
Dar es Salaam – Tanzania, kupitia mrembo wake Jihan Dimack, Miss Grand Tanzania 2026, imefanikiwa kuingia katika hatua ya pili ya kipengele cha Country’s Power of the Year kwenye mashindano ya Miss Grand International 2026.
Baada ya kukamilika kwa Round 1, jumla ya washiriki 40 bora wamefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya pili, ambapo wamegawanywa kwa bahati nasibu katika makundi manne yenye washiriki 10 kila moja.

Tanzania kupitia Jihan Dimack imepangwa katika Group A, pamoja na washiriki wengine tisa kutoka mataifa tofauti.
Katika hatua hii, washiriki wawili bora kutoka kila kundi ndio watakaofuzu kwenda hatua inayofuata.
Hii ina maana kwamba kati ya washiriki 40 waliopo Round 2, ni jumla ya washiriki wanane pekee watakaosonga mbele.
KURA ZA SAA 48
Kwa mujibu wa taarifa ya Miss Grand International, upigaji kura wa Round 2 umeanza Septemba 28, 2026 saa 5:00 jioni kwa saa za GMT+7, na utafikia mwisho Septemba 30, 2026 saa 5:00 jioni kwa saa za GMT+7.
Hivyo, zoezi hilo litadumu kwa muda wa saa 48 pekee.

JINSI YA KUMPIA KURA JIHAN
Kura zinapigwa kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya Miss Grand International.
Ili kushiriki katika kura, shabiki anatakiwa kwanza kuifuatilia akaunti rasmi ya Miss Grand International, kisha kushiriki katika chapisho maalum la kundi la Round 2 lililotengwa kwa ajili ya upigaji kura.
Kwa Tanzania, Watanzania wanatakiwa kufuatilia akaunti rasmi ya mashindano na kushiriki kwenye chapisho linalomhusu Jihan Dimack ili kumuongezea nafasi ya kusonga mbele.
MFUMO WA UPATIKANAJI WA POINTI
Katika Round 2, mfumo wa alama umeweka uzito mkubwa kwenye New Followers, ambao unachangia asilimia 95 ya alama zote.
-
95% – New Followers: Alama zitazingatia idadi ya wafuasi wapya wanaohusishwa na chapisho la kura la kila mshiriki katika kipindi rasmi cha upigaji kura.
-
5% – Engagement: Ushiriki wa mashabiki kupitia Like, Repost na Comment pia utachangia katika matokeo.
Kwa upande wa engagement, mfumo umeainisha:
-
❤️ Like = Pointi 1
-
🔄 Repost = Pointi 2
-
💬 Comment = Pointi 1
Alama za New Followers na Engagement zitahesabiwa kwa uwiano ili kupata alama ya mwisho ya kila mshiriki.
DATA YA INSTAGRAM NDIYO ITAKAYOTUMIKA
Waandaaji wameeleza kuwa matokeo yatategemea Instagram Insights kutoka kwenye akaunti rasmi ya Miss Grand International.
Data itakayohesabiwa ni ile iliyorekodiwa ndani ya muda rasmi wa upigaji kura pekee.
Endapo washiriki wawili watakuwa na alama zinazolingana, mshiriki mwenye alama nyingi zaidi kutoka kwa New Followers ndiye atakayepewa nafasi ya kusonga mbele.
Kwa ufupi, mfumo wa Round 2 ni:
Washiriki 40 → Makundi 4 → Washiriki 10 kila kundi → Washiriki 2 bora kutoka kila kundi → Washiriki 8 wanafuzu.
Kwa Jihan Dimack na Tanzania, kipindi cha saa 48 ni muhimu huku Watanzania wakihamasishwa kujitokeza kwa wingi kwenye Instagram ya Miss Grand International, kumfuatilia Jihan na kushiriki katika chapisho lake la kura.

