Zanzibar: Wajumbe wa Kamati ya Pamoja CCM na ACT Wazalendo Watangazwa

Global Publishers
September 13, 2026
0 views
0 Comments

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Ofisi ya Baraza la Mapinduzi imetangaza majina ya Wajumbe wa Kamati ya Pamoja ya Majadiliano kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha ACT Wazalendo.

Hatua hiyo inafuatia makubaliano yaliyofikiwa na vyama hivyo viwili tarehe 9 Julai 2026, ambapo vilitia saini Tamko la Pamoja la Makubaliano kuhusu Ajenda za Kufanyiwa Kazi katika hafla iliyofanyika Ikulu, Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Septemba 13, 2026, Kamati hiyo imeundwa na wajumbe 10, ambao ni:

  1. Ndg. Abdi Mahmoud Abdi – Mjumbe na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati
  2. Ndg. Omar Ali Shehe – Mjumbe na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati
  3. Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed – Mjumbe
  4. Mhe. Najma Murtaza Giga – Mjumbe
  5. Mhe. Masoud Ali Mohamed – Mjumbe
  6. Mhe. Mgeni Hassan Juma – Mjumbe
  7. Ndg. Omar Said Shaaban – Mjumbe
  8. Ndg. Fatma Abdulhabib Fereji – Mjumbe
  9. Mhe. Said Ali Mbarouk – Mjumbe
  10. Ndg. Mohamed Nur Mohamed – Mjumbe

Aidha, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewateua Makatibu na Sekretarieti ya Kamati hiyo kama ifuatavyo:

Makatibu wa Kamati

  1. Ndg. Mwalim Ali Mwalim
  2. Ndg. Seif Khamis Mohamed

Sekretarieti ya Kamati

  1. Ndg. Hamid Saleh Mhina
  2. Ndg. Mohamed Yusuf Nuh
  3. Ndg. Ali Salim Khamis
  4. Ndg. Abdalla Mussa Hijja

Kamati hiyo inatarajiwa kuanza rasmi majukumu yake siku ya Jumatatu, tarehe 14 Septemba 2026, saa 5:00 asubuhi, Ikulu Zanzibar.

Vita vya Pointi Ulaya: Manchester Derby, PSG na Atletico Uwanjani

Global Publishers
September 13, 2026
0 views
0 Comments

Wikendi hii inatarajiwa kuwa na ratiba yenye michezo mbalimbali kutoka katika ligi kubwa za soka barani Ulaya, huku baadhi ya timu zikitafuta pointi muhimu katika hatua za mwanzo za msimu.

Nchini Ufaransa, Ligue 1 itaendelea kwa mechi kadhaa, ikiwemo mchezo kati ya Brest na Paris Saint-Germain (PSG). PSG itaingia katika mchezo huo ikitafuta matokeo mazuri baada ya kuanza msimu kwa matokeo ambayo hayajakidhi matarajio yao.

Takwimu za mikutano ya hivi karibuni zinaonesha kuwa PSG imekuwa na matokeo mazuri dhidi ya Brest. Hata hivyo, mchezo wa wikendi hii unatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na umuhimu wa pointi kwa timu zote mbili.

Nchini England, macho yatakuwa kwenye Premier League, ambako Manchester United na Manchester City zitakutana katika mchezo wa Manchester Derby. Mchezo huo ni miongoni mwa mechi zinazovuta hisia kubwa kutokana na historia ya ushindani kati ya timu hizo.

Manchester United imeanza msimu kwa kupata mchanganyiko wa matokeo katika michezo yake ya awali, wakati Manchester City imekuwa na mwanzo mzuri zaidi. Historia ya derby inaonesha kuwa michezo kati ya timu hizi mara nyingi imekuwa na ushindani mkubwa.

Hispania pia kutakuwa na mchezo kati ya Real Sociedad na Atletico Madrid katika La Liga. Atletico itaingia katika mchezo huo baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika michezo yake ya hivi karibuni, huku Real Sociedad ikiwa inatafuta kutumia uwanja wa nyumbani kupata pointi muhimu.

Mikutano ya nyuma kati ya timu hizo imekuwa na ushindani mkubwa, huku Atletico ikiwa imekuwa na matokeo mazuri katika baadhi ya michezo yao ya hivi karibuni.

Meridianbet, ambayo hutoa taarifa na huduma zinazohusiana na michezo, ni miongoni mwa majukwaa ambayo yanaweza kutumika kufuatilia taarifa za ratiba na michezo mbalimbali ya soka.

MKUMBO AMFARIJI MWENYEKITI WA KAMPUNI ZA UDALALI TANZANIA KWA KIFO CHA MKEWE

 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

MKURUGENZI wa Kampuni ya Udalali ya Kapondogoro Auction Mart, Methew Mkumbo, ameshiriki mazishi ya marehemu Stalla Mosha, aliyekuwa mke wa Mwenyekiti wa Kampuni za Udalali Tanzania Fidelis katundu ,na kutoa salamu za pole kwa familia kufuatia msiba huo.

Mazishi hayo yaliyofanyika jana yalihudhuriwa na ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wadau mbalimbali waliofika kuungana na familia katika kumpumzisha marehemu na kutoa faraja kwa wafiwa.

Akizungumza baada ya kushiriki mazishi hayo, Mkumbo alisema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Stalla Mosha na kwamba ameguswa na msiba uliompata mwenyekiti huyo pamoja na familia yake.

Mkumbo alisema kipindi cha msiba ni wakati mgumu kwa familia, hivyo uwepo wa ndugu, jamaa, marafiki na wadau ni muhimu katika kuwapa moyo na kuwafariji wafiwa.

“Napenda kutoa pole nyingi kwa Mwenyekiti wetu, familia, ndugu, jamaa na marafiki wote kwa kuondokewa na mpendwa wao Stalla Mosha Huu ni wakati mgumu sana kwa familia Tunawaombea Mungu awape nguvu, subira na faraja katika kipindi hiki cha majonzi,” alisema Mkumbo.

Aidha, Mkumbo alisema wadau wa sekta ya udalali wameguswa na msiba huo na wanaungana na mwenyekiti pamoja na familia yake katika kuomboleza.

Alisema kifo ni pigo kwa familia na jamii kwa ujumla, hivyo akawaomba wote walioguswa na msiba huo kuendelea kuwa karibu na familia na kuwapa moyo katika kipindi hiki.

Mkumbo alisema wataendelea kumuombea marehemu Stalla Mosha apumzike kwa amani na familia yake iendelee kupata nguvu na faraja.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.

Una Ujasiri? Gates Of Halloween Inakusubiri Meridianbet

Global Publishers
September 13, 2026
0 views
0 Comments

Halloween ni wakati wa mavazi ya kutisha, hadithi za kusisimua na burudani isiyo ya kawaida, lakini mwaka huu Meridianbet imeamua kuanza sherehe mapema kwa kuleta Gates of Halloween. Ukiwa umesalia takribani mwezi mmoja kabla ya Halloween 2026, mchezo huu unawapeleka wapenzi wa kasino mtandaoni kwenye ulimwengu wa giza uliojaa viumbe wa ajabu na raundi za bonasi.

Mchezo huu umeundwa kwa ajili ya kuongeza msisimko kila unapocheza. Unapopata alama nane au zaidi zinazofanana popote kwenye mchezo, ushindi unaweza kuanza na kisha cascading tumbles kuendelea kuleta alama mpya. Alama zilizoshinda huondoka na nafasi zake kujazwa tena, hivyo mfululizo wa ushindi unaweza kuendelea ndani ya raundi moja.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Na kama hilo halitoshi, Gates of Halloween imeficha nguvu kubwa ndani ya vizidishi vya dau lako ambapo dau unaloweka linaweza kuzidishwa hadi mara 1000. Wakati huo huo, Scatter nne au zaidi zinaweza kufungua raundi za bonasi na hapo ndipo safari inaweza kubadilika na kuwa tukio kubwa zaidi, huku wachezaji wakifuatilia kila raundi kwa matarajio.

Kwa wale wanaotaka kuchukua njia ya mkato kuelekea raundi za bonasi, Bonus Buy inaruhusu kuingia moja kwa moja kwenye kipengele hicho kwa x100 ya dau lako. Gates of Halloween ni mchezo wenye mandhari ya Halloween na mfumo wa kucheza unaotoa nafasi ya mfululizo wa matukio ndani ya raundi moja.

Sasa lango limefunguliwa, taa zimezimwa na safari imeanza. Je, wewe ni jasiri wa kutosha kuvuka Gates of Halloween? Meridianbet inakualika kuingia kwenye mchezo huu na kuanza burudani yako kuelekea Halloween 2026. Jisajili Meridianbet leo, cheza na uthubutu kukutana na kile kilichofichwa nyuma ya lango.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Watangaza Nafasi Nne za Kazi

Kampuni ya Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited imetangaza nafasi za kazi kwa Watanzania wenye sifa na uzoefu katika sekta ya bima, mauzo, masoko, biashara, uhasibu na nyanja zinazohusiana.

Nafasi zilizotangazwa ni Business Development Executive, Accountant pamoja na Insurance Sales Executives, huku waombaji wakitakiwa kutimiza vigezo vilivyowekwa kwa kila nafasi.

1. Business Development Executive

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Insurance and Risk Management, Sales and Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima, maendeleo ya biashara, mauzo au masoko.

2. Accountant

Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Kwanza katika Accounting au Finance, pamoja na uzoefu wa angalau miaka miwili katika sekta ya bima. Sifa ya CPA ni nyongeza.

3. Insurance Sales Executives

Waombaji wanatakiwa kuwa na Cheti katika Insurance and Risk Management, Sales, Marketing, Business Administration au fani nyingine inayohusiana.

Uzoefu katika sekta ya bima na kazi za mauzo ni nyongeza.

Jinsi ya Kutuma Maombi

Waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi yao pamoja na viambatisho muhimu vilivyothibitishwa kupitia barua pepe au kwa anuani ya ofisi ya kampuni kabla ya Septemba 30, 2026.

Wezesha Mzawa Insurance Broker Limited
P.O. Box 7534, Sinza Mori
Global Group House/Building, Opposite Wanyama Hotel
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: [email protected]

Mlipuko wa Ebola Wapanuka DRC, Hofu ya Kuvuka Mipaka Yatanda

Global Publishers
September 13, 2026
0 views
0 Comments

KINSHASA: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imethibitisha kuenea kwa mlipuko wa Ebola hadi eneo jingine nchini humo, hatua inayoongeza hofu ya kusambaa kwa ugonjwa huo katika maeneo zaidi.

Gavana wa jimbo la South Ubangi, kaskazini-magharibi mwa DRC, amesema vipimo vimethibitisha uwepo wa aina ya Ebola ya Bundibugyo, inayohusishwa na mlipuko unaoendelea nchini humo.

Kutokana na hali hiyo, Gavana amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuzingatia hatua za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo, ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara na kuepuka mikusanyiko ya watu.

Taarifa zinaeleza kuwa mlipuko huo tayari umesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000 nchini DRC.

Wasiwasi mkubwa kwa sasa ni uwezekano wa ugonjwa huo kuvuka mipaka na kuingia katika nchi jirani, kutokana na eneo la South Ubangi kuwa na mipaka na Jamhuri ya Afrika ya Kati pamoja na Jamhuri ya Congo.

Mamlaka zinaendelea kusisitiza umuhimu wa wananchi kuchukua tahadhari na kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya ili kupunguza hatari ya maambukizi zaidi.

Filamu 8 Zilizoingiza Pesa Nyingi Zaidi Duniani Katika Historia

Sekta ya filamu imeendelea kuvunja rekodi za mapato duniani, huku baadhi ya filamu chache zikifanikiwa kuvuka alama ya dola bilioni 2 katika mauzo ya tiketi.

Hadi Agosti 2026, filamu kutoka kwenye franchise maarufu kama Avatar, Avengers, Star Wars na Spider-Man zimeendelea kutawala orodha ya filamu zenye mapato makubwa zaidi ya wakati wote.

Hizi ndizo filamu 8 zilizoingiza fedha nyingi zaidi duniani bila kuzingatia mabadiliko ya thamani ya fedha kutokana na mfumuko wa bei:

1. Avatar (2009) – Dola Bilioni 2.9 (Sh Trilioni 7.6)
Filamu ya kisayansi ya mkurugenzi James Cameron ndiyo inayoongoza kwa mapato makubwa zaidi duniani, ikiwa imeingiza takribani dola 2.92 bilioni. Filamu hiyo iliwaweka pamoja waigizaji Zoe Saldaña na Sam Worthington.

2. Avengers: Endgame (2019) – Dola Bilioni 2.7 (Sh Trilioni 7.2)
Filamu hii ya Marvel Cinematic Universe ilivunja rekodi nyingi baada ya kuingiza zaidi ya dola 2.79 bilioni duniani na kuwa moja ya filamu zilizofanikiwa zaidi katika historia ya sinema.

3. Avatar: The Way of Water (2022) – Dola Bilioni 2.3 (Zaidi ya Sh Trilioni 6)
Muendelezo wa Avatar uliendelea kufanya vizuri sokoni na kukusanya zaidi ya dola 2.33 bilioni duniani.

4. Titanic (1997) – Dola Bilioni 2.26 (Zaidi ya Sh Trilioni 5.8)
Filamu ya mapenzi na historia iliyoongozwa na James Cameron, ikiwa na waigizaji Leonardo DiCaprio na Kate Winslet, imeingiza zaidi ya dola 2.26 bilioni tangu ilipotolewa.

5. Ne Zha 2 (2025) – Dola Bilioni 2.26 (Zaidi ya Sh Trilioni 5.8)
Filamu ya uhuishaji kutoka China ilivunja rekodi kadhaa za mauzo ya tiketi baada ya kuingiza zaidi ya dola 2.26 bilioni duniani.

6. Star Wars: The Force Awakens (2015) – Dola Bilioni 2.07 (Zaidi ya Sh Trilioni 5.3)
Filamu hii ya Star Wars iliyoongozwa na J.J. Abrams ilifanikiwa kuvuka dola bilioni 2 na kufikisha takribani dola 2.07 bilioni.

7. Avengers: Infinity War (2018) – Dola Bilioni 2.05 (Zaidi ya Sh Trilioni 5.3)
Kabla ya mafanikio ya Avengers: Endgame, filamu hii ilikuwa miongoni mwa filamu za mashujaa zilizovunja rekodi baada ya kuingiza zaidi ya dola 2.05 bilioni.

8. Spider-Man: No Way Home (2021) – Dola Bilioni 1.9 (Zaidi ya Sh Trilioni 4.9)
Filamu hii iliyomshirikisha Tom Holland kama Spider-Man iliingiza zaidi ya dola 1.92 bilioni, na kuwa filamu yenye mapato makubwa zaidi katika historia ya Spider-Man.

Kwa sasa, filamu mpya kama The Odyssey na Spider-Man: Brand New Day zinaendelea kufanya vizuri katika majumba ya sinema na zina nafasi ya kuingia kwenye orodha hii endapo zitaendelea kuvunja rekodi za mapato.

Fahamu Maajabu ya Vioo vya TV za Kisasa na Tofauti Zake OLED dhidi ya QLED

Enzi za televisheni zenye boksi kubwa na skrini nzito zimepita. Leo hii, teknolojia imebadilisha TV kuwa kifaa chenye uwezo mkubwa wa kuona sinema, michezo, muziki na dunia nzima sebuleni.

Lakini unapofika dukani, unaweza kukutana na maneno kama LED, QLED, Mini-LED, OLED na QD-OLED. Je, yana maana gani? Na ni teknolojia ipi inayokufaa?

Hebu tufahamu.

LED – Mwanzo wa TV nyembamba za kisasa

LED TV ni miongoni mwa teknolojia zinazopatikana kwa wingi. TV hizi hutumia paneli ya LCD inayowashwa kwa kutumia taa za LED.

Faida yake kubwa ni bei rafiki, matumizi mazuri ya umeme na upatikanaji wa ukubwa mbalimbali. Kwa mtu anayehitaji TV kwa kuangalia taarifa, YouTube, mpira na vipindi vya kawaida bila kutumia fedha nyingi, LED inaweza kuwa chaguo zuri.

Hata hivyo, inapokuja kwenye ubora wa rangi nyeusi na contrast, teknolojia za juu zaidi zinaweza kuonyesha picha bora.

QLED – Rangi zinazovutia macho

QLED imeleta hatua nyingine katika ubora wa picha. Teknolojia hii hutumia mfumo wa Quantum Dot kusaidia kuboresha rangi na mwangaza.

Matokeo yake ni picha zenye rangi ang’avu na mwangaza mkubwa, jambo linalofanya QLED kuvutia zaidi kwenye vyumba vyenye mwanga mwingi.

Kwa mtu anayetaka picha nzuri bila kufikia bei za baadhi ya TV za OLED, QLED inaweza kuwa chaguo lenye uwiano mzuri.

Mini-LED – Taa ndogo, udhibiti mkubwa

Hapa ndipo teknolojia inaanza kuwa ya kuvutia zaidi.

Mini-LED hutumia taa nyingi ndogo sana nyuma ya skrini, zinazowezesha TV kudhibiti mwangaza katika maeneo mbalimbali ya picha.

Kwa mfano, unapokuwa unaangalia anga lenye nyota, TV inaweza kufanya eneo lenye nyota liwe ang’avu huku maeneo mengine yakiwa meusi zaidi.

Matokeo yake ni contrast nzuri, HDR yenye kuvutia na mwangaza mkubwa.

OLED – Kila pixel ina uwezo wake

OLED ni moja ya teknolojia zinazotajwa sana linapokuja suala la ubora wa picha.

Tofauti kubwa ni kwamba katika OLED, kila pixel inaweza kujimulika yenyewe. Hivyo, inapohitajika kuonyesha rangi nyeusi, pixel inaweza kuzimwa kabisa.

Hii ndiyo sababu OLED inaweza kutoa nyeusi halisi, contrast ya hali ya juu na picha yenye kuvutia sana.

Pia OLED inaweza kutengeneza TV nyembamba sana.

Hata hivyo, kwa matumizi yenye picha zilezile zinazobaki kwenye skrini kwa muda mrefu na kurudiwa mara kwa mara, kuna hatari ya burn-in kwenye baadhi ya paneli za OLED.

QD-OLED – Mchanganyiko wa teknolojia mbili

Fikiria kupata faida za OLED na teknolojia ya Quantum Dot kwa pamoja.

Hapo ndipo QD-OLED inapoingia.

Teknolojia hii inalenga kutoa black levels bora za OLED pamoja na rangi ang’avu na mwangaza mkubwa.

Ndiyo maana TV za QD-OLED mara nyingi huvutia watu wanaotafuta kiwango cha juu zaidi cha ubora wa picha na wako tayari kulipia zaidi.

Sasa ipi ni bora?

Hakuna jibu moja kwa kila mtu. Chaguo bora linategemea matumizi yako na bajeti.

Unatafuta TV ya bei nafuu? LED inaweza kukufaa.

Unataka rangi nzuri na mwangaza mkubwa? QLED ni chaguo zuri.

Unataka mwangaza mkubwa, HDR na contrast nzuri bila kwenda moja kwa moja kwenye OLED? Mini-LED ni chaguo la kuangalia.

Unataka black levels na contrast bora kwa sinema? OLED inavutia sana.

Unataka teknolojia ya kiwango cha juu zaidi? QD-OLED inaweza kuwa miongoni mwa chaguo bora.

Usidanganywe na neno “4K”

Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba 4K si aina ya kioo. 4K inaelezea resolution ya picha, yaani idadi ya pixels zinazounda picha.

Kwa hiyo unaweza kuwa na 4K LED, 4K QLED, 4K Mini-LED au 4K OLED.

Unaponunua TV, usiangalie tu ukubwa wa skrini au neno “4K”. Angalia pia aina ya paneli, brightness, contrast, HDR, refresh rate, mfumo wa Smart TV na matumizi yako halisi.

Hitimisho

TV za kisasa si suala la ukubwa wa skrini pekee. Teknolojia iliyopo nyuma ya kioo ndiyo inayoweza kuamua kama utaona picha ya kawaida au picha yenye rangi hai, nyeusi halisi, mwangaza mkubwa na maelezo yanayokufanya uhisi kama tukio lipo mbele yako.

Kwa kifupi, LED ni rahisi na rafiki kwa bajeti, QLED inaleta rangi na mwangaza, Mini-LED inaongeza udhibiti wa mwanga, OLED inaleta contrast ya kipekee, huku QD-OLED ikichanganya teknolojia kwa kiwango cha juu zaidi.

Mfano wa bei za soko nchini Tanzania

SAMSUNG CRYSTAL UHD
👉43” Smart 4K 🔥 1,050,000/=
👉50” Smart 4K 🔥 1,250,000/=
👉55” Smart 4K 🔥 1,550,000/=
👉58” Smart 4K 🔥1,785,000/=
👉65” Smart 4K 🔥 2,050,000/=
👉75” Smart 4K 🔥 3,150,000/=
👉85” Smart 4K 🔥 5,250,000/=

SAMSUNG QLED
👉55” QLED 🔥 1,750,000/=
👉65” QLED 🔥2,450,000/=
👉75” QLED 🔥3,650,000/=
👉85” QLED 🔥5,850,000/=
👉98” QLED 🔥 11,500,000/=
👉100” QLED 🔥16,500,000/=

SAMSUNG NEW OLED TV
👉55” OLED 🔥4,250,000/=
👉65” OLED 🔥6,250,000/=
👉77” OLED 🔥10,500,000/=