FAMILIA ZATAKIWA KUJITOKEZA KUTAMBUA NDUGU WALIOPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI YA MKAMBARANI

Matukio Daima Media, Morogoro

Familia zenye ndugu waliokuwa safarini na ambao hawajulikani walipo zimetakiwa kujitokeza kushirikiana na mamlaka katika zoezi la utambuzi wa mabaki ya miili ya waliofariki katika ajali ya Mkambarani mkoani Morogoro.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Queen Sendiga, aliyesema utambuzi huo unafanyika kwa kutumia vipimo vya vinasaba ili kusaidia kubaini utambulisho wa marehemu na kutoa majibu kwa familia zinazotafuta ndugu zao.

Sendiga ameeleza kuwa zoezi hilo linaendelea, huku akihimiza ushirikiano wa wananchi wenye ndugu waliopotea ili kurahisisha utambuzi wa mabaki ya miili na kuhakikisha familia zinapata taarifa sahihi kuhusu ndugu zao.

Mwisho