamilisha maandalizi ya safari.

“Global imenisaidia katika process nzima kabisa. Wametuelekeza hatua moja hadi nyingine na wamekuwa kiungo kati yetu, wazazi wetu na chuo mpaka tumefikia hapa airport tayari kuondoka,” amesema.

Mwanafunzi mwingine anayekwenda kusomea masomo yanayohusiana na Computer Science na Artificial Intelligence amesema anatarajia kuwa mtaalamu wa data na teknolojia katika miaka ijayo.

Amesema AI imeanza kuwa sehemu muhimu katika benki, hospitali, biashara, serikali na sekta nyingine, na hivyo anaamini elimu katika eneo hilo itamwezesha kuwa sehemu ya maendeleo ya kiteknolojia nchini Tanzania.

Naye mwanafunzi anayekwenda kusomea programu jumuishi ya Bachelor of Business Administration na Bachelor of Laws amesema ana ndoto ya kuwa mwanasheria na mfanyabiashara mwenye mafanikio baada ya kumaliza masomo yake.

Amesema Global Education Link imechangia kwa kiasi kikubwa kumfikisha katika hatua ya kuondoka kwenda masomoni.

“Global Education imetusaidia sana, hasa kwenye visa processing, kupata chuo na maandalizi mengine ya safari. Ushirikiano kati yangu, wazazi wangu na Global ndio umetufikisha hapa leo,” amesema.

Wazazi waliowasindikiza watoto wao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pia wameipongeza Global Education Link kwa namna ilivyosimamia mchakato wa watoto wao kuanzia hatua za awali hadi siku ya safari.

Donald Kito, mzazi wa Isaac Donald Kito anayekwenda Lovely Professional University kusomea Diploma ya Civil Engineering, amesema familia yake ilifahamu huduma za Global Education Link kupitia matangazo na baada ya kuwasiliana nao walipata maelezo yaliyowapa imani ya kuendelea na mchakato.

Mwisho

Tundu Lissu Kuendelea Kujitetea Kesi ya Uhaini Leo Mahakamani

Shauri la uhaini namba 19605/2025 linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, linaendelea leo Agosti 24, 2026 katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Kesi hiyo inaendelea katika hatua ya ushahidi wa utetezi, mbele ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.

Hatua hiyo ilianza Ijumaa, Agosti 21, baada ya Mahakama kumkuta Lissu ana kesi ya kujibu na kumpa nafasi ya kuanza kujitetea dhidi ya mashtaka yanayomkabili.

Lissu, ambaye ameamua kujitetea mwenyewe, alianza kutoa ushahidi wake siku hiyo na pia akawasilisha orodha ya mashahidi anaotarajia kuwaita mahakamani.

Miongoni mwa mashahidi aliowataja ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan; Makamu wa Rais mstaafu, Philip Isdor Mpango; pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Kassim Majaliwa.

Aidha, Lissu amewataja baadhi ya viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi wa CHADEMA, akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche, Katibu Mkuu John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Amani Golugwa na Brenda Rupia.

Leo, Lissu anatarajiwa kuendelea na ushahidi wake wa kujitetea kama shahidi wa kwanza. Baada ya kukamilisha ushahidi wake, mashahidi wengine wa upande wa utetezi wanatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wao.

Hata hivyo, suala la kuwaita viongozi wa Serikali, wakiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, limezua mvutano kati ya pande hizo mbili.

Upande wa mashtaka umepinga wito wa viongozi hao kufika mahakamani, ukieleza kuwa Jamhuri tayari imekamilisha ushahidi wake na kwamba si jambo la busara kumtaka Rais kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Kwa upande wake, Lissu amepinga hoja hiyo akisisitiza kuwa sheria inapaswa kutumika kwa kila mtu bila kujali cheo au nafasi yake.

Kesi hiyo inaendelea huku ikifuatiliwa kwa karibu kutokana na uzito wa mashtaka na majina ya viongozi wakuu wa Serikali yaliyotajwa kuwa sehemu ya mashahidi wa utetezi.

Iran Yatoa Onyo Kali Kuhusu Vikwazo Vipya vya Marekani

Iran imeonya kuwa nchi yoyote itakayounga mkono vikwazo vipya vya kiuchumi vinavyotarajiwa kutangazwa na Marekani dhidi ya Iran itachukuliwa kuwa imefanya kitendo cha vita.

Onyo hilo limetolewa na mkuu mpya wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohsen Rezaei, wakati mvutano kati ya Iran na Marekani ukiendelea kuongezeka.

Rezaei amesema Iran iko tayari kulipiza kisasi kwa nguvu endapo Marekani itaendelea kuongeza shinikizo la kiuchumi. Pia ametishia kulenga njia nyingine za usafirishaji wa mafuta katika Ghuba ya Uajemi endapo hali itaendelea kuwa mbaya.

Wakati huo huo, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian ameonyesha nia ya kuendelea na mazungumzo na Marekani. Amesema makubaliano ya awali yaliyofikiwa mwezi Juni ndiyo njia bora ya kuondokana na hali ya “si vita wala amani” iliyopo kati ya mataifa hayo.

Hata hivyo, kipindi cha siku 60 kilichowekwa kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kimekwisha bila kufikiwa kwa makubaliano mapya.

Mvutano pia umeendelea katika Mlango wa Hormuz, njia muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani. Hakuna mashambulizi yaliyothibitishwa katika eneo hilo katika saa 48 zilizopita, lakini idadi ya meli zinazopita imeendelea kuwa ndogo.

Iran pia imetangaza orodha ya meli kadhaa ambazo inasema zilikiuka masharti ya usafirishaji katika eneo hilo na inaweza kuziwekea faini au kuzizuia siku zijazo.

Katika juhudi za kupunguza mvutano, Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Field Marshal Asim Munir, anatarajiwa kutembelea Tehran. Pakistan inajaribu kusaidia kuwarudisha Marekani na Iran kwenye meza ya mazungumzo.

Wakati hayo yakiendelea, hali ya Mashariki ya Kati bado ni tete. Mashambulizi yameripotiwa Gaza na Ukingo wa Magharibi, huku mtoto wa miaka minne akiuawa katika shambulio la anga la Israel huko Gaza, kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina.

Kwa ujumla, mvutano kati ya Iran na Marekani unaendelea kuwa tishio kwa usalama wa Mashariki ya Kati na pia kwa usafirishaji wa mafuta duniani, hasa kupitia Mlango wa Hormuz.