Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Awasili Qatar kwa Ziara ya Kikazi

Global Publishers
September 26, 2026
0 views
0 Comments

DOHA, QATAR: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili nchini Qatar leo, Septemba 25, 2026, kwa ziara ya kikazi.

Dkt. Mwigulu amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad, jijini Doha, ambapo amepokelewa na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Balozi Ibrahim bin Yousif Fakhroo.

Pamoja na viongozi hao, Waziri Mkuu amepokelewa pia na Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Habibu Awesi Mohamed.

Ziara hiyo ya kikazi inatarajiwa kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar katika maeneo mbalimbali yenye maslahi kwa mataifa hayo mawili.