Fursa Mpya ya Ajira NEEC, Mwisho wa Maombi Oktoba 1, 2026

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza nafasi moja ya Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC) kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika. Tangazo hilo limetolewa Septemba 18, 2026, kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

NEEC limeanzishwa chini ya Sheria ya Uwezeshaji Kiuchumi Na. 16 ya mwaka 2004 na lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Majukumu yake ni pamoja na kusimamia, kuratibu, kuwezesha na kufuatilia shughuli za uwezeshaji kiuchumi nchini.

Sifa za mwombaji

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uzamili katika mojawapo ya fani zifuatazo:

  • Utawala wa Umma
  • Ujasiriamali
  • Fedha
  • Uhasibu
  • Utawala wa Biashara
  • Biashara, akiwa amebobea katika Ujasiriamali, Masoko au Fedha
  • Uchumi
  • Uchumi wa Kilimo
  • Au sifa zinazolingana kutoka taasisi inayotambuliwa.

Shahada ya Uzamili inapaswa kuhusiana na Shahada ya Kwanza ya mwombaji.

Mwombaji anatakiwa pia kuwa na uzoefu wa kazi wa angalau miaka 12 katika maeneo yanayohusiana, ambapo angalau miaka mitatu iwe katika nafasi ya kiutawala. Uelewa wa masuala ya uwezeshaji kiuchumi umetajwa kuwa ni sifa ya ziada.

Majukumu ya Mtendaji Mkuu

Mtendaji Mkuu atawajibika kusimamia shughuli za kiutawala za Baraza na kuwa msemaji wake. Pia atasimamia utekelezaji wa majukumu ya Baraza, maandalizi ya mipango ya kimkakati na bajeti, taarifa za fedha na maendeleo, pamoja na utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Baraza.

Majukumu mengine ni kusimamia utekelezaji na tathmini ya mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu, kuendesha shughuli za kila siku za Sekretarieti, kuandaa mikakati ya kuongeza ufanisi, kusimamia uundaji na utekelezaji wa sera pamoja na kuongoza juhudi za kutafuta rasilimali za kifedha kwa ajili ya miradi ya Baraza.

Nafasi hiyo ni ya ajira ya kudumu na yenye mafao ya kustaafu, huku mshahara ukiwa kwa mujibu wa kiwango kilichoidhinishwa cha NEECS 13.

Waombaji wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania na kwa ujumla wasizidi umri wa miaka 45, isipokuwa watumishi wa umma. Pia wanapaswa kuambatanisha CV, nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu na taaluma, cheti cha kuzaliwa pamoja na picha ya pasipoti.

Mwisho wa kutuma maombi ni Oktoba 1, 2026. Maombi yanapaswa kutumwa kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Pelican Payday Yachangamsha Meridianbet, Safari Mpya Ya Mizunguko Yaanza

Global Publishers
September 26, 2026
0 views
0 Comments

Burudani mpya imefika na safari ya kuelekea kwenye ulimwengu wa mizunguko ya kasino imeanza rasmi. Pelican Payday kutoka Pragmatic Play sasa inapatikana ndani ya Meridianbet kasino, ikiwa tayari kuwapa wapenzi wa kasino uzoefu mpya wa kusisimua. Huu si mchezo wa kupita tu, bali ni safari inayokualika kuzungusha reels, kufuatilia kinachotokea na kufurahia kila hatua kabla mchezo haujachukua safari yake rasmi.

Fikiria ukiwa tayari kuanza safari, reels zikianza kuzunguka huku macho yako yakifuatilia kila kinachotokea. Hiyo ndiyo ladha inayokuja na Pelican Payday, mchezo uliobuniwa kuongeza burudani na msisimko kwa kila mzunguko. Kila mzunguko unafungua ukurasa mwingine wa safari, huku matarajio ya kuona matokeo yakifanya mchezo kuwa wa kuvutia zaidi.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kupitia Meridianbet kasino, wachezaji sasa wana nafasi ya kuingia kwenye mchezo huu mpya kutoka Pragmatic Play na kuonja burudani yake. Ujio wa Pelican Payday unaongeza chaguo jingine kwa wale wanaopenda michezo ya kasino yenye mandhari na uzoefu tofauti. Ni muda wa kuacha safari za kawaida na kujaribu upepo mpya unaokuja na mchezo huu.

Kila mzunguko ni sehemu ya hadithi, na kila hatua inaweza kuongeza msisimko wa safari. Unapozungusha reels, unachofanya ni kuingia kwenye burudani na kufuatilia kile ambacho mchezo umeandaa. Kwa anayependa kufurahia kasino kwa mtindo mpya, Pelican Payday inaweza kuwa kitu cha kuangalia.

Sasa pelican ameshatua Meridianbet. Ingia Meridianbet kasino, tafuta Pelican Payday kutoka Pragmatic Play na anza safari yako ya kucheza. Burudani imeanza, reels ziko tayari na safari ya kutafuta ushindi mkubwa inakungoja.

WANAWAKE WA KIISLAMU TUMIENI MITANDAO KUENEZA ELIMU, KUJENGA UCHUMI-ASIA ABDALLAH

 Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media

Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutoka Mkoa wa Dodoma, Asia Abdallah, amewataka wanawake wa Kiislamu kutumia elimu ya dini waliyonayo kuelimisha jamii kupitia mitandao ya kijamii, huku wakizingatia stara na maadili ya Kiislamu.

Asia Abdallah ametoa rai hiyo katika hafla ya Maulid ya wanawake iliyofanyika katika Msikiti wa Abdul Aziz, Chang’ombe mkoani Dodoma, ambapo amesema mitandao ya kijamii ni sehemu muhimu ya maisha ya sasa na inaweza kutumika kueneza elimu ya dini, kujenga jamii na pia kuwa chanzo cha kipato.

Amesema wanawake wa Kiislamu wanapaswa kuhakikisha wanatumia mitandao kwa mambo yenye manufaa badala ya kuchapisha maudhui yasiyokuwa na ujumbe wa kujenga, akisisitiza kuwa mwanamke anaweza kuwa mtumiaji mzuri wa mitandao bila kuacha misingi ya stara.

“Dunia imehamia mitandaoni. Sidhani kama kuna mtu anaharamisha mitandao, lakini unaweza ukaitumia kwa njia nzuri ikakusaidia wewe, ukajiongezea kipato na pia ukatoa elimu kwa umma,” amesema.

Asia amewataka wanawake wanaosoma Qur’an na wenye elimu ya dini kutumia majukwaa kama Instagram, Facebook, TikTok na mitandao mingine kusambaza elimu hiyo ili kuwafikia watu wengi zaidi.

Amesema wakati umefika kwa wanawake wa Kiislamu kushindana katika kusoma na kuifahamu Qur’an Tukufu na kutumia elimu hiyo kuwafikia watu wengi, badala ya kushindana katika mambo yasiyokuwa na manufaa kwenye mitandao.

“Wapo wasomaji wengi wa Qur’an humu ndani, lakini ni wangapi wanafikisha elimu hiyo kwa ukubwa wake? Mitandao inaweza kukufikisha kwa watu elfu 10, elfu 30, elfu 80 au hata zaidi, na huwezi kujua ni nani atakayesikia neno lako na likamsaidia,” amesema.

Aidha, amewataka wanawake wa Kiislamu kutumia mitandao kujenga uchumi wao, akisema kuwa matumizi sahihi ya majukwaa hayo yanaweza kuwapatia fursa za kipato kupitia utengenezaji wa maudhui pamoja na fursa nyingine za kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Asia Abdallah amewahamasisha wanawake hao kuchangamkia mikopo inayotolewa na Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kuwawezesha kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi.

Amesema mwanamke anapaswa kuwa na elimu ya dini sambamba na uelewa wa maisha na uchumi, ili aweze kujitegemea na kuimarisha familia na jamii kwa ujumla.

“Mwanamke imara utakuwa imara zaidi kama utakuwa unaijua dini, ukajua na maisha yanavyoenda, lakini ukawa umetengeneza na uchumi,” amesema.

Katika hafla hiyo, Asia Abdallah  pia alishiriki katika harambee ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanawake, ambapo aliahidi kuchangia Shilingi milioni moja.

WAONYWA KUWAPELEKA MIKOANI DARASA LA SABA 2026 KABLA YA MATOKEO ‎

 

‎

‎Wazazi, walezi na jamii wametakiwa kuwa na tahadhari ya kuwapeleka Jijini Dar es Salaam na mikoa mingine mikubwa wahitimu wa Darasa la Saba wa mwaka huu, kabla ya kutangazwa matokeo ya kitaifa, kwa kuwa hatua hiyo inaweza kusababisha baadhi yao kushindwa kujiunga Kidato cha Kwanza Januari 2027. 

‎Wito huo umetolewa na wananchi wa Kijiji cha Samamba, Kata ya Kituntu, Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, wakati wa mahafali ya nne ya Shule ya Msingi Samamba, iliyoshika nafasi ya kwanza kimkoa kwa miaka mitatu mfululizo.

‎Aidha Wananchi hao wameitaka jamii kutambua na kuunga mkono juhudi za walimu wanapofanya kazi kwenye mazingira magumu, yenye changamoto, ikiwemo kuwapa pongezi na motisha wanapofanya vizuri, ili kuongeza bidii na ari zaidi ya kuendelea kuboresha ufaulu wa wanafunzi.

‎Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Samamba, Adinani Mkuki, ameeleza mambo mbalimbali yanayochangia mafanikio ya shule hiyo katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo, kwa kutaja ushirikiano baina ya wazazi, walimu na serikali kama silaha kuu ya mafanikio.

‎Diwani wa Kata ya Kituntu, Ali Ramadhani, ametoa tahadhari kuhusu watu wanaowarubuni wanafunzi, hususan wasichana, kwa ahadi za kuwapeleka mijini au mikoani kwenda kufanya kazi za ndani kabla ya matokeo. Naye mwakilishi wa benki ya NMB Tawi la Singida Mjini,Chimlumbe Wenda,ametaka wazazi na walezi kushirikiana kuwalinda wahitimu hao, dhidi ya vishawishi hivyo.

‎Kwa upande wao, wahitimu wa Darasa la Saba akiwemo Amosi Masanja ameeleza kuwa pamoja na kufanya vizuri kitaaluma, shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madawati na vyumba vya madarasa.

‎Shule ya Msingi Samamba ilianzishwa mwaka 2014 kwa nguvu za wazazi na sasa ina wanafunzi 666, wakiwemo wasichana 334, pamoja na walimu 11, lakini kutokana na upungufu wa walimu, wazazi wamekuwa wakigharamia posho za walimu watatu wa kujitolea ili wanafunzi waendelee kupata huduma bora ya elimu bila kukwama.

‎

MAGEREZA YAITIKISA NGOME YA JWTZ, YAIBUKA NA USHINDI WA SETI 3–2

Na Ssgt Mawazo Mtondo – MWANZA

Timu ya mpira wa wavu wanaume ya Jeshi la Magereza 25 Septemba, 2026 imepata ushindi wa kusisimua wa seti 3–2 dhidi ya Timu ya Ngome ya JWTZ, katika mchezo mkali na wa kuvutia wa Mashindano ya Bammata 2026 yanayoendelea Jijini Mwanza.

Mchezo huo uliokuwa na mashambulizi makali, ulinzi imara na mabadiliko ya kasi ya mchezo, uliifanya kila timu kupigania kila pointi. Magereza ilionyesha uthubutu na umakini hadi hatua za mwisho na hatimaye kuibuka na ushindi huo wa muhimu, uliowapa wachezaji morali na hamasa zaidi kuelekea michezo inayofuata.

Kocha Mkuu wa timu hiyo, Ssgt Mussa Shabani, amesema ushindi huo umetokana na umoja, nidhamu, kujituma na kupambana kwa wachezaji, huku akisisitiza kuwa timu itaendelea kuongeza nguvu na kuboresha maeneo yaliyobainika katika mchezo huo.

Naye Kapteni wa timu hiyo, Wdr Martin Anthony, amesema ushindi huo umeongeza morali ndani ya kikosi na kwamba wachezaji wataendelea kupambana kwa moyo, nguvu na mshikamano, wakilenga kufanya vizuri katika michezo iliyosalia ya mashindano hayo.

 

INSP CATHERINE LANGE AENDELEA KUNG’ARA RIADHA BAMMATA 2026

Na Ssgt Mawazo Mtondo – MWANZA

Mashindano ya Riadha ya Bammata 2026 yameendelea, Septemba 25, 2026, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kwa mbio za mita 5,000, sawa na kuzunguka uwanja mara 12.

Mkaguzi wa Magereza INSP Catherine Lange ameendelea kuonyesha ushindani baada ya kushika nafasi ya tatu, akirudia mafanikio aliyoyapata jana katika mbio za mita 10,000 za wanawake.

 

Mikopo ya asilimia kumi yazidi kuinua wananchi Bukoba – HabariLeo

KAGERA: KATIBU Tawala wa Wilaya ya Bukoba, Proscovia Mwambi, amesema Manispaa ya Bukoba imetoa mikopo ya zaidi ya Sh milioni 800 kwa vikundi 123 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na serikali bila riba.

Amesema vikundi vilivyonufaika ni 68 vya wanawake, 37 vya vijana na tisa vya watu wenye ulemavu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wananchi kiuchumi na kukuza shughuli zao za uzalishaji mali.

Akizindua Mwezi wa Maendeleo ya Jamii, Mwambi amesema idadi ya wanufaika inaweza kuongezeka endapo vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu vitashiriki kikamilifu katika kutambua na kutumia fursa zinazotolewa na serikali.

Amesema mikopo hiyo hutolewa bila riba kwa vikundi vinavyokidhi vigezo vilivyowekwa, bila ubaguzi, huku vikundi vinavyorejesha mikopo yao vizuri vikiendelea kupewa fursa zaidi hadi vitakapojitegemea kiuchumi.

Katika hatua nyingine, amesema Manispaa ya Bukoba imesajili vikundi 164 katika mfumo wa manunuzi ya umma wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), ili viweze kunufaika na fursa ya asilimia 30 ya manunuzi katika taasisi za serikali kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023.

Amesema kupitia mfumo huo, vikundi viwili tayari vimepata zabuni zenye thamani ya Sh milioni 491, huku vingine vikiendelea kupata fursa hizo kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa.

Aidha, amesema manispaa hiyo ina wafanyabiashara wadogo 805, ambapo 206 tayari wamepata vitambulisho, huku wafanyabiashara wengine 66 wakinufaika na mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya Sh milioni 105.

Kwa niaba ya Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Bukoba, Faraja Chaula, amesema maafisa maendeleo ya jamii watatumia Mwezi wa Maendeleo ya Jamii kufuatilia wanufaika wa mikopo ya asilimia 10, kukagua miradi wanayoitekeleza na kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya fedha za mikopo.

Amesema mwezi huo pia utatumika kutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo kuhusu fursa za mikopo ya masharti nafuu, umuhimu wa lishe bora, kuchangia chakula shuleni na masuala ya afya ya jamii.

Ameongeza kuwa shughuli nyingine ni kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia na kuimarisha mawasiliano kati ya serikali, wananchi na wadau wa maendeleo.

Kongamano la uzinduzi wa Mwezi wa Maendeleo ya Jamii lilihudhuriwa na mamia ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba, ambao walipata fursa ya kuelimishwa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na semina ya uwekezaji na matumizi sahihi ya fedha kupitia vikundi vyao.

Kaulimbiu ya Mwezi wa Maendeleo ya Jamii mwaka huu ni: “Familia Imara, Jamii na Taifa Imara Kuelekea Dira ya Maendeleo 2050.”

Wachimbaji Wadogo Geita Watakiwa Kuchukua Tahadhari Dhidi ya Mvua Kubwa

GEITA: Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amewataka wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita kuchukua tahadhari dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha nchini.

Sangu ametoa agizo hilo wakati akifungua mafunzo ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi kwa wachimbaji wadogo wa madini mkoani Geita, akisisitiza umuhimu wa wachimbaji kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ili waweze kuchukua hatua mapema.

Amesema tahadhari hiyo ni muhimu zaidi kwa kuwa shughuli nyingi za uchimbaji zinazofanywa na wachimbaji hao ni za chini ya ardhi, hivyo uwepo wa mvua kubwa unaweza kuongeza vihatarishi katika maeneo ya uchimbaji.

“Niwatake wachimbaji wote kuendelea kuchukua tahadhari ikiwemo kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa, ili kuchukua tahadhari mapema. Uchimbaji wetu ni wa underground, hivyo ni muhimu kujiridhisha kabla ya kuanza kufanya uchimbaji,” amesema Mhe. Sangu.

Ameongeza kuwa endapo kutatokea madhara yoyote katika maeneo ya uchimbaji, taarifa zinapaswa kutolewa mapema kwa OSHA na mamlaka nyingine zinazohusika ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Waziri Sangu pia amewataka wachimbaji kutumia elimu wanayopewa kuhusu usalama na afya mahali pa kazi, pamoja na kutumia ipasavyo vifaa kinga walivyokabidhiwa, huku akisisitiza umuhimu wa wachimbaji kukumbushana mara kwa mara kuhusu uzingatiaji wa taratibu za usalama.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), Bi. Khadija Mwenda, amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha makundi mbalimbali ya wafanyakazi, wakiwemo wachimbaji wadogo, yanapatiwa elimu kuhusu usalama na afya mahali pa kazi.

Amesema OSHA imekuwa ikiendesha mafunzo kama hayo katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na Wilaya za Bukombe mkoani Geita na Namungo mkoani Lindi.

Kwa mujibu wa Bi. Mwenda, wachimbaji wadogo wanakabiliwa na vihatarishi mbalimbali kutokana na aina ya shughuli wanazofanya, jambo lililosababisha OSHA kuamua kuwafikia moja kwa moja kwa kutoa elimu ya usalama na afya pamoja na kuwapatia vifaa vya kujikinga (PPE).

Mafunzo hayo yamewashirikisha wachimbaji kutoka Mbogwe na Geita, pamoja na wachimbaji kutoka Uganda, ambapo wamefundishwa namna ya kutambua na kudhibiti vihatarishi katika maeneo ya kazi pamoja na utoaji wa huduma ya kwanza.

Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa Uganda nchini Tanzania, mwakilishi wa Ubalozi huo, Brigedia Jenerali Julius Mbaine, amesema ushiriki wa wachimbaji kutoka Uganda umefungua fursa ya kubadilishana uzoefu na kutambua maeneo ambayo Tanzania na Uganda zinaweza kushirikiana katika sekta ya madini.

Amesema sekta ya madini inaweza kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili, hususan katika uwekezaji, biashara na mnyororo wa thamani wa madini.

“Sekta ya madini inatoa jukwaa muhimu la kuimarisha mahusiano. Ubalozi wa Uganda nchini Tanzania uko tayari kusaidia kuimarisha uhusiano wa kitaasisi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili, hususan katika kukuza uwekezaji, biashara na mnyororo wa thamani wa madini,” amesema Brigedia Jenerali Mbaine.

Ameongeza kuwa mazungumzo yaliyofanyika kati ya ujumbe wa Uganda na wadau wa madini mkoani Geita yamewapa fursa ya kuelewa zaidi sekta ya madini nchini Tanzania na kubaini maeneo yenye maslahi ya pamoja.

Kwa upande wake, Mbunge wa Geita Mjini, Chacha Mwita Wambura, amepongeza juhudi zinazofanywa na OSHA katika kusimamia usalama na afya mahali pa kazi nchini.

Amesema shughuli za uchimbaji madini zina vihatarishi mbalimbali, hivyo elimu na uzingatiaji wa taratibu za usalama ni muhimu katika kulinda maisha na afya za wachimbaji.

Mafunzo hayo yameandaliwa na OSHA kwa kushirikiana na Mkoa wa Geita ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya 9 ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika mkoani humo.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba Awasili Qatar kwa Ziara ya Kikazi

Global Publishers
September 26, 2026
0 views
0 Comments

DOHA, QATAR: Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili nchini Qatar leo, Septemba 25, 2026, kwa ziara ya kikazi.

Dkt. Mwigulu amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad, jijini Doha, ambapo amepokelewa na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Balozi Ibrahim bin Yousif Fakhroo.

Pamoja na viongozi hao, Waziri Mkuu amepokelewa pia na Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Habibu Awesi Mohamed.

Ziara hiyo ya kikazi inatarajiwa kuendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar katika maeneo mbalimbali yenye maslahi kwa mataifa hayo mawili.

WAKALA WA VIPIMO (WMA) WASHIRIKI MAONYESHO YA TEKNOLOJIA YA MADINI GEITA

Na Mwandishi wetu, Geita 

WAKALA wa vipimo (WMA) wameshiriki maonyesho ya kitaifa ya tisa ya teknolojia ya madini yanayofanyika mjini Geita kwa kuitaka jamii kutembelea banda lao ili kupatiwa elimu juu ya vipimo.

Meneja wa wakala wa vipimo Mwanza Karim Zuberi akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini Manispaa ya Geita amesema WMA inawakaribisha wadau wote.

Zuberi wadau wote wa maendeleo na wananchi kwa ujumla wanakaribishwa kutembelea banda lao ili kupata elimu juu ya wakala wa vipimo na wanaruhusiwa kuuliza maswali.

Amesema kwenye maonyesho hayo ya teknolojia ya madini wakala wa vipimo ina hakiki mizani zinazotumika kununua madini na vito vya thamani na migodini.

“Katika masoko ya kuuzia madini na kwa wauzaji wa madini (sonara) pia tunatoa ushauri wa kitaalamu kwa Wizara inayohusika na madini mara kwa mara panapohitajika,” amesema.

Amesema wakala wa madini inafanya uhakiki wa vipimo katika maeneo mbalimbali ya biashara kama maduka ya kuuzia nyama, viwandani, mizani inayotumia kuuzia bidhaa masokoni ikiwemo bidhaa zinazofungashwa.

“Wakala wa vipimo hufanya hivyo ili kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa kwa usahihi kulingana na thamani ya fedha inayotolewa na siyo vinginevyo,” amesema.

Amesema kwamba kwenye sekta ya maji wakala wa vipimo inafanya uhakiki wa mizani zote zinazotumika wakati wa ununuzi wa mazao mbalimbali kama vile pamba, korosho na ufuta.

Ameeleza kuwa uhakiki huo wa mizani ya vyama vya msingi vya ushirika na makampuni yanayonunua mazao hufanyika kwa msimu kuanza na  usimamizi mara baada ya msimu kuanza ili kujiridhisha kama inatumika kwa usahihi.

Hata hivyo amewakaribisha wakati wa Geita na wananchi wote wanaoshiriki kwenye maonyesho ya kitaifa ya teknolojia ya madini kupita katika banda lao la wakala wa vipimo ili kupata elimu zaidi juu ya vipimo.

MWISHO