Masauni ataka ubunifu kukabili tabianchi – HabariLeo

ARUSHA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amezitaka nchi za Afrika kutumia changamoto za mabadiliko ya tabianchi kuibua ubunifu, utafiti na maendeleo badala ya kujiona waathirika pekee.

Masauni ametoa wito huo jijini Arusha wakati akifunga Kongamano la Vyuo Vikuu Vitano lililofanyika katika Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia (NM-AIST).

Amesema athari za mabadiliko ya tabianchi tayari zinaonekana katika sekta mbalimbali, ikiwemo kilimo, maji, afya, miundombinu, nishati na mifumo ya ikolojia, hivyo ni muhimu ustahimilivu dhidi ya athari hizo kupewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo, tafiti na sera.

“Afrika haipaswi kuangalia changamoto ya tabianchi kwa mtazamo wa kuwa waathirika pekee. Tunapaswa pia kuangalia fursa, ubunifu na uongozi,” amesema Masauni.

Amesema hatua hiyo itasaidia nchi za Afrika kutumia maarifa na tafiti zinazozalishwa na taasisi za elimu ya juu katika kutafuta suluhisho la changamoto za tabianchi na kuimarisha maendeleo ya jamii.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa NM-AIST, Profesa Maulilio Kipanyula, amesema tafiti zinazofanywa na vyuo vikuu hazipaswi kubaki katika machapisho ya kitaaluma, bali zinapaswa kuwafikia wadau na kutumika kutatua changamoto zinazozikabili jamii.

“Utafiti pekee hautoshi. Utafiti lazima uwasilishwe, ueleweke na utumike na wadau,” alisema Profesa Kipanyula.

Amesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya vyuo vikuu, watafiti na wadau mbalimbali ili kuhakikisha matokeo ya tafiti yanageuzwa kuwa suluhisho la vitendo kwa changamoto za maendeleo na mabadiliko ya tabianchi.

CCM Kigoma yataka miradi ianze kutoka huduma – HabariLeo

KIGOMA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma kimezitaka halmashauri za mkoa huo kushughulikia changamoto zinazokwamisha miradi ya maendeleo ili iweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi licha ya kukamilika kwa baadhi ya majengo.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma, Jamal Tamim, wakati akiongoza Kamati ya Siasa ya chama hicho kukagua miradi ya maendeleo wilayani Buhigwe na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.

Akiwa katika Kituo cha Afya Rusaba wilayani Buhigwe, Tamim alishuhudia kituo hicho kushindwa kuanza kutoa huduma za upasuaji kutokana na ukosefu wa huduma ya maji, licha ya majengo ya huduma hiyo kukamilika.

Aidha, kamati hiyo ilibaini kuwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Bilate, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, kimeshindwa kuanza kutoa huduma licha ya kukamilika miaka miwili iliyopita, kwa sababu ya kuhitaji kupakwa rangi upya baada ya rangi ya awali kuchakaa.

Tamim alisema hali hiyo haikubaliki, akieleza kuwa Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi, hivyo ni jambo lisilofaa miradi kushindwa kutoa huduma kwa sababu ya changamoto zinazoweza kutatuliwa.

Alizitaka halmashauri kuhakikisha changamoto hizo zinashughulikiwa kwa wakati na kuwataka wakuu wa wilaya kuwa wakali katika usimamizi wa miradi ili kuhakikisha inakamilika na kuanza kutoa huduma zilizokusudiwa kwa wananchi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Kituo cha Afya Rusaba, Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Yohana Milinde, alisema jumla ya majengo tisa yamejengwa katika mradi huo ambao umegharimu Sh milioni 770.

Milinde alisema kuwa baada ya kukamilika kwa majengo ya kipaumbele, ikiwemo jengo la wagonjwa wa nje, jengo la huduma za uzazi na jengo la upasuaji, baadhi ya huduma zilianza kutolewa.

Hata hivyo, alisema huduma za upasuaji hazijaanza kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya maji, huku jitihada zikiendelea kufanyika kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa ili huduma hizo zianze kutolewa kwa wananchi.

Morocco, Ufaransa na Italia Kuongoza Kivumbi cha Mechi Kali Leo

Je unajua kuwa wikendi iliyopita kuna watu wameweza kubadili maisha yao kwa dau dogo kabisa la shilingi mia tano?. Huenda leo ikawa ni nafasi yako na wewe na unachotakiwa kufanya ni kutengeneza jamvi lako na ubeti sasa.

Kivumbi kitawaka mechi ya Uturuki dhidi ya Ufaransa ambao ni mabingwa wa Kombe la Dunia 2018 kikiwa ni kikosi chenye wachezaji wenye uwezo mkubwa sana kikiongozwa na nahodha wao Kylian Mbappe.

Ufaransa mpaka sasa ina kocha mpya ambaye ni Zinedine Zidane ambaye alichukua mikoba ya Deschamps amabye aliachia kazi ya kunoa kikosi icho la Bleus baada ya kumaliza nafasi ya 4 kwenye Kombe la Dunia.

Kikosi hicho kina wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa kama vile, Olise, Thuram, Dembele, Mbappe, Maignan na wengine wengi ambao kwa pamoja wana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu. Jisajili hapa.

Huku kwa Uturuki wao ni timu ambayo ina mchanganyiko wa wachezaji wenye uwezo tofauti tofauti ambao wengi wanacheza kwenye ligi ya Uturuki, lakini wachache ndio wapo kwenye ligi zingine kama vile kina Kenan Yildiz.

Pesa ndefu ipo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Timu hizi zinatarajiwa kuchuana vikali kuwania pointi 3 muhimu kwenye mechi ya kwanza ya UEFA Nations League huku takwimu zikionesha kuwa mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni 2019 ambapo hakuna aliyekuwa mbabe kati yao. Beti mechi hii.

Pesa ipo mechi ya  Italia dhidi ya Ubelgiji, mechi ambayo inaenda kuamuliwa  kwa uwezo wa wachezaji kwani zote hizi ni timu kubwa Duniani ambazo zina wachezaji wenye uwezo wa kufanana.

Timu ya Taifa ya Italia chini ya kocha mkuu Roberto Mancini ni timu ambayo ina uwezo mkubwa wa kutawala mpira, kujenga mashambulizi huku wakitarajiwa kutumia nafasi ambazo wanazitengeneza, na wachezaji wa kufanya hayo yote wapo kikosini hapo.

Licha ya kutoshiriki Kombe la Dunia kwa kutokufuzu, bado haiwapi wapinzani wao nafasi ya kuwabeza kwani bado wanajiamini na kujua kuwa wana nafasi ya kuondoka na ushindi leo.

Kwa upande wa Ubelgiji ni timu ambayo ina uwezo mkubwa wa kujilinda na kufanya mashambulizi kwani wachezaji wenye kasi kwenda mbele kushambulia wapo wakiongozwa na Doku, Trossard, Ketelaere, lakini pia wana wachezaji wazuri kwenye eneo la kiungo wakiongozwa na De Bruyne.

Timu hizi mara ya mwisho kukutana ilikuwa ni msimu wa 2024 ambapo Italia waliondoka na pointi 4 huku nafasi ya ushindi kule Meridianbet leo akipewa mwenyeji. Lakini pia Odds kubwa zipo kwenye mechi hii.

Halikadhalika miichuano ya AFCON itaendelea ambapo Morocco itamenyana dhidi ya  Gabon katika mchezo wa kwanza wa Kundi A kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat.

Morocco inaingia ikiwa na faida ya kucheza nyumbani na ikiwa imefanya vizuri kwenye Kombe la Dunia 2026, ambako ilifika robo fainali.

Simba wa Atlas ndiyo timu inayobeba presha kubwa zaidi kwenye mchezo huu. Ikiwa nyumbani, matarajio ni kuona wakitawala mpira, wakicheza kwa kasi kupitia pembeni na kuilazimisha Gabon kujilinda kwa muda mrefu.

Lakini pia The Atlas ina kumbukumbu nzuri sana dhidi ya Gabon katika mechi zao za hivi karibuni. Iliifunga Gabon 4-1 nyumbani mwaka 2024 kabla ya kushinda tena 5-1 ugenini.

Vilevile kwa upande wa Gabon wao ni timu ambayo haiwezi kudharauliwa. Ina wachezaji wenye uwezo wa kubadilisha mchezo kupitia mashambulizi ya haraka, lakini tatizo kubwa litakuwa namna ya kuhimili Morocco ikiwa wenyeji wataanza kulisukuma eneo lao.

Meridianbet wameipa mechi hii machaguo zaidi ya 1000, hivyo unaweza ukasuka jamvi lako la ushindi na ukaibuka bingwa siku ya leo.

Kenya Yakabiliwa na Uhaba Mkubwa wa Chakula

Global Publishers
September 25, 2026
0 views
0 Comments

Hali ya upatikanaji wa chakula nchini Kenya imeendelea kuwa ya changamoto, huku takribani watu milioni 2.7 wanaoishi katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame na mvua chache wakikabiliwa na uhaba wa chakula na njaa kali.

Kati ya idadi hiyo, takribani watu 348,000 wanatajwa kuwa katika hali ya dharura, hali inayohitaji utoaji wa msaada wa haraka wa chakula pamoja na hatua madhubuti za kukabiliana na hali hiyo kabla haijazua madhara makubwa zaidi.

Takwimu kutoka katika tathmini ya usalama wa chakula ya IPC zinaonesha kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na hali hiyo imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 55, ikilinganishwa na makadirio yaliyotolewa awali.

Hali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabianchi, mvua zisizotabirika na athari za ukame wa muda mrefu, mambo ambayo yameendelea kuathiri uzalishaji na upatikanaji wa chakula katika jamii mbalimbali nchini humo.

Wakati huohuo, matarajio ya mvua za vuli katika baadhi ya maeneo yameongeza hofu kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mafuriko, huku mamlaka za kaunti zikichukua hatua za maandalizi ili kukabiliana na majanga yanayoweza kujitokeza.

Aidha, zaidi ya watoto 883,000, pamoja na maelfu ya wanawake wajawazito na wanaonyonyesha, wanatajwa kuwa miongoni mwa makundi yaliyo katika hatari zaidi na yanayohitaji msaada wa haraka.

Hali hiyo inasisitiza umuhimu wa kuimarisha hatua za kukabiliana na uhaba wa chakula, kusaidia kaya zilizo katika mazingira hatarishi na kujiandaa mapema dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi na majanga ya asili.

Na Florah Anderson



 

 

Elimu ya mbegu yatolewa Shinyanga – HabariLeo

SHINYANGA: WAKULIMA mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mbegu na pembejeo za kilimo kuelekea msimu wa kilimo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kampeni ya Mali Shambani kupitia Programu ya Maendeleo ya Kilimo na Uvuvi (AFDP).

Mafunzo hayo yametolewa Septemba 23, 2026, wakati wa Maonesho ya Pembejeo Bora na Mbegu Bora za Mazao (Innovation Seed Fair), yaliyoshirikisha wataalamu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Taasisi ya Kuthibiti Mbegu Bora Tanzania (TOSCI) na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA).

Maonesho hayo pia yameshirikisha wawakilishi wa kampuni mbalimbali zinazozalisha mbegu pamoja na wauzaji wa pembejeo za kilimo, kwa lengo la kuwawezesha wakulima kupata elimu na taarifa sahihi kuhusu pembejeo na mbegu wanazoweza kutumia katika uzalishaji.

Akizungumzia zoezi hilo, mtaalamu kutoka Wizara ya Kilimo, Ernest Kibulei, amesema mafunzo hayo yanatolewa Shinyanga Vijijini na Manispaa ya Kahama, kabla ya kuendelea mkoani Tabora katika Wilaya za Igunga na Nzega.

Amesema wataalamu hao wanatoa elimu kuhusu matumizi ya mbegu bora, huduma ya upimaji wa afya ya udongo na kanuni bora za kilimo, pamoja na namna ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kibulei amesema elimu hiyo pia inahusisha maandalizi ya wakulima kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo mvua za El Niño, ili kuwawezesha kufanya maandalizi sahihi kabla na wakati wa msimu wa kilimo.

Lissu: Uhaini wa Maneno Haujawahi Kuwa Sehemu ya Sheria za Tanzania

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameieleza Mahakama Kuu kuwa, kwa mujibu wa historia ya sheria za Tanzania, hakuna kosa la “uhaini wa maneno”, akidai kuwa upande wa mashtaka unajaribu kuingiza tafsiri hiyo katika sheria za Tanzania.

Lissu ametoa kauli hiyo leo, Septemba 25, 2026, wakati akiendelea kutoa hoja zake za mwisho (Final Submission) katika kesi ya uhaini inayomkabili mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru.

Amesema:

“Uhaini wa maneno haujawahi kuwa sehemu ya sheria zetu milele.”

Akifafanua historia ya sheria ya uhaini nchini, Lissu amesema sheria hiyo ilianzia katika kipindi cha utawala wa Waingereza wakati wa ukoloni, akidai kuwa hata katika kipindi hicho maneno pekee hayakutosha kuunda kosa la uhaini, bali kulihitajika kitendo cha wazi (overt act).

Kwa mujibu wa hoja zake, Lissu amesema sheria ya uhaini ilianzishwa katika miaka ya 1920 na kutumika katika maeneo yaliyokuwa chini ya utawala wa Waingereza, ikiwamo Tanganyika, Kenya na Uganda. Hata hivyo, amedai kuwa Uganda pekee ndiyo iliyokuwa na kipengele kinachohusu uhaini unaotokana na maneno, huku Tanzania na Kenya zikiwa hazina kifungu hicho kwa namna hiyo.

Lissu pia amerejea maamuzi ya kesi za awali, akitaja kesi ya Khatib Ghandi and Others v. Republic, akisema Jaji Mkuu wa zamani Francis Nyalali alieleza kuwa maneno matupu hayawezi, kwa ujumla, kuwa overt act au deed katika shtaka la uhaini.

Kwa hoja hiyo, Lissu amepinga tafsiri ya upande wa mashtaka kwamba maneno aliyodaiwa kuyasema yanaweza kuchukuliwa kama “tendo” linalokidhi matakwa ya sheria ya uhaini. Hoja hiyo pia imekuwa sehemu ya majumuisho yake ya mwisho katika siku za hivi karibuni.

Amedai kuwa upande wa mashtaka, kwa kuhusisha maneno yake na kosa la uhaini, unajaribu kuingiza katika sheria za Tanzania jambo ambalo, kwa maelezo yake, Waingereza walioanzisha sheria hiyo waliliacha katika kipindi cha nyuma.

Kesi hiyo bado iko katika hatua ya mawasilisho ya mwisho, na Mahakama haijatoa uamuzi kuhusu hoja hizo.

Mwanamume Ampiga Risasi Ex-Wake Baada Ya Kudai Msaada wa Malezi

Mwanamume mwenye umri wa miaka 63 nchini Marekani, Darrell Long, amepatikana na hatia ya jaribio la kumuua kwa makusudi mke wake wa zamani, Dawn, baada ya kumpiga risasi mara tano katika nyumba aliyokuwa akiishi pamoja na mtoto wao wa kiume.

Long, mkazi wa Pennsylvania, alipatikana na hatia Jumanne, Septemba 22, 2026, kwa makosa mbalimbali likiwemo jaribio la mauaji ya daraja la kwanza, uvamizi wa nyumba, shambulio la kusababisha majeraha makubwa, shambulio kwa kutumia silaha na unyanyasaji.

Tukio hilo lilitokea Machi 25, 2025, baada ya Long kuvamia nyumba ya Dawn wakati akiwa amelala kwenye sofa sebuleni. Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka wa Kaunti ya Lebanon, Pier Hess Graf, Long alimpiga Dawn usoni kwa kutumia bunduki kabla ya kumpiga risasi mara kadhaa.

Dawn alijaribu kujitetea na katika purukushani hiyo alifanikiwa kumng’ang’ania Long na kumwangusha chini. Hata hivyo, Long aliendelea kutumia bunduki hiyo na kumpiga risasi nyingine, ikiwemo moja iliyompiga mkononi na kusababisha jeraha kubwa kwenye kidole chake cha shahada.

Bunduki hiyo ilikwama wakati wa mapambano, lakini baada ya Long kujaribu kuirekebisha, alifanikiwa kuendelea kumpiga Dawn risasi. Mwathiriwa, akiwa amejeruhiwa katika sehemu kadhaa za mwili, alijikokota hadi chumbani na kujifungia.

Dawn alifanikiwa kupiga simu ya dharura 911 kwa kutumia Apple Watch yake baada ya kuvunja sehemu ya kifaa hicho ili kuanzisha huduma ya dharura.

Long alikimbia kutoka eneo la tukio kabla ya polisi kumkamata. Mwendesha mashtaka amesema alifunga mlango kabla ya kuondoka, jambo ambalo lingeweza kuchelewesha msaada kwa Dawn.

Kwa mujibu wa mwendesha mashtaka, shambulio hilo lilihusishwa na mzozo kuhusu msaada wa malezi ya mtoto. Dawn aliwasilisha madai ya msaada wa malezi baada ya kuanza mchakato wa talaka mwaka 2023.

Pia imeelezwa kuwa katika mwezi mmoja kabla ya tukio hilo, Long alimtumia mtoto wao jumbe 23 zenye maneno makali kuhusu Dawn, akitaka mtoto huyo amfikishie ujumbe mama yake ambaye alikuwa amemzuia Long kuwasiliana naye moja kwa moja.

Mmoja wa jumbe hizo, uliotumwa siku 17 kabla ya shambulio, ulidaiwa kuwa na tishio kwamba endapo Dawn angebadilika mwenendo, mtoto wao angeishia kuwapoteza wazazi wote wawili.

Mwendesha mashtaka Hess Graf amesema Long bado anaendelea kumlaumu Dawn kwa shambulio hilo, huku akidai kuwa hakujutia alichokifanya.

Wizara Yabadilisha Ratiba ya Mitihani ya Taifa 2026 Kwa Hofu ya El Nino – Video

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya marekebisho ya ratiba ya upimaji na mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026, kwa lengo la kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na uwezekano wa mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Septemba 25, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya Serikali kufuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa na kutathmini athari zinazoweza kujitokeza katika uendeshaji wa upimaji na mitihani ya Taifa.

Amesema kwa mujibu wa utabiri rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, kuna uwezekano wa kutokea kwa El Nino yenye nguvu, huku mvua zikitarajiwa kuanza katika baadhi ya maeneo mwezi Oktoba 2026 na kuwa nyingi zaidi mwezi Novemba 2026, hali ambayo inaweza kuathiri usafiri na kufikika kwa baadhi ya vituo vya mitihani.

Ameeleza kuwa kwa kuzingatia jiografia ya nchi na uwezekano wa baadhi ya maeneo kukumbwa na mafuriko, changamoto za usafiri na athari nyingine zinazoweza kusababishwa na hali ya hewa, Wizara kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania imefanya marekebisho ya ratiba ya upimaji na mitihani ya Taifa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyorekebishwa, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili Ngazi ya Shule utafanyika Oktoba 7 hadi 8, 2026, wakati Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika Oktoba 5 hadi 6, 2026.

Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili utafanyika Oktoba 12 hadi 23, 2026, huku Mitihani ya Kidato cha Nne ikifanyika kuanzia Oktoba 19 hadi Novemba 6, 2026.

Amesema marekebisho hayo yanalenga kuhakikisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi, maafisa na wadau wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani, pamoja na kulinda mitihani, vifaa na nyaraka muhimu.

Wizara imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa hali ya hewa na kuchukua hatua stahiki kwa kushirikiana na mamlaka na taasisi husika, ili kuhakikisha upimaji na mitihani ya Taifa inafanyika kwa utaratibu unaofaa, huku usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na wadau wengine ukipewa kipaumbele.

Dkt. Mwigulu Atembelea Vatican City, Akutana na Mkuu wa Itifaki

Global Publishers
September 25, 2026
12 views
0 Comments

ROME, ITALIA — Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametembelea Vatican City jijini Roma, Italia, katika ziara ya kando ya ushiriki wake kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo.

Mkutano huo ulifanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), jijini Roma.

Akiwa Vatican City Alhamisi, Septemba 24, Dkt. Mwigulu alikutana na Mkuu wa Itifaki wa Sekretarieti ya Nchi ya Vatican, Monsinyori Javier Domingo Fernández González, katika ziara iliyompa fursa ya kutembelea pia maeneo mbalimbali ya Vatican.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alitembelea maeneo ya kihistoria na kiutamaduni ya Vatican City, ambayo yana nafasi muhimu katika historia ya Kanisa Katoliki na urithi wa dunia.

Ziara hiyo imefanyika wakati Dkt. Mwigulu akiwa Roma kwa ajili ya kushiriki katika mjadala wa kimataifa unaohusu Afya Moja, chakula na mifumo ya kilimo, masuala yanayohusisha afya ya binadamu, wanyama na mazingira.

Vatican City ni makao makuu ya Kanisa Katoliki na ni eneo lenye taasisi mbalimbali za kihistoria na kidini.

Wizara Yabadilisha Ratiba ya Mitihani ya Taifa 2026 Kwa Hofu ya El Nino

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya marekebisho ya ratiba ya upimaji na mitihani ya Taifa kwa mwaka 2026, kwa lengo la kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na uwezekano wa mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa katika baadhi ya maeneo nchini.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Septemba 25, 2026, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya Serikali kufuatilia kwa karibu taarifa za hali ya hewa na kutathmini athari zinazoweza kujitokeza katika uendeshaji wa upimaji na mitihani ya Taifa.

Amesema kwa mujibu wa utabiri rasmi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, kuna uwezekano wa kutokea kwa El Nino yenye nguvu, huku mvua zikitarajiwa kuanza katika baadhi ya maeneo mwezi Oktoba 2026 na kuwa nyingi zaidi mwezi Novemba 2026, hali ambayo inaweza kuathiri usafiri na kufikika kwa baadhi ya vituo vya mitihani.

Ameeleza kuwa kwa kuzingatia jiografia ya nchi na uwezekano wa baadhi ya maeneo kukumbwa na mafuriko, changamoto za usafiri na athari nyingine zinazoweza kusababishwa na hali ya hewa, Wizara kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Tanzania imefanya marekebisho ya ratiba ya upimaji na mitihani ya Taifa.

Kwa mujibu wa ratiba iliyorekebishwa, Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Pili Ngazi ya Shule utafanyika Oktoba 7 hadi 8, 2026, wakati Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne utafanyika Oktoba 5 hadi 6, 2026.

Aidha, Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili utafanyika Oktoba 12 hadi 23, 2026, huku Mitihani ya Kidato cha Nne ikifanyika kuanzia Oktoba 19 hadi Novemba 6, 2026.

Amesema marekebisho hayo yanalenga kuhakikisha usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi, maafisa na wadau wengine wanaohusika na uendeshaji wa mitihani, pamoja na kulinda mitihani, vifaa na nyaraka muhimu.

Wizara imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa hali ya hewa na kuchukua hatua stahiki kwa kushirikiana na mamlaka na taasisi husika, ili kuhakikisha upimaji na mitihani ya Taifa inafanyika kwa utaratibu unaofaa, huku usalama wa wanafunzi, walimu, wasimamizi na wadau wengine ukipewa kipaumbele.