Wakala wa Vipimo Atangaza Nafasi Tisa (9) za Kazi za Kujitolea, Maombi Mwisho Oktoba 2

Global Publishers
September 24, 2026
996 views
0 Comments

Wakala wa Vipimo (WMA) umetangaza nafasi tisa (9) za kazi za kujitolea kwa wahitimu wa Kitanzania, kwa kipindi cha miezi 12, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuwawezesha vijana kupata ujuzi na uzoefu wa vitendo katika mazingira ya kazi. Tangazo hilo limetolewa Septemba 18, 2026.

Nafasi hizo ni kama ifuatavyo:

  • Afisa Msaidizi wa Vipimo (Assistant Weights and Measures Officer) – nafasi 5: Mwombaji anatakiwa kuwa na Stashahada ya Legal and Industrial Metrology kutoka taasisi inayotambuliwa.
  • Afisa Uhusiano kwa Umma II (Public Relations Officer II) – nafasi 2: Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Mawasiliano ya Umma, Uandishi wa Habari, Uhusiano kwa Umma, Mawasiliano ya Biashara au fani inayohusiana.
  • Afisa TEHAMA II (ICT Officer II) – nafasi 1: Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada katika Sayansi ya Kompyuta, Uhandisi wa Programu, Uhandisi wa Mawasiliano, Uhandisi wa Elektroniki, Uhandisi wa Mitandao, Mifumo ya Habari, Usalama wa Mtandao, Teknolojia ya Habari, Uhandisi wa Kompyuta au fani inayohusiana.
  • Mchumi II (Economist II) – nafasi 1: Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uchumi, Takwimu, Uchumi wa Kilimo, Mipango na Uwekezaji, Mipango ya Kiuchumi, Mipango na Usimamizi wa Miradi au sifa zinazolingana.

Sifa na masharti ya jumla

Waombaji wanapaswa kuwa raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 18 na 35. Wanatakiwa kuwasilisha CV yenye mawasiliano sahihi, nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu na taaluma, transcripts pamoja na cheti cha kuzaliwa. Pia wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa umma na barua ya utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa au mamlaka husika ya Serikali za Mitaa.

Mwombaji pia anatakiwa kuambatanisha nakala ya kitambulisho cha Taifa (NIDA), asiwe amewahi kuhukumiwa na mahakama kwa makosa ya jinai au kinidhamu, na asiwe amewahi kuajiriwa na taasisi ya umma tangu alipohitimu masomo. Vyeti vya kigeni vinapaswa kutambuliwa na mamlaka husika kama TCU, NECTA au NACTVET.

WMA imeeleza kuwa mpango huo ni kwa ajili ya kujenga ujuzi na kupata uzoefu wa kazi, na haupaswi kutafsiriwa kuwa msingi wa kuajiriwa moja kwa moja katika Utumishi wa Umma.

Jinsi ya kuomba

Barua ya maombi iliyosainiwa, ikiandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza, inapaswa kuelekezwa kwa:

Chief Executive Officer,
Weights and Measures Agency (WMA),
P.O. Box 2014,
Vipimo House,
Dodoma.

Waombaji walioteuliwa kwa usaili ndio watakaowasiliana nao. Maombi yanapaswa kufika ndani ya siku 14 tangu tarehe ya tangazo, yaani hadi takribani Oktoba 2, 2026.

TANZANIA NA RWANDA ZAZUNGUMZIA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amefanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Mhe. Olivier Nduhungirehe, pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani.

Mazungumzo hayo yamejikita katika masuala ya kidiplomasia, kiuchumi na kimataifa, yakilenga kuimarisha ushirikiano na uhusiano ya kihistoria kati ya Tanzania na Rwanda, kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.

 

MAGAZETINI LEO ALHAMIS SEPT 24/2026:DAWA ZA KUACHA POMBE ZAWASILI,TANZANIA YAANIKA MAFANIKIO YA AFYA UN.

 .

 

 

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

3:TUZO YA AFYA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

🚨ZIMEBAKI SIKU 6 ZOEZI KUFUNGWA

DAWA YA KUACHA POMBE YAINGIA NCHINI

CHANGAMOTO ya baadhi ya watu kulewa kupitia kiasi na hata baadhi yao pombe kuwaletea madhara makubwa ya kiafya sasa imepatiwa ufumbuzi baada ya Bohari ya Dawa (MSD) imefanikiwa kuingiza shehena ya kwanza ya dawa ya tiba ya uraibu wa pombe iitwayo Naltrexone.

Hatua hii ni matokeo ya ushirikiano wa kimkakati kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe katika kuimarisha matibabu ya uraibu wa pombe nchini. 

 

Taarifa iliyotolewa na Etty Kusiluka, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Bohari ya Dawa (MSD) imesema hatua hii pia ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa makubaliano ya uimarishaji huduma kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili-Mirembe kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za udhibiti wa urahibu wa pomnbe.

Dawa ya Naltrexone itapatikana na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe huku ikiwa ni bidhaa itakayo endelea kununuliwa na MSD kwa ajili ya taasisi hiyo. 

Mapema mwezi huu, wakati wa mafunzo kuhusu matumizi ya dawa ya Naltrexone, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe aliwaagiza MSD kuharakisha upatikanaji wa vidonge hivyo.

MSD imepokea na kuingiza shehena hii nchini ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za afya ya akili na tiba ya uraibu pombe. Mafanikio haya yanaonesha juhudi za Serikali kupitia MSD na wadau wa sekta ya afya kuhakikisha bidhaa muhimu za afya na za kimkakati zinapatikana nchini kwa wakati.

KUPIGA KURA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS 2026 INGIA HAPA

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

3:TUZO YA AFYA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

🚨ZIMEBAKI SIKU 6 ZOEZI KUFUNGWA

DAWA YA KUACHA POMBE YAINGIA NCHINI

CHANGAMOTO ya baadhi ya watu kulewa kupitia kiasi na hata baadhi yao pombe kuwaletea madhara makubwa ya kiafya sasa imepatiwa ufumbuzi baada ya Bohari ya Dawa (MSD) imefanikiwa kuingiza shehena ya kwanza ya dawa ya tiba ya uraibu wa pombe iitwayo Naltrexone.

Hatua hii ni matokeo ya ushirikiano wa kimkakati kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe katika kuimarisha matibabu ya uraibu wa pombe nchini. 

 

Taarifa iliyotolewa na Etty Kusiluka, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Bohari ya Dawa (MSD) imesema hatua hii pia ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa makubaliano ya uimarishaji huduma kati ya MSD na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili-Mirembe kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za udhibiti wa urahibu wa pomnbe.

Dawa ya Naltrexone itapatikana na kuratibiwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe huku ikiwa ni bidhaa itakayo endelea kununuliwa na MSD kwa ajili ya taasisi hiyo. 

Mapema mwezi huu, wakati wa mafunzo kuhusu matumizi ya dawa ya Naltrexone, yaliyoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe aliwaagiza MSD kuharakisha upatikanaji wa vidonge hivyo.

MSD imepokea na kuingiza shehena hii nchini ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha huduma za afya ya akili na tiba ya uraibu pombe. Mafanikio haya yanaonesha juhudi za Serikali kupitia MSD na wadau wa sekta ya afya kuhakikisha bidhaa muhimu za afya na za kimkakati zinapatikana nchini kwa wakati.

DC Kilosa afanya ziara kusikiliza kero, kutatua migogoro – HabariLeo

MOROGORO; Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka, akiwa ameambatana na  Kamati ya Usalama Wilaya, amefanya ziara ya kusikiliza kero za wananchi Tarafa ya Mikumi na kutatua kutatua migogoro.

Pia katika ziara hiyo amekagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Nyamfisi na kufanya mikutano ya hadhara kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo katika Kata za Vidunda, Ruhembe, Kidodi na Ruaha.

SERIKALI YAANDAA MKAKATI WA KUONGEZA UZALISHAJI WA VIFARANGA BORA VYA SAMAKI

 Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa vijana na wajasiriamali wanaofuga samaki ili kuwajengea uwezo wa kuzalisha vifaranga bora, hatua inayolenga kupunguza uhaba wa vifaranga hivyo nchini.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ongezeko la mahitaji ya vifaranga bora linalochangiwa na kukua kwa teknolojia za uzalishaji na ufugaji wa samaki kwa kiwango kikubwa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa vijana zaidi ya 60 kutoka mikoa mbalimbali nchini, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Maji katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Janeth Rukanda, amesema lengo la Serikali ni kuwajengea uwezo vijana wengi zaidi kuhusu uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki.

Rukanda amesema hatua hiyo itawawezesha vijana kufanya ufugaji wa samaki kwa tija, kuongeza kipato chao na kuongeza idadi ya wataalamu na wajuzi katika sekta ya ufugaji wa samaki nchini.

Amesema tafiti zilizofanyika katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025 zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji wa vifaranga vya samaki. Hata hivyo, amesema ongezeko hilo limekwenda sambamba na kuongezeka kwa mahitaji ya vifaranga kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika sekta ya ufugaji wa samaki.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi

(FETA)  Merisia Mparazo, amewataka vijana wanaoshiriki mafunzo hayo ya siku nne kuzingatia kwa umakini mafunzo wanayopewa, akisema ujuzi watakaoupata utawasaidia kufanya ufugaji wenye tija na kujikwamua kiuchumi.

“Bila kuzingatia mafunzo haya, mtakuwa mmefika hapa bila kufahamu vizuri kuhusu ufugaji. Msipokuwa makini na kuwasikiliza ipasavyo wakufunzi, mtaondoka bila kupata maarifa ya kutosha. Hili litakuwa hasara kwenu na kwa Serikali, kwa sababu mafunzo kama haya yanatumia gharama kubwa,” alisema Mparazo.

Miongoni mwa vijana wanaoshiriki mafunzo hayo ni Gojo Muhammed na Radhia Suleiman, ambao wameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwapatia mafunzo hayo, wakisema yatawasaidia kuongeza ujuzi na kuwajengea uwezo wa kuzalisha vifaranga bora vya samaki.

 

Rais wa Iran: Hatutapiga Magoti Mbele ya Shinikizo la Marekani

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema nchi yake haitasalimu amri wala “kupiga magoti” mbele ya shinikizo kutoka Marekani, akitoa kauli hiyo wakati akihutubia Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) mjini New York.

Pezeshkian amesema Iran itaendelea kupinga vikwazo, shinikizo na kile alichokiita vitisho dhidi ya nchi yake, akimlenga Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye siku moja kabla alitoa kauli kuhusu uwezekano wa kuchukua hatua kali dhidi ya Iran huku akisema mazungumzo kati ya Washington na Tehran yanaendelea.

Katika hotuba yake, Pezeshkian aliishutumu Marekani kwa kile alichokiita “ugaidi”, akirejea kuuawa kwa aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, mwanzoni mwa vita. Pia alionyesha picha ya Khamenei pamoja na picha za watoto wa shule wa Iran waliouawa katika siku za mwanzo za mashambulizi.

Rais huyo amesisitiza kuwa Iran haikuanza vita na kwamba nchi yake ilichukua hatua za kujilinda dhidi ya mashambulizi kutoka Marekani na Israel.

“Upinzani wa watu wa Iran utaongezeka tu mbele ya vikwazo, shinikizo na vitisho vinavyoongezeka. Hatutainamisha vichwa vyetu wala kupiga magoti,” Pezeshkian alisema.

Pezeshkian pia amezungumzia Mlango wa Hormuz, akisema Tehran haitaruhusu njia hiyo ya kimkakati ya usafirishaji wa mafuta itumike kama chombo cha mashambulizi dhidi ya Iran.

Amesema Iran haiwezi kuruhusu baadhi ya nchi kutumia njia hiyo kwa uhuru na kunufaika nayo huku ikitumiwa pia kuendeleza kile alichokiita uchokozi dhidi ya nchi yake.

Licha ya msimamo huo mkali, Pezeshkian amesema Iran iko tayari kwa mazungumzo na diplomasia, lakini si mazungumzo yanayoendeshwa kwa lugha ya vitisho au matumizi ya nguvu.

Hotuba hiyo imekuja siku moja baada ya Trump kuhutubia UN na kueleza msimamo wake kuhusu Iran, huku akitaja pia uwezekano wa makubaliano kati ya Marekani na Tehran. Kauli hizo zinafuatia kipindi cha mvutano mkubwa kati ya pande hizo kuhusu vita na masuala mengine ya usalama katika eneo hilo.

HOFU YA MAPOROMOKO YA ARDHI, KAYA 40 CHOME, WILAYA YA SAME ZATAKIWA KUONDOKA

Na Ashrack Miraji Same Kilimanjaro 

Takribani kaya 40 katika kijiji cha Marieni, Kata ya Chome wilayani Same, zimeagizwa kuhama haraka katika maeneo hayo baada ya ardhi kusogea na kusababisha nyufa kubwa kujitokeza ardhini na kuleta uharibifu wa takribani nyumba 10 pamoja na kanisa moja, ambapo Serikali imesema hatua hiyo ni ya haraka kutokana na hatari ya kutokea kwa maafa katika eneo hilo lenye milima na miteremko kwa hofu ya kuporomoka kwa miamba.

Agizo hilo limetolewa baada ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) iliyopo chini ya wizara ya Madini kufanya utafiti na kubaini mabadiliko ya kijiolojia yanayoendelea chini ya ardhi katika eneo hilo na kusababisha nyufa na uharibifu huo. Mjiolojia kutoka GST Mjiolojia Mwandamizi Gabriel Mbogoni amesema utafiti umeonesha uwepo wa tabaka nene la udongo wa mfinyanzi ambalo lina maji, hali inayofanya ardhi kupoteza uimara na kuongeza uwezekano wa kusogea zaidi au kuporomoka.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, nyufa zimeonekana kuanzia maeneo ya juu ya mlima hadi katika mashamba na maeneo ya karibu na kanisa lililoharibiwa, huku baadhi ya miundombinu ya zege ikionekana kuinuka kutokana na msukumo unaotokea chini ya ardhi, amesema vipimo vya jiolojia na usumaku pia vimeonesha uwepo wa maeneo yenye tabaka kubwa la udongo wa mfinyanzi.

Mjiolojia huyo amesema hali hiyo ni matokeo ya mchakato wa muda mrefu wa kijiolojia, lakini shughuli za binadamu zimechangia kudhoofisha zaidi ardhi hiyo. Ametaja ukataji wa miti, kilimo na matumizi ya mifereji ya wazi ya umwagiliaji kuwa miongoni mwa mambo yanayofanya maji kubaki ardhini kwa muda mrefu na kupunguza uimara wa udongo wa mfinyanzi.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Makandeni, Marry Abuduel, amesema wamepokea maelekezo ya Serikali na wako tayari kuyatekeleza, lakini changamoto kubwa ni kupata maeneo salama ya kuwapeleka wananchi watakaohama aidha, ameomba TANESCO kuchukua hatua kuhusu baadhi ya nguzo za umeme katika maeneo hayo, akisema zimekuwa zikitumika kwa zaidi ya miaka 26, nyingine zimeanza kuoza na baadhi ya nyaya ziko karibu na ardhi yenye nyufa.

Mwananchi Elisa Mtera amesema hali hiyo imewaweka wananchi katika hofu kubwa kutokana na kuendelea kwa nyufa, huku familia zikikabiliwa na changamoto ya kutokuwa na maeneo ya kwenda endapo wataondoka, amesema wananchi, wazazi na watoto hawaishi kwa amani kutokana na hofu ya maafa, hasa wakati wa mvua za el nino, na kuiomba Serikali kuwapatia maeneo mbadala kwa haraka.

Akitoa maelekezo ya Serikali, Mkuu wa Wilaya Shikizi ya Same, Rukia Zuberi, amesema baada ya kusikiliza wataalamu, Serikali imebaini kuwa maeneo hayo si salama tena kwa makazi wala shughuli za maendeleo, hivyo wananchi wanapaswa kuondoka haraka huku akuwaagiza viongozi wa Halmashauri, kata na vijiji wana wajibu wa kuanza mchakato wa kutafuta maeneo salama ya makazi ya kudumu, huku wananchi wakitakiwa kuchukua hatua mapema za kuokoa maisha na mali zao.

 

Rukia amesema wananchi hawapaswi kusubiri maafa yatokee ndipo wachukue hatua, kwa kuwa maporomoko ya ardhi yanaweza kutokea wakati wowote na muda wake hauwezi kutabirika kwa usahihi. Amesisitiza kuwa tahadhari hiyo haiwahusu wakazi wa Chome pekee, bali wananchi wote wanaoishi katika maeneo yaliyobainishwa kuwa hatarishi, akiwataka kuondoka mapema wakati Serikali ikiendelea na mchakato wa kuwapatia maeneo salama ya kuishi.