Halmashauri Ya Mbozi Yatangaza Nafasi 10 Za Kazi

Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imetangaza nafasi 10 za kazi kwa Watanzania wenye sifa, zikiwemo nafasi tano za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II na nafasi tano za Dereva Daraja la II.

Tangazo hilo limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, kufuatia kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Nafasi za Mwandishi Mwendesha Ofisi

Kwa nafasi tano za Mwandishi Mwendesha Ofisi Daraja la II, majukumu yanajumuisha kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na za siri, kupokea wageni na kuwaelekeza sehemu husika, kutunza taarifa na kumbukumbu za matukio, miadi, wageni na ratiba za kazi.

Majukumu mengine ni kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika, kupokea na kusambaza majalada kwa maofisa husika, kutunza majalada na nyaraka, kuandaa maandalizi ya vikao pamoja na orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.

Mwombaji wa nafasi hiyo anatakiwa kuwa na Elimu ya Kidato cha Nne au Sita na Stashahada ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 ya Uhazili. Pia anatakiwa kuwa amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza kwa maneno 100 kwa dakika moja na kuwa na ujuzi wa programu za kompyuta za ofisi, ikiwemo Word, Excel, PowerPoint, Internet, E-mail na Publisher.

Nafasi hiyo ina mshahara wa TGS C.

Nafasi za Dereva

Halmashauri pia imetangaza nafasi tano za Dereva Daraja la II.

Majukumu ya dereva ni pamoja na kukagua gari kabla na baada ya safari, kuwapeleka watumishi katika maeneo mbalimbali kwa safari za kikazi, kufanya matengenezo madogo ya gari, kukusanya na kusambaza nyaraka, kutunza taarifa za safari katika daftari la safari na kufanya usafi wa gari.

Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne pamoja na Leseni ya Daraja E au C, akiwa na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Pia anatakiwa kuwa na vyeti vya mafunzo vilivyompatia sifa ya kupata madaraja hayo na kuwa amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari yanayotolewa na VETA au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

Nafasi hiyo ina mshahara wa TGS B1.

Masharti kwa waombaji

Tangazo limeeleza kuwa waombaji wote wanapaswa kuwa raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 45. Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanatakiwa kuainisha ulemavu walionao kwenye mfumo wa kuombea ajira.

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha CV yenye maelezo binafsi, anuani, namba za simu, barua pepe pamoja na majina ya wadhamini watatu, na kuambatanisha vyeti vya elimu na taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.

Aidha, “Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of Results” pamoja na hati za matokeo za Kidato cha Nne na Sita hazitakubaliwa. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na kuthibitishwa na mamlaka husika.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni Oktoba 1, 2026. Waombaji wanatakiwa kuambatanisha barua ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. Barua hiyo ielekezwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W), Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, S.L.P. 3, Mbozi.

Maombi yote yanapaswa kutumwa kielektroniki kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira. Tangazo limeeleza kuwa maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu huo hayatafanyiwa kazi.

Rais Samia Atoa Pole Kifo cha Mama Fatma Karume

Global Publishers
September 22, 2026
0 views
0 Comments

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, leo Septemba 22, 2026, imesema Rais Samia amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mama Fatma Karume, ambaye pia alikuwa mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika salamu zake, Rais Samia ametoa pole kwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Karume, pamoja na familia, ndugu, jamaa na wananchi wote wa Zanzibar kutokana na msiba huo.

Aidha, Rais Samia amewaombea wafiwa wote subira na faraja katika kipindi hiki cha majonzi.

“Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amin,” imeeleza sehemu ya salamu hizo.

Salamu hizo zimetolewa kwa niaba ya Rais Samia na Bakari S. Machumu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

NSSF YAJIVUNIA MIAKA MITANO YA MAFANIKIO MAKUBWA

 

Na Matukio DaimaMedia 

Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeeleza kurekodi mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka mitano, huku thamani ya Mfuko ikipanda kwa asilimia 125 na kufikia Sh11.41 trilioni Juni 2026, kutoka Sh5.06 trilioni mwaka 2020/21.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya Mfuko huo mbele ya Wahariri wa Vyombo vya Habari.

Amesema ukuaji huo umeenda sambamba na ongezeko la wanachama, makusanyo ya michango, thamani ya vitega uchumi na kasi ya ulipaji wa mafao kwa wastaafu na wanufaika.

Kwa mujibu wa Mshomba, thamani ya vitega uchumi vya NSSF imeongezeka kwa asilimia 108, kutoka Sh4.62 trilioni mwaka 2020/21 hadi Sh9.60 trilioni mwaka 2025/26.

“Ukuaji huu mkubwa unathibitisha kuwa NSSF ipo imara na endelevu. Ongezeko hili limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa thamani ya vitega uchumi, michango ya wanachama pamoja na mapato yatokanayo na uwekezaji katika miradi mbalimbali ya kimkakati,” amesema.

Katika kipindi hicho, NSSF imeandikisha wanachama wapya 1,486,930, huku idadi ya wanachama wachangiaji ikiongezeka kwa asilimia 130, kutoka 932,112 Juni 2021 hadi 2,144,906 Juni 2026.

Ongezeko hilo limekwenda sambamba na kuimarika kwa makusanyo ya michango, ambayo yamepanda kwa asilimia 147 kutoka Sh1.17 trilioni mwaka 2020/21 hadi Sh2.90 trilioni katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2026.

Mshomba amesema NSSF pia imefanya maboresho katika viwango vya mafao, ambapo malipo ya mafao ya mkupuo yameongezeka kutoka asilimia 25 hadi 35.

Aidha, kima cha chini cha pensheni ya kila mwezi kimeongezeka kutoka Sh100,000 hadi Sh150,000, huku viwango vya pensheni kwa baadhi ya wastaafu vikiongezeka kati ya asilimia mbili na 20.

Malipo ya mafao kwa wastaafu na wanufaika yameongezeka kutoka Sh594.33 bilioni mwaka 2020/21 hadi Sh1.16 trilioni mwaka 2025/26.

Mshomba amesema NSSF pia imepunguza muda wa kushughulikia madai, ambapo wastani wa siku za kulipa madai yaliyokamilika umeshuka kutoka siku 63 mwaka 2021 hadi siku 19 Juni 2026.

Amesema asilimia 99 ya madai ya mafao yaliyofunguliwa yamelipwa ndani ya muda wa kisheria wa siku 60.

Katika uwekezaji, Mshomba amesema miradi kadhaa iliyokuwa imesimama, ikiwamo nyumba za makazi za Dungu, Toangoma, Mtoni Kijichi na Jengo la Mzizima, ilirejelewa mwaka 2023 baada ya kufanyika kwa ukaguzi maalum.

Miradi hiyo inatarajiwa kukamilika kati ya Desemba 2026 na Machi 2027.

Kuhusu Kiwanda cha Sukari Mkulazi, amesema kimezalisha tani 45,594 za sukari ya majumbani, kikiingiza mapato ya Sh107.90 bilioni na kupata faida ya Sh4.56 bilioni katika mwaka wa fedha 2025/26.

Akizungumzia mipango ijayo, Mshomba amesema kupitia Mpango Mkakati wa Nane wa NSSF wa 2026–2031, Mfuko unalenga kuongeza thamani yake hadi Sh24.75 trilioni na kuandikisha wanachama wapya milioni 5.8 ifikapo Juni 2031.

Awali, mwakilishi wa Msajili wa Hazina (TR), Sabato Kosuri, amesema mkutano huo ni sehemu ya mkakati wa Ofisi ya Msajili wa Hazina wa kuziwezesha taasisi za umma kukutana na wahariri na kueleza shughuli zake kwa Watanzania.

“Hii ni awamu ya pili ya mikutano hii na NSSF inakuwa taasisi ya kwanza kukutana na wahariri. Zipo taasisi zaidi ya 400 ambazo tutazifanyia mikutano kama hii ili kuwapa fursa Watanzania kujua taasisi hizi za umma zinatendaje kazi zake,” amesema Kosuri.

DIT YASHIRIKI MAFUNZO YA KITAIFA, YAWAWEZESHA VIJANA KUTUMIA TEHAMA KUTANGAZA UJUZI

  Na Mwandishi Wetu.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewataka vijana nchini kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kutangaza ujuzi na ubunifu wao, kujiajiri pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza, ikiwemo fursa zinazotarajiwa kutokana na ujio wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Wito huo umetolewa leo na Dkt. Maryam Ismail, Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Juu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, aliyemwakilisha Mkurugenzi Prof. Stephen Oswald Maluka, wakati wa ufunguzi wa kitaifa wa mafunzo ya mradi wa majaribio unaolenga kuimarisha uwezo wa vijana na kuwaongezea fursa za ajira kupitia ujuzi wa kidigitali.

Mafunzo hayo pia yanalenga kupanua fursa za vijana katika kujifunza na kutumia teknolojia katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Tukio hilo limehusisha taasisi sita za elimu ya juu ambazo ni Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IAА), Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dodoma.

Taasisi hizo zimeshiriki mafunzo hayo kwa njia ya mtandao, huku shughuli kuu za ufunguzi zikifanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), Morogoro.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Dkt. Mariam amesema ujuzi wa kidigitali si jambo la ziada katika elimu, bali ni sehemu muhimu ya ujuzi wa msingi unaohitajika katika maisha, ajira, biashara na ujasiriamali kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Amesema vijana wanapaswa kutumia majukwaa ya kidigitali kutangaza uwezo, ubunifu na bidhaa zao ili kuongeza fursa za kiuchumi na kuwa sehemu ya kunufaika na fursa zinazotokana na maendeleo ya teknolojia pamoja na matukio makubwa ya kimataifa yanayofanyika nchini.

Kwa upande wake, Naibu Mkuu wa Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Prof. Ezekiel Amri, amesema DIT ni taasisi iliyobobea katika masuala ya teknolojia ya habari na kwamba inajikita katika kuwapatia vijana ujuzi wa kidigitali utakaowasaidia kuboresha shughuli zao za kibiashara, ubunifu na utengenezaji wa maudhui.

Amri amesema mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha vijana kutumia teknolojia kama nyenzo ya kuongeza thamani katika shughuli zao na kufungua milango ya fursa mbalimbali.

Naye Mhadhiri kutoka Idara ya Kompyuta wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Phinian Mwalongo, amesema kupitia mafunzo hayo vijana watajengewa uwezo wa namna ya kuweka na kuwasilisha ujuzi wao kwenye kurasa zao za majukwaa ya kidigitali.

Amesema hatua hiyo itasaidia kurahisisha upatikanaji wao na waajiri, wateja na wadau mbalimbali wanaoweza kuhitaji ujuzi na huduma wanazozitoa.

Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za kuwawezesha vijana kutumia teknolojia ya kidigitali katika kujitangaza, kujiajiri, kubuni bidhaa na huduma pamoja na kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia uchumi wa kidigitali.

Wakala wa Vipimo Atangaza Nafasi Tisa (9) za Kazi za Kujitolea, Maombi Mwisho Oktoba 2

Global Publishers
September 22, 2026
0 views
0 Comments

Wakala wa Vipimo (WMA) umetangaza nafasi tisa (9) za kazi za kujitolea kwa wahitimu wa Kitanzania, kwa kipindi cha miezi 12, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuwawezesha vijana kupata ujuzi na uzoefu wa vitendo katika mazingira ya kazi. Tangazo hilo limetolewa Septemba 18, 2026.

Nafasi hizo ni kama ifuatavyo:

  • Afisa Msaidizi wa Vipimo (Assistant Weights and Measures Officer) – nafasi 5: Mwombaji anatakiwa kuwa na Stashahada ya Legal and Industrial Metrology kutoka taasisi inayotambuliwa.
  • Afisa Uhusiano kwa Umma II (Public Relations Officer II) – nafasi 2: Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Mawasiliano ya Umma, Uandishi wa Habari, Uhusiano kwa Umma, Mawasiliano ya Biashara au fani inayohusiana.
  • Afisa TEHAMA II (ICT Officer II) – nafasi 1: Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada katika Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa Programu, Uhandisi wa Mawasiliano, Uhandisi wa Elektroniki, Uhandisi wa Mitandao, Mifumo ya Habari, Usalama wa Mtandao, Teknolojia ya Habari, Uhandisi wa Kompyuta au fani inayohusiana.
  • Mchumi II (Economist II) – nafasi 1: Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uchumi, Takwimu, Uchumi wa Kilimo, Mipango na Uwekezaji, Mipango ya Kiuchumi, Mipango na Usimamizi wa Miradi au sifa zinazolingana.

Sifa na masharti ya jumla

Waombaji wanapaswa kuwa raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 na 35. Wanatakiwa kuwasilisha CV yenye mawasiliano sahihi, nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu na taaluma, transcripts pamoja na cheti cha kuzaliwa. Pia wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa umma na barua ya utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa au mamlaka husika ya Serikali za Mitaa.

Mwombaji pia anatakiwa kuambatanisha nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA), asiwe amewahi kuhukumiwa na mahakama kwa makosa ya jinai au kinidhamu, na asiwe amewahi kuajiriwa na taasisi ya umma tangu alipohitimu masomo. Vyeti vya kigeni vinapaswa kutambuliwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA au NACTVET.

WMA imeeleza kuwa mpango huo ni kwa ajili ya kujenga ujuzi na kupata uzoefu wa kazi, na haupaswi kutafsiriwa kuwa msingi wa kuajiriwa moja kwa moja katika Utumishi wa Umma.

Jinsi ya kuomba

Barua ya maombi iliyosainiwa, ikiandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza, inapaswa kuelekezwa kwa:

Chief Executive Officer,
Weights and Measures Agency (WMA),
P.O. Box 2014,
Vipimo House,
Dodoma.

Waombaji walioteuliwa kwa usaili ndio watakaowasiliana nao. Maombi yanapaswa kufika ndani ya siku 14 tangu tarehe ya tangazo, yaani hadi takribani Oktoba 2, 2026.

TANZANIA, MISRI ZAAZIMIA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIDIPLOMASIA NA KIUCHUMI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amesema Tanzania na Misri zimedhamiria kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa nchi hizo katika biashara, uwekezaji, miundombinu, elimu, afya na masuala ya kimataifa.

Waziri Kombo amesema hayo katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje anayeshughulikia pia Ushirikiano wa Kimataifa na masuala ya Wamisri waishio Nje ya Nchi, Mhe. Dkt. Badr Abdelatty, yaliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York, nchini Marekani ambapo amesisitiza umuhimu wa kuongeza biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo.

Amesema Misri ina miradi 61 ya uwekezaji nchini Tanzania yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.5, inayotekelezwa katika sekta mbalimbali na kutoa ajira 5,364.

Akizungumzia ushirikiano wa kimkakati, Waziri Kombo amesema Tanzania inathamini mchango wa kampuni za Misri katika kutekeleza miradi ya maendeleo nchini, hususan Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115. Mradi huo ulitekelezwa na kampuni za Misri na kuzinduliwa Agosti 22, 2026.

Katika sekta za kijamii, Tanzania na Misri zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika elimu, afya, kilimo, maji na teknolojia. Misri imeahidi kutoa nafasi 10 za ufadhili kupitia Samia Scholarship, huku zaidi ya Watanzania 420 wenye matatizo makubwa ya moyo wakinufaika na huduma za upasuaji kupitia kambi za madaktari wa Misri nchini Tanzania.

Kwa upande wake, Mhe. Abdelatty amesisitiza dhamira ya Misri ya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kiuchumi, kijamii, kidiplomasia na ushirikiano wa kimataifa kwa maslahi ya wananchi wa nchi hizo mbili.

 

UDOM Yatangaza Nafasi Mpya za Kazi 15, Maombi Septemba 28, 2026

Global Publishers
September 22, 2026
0 views
0 Comments

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetangaza nafasi mbalimbali za ajira kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika, kwa ajili ya kujaza nafasi za kitaaluma. Tangazo hilo limetolewa Septemba 15, 2026.

Nafasi zilizotangazwa

  1. Tutorial Assistant – Fine Arts and Design – Nafasi 1
  2. Tutorial Assistant – International Relations – Nafasi 1
  3. Tutorial Assistant – History – Nafasi 1
  4. Tutorial Assistant – Chinese Language – Nafasi 1
  5. Tutorial Assistant – Biotechnology and Bioinformatics – Nafasi 1
  6. Tutorial Assistant – Applied Entomology – Nafasi 1
  7. Tutorial Assistant – Biomedical Engineering – Nafasi 1
  8. Tutorial Assistant – Psychiatry and Mental Health – Nafasi 1
  9. Tutorial Assistant – Pathology – Nafasi 1
  10. Tutorial Assistant – Physics Teaching Methods – Nafasi 1
  11. Tutorial Assistant – Biology Teaching Methods – Nafasi 2
  12. Tutorial Assistant – Nursing Nephrology – Nafasi 2
  13. Tutorial Assistant – Health Information Science – Nafasi 1

Kwa nafasi nyingi za Tutorial Assistant, mwombaji anatakiwa kuwa na shahada husika yenye GPA ya angalau 3.8 kati ya 5, ingawa sifa zinatofautiana kulingana na nafasi.

Masharti muhimu

Waombaji wote wanapaswa kuwa raia wa Tanzania na wasiwe na umri zaidi ya miaka 45. Pia wanatakiwa kuambatanisha CV yenye mawasiliano sahihi pamoja na nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu, transcripts, vyeti vya Form IV na Form VI, vyeti vya usajili wa kitaaluma pale inapohitajika, pamoja na cheti cha kuzaliwa.

Waombaji walio katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi, kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa kwenye tangazo.

Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 28, 2026. Maombi yote yanatakiwa kutumwa kupitia Recruitment Portal ya Ajira iliyoainishwa kwenye tangazo.

Davido Atangaza Shoo Kubwa ya Siku Tatu Lagos, Nigeria

Global Publishers
September 22, 2026
0 views
0 Comments

Msanii mkubwa wa Nigeria, Davido, ametangaza kufanya maonyesho maalum ya siku tatu mfululizo katika jiji la Lagos, Nigeria, kuelekea mwisho wa mwaka 2026.

Davido ametangaza show hiyo ya siku tatu katika National Theatre, Lagos, itakayofanyika kuanzia Desemba 17 hadi 19, 2026.

Katika maonyesho hayo, Davido anatarajiwa ku-perform kwa mara ya kwanza album yake mpya, ORIADE, kwa ukamilifu mjini Lagos, pamoja na nyimbo zake nyingine kubwa zilizomjengea jina katika kipindi cha miaka 15 ya safari yake ya muziki.

Tukio hilo pia lina umuhimu mkubwa kwa Davido kwa sababu linakuja wakati anatimiza miaka 15 tangu aanze safari yake ya muziki. Waandaaji pia wametangaza kuwa kutakuwa na wageni maalum watakaoshiriki katika baadhi ya siku hizo tatu.

Tangazo hilo limeambatana na trailer ya residency hiyo pamoja na video mpya ya Davido ya wimbo “On The Road,” ambayo inaonyesha vipande mbalimbali vya safari yake ya kimuziki katika mwaka uliopita.

Na RAZAKU RAMADHAN | GPL- TUDACO

MAGAZETINI LEO JUMANNE SEPT 22/2026: AJALI YAUA MAHABUSU SABA NA ASKARI WATANO …

 

 

Wapendwa wangu, nawashukuru sana kwa moyo wenu wa upendo na kwa kila kura mnayonipigia kwenye Samia Kalamu Awards 2026.

Ninaithamini sana sapoti yenu. Naomba tuendelee na safari hii pamoja kwa kunipigia kura yako kila baada ya saa 24 

Tafadhali pia mshirikishe ndugu, jamaa na rafiki ili tuzidi kusonga mbele.

Asanteni sana kwa kutuamini na kusimama na Matukio Daima Media . Mungu awabariki sana. 

KUENDELEA KUTUPIGIA KURA FUATA MAELEKEZO HAYA CHINI ⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

3:TUZO YA AFYA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

Rais Mwinyi Atuma Salamu za Pole kwa Familia ya Mama Fatma Karume

Global Publishers
September 22, 2026
0 views
0 Comments

ZANZIBAR: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametuma salamu za pole kwa Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, pamoja na familia, ndugu na jamaa kufuatia kifo cha Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Mama Fatma Karume amefariki dunia Septemba 21, 2026.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Ikulu Zanzibar, Rais Dkt. Mwinyi amesema amepokea taarifa hiyo kwa masikitiko makubwa na kueleza kuwa anaungana na familia ya Hayati Sheikh Abeid Amani Karume pamoja na wananchi wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki cha majonzi.

Rais Mwinyi amesema Marehemu Mama Fatma Karume amekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania, akiwa mjane wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amemuomba Mwenyezi Mungu amsamehe na amrehemu Marehemu Mama Fatma Karume, amjaalie mahala pema Peponi, pamoja na kuipa familia subira katika kipindi hiki kigumu.

“Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Raji’un.”