Fahamu Njia Sahihi ya Kupaki Gari la Automatic, Linda Gearbox Yako

Global Publishers
September 26, 2026
5,764 views
0 Comments

Wataalamu wa magari wameeleza kuwa kuna utaratibu muhimu unaoshauriwa kufuatwa wakati wa kupaki gari aina ya automatic ili kulinda mfumo wa gia na kuongeza usalama.

Utaratibu huo huanza kwa dereva kuhakikisha gari limesimama kabisa akiwa amekanyaga breki. Kisha gia hutolewa kutoka kwenye “Drive (D)” kwenda “Neutral (N)” kabla ya kuvuta breki ya mkono (hand brake).

Baada ya kuvuta hand brake, dereva anatakiwa kuondoa mguu taratibu kwenye breki ili uzito wa gari ushikiliwe na breki ya mkono badala ya mfumo wa gia. Hatua hiyo husaidia kupunguza presha kwenye gia hasa gari linapokuwa limeegeshwa kwenye mteremko.

Kisha dereva hukanyaga tena breki na kuhamisha gia kwenda “Parking (P)” kabla ya kuzima injini. Wataalamu wanasema njia hiyo ni salama zaidi na inaweza kusaidia kuongeza uimara wa mfumo wa transmission ya gari.

Madereva wanashauriwa kuzoea utaratibu huo ili kuepuka uharibifu wa mapema wa gearbox pamoja na kuongeza usalama wa gari linapokuwa limeegeshwa.

KIHONGOSI AKAGUA MRADI WA SH BILIONI 2.5 WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA CCM TANGA.

 

NA AMINA SAIDI TANGA,

​Katibu wa Halmashauri Kuu ya (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, anafanya ziara ya siku mbili mkoani Tanga kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho,

Ambapo ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa chama hicho unaogharimu jumla ya Shilingi bilioni 2.5.  

​Katika mradi huo unaolenga kuboresha mazingira ya kazi na makazi kwa watumishi wa CCM.

 Jumla ya nyumba 36 zitajengwa katika wilaya zote tisa za mkoa wa Tanga, ambapo kila wilaya itapata fursa ya kujengewa nyumba nne za kisasa.

​Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga amethibitisha kuwa tayari ameshatoa  Shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuwezesha na kuharakisha utekelezaji wa ujenzi wa nyumba hizo katika ngazi za wilaya.

​Ujenzi huo wa miundombinu unalenga kukamilika rasmi ifikapo mwezi Februari mwakani, hatua inayotajwa kuwa itaongeza ufanisi wa utendaji kazi wa viongozi na watumishi wa chama hicho waliopo katika maeneo mbalimbali ya mkoa.

​Kihongosi amepongeza uongozi wa CCM Mkoa wa Tanga kwa hatua hiyo madhubuti ya utekelezaji wa maelekezo ya chama na kusisitiza kuwa uimarishaji wa miundombinu ya chama ni nguzo muhimu katika kuhakikisha utekelezaji bora wa Ilani ya CCM kwa maslahi ya wananchi.

⬇️⬇️

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

Basata Yatoa Adhabu Kwa Dudubaya na Mratibu wa Tamasha la Miaka 30 Bongo Flava -Video

Global Publishers
September 26, 2026
12 views
0 Comments

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa adhabu kwa msanii Godfrey Tumaini maarufu Dudubaya, pamoja na Mratibu Mkuu wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava, kufuatia tukio lililotokea Septemba 19, 2026 katika Viwanja vya General Tyre, Jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BASATA, Dudubaya anadaiwa kukiuka Kanuni ya 20(a) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, Tangazo la Serikali Na. 137 la tarehe 22 Mei 2026, baada ya kuzungumza maneno yaliyolalamikiwa kuwa ya kashfa na matusi wakati akitumbuiza katika tamasha hilo.

BASATA imesema baada ya kufuatilia tukio hilo na kujiridhisha kuwa kosa lilitendeka, imechukua hatua kwa mujibu wa Kanuni ya 45, ambapo Dudubaya ametakiwa:

  • Kuzingatia Sheria, Kanuni na Miiongozo ya BASATA katika uendeshaji wa sanaa.
  • Kulipa faini ya Shilingi Milioni Tatu (Tsh 3,000,000) ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.
  • Kutohusisha na shughuli za sanaa kwa jina lolote kuanzia tarehe ya uamuzi hadi pale atakapotekeleza maamuzi hayo.

MRATIBU WA TAMASHA NAYE AADHIBIWA

BASATA pia imemchukulia hatua Mratibu Mkuu wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava, baada ya kubainika kuwa alimwezesha Dudubaya kutumbuiza jukwaani na kufanya kosa hilo licha ya kuwepo kwa masharti ya usimamizi wa tamasha.

BASATA imesema mratibu huyo alipaswa kuhakikisha kuwa shughuli za tamasha zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya BASATA, pamoja na kuhakikisha kuwa hakuna vitendo vinavyoweza kuleta changamoto kwa wasanii wanaoshiriki.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 45, mratibu huyo ameagizwa:

  • Kuzingatia Kanuni na Miiongozo ya BASATA katika uendeshaji wa matukio ya sanaa.
  • Kulipa faini ya Shilingi Milioni Tatu (Tsh 3,000,000) ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.
  • Kutohusisha na shughuli za sanaa kwa jina lolote kuanzia tarehe ya uamuzi hadi atakapotekeleza maamuzi hayo.

BASATA imetoa rai kwa Wasanii na Wadau wa Sanaa kuhakikisha wanazingatia Sheria, Kanuni, Miiongozo na Maadili ya Tanzania wanapotekeleza kazi zao za sanaa.

WANAWAKE WACHIMBAJI GEITA WATOA WITO: “WANAWAKE JITOSENI KWENYE UCHIMBAJI, NI FURSA YA UCHUMI NA UWEZESHAJI”

 

Na Matukio Daima Geita

MWENYEKITI wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Mkoa wa Geita (GEWOMA), Asia Masimba, amewataka wanawake nchini kujitokeza kwa wingi na kujihusisha na shughuli za uchimbaji madini, akisema sekta hiyo ni miongoni mwa fursa muhimu zinazoweza kuwainua kiuchumi, kuongeza heshima na kuimarisha maisha ya familia

Masimba ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Geita, katika Maonesho ya Tisa ya Madini, yanayofanyika mkoani humo.

Amesema GEWOMA ina zaidi ya wanawake wachimbaji 400 katika Mkoa wa Geita, ambao wamejikita katika shughuli mbalimbali za uchimbaji na sasa wamekuwa mfano wa kuigwa kutokana na hatua kubwa wanazopiga katika kujikwamua kiuchumi.

Kwa mujibu wa Masimba, wanawake hao si tu kwamba wameweza kuongeza kipato chao, bali pia wamekuwa na mchango mkubwa katika kuendesha familia zao na kuboresha maisha ya jamii zinazowazunguka.

“Tunawahamasisha wanawake wajitokeze na kuingia kwenye uchimbaji kwa sababu hii ni kazi yenye fursa kubwa. Wanawake wanaweza kufanya kazi hii na kujenga maisha yao pamoja na kusaidia familia zao,” alisema Masimba.

Aidha, amewataka wanaume kuwaunga mkono wake zao wanaotaka kujihusisha na shughuli za uchimbaji madini, akisisitiza kuwa sekta hiyo inaweza kuwa chanzo muhimu cha kipato na maendeleo ya familia.

Amesema uchimbaji madini si suala la wanaume pekee, bali ni eneo ambalo wanawake wanaweza kushiriki kikamilifu na kutumia fursa zilizopo kujenga uchumi wao.

“Tunawaomba wanaume wawaruhusu na kuwaunga mkono wake zao wanaotaka kufanya uchimbaji. Uchimbaji ni maisha, ni fursa na ni utajiri ambao unaweza kubadilisha maisha ya familia,” amesema.

Akizungumzia ushiriki wao katika Maonesho ya Tisa ya Madini, Masimba amesema wanawake hao wamekuja na bidhaa mbalimbali, zikiwemo dhahabu na shaba, huku wakitumia fursa hiyo kujifunza teknolojia mpya zinazotumika katika shughuli za uchimbaji.

Amesema teknolojia hiyo imeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya madini, tofauti na zamani ambapo wachimbaji walilazimika kutegemea zaidi nguvu za mikono na uzoefu wa kutafuta maeneo yenye madini.

“Zamani tulikuwa tunatumia zaidi mikono katika kutafuta madini, lakini sasa kuna teknolojia mpya ambazo zinaweza kusaidia kubaini kama eneo lina dhahabu au halina. Hii inatusaidia kufanya uchimbaji kwa ufanisi zaidi,” amesema.

Amesema wanawake wa GEWOMA wameendelea kujifunza mbinu mbalimbali za uchimbaji, kuanzia kuchimba na kutoa mawe hadi kuyafanyia uchakataji ili kupata dhahabu, huku wakijengewa uwezo wa kutumia zana na teknolojia zinazorahisisha kazi hiyo

Masimba amesema hatua hiyo inaonyesha namna wanawake wanavyoendelea kubadilika na kuingia katika shughuli za uchimbaji kwa ujasiri, maarifa na teknolojia, jambo analodai linaweza kuongeza tija na manufaa ya shughuli za madini kwa wanawake na jamii kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa wanawake wanapaswa kutumia fursa zinazopatikana katika sekta ya madini, kujenga vikundi imara, kuongeza ujuzi na kutumia teknolojia ili kuongeza thamani ya kazi wanayoifanya.

MWISHO

⬇️⬇️⬇️

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

Diamond na Joel Lwaga Waungana Kwenye Wimbo Mpya “Nikumbuke”

Global Publishers
September 26, 2026
1,092 views
0 Comments

Wasanii wakubwa kutoka Tanzania, Diamond Platnumz na Joel Lwaga, wameungana kwa mara ya kwanza katika wimbo mpya unaokwenda kwa jina la “Nikumbuke”, uliotoka rasmi Septemba 23, 2026.

Ushirikiano huo umekutanisha wasanii wawili wanaotoka katika mazingira tofauti ya muziki, huku Diamond Platnumz akijulikana zaidi kupitia Bongo Flava na Afropop, wakati Joel Lwaga akitambulika kwa kazi zake katika muziki wa Injili.

“Nikumbuke” umejengwa katika ujumbe wa imani, subira na matumaini, ukielezea hali ya mtu anayepitia changamoto lakini bado anaendelea kumtegemea Mungu na kusubiri majibu ya maombi yake.

Kupitia wimbo huo, wasanii hao wameleta ladha tofauti za muziki na kuunganisha mashabiki wa Bongo Flava pamoja na wale wanaopenda muziki wa Injili.

Kwa Diamond, ushirikiano huo unamuweka kwenye mazingira yenye ujumbe wa kiroho zaidi, huku Joel Lwaga akiendelea kusimamia aina ya muziki ambao amejijengea jina kwa miaka kadhaa.

Wimbo huo tayari umeanza kupata uangalizi kutoka kwa mashabiki kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki na mitandao ya kijamii.

Taarifa zilizopo kwenye YouTube zinaonyesha kuwa lyric video ya “Nikumbuke” iliwekwa kwenye ukurasa wa Joel Lwaga Septemba 23, 2026, siku ambayo wimbo huo ulitolewa rasmi.

Ushirikiano wa Diamond na Joel Lwaga unaifanya “Nikumbuke” kuwa moja ya kazi zinazowakutanisha wasanii wenye mitazamo tofauti ya muziki, huku ujumbe wake ukilenga kuhamasisha watu kuendelea kuwa na matumaini, subira na imani hata wanapopitia nyakati ngumu.

Stori na Anifa Mwegelo | GPL -TUDACO

KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026 HAPA

 

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

Rayvanny Kutumbuiza Afro Nation Portugal 2027

 

 

Msanii wa Tanzania, Rayvanny, ametangazwa kuwa miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza katika tamasha kubwa la Afro Nation Portugal 2027, nchini Ureno.

Jina la Rayvanny limeonekana katika orodha ya kwanza ya wasanii iliyotangazwa na waandaaji wa tamasha hilo Septemba 23, 2026, hatua inayomweka tena msanii huyo wa Tanzania kwenye jukwaa kubwa la muziki wa Afrika kimataifa.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 9 hadi 11, 2027, katika ufukwe wa Praia da Rocha, Portimão, nchini Portugal, likiwa na lengo la kuunganisha muziki, utamaduni na burudani kutoka Afrika na maeneo mbalimbali duniani.

Rayvanny atashiriki jukwaa hilo pamoja na baadhi ya majina makubwa katika muziki wa Afrika na kimataifa, akiwemo Davido, Rema, Fally Ipupa, Omah Lay, Victony na Shenseea.

Davido, Rema na Fally Ipupa wametajwa miongoni mwa wasanii wakuu watakaotumbuiza katika tamasha hilo.

Kwa upande wa muziki wa Amapiano, jukwaa la Piano People Stage linatarajiwa kuwakutanisha wasanii mbalimbali, akiwemo Kabza De Small, TxC na Dlala Thukzin.

Waandaaji wa Afro Nation wamesema orodha hiyo bado haijakamilika, huku wasanii wengine wakitarajiwa kutangazwa katika awamu zijazo kuelekea tamasha hilo.

Kwa Rayvanny ushiriki huo unampa nafasi ya kuwakilisha muziki wa Tanzania katika moja ya matukio ya kimataifa yanayolenga Afrobeats, Amapiano na muziki wa Afrika. Tamasha hilo limekuwa likifanyika Portugal tangu mwaka 2019 na limeendelea kuwaleta pamoja wasanii na mashabiki kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Na Anifa Mwegelo



PSSSF YAWEKA REKODI MPYA , THAMANI YAFIKA SH TRILIONI 16.96

 

Na Matukio Daima Geita

Serikali imeeleza kuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeendelea kuimarika na kuwa mfano katika utoaji wa huduma za hifadhi na kinga ya jamii nchini, huku thamani ya mfuko huo ikifikia Sh trilioni 16.96.

Akizungumza wakati wa Maonyesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani Geita, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amesema ameridhishwa na jitihada zinazofanywa na PSSSF katika kuhakikisha waajiri na wastaafu wanapata elimu kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii na maandalizi ya maisha baada ya kustaafu.

Sangu amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika kuimarisha PSSF, hatua ambayo imechangia ongezeko kubwa la thamani ya mfuko huo.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, thamani ya PSSSF imeongezeka kutoka Sh trilioni 7.4 wakati Rais Samia alipoingia madarakani hadi kufikia Sh trilioni 16.96, ongezeko analolitaja kuwa ni hatua kubwa katika historia ya mfuko huo.

Amesema ukuaji huo umewezesha PSSSF kuboresha zaidi huduma kwa wastaafu, ikiwemo kuhakikisha wanapata pensheni zao kwa wakati.

“Tunalipa jana,” ni kaulimbiu ambayo, kwa mujibu wa Sangu, imeendelea kutekelezwa kwa vitendo, ambapo wastaafu hulipwa pensheni zao kila tarehe 25 ya mwezi bila kuchelewa.

Aidha, amesema kiwango cha chini cha pensheni kwa sasa kimefikia Sh 250,000, hatua inayolenga kuimarisha ustawi wa wastaafu baada ya kumaliza safari yao ya utumishi.

Waziri Sangu pia amepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na PSSSF katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), akisema umeleta mabadiliko katika upatikanaji wa huduma kwa wastaafu.

Amesema hapo awali wastaafu walilazimika kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao, lakini kwa sasa huduma hizo zimeboreshwa kupitia mifumo ya kidijitali, hivyo kupunguza usumbufu na kurahisisha upatikanaji wa huduma.

Ameeleza kuwa matumizi ya teknolojia yanaendelea kuwa sehemu muhimu katika kuboresha huduma za PSSSF na kuhakikisha wanachama na wastaafu wanapata huduma kwa urahisi, ufanisi na kwa wakati.

MAGAZETINI LEO JUMAMOSI SEPT 26/2026:EL -NINO YABADILI RATIBU YA MITIHANI..

 .

 

 

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

3:TUZO YA AFYA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

🚨ZIMEBAKI SIKU 5 ZOEZI KUFUNGWA