𝑴𝑨𝑲𝑨𝑴𝑼 𝑾𝑨 𝑹𝑨𝑰𝑺 𝑨𝑾𝑨𝑺𝑰𝑳𝑰 𝑡𝑬𝑾 𝒀𝑢𝑹𝑲 – 𝑴𝑨𝑹𝑬𝑲𝑨𝑡𝑰, 𝑲𝑼𝑴𝑾𝑨𝑲𝑰𝑳𝑰𝑺𝑯𝑨 𝑹𝑨𝑰𝑺 𝑫𝑲𝑻. 𝑺𝑨𝑴𝑰𝑨 𝑺𝑼𝑳𝑼𝑯𝑼 𝑯𝑨𝑺𝑺𝑨𝑡 𝑲𝑨𝑻𝑰𝑲𝑨 𝑴𝑲𝑼𝑻𝑨𝑡𝑢 𝑾𝑨 81 𝑾𝑨 𝑩𝑨𝑹𝑨𝒁𝑨 𝑲𝑼𝑼 𝑳𝑨 𝑼𝑴𝑢𝑱𝑨 𝑾𝑨 𝑴𝑨𝑻𝑨𝑰𝑭𝑨

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amewasili New York nchini Marekani, ambapo anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA81) Unaofanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York.
 
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa John F Kennedy, Makamu wa Rais amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Balozi Elsie Kanza, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa – New York Mhe. Balozi Togolani Mavura pamoja na maafisa mbalimbali.
 
Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinachoshirikisha Wakuu wa Nchi na Viongozi mbalimbali ni Mkutano muhimu ambao, pamoja na mambo mengine, hujadili masuala ya kiuchumi, kisiasa, mazingira na haki za binadamu.
Kikao hicho kinafanyika chini ya Kaulimbiu isemayo β€œKurudisha Imani, Kusimamia Mabadiliko, Umoja wa Mataifa unaohudumia wote” (Restoring Trust, Managing Transformation: A United Nations That Delivers for All). Kaulimbiu hiyo ni wito wa pamoja wa kujenga upya uaminifu na ushirikiano wa kimataifa pamoja na kusimamia vema mabadiliko makubwa yanayoendelea ulimwenguni ikiwemo kasi ya ukuaji wa akili unde (AI).
Aidha, Mheshimiwa Makamu wa Rais anatarajiwa kuhutubia Kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pamoja na kushiriki kwenye vikao mbalimbali ikiwemo Mjadala Mkuu (General Debate), Mikutano ya pembezoni na Mikutano ya pande mbili (Bilateral Meetings)