Waziri Katambi Awasili Stendi ya Mbezi Magufuli Kufuatia Mgomo wa Madereva – Live

Global Publishers
September 29, 2026
18 views
0 Comments


DAR ES SALAAM: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewasili katika Stendi Kuu ya Mabasi ya Mbezi Magufuli jijini Dar es Salaam, kufuatia kusitishwa kwa safari za mabasi kunakodaiwa kusababishwa na mgomo wa madereva.

Katambi amefika stendi hiyo jioni hii kwa ajili ya kukutana na madereva pamoja na abiria waliokwama kutokana na kusitishwa kwa safari za mabasi.

Waziri huyo anatarajiwa kuzungumza na madereva na abiria mbele ya vyombo vya habari, huku akieleza hatua zitakazochukuliwa kuhusu hali hiyo.

Mgomo huo umeathiri huduma za usafiri katika baadhi ya vituo vya mabasi nchini, huku madereva wakieleza kuwa wanapinga masuala mbalimbali yanayohusiana na adhabu na faini za usalama barabarani.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya abiria kushindwa kuendelea na safari zao, huku mabasi yaliyokuwa yamepangwa kuondoka yakiwa hayajaanza safari.