Inter Milan Kuanza na BK Häcken Ligi ya Mabingwa Ulaya

Global Publishers
September 22, 2026
42 views
0 Comments

 

Mechi ya kwanza ya hatua ya ligi ya Mabingwa ya Wanawake UEFA itafanyika Jumanne, Septemba 22, 2026, saa 19:45 usiku, ambapo timu ya wanawake ya Inter Milan watakaribisha timu ya wanawake ya BK Häcken katika Uwanja wa Brianteo, Monza.

Huu ni mchezo wa kihistoria kwa Inter Milan kwani ni mara yao ya kwanza kabisa kushiriki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake UEFA .

Timu hii ya Italia ilifuzu baada ya kumaliza nafasi ya pili katika Serie A ya msimu uliopita na kupita hatua ya kufuzu kwa ushindi dhidi ya Wolfsburg.

Kwa timu ya wanawake ya BK Häcken, hii ni fursa ya kujithibitisha zaidi baada ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Damallsvenskan nchini Uswisi.

Mchezo huu unakuja wakati ambapo timu zote mbili zinajua umuhimu wake katika mfumo mpya wa ligi. Hatua ya ligi ina timu 18 zinazoshindana, ambapo nne za juu zinapata nafasi ya moja kwa moja kwenye robo fainali na nane zinazofuata zinaingia hatua ya playoff.

Inter Milan wamejiandaa vyema chini ya kocha wao David Sassarini, wakati BK Häcken wanakuja na uzoefu wa mashindano ya Uropa.

Kwa haya na mengine mengi ya kimichezo, tembelea Jukwaa la Meridianbet kwa Taarifa, takwimu, uchambuzi na matokeo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni.

Inter Milan Women wanatarajia kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kuanza vyema kampeni yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa. BK Häcken Women, upande wa pili, wanajua kwamba kuanza na pointi ugenini.

Mchezo huu muhimu katika safari yao ndefu ya hatua ya ligi. Mechi hii inaweza kuwa ya kwanza tu, lakini matokeo yake yanaweza kuamua mwelekeo wa timu zote mbili katika mashindano haya makubwa ya Uropa.

Vyombo vya Habari Vyaungana Kususia Habari za Trump, White House Yazindua “Trump Tv”

Vyombo vikubwa vya televisheni nchini Marekani vimesitisha kwa pamoja huduma ya kurusha picha za shughuli za Rais Donald Trump baada ya utawala wake kumzuia mtandao wa CNN kushiriki katika mfumo wa pamoja wa kuripoti shughuli za rais unaojulikana kama White House TV Pool.

Mfumo huo unahusisha ABC, CBS, CNN, Fox News na NBC, ambazo hubadilishana zamu ya kurekodi na kusambaza picha za shughuli za rais kwa vyombo vingine vya habari. CNN ilikuwa imepangwa kuwa mwakilishi wa mfumo huo Jumatatu, Septemba 21, lakini haikuruhusiwa kutekeleza jukumu hilo.

Baada ya CNN kuzuiwa, ABC, CBS, Fox News na NBC zilikataa kutuma mtandao mwingine kuchukua nafasi yake, hatua iliyosababisha kusitishwa kwa muda kwa huduma hiyo ya pamoja ya televisheni. Mitandao hiyo ilisema umma una maslahi ya kupata taarifa sahihi na huru kuhusu shughuli za serikali.

Hatua hiyo iliathiri pia matangazo ya baadhi ya shughuli za Trump. Katika tukio la uzinduzi wa helipad mpya katika Ikulu ya White House, watazamaji waliweza kuona picha za rais lakini bila sauti ya kawaida kutoka kwenye mfumo wa TV Pool.

CNN, MS NOW NA POLITICO ZAFUNGUA KESI

Mzozo huo umeibuka baada ya utawala wa Trump kuzuia waandishi wa CNN, MS NOW na Politico kuingia katika eneo la White House na kuondoa vitambulisho vyao vya waandishi.

Vyombo hivyo vitatu vimefungua kesi katika mahakama ya shirikisho dhidi ya utawala wa Trump, vikidai kuwa hatua hiyo inakiuka haki zao chini ya Marekebisho ya Kwanza ya Katiba ya Marekani, yanayolinda uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari, pamoja na haki za kisheria zinazohusiana na mchakato unaostahili.

Trump ametetea uamuzi huo, akisema vyombo hivyo vimekuwa vikitoa kile anachokiita taarifa za uongo kuhusu yeye na utawala wake. Utawala wake umesema suala hilo linahusu upatikanaji wa White House na kwamba vyombo vya habari havina haki ya kudumu ya kupata nafasi ndani ya Ikulu.

WHITE HOUSE YAZINDUA “TRUMP TV”

Wakati mvutano huo ukiendelea, White House imezindua kituo cha mtandaoni kinachoitwa “TRUMP TV: The Essentials Station.” Kituo hicho kilizinduliwa Septemba 21, 2026, na kinatoa video na maudhui yanayohusiana na Rais Trump na shughuli za utawala wake.

Taarifa zilizochapishwa kuhusu kituo hicho zinaeleza kuwa kinatoa matangazo ya shughuli za rais, hotuba, taarifa za utawala pamoja na video za matukio mbalimbali ya Trump, huku huduma hiyo ikipatikana mtandaoni.

Uzinduzi wa TRUMP TV umefanyika siku hiyo hiyo ambayo mitandao mikubwa ya televisheni ilisimamisha huduma ya pamoja ya TV Pool, hivyo kuongeza mjadala kuhusu namna shughuli za rais zinavyopaswa kuripotiwa na vyombo huru vya habari.

Kwa sasa, mzozo huo unaendelea pia mahakamani, huku CNN, MS NOW na Politico zikiiomba mahakama kurejesha upatikanaji wao wa White House wakati kesi yao ikiendelea.

Stori na Ashura Karimu | GPL -TUDACO

BLOG POST Vyombo vya Habari Vasitisha Matangazo ya Trump, White House Yazindua “Trump Tv”

Vyombo vikubwa vya televisheni nchini Marekani vimesitisha kwa pamoja huduma ya kurusha picha za shughuli za Rais Donald Trump baada ya utawala wake kumzuia mtandao wa CNN kushiriki katika mfumo wa pamoja wa kuripoti shughuli za rais unaojulikana kama White House TV Pool.

Mfumo huo unahusisha ABC, CBS, CNN, Fox News na NBC, ambazo hubadilishana zamu ya kurekodi na kusambaza picha za shughuli za rais kwa vyombo vingine vya habari. CNN ilikuwa imepangwa kuwa mwakilishi wa mfumo huo Jumatatu, Septemba 21, lakini haikuruhusiwa kutekeleza jukumu hilo.

Baada ya CNN kuzuiwa, ABC, CBS, Fox News na NBC zilikataa kutuma mtandao mwingine kuchukua nafasi yake, hatua iliyosababisha kusitishwa kwa muda kwa huduma hiyo ya pamoja ya televisheni. Mitandao hiyo ilisema umma una maslahi ya kupata taarifa sahihi na huru kuhusu shughuli za serikali.

Hatua hiyo iliathiri pia matangazo ya baadhi ya shughuli za Trump. Katika tukio la uzinduzi wa helipad mpya katika Ikulu ya White House, watazamaji waliweza kuona picha za rais lakini bila sauti ya kawaida kutoka kwenye mfumo wa TV Pool.

CNN, MS NOW NA POLITICO ZAFUNGUA KESI

Mzozo huo umeibuka baada ya utawala wa Trump kuzuia waandishi wa CNN, MS NOW na Politico kuingia katika eneo la White House na kuondoa vitambulisho vyao vya waandishi.

Vyombo hivyo vitatu vimefungua kesi katika mahakama ya shirikisho dhidi ya utawala wa Trump, vikidai kuwa hatua hiyo inakiuka haki zao chini ya Marekebisho ya Kwanza ya Katiba ya Marekani, yanayolinda uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari, pamoja na haki za kisheria zinazohusiana na mchakato unaostahili.

Trump ametetea uamuzi huo, akisema vyombo hivyo vimekuwa vikitoa kile anachokiita taarifa za uongo kuhusu yeye na utawala wake. Utawala wake umesema suala hilo linahusu upatikanaji wa White House na kwamba vyombo vya habari havina haki ya kudumu ya kupata nafasi ndani ya Ikulu.

WHITE HOUSE YAZINDUA “TRUMP TV”

Wakati mvutano huo ukiendelea, White House imezindua kituo cha mtandaoni kinachoitwa “TRUMP TV: The Essentials Station.” Kituo hicho kilizinduliwa Septemba 21, 2026, na kinatoa video na maudhui yanayohusiana na Rais Trump na shughuli za utawala wake. (

Taarifa zilizochapishwa kuhusu kituo hicho zinaeleza kuwa kinatoa matangazo ya shughuli za rais, hotuba, taarifa za utawala pamoja na video za matukio mbalimbali ya Trump, huku huduma hiyo ikipatikana mtandaoni.

Uzinduzi wa TRUMP TV umefanyika siku hiyo hiyo ambayo mitandao mikubwa ya televisheni ilisimamisha huduma ya pamoja ya TV Pool, hivyo kuongeza mjadala kuhusu namna shughuli za rais zinavyopaswa kuripotiwa na vyombo huru vya habari.

Kwa sasa, mzozo huo unaendelea pia mahakamani, huku CNN, MS NOW na Politico zikiiomba mahakama kurejesha upatikanaji wao wa White House wakati kesi yao ikiendelea.

Stori na Ashura Karimu | GPL -TUDACO

Mashabiki Kukutana Uso Kwa Uso na Wachezaji wa Taifa Stars

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezindua tukio la ‘Mashabiki Open Day’, litakalowapa mashabiki na wadau wa soka nchini fursa ya kukutana kwa karibu na wachezaji pamoja na benchi la ufundi la Timu ya Taifa, Taifa Stars.

Tukio hilo linatarajiwa kufanyika kesho Jumatano, Septemba 23, 2026, kuanzia saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa TFF, hatua hiyo inalenga kuwawezesha mashabiki kushuhudia kwa karibu mazoezi ya Taifa Stars, huku ikiwa sehemu ya maandalizi ya timu kuelekea michezo ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 pamoja na mchezo wa kirafiki.

Mashabiki watakaohudhuria watapata fursa ya kuona maandalizi ya timu kwa karibu, huku pia wakipewa nafasi ya kupiga picha na kujipiga selfie pamoja na wachezaji na benchi la ufundi.

TFF imeeleza kuwa tukio hilo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uhusiano kati ya Taifa Stars na mashabiki wake, pamoja na kuongeza morali kwa wachezaji na benchi la ufundi kuelekea michezo ijayo.

Stori na Peter Jinanai| GPL -TUDACO

The post Mashabiki Kukutana Uso Kwa Uso na Wachezaji wa Taifa Stars appeared first on Global Publishers.

OMDTZ YAFANIKISHA MIPANGO YA KUKABILIANA NA MAFURIKO DAR ES SALAAM

 

Na, Matukio Daima Media- Dar es Salaam

Taasisi ya OpenMap Development Tanzania (OMDTZ), kwa kushirikiana na Serikali, imekamilisha zoezi la kukabidhi Mipango ya Maandalizi na Kukabiliana na Mafuriko kwa jamii katika kata tano za Jiji la Dar es Salaam.

Zoezi hilo limewezesha zaidi ya washiriki 1,345 kutoka katika kata za Keko, Mabibo, Ubungo, Makurumla na Tabata kupata mipango, elimu na taarifa muhimu za maandalizi na mwitikio wa mafuriko.

Aidha utekelezaji wa zoezi hilo umepitia Mradi wa “Ramani Zetu, Sauti Zetu”, unaofadhiliwa na Zayed Sustainability Prize, kwa lengo la kuhakikisha jamii na viongozi wa kata hizo wanakuwa na taarifa sahihi kuhusu maeneo yao ili kuwawezesha kujiandaa kabla ya mafuriko, kuchukua hatua wakati wa hatari na kuendelea kuwa salama baada ya tukio.

Katika kata hizo wananchi walipatiwa taarifa kuhusu maeneo hatarishi, njia salama za uhamishaji, maeneo ya mikusanyiko na maeneo yanayohitaji uangalizi zaidi wakati wa mafuriko.

Aidha, walipata elimu kuhusu hatua za kuchukua kabla na wakati wa mafuriko, matumizi ya Mifumo ya Tahadhari za Mapema, hatua za msingi za uokoaji na taarifa kuhusu mwenendo wa mvua za El Niño.

Akifunga rasmi zoezi hilo katika Kata ya Tabata, Diwani wa Kata hiyo, Mheshimiwa Masudi Masudi, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano kati ya jamii, viongozi na wadau katika kukabiliana na changamoto za mafuriko.

“Ushirikiano kati ya OMDTZ, viongozi na jamii umetusaidia kutambua changamoto na kuchukua hatua katika maeneo yetu. Mfano ni eneo la Mtaa wa Msimbazi Magharibi ambapo hatua zimechukuliwa na OMDTZ kwa kujenga mfereji wa kupokea maji. Tunahitaji kuendelea na ushirikiano huu ili kuhakikisha maandalizi yanaendelea kuwa sehemu ya maisha ya jamii,” amesema Mhe. Masudi

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa OpenMap Development Tanzania, Bw. Innocent Maholi, amesema kukamilika kwa zoezi hilo ni hatua muhimu katika kuhakikisha mipango na taarifa zilizotengenezwa kwa kushirikisha wananchi zinarejeshwa kwa jamii na kutumika katika kuchukua hatua.

Amehimiza viongozi na wananchi kuendelea kutumia zana zilizotolewa na OMDTZ katika shughuli za usafi wa mazingira, hususan usafishaji wa mifereji na maeneo yanayoweza kuziba na kusababisha maji kutuama.

“Mradi wa Ramani Zetu, Sauti Zetu unalenga kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya mafuriko kupitia matumizi ya ramani shirikishi, taarifa za jamii, mipango ya maandalizi na mwitikio wa maafa pamoja na uhamasishaji wa hatua za mapema,” alisema Maholi

Aliongezea kuwa kupitia mradi huo, OMDTZ itaendelea katika Mikoa ya Pwani na Morogoro  kushirikiana na Serikali na jamii katika kutumia taarifa za maeneo husika kuimarisha maandalizi, kupunguza vihatarishi na kuongeza uwezo wa jamii kukabiliana na athari za mafuriko.

Cédric Kaze Atangazwa Kocha Mkuu Mpya wa Kagera Sugar

Global Publishers
September 22, 2026
492 views
0 Comments

Klabu ya soka ya Kagera Sugar imemtangaza rasmi kocha mzoefu Cédric Kaze kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Kaze, raia wa Burundi, anachukua nafasi hiyo baada ya Juma Kaseja kuondolewa kwenye nafasi ya Kocha Mkuu kufuatia mwenendo usioridhisha wa timu katika michezo ya mwanzo ya msimu.

Kaseja aliondolewa baada ya Kagera Sugar kuanza vibaya msimu huu, ikikusanya alama mbili pekee katika michezo sita ya kwanza bila kupata ushindi.

Kaze anajiunga na Kagera Sugar akitokea nchini Afrika Kusini, ambako alikuwa akiifundisha klabu ya Sekhukhune United.

Uongozi wa Kagera Sugar umeamua kumpa nafasi Kaze kutokana na uzoefu wake katika soka la Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Kabla ya kujiunga na Kagera Sugar, Kaze amewahi kuifundisha Yanga SC, huku pia akiwa amefanya kazi kama Kocha Mkuu na Kocha Msaidizi katika klabu za Kaizer Chiefs na Sekhukhune United za Afrika Kusini.

Akizungumza mara baada ya kutambulishwa, Kaze ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kutumia kila jitihada kuhakikisha anairejesha Kagera Sugar kwenye mstari wa ushindi na kuipa mafanikio katika michezo ijayo.

Stori na Peter Jinanai | GPL -TUDACO

Yanga Yaipiga Bao Simba Ufungaji Shalulile Ampoteza Doumbia

Global Publishers
September 22, 2026
0 views
0 Comments

Kikosi cha Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi ni namba moja eneo la ufungaji safu hiyo ya ushambuliaji inayoongozwa na Peter Shalulile imeipoteza ile ya Simb SC inayoongozwa na Ibrahim Doumbia.

Yanga SC baada ya mechi 6 ambazo ni dakika 540, safu ya ushambuliaji imefunga mabao 16,ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 16 msimu wa 2026/27.

Ni Singida Black Stars yenye Jonathan Sowah, hii ni namba mbili kwa safu kali za ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 13 baada ya mechi 6 ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 41.

 

Simba SC ni namba tatu kwa timu zenye mabao mengi ikiwa imetupia mabao 11 ina wastani wakufunga bao 1 kila baada ya dakika 49.

Timu hii inanolewa na Kocha Mkuu, Steve Barker imefunga mabao sawa na Azam FC iliyocheza mechi 7 ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 57.

Azam FC kwenye msimamo ni nafasi ya 3 imecheza mechi 7 ambazo ni dakika 630 imekusanya jumla ya pointi 14 huku Simba SC ikiwa na pointi 18 nafasi ya pili vinara ni Yanga SC wenye pointi 18.

Na Lunyamadzo Mlyuka



KIGAILA APOKEA WANACHAMA WAPYA ZAIDI YA 300 CHAUMMA BAHI

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Basi

KATIBU Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Benson Kigaila, amepokea wanachama wapya zaidi ya 300 kutoka Wilaya ya Bahi, mkoani Dodoma, walioamua kujiunga na chama hicho.

Wanachama hao wamekabidhiwa kadi za uanachama na Kigaila leo Septemba 22,2026  katika Kijiji cha Mpinga, Kata ya Mpinga, Wilaya ya Bahi.

Kigaila alikuwa ameambatana na Mkurugenzi wa Bunge, Halmashauri na Tawala za Mikoa wa Chaumma, Kayombo Kabutal, pamoja na Katibu wa Chaumma Mkoa wa Dodoma, Mathias Nyakapala.

Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla hiyo, Kigaila amesema hali ya umaskini inayowakabili baadhi ya wananchi wa Bahi imesababishwa na kuendelea kukichagua Chama cha Mapinduzi (CCM).

Amesema wakati umefika kwa wananchi hao kufanya mabadiliko ya kisiasa kwa kuondoa CCM madarakani na kukipa nafasi Chaumma, akieleza kuwa chama hicho kinaamini kinaweza kuleta maendeleo ambayo wananchi wa Bahi wamekuwa wakiyahitaji kwa muda mrefu.

“Nyinyi ni maskini wa kutupa kwa sababu ya kuichagua CCM. Wamewatelekeza na ninyi mpo tu, maisha yenu hayaeleweki. Hebu jitathmini, achaneni na CCM sasa, chagueni Chaumma,” amesema Kigaila.

Kwa upande wake, Kabutal alisema pamoja na Wilaya ya Bahi kuwa na utajiri wa rasilimali za madini ikiwemo Uranium, wananchi wake bado wameendelea kukabiliwa na hali ya umaskini.

Kutokana na hali hiyo, amewaomba wananchi wa Bahi kukiamini Chaumma na kukipa nafasi ya kushiriki katika uongozi ili kutekeleza sera na mipango yake ya maendeleo.

Naye Novatus Madanya, mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na Chaumma, alisema ameamua kuunga mkono chama hicho kutokana na kuridhishwa na sera zake.

Amesema anaamini sera hizo zinaweza kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi wa Bahi.

Kwa upande wake, Neema Mlay alisema wananchi wa Bahi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo ukosefu wa maji kwa muda mrefu.

Mlay amesema hali hiyo imewafanya baadhi ya wananchi kuhisi kama wametelekezwa na kunyanyaswa licha ya kuwa sehemu ya nchi yenye rasilimali mbalimbali.

Amesema wananchi wanahitaji kuona mabadiliko katika huduma za msingi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuboresha maisha yao.

Aliyekuwa Mtayarishaji wa Fox News Jennifer Eckhart Afariki

Jennifer Eckhart, aliyewahi kufanya kazi kama mtayarishaji msaidizi katika kituo cha televisheni cha Fox News nchini Marekani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 36.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMZ, Jennifer amefariki katika jimbo la Florida, huku ofisi ya Martin County Medical Examiner ikithibitisha kifo hicho. Vyanzo vya vyombo vya sheria vimeeleza kuwa kifo chake kimeainishwa kuwa kujiua.

Jennifer alikutwa amefariki katika nyumba yake iliyopo Hobe Sound, Florida, Jumamosi asubuhi, huku uwepo mkubwa wa polisi ukiripotiwa katika eneo hilo.

Jennifer alifahamika zaidi mwaka 2020 baada ya kumfungulia mashtaka aliyekuwa mtangazaji wa Fox News, Ed Henry, akimtuhumu kwa kumbaka wakati wote wawili walipokuwa wakifanya kazi katika kituo hicho.

Katika madai yake, Jennifer alisema Henry alimgusa kingono bila ridhaa yake na kwamba aliogopa kuwa alikuwa na mamlaka ya kuharibu taaluma yake. Henry alikanusha madai hayo na kusema uhusiano wao ulikuwa wa makubaliano.

Fox News ilimfuta kazi Henry mwezi Julai 2020 baada ya kupokea malalamiko ya Jennifer na kufanya uchunguzi wa ndani.

Mapambano ya kisheria kati ya Jennifer na Henry yaliendelea kwa miaka kadhaa, kabla ya wawili hao kufikia makubaliano ya kisheria mwaka 2024, muda mfupi kabla kesi hiyo kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa.

Jennifer pia aliishtaki Fox News, akiishutumu kampuni hiyo kwa kushindwa kumlinda dhidi ya Henry na kutomchukulia hatua ipasavyo kutokana na madai ya mwenendo wake.

Hata hivyo, madai hayo dhidi ya Fox News yalitupiliwa mbali, na Mahakama ya Rufaa ya Shirikisho iliunga mkono uamuzi huo mwezi Aprili 2025, ikisema Fox News haikuwa na taarifa kuhusu madai ya mwenendo wa Henry kabla Jennifer hajatoa malalamiko yake.

Baadaye Jennifer alizungumza hadharani kuhusu madai hayo, akieleza kuwa kipindi alichokuwa akifanya kazi Fox News kilimfanya kuishi katika hali ya hofu.

Waziri wa Mambo ya Nje Iran Awasili Marekani Kwa Mkutano wa UN

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amewasili mjini New York, Marekani, akiwa anaongoza ujumbe wa kidiplomasia wa Iran katika Mkutano Mkuu wa 81 wa Umoja wa Mataifa (UNGA) unaofanyika wiki hii.

Araghchi amekuwa afisa wa ngazi ya juu zaidi kutoka Iran kuingia nchini Marekani tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani na Iran, hali inayofanya ziara yake kufanyika katika mazingira ya mvutano mkubwa wa kidiplomasia.

Marekani imeidhinisha ujumbe wa msingi wa Iran, ukiwemo Rais Masoud Pezeshkian na Waziri Araghchi, kuhudhuria Mkutano Mkuu wa UN, lakini imeweka masharti kuhusu safari na matumizi yao wakiwa New York. Miongoni mwa masharti hayo ni marufuku ya kununua bidhaa za kifahari, huku pia harakati za wajumbe hao zikiwa zimewekewa mipaka katika maeneo maalumu.

Baada ya kuwasili New York, Araghchi alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ambapo walibadilishana maoni kuhusu ajenda ya Mkutano Mkuu wa UN na masuala yanayohusiana na mkutano huo.

Awali, Iran ilikuwa imetangaza kuwa ujumbe wake ungeongozwa na Rais Pezeshkian. Hata hivyo, ripoti kutoka Iran zilisema baadhi ya wajumbe, wakiwemo watu katika timu ya mawasiliano ya Rais, walikumbana na changamoto za kupata visa vya kuingia Marekani.

Rais Pezeshkian pia anatarajiwa kwenda New York kuhudhuria Mkutano Mkuu wa UN na kutoa hotuba, huku Araghchi akitarajiwa kushiriki katika vikao mbalimbali na kufanya mazungumzo na mawaziri wa mambo ya nje pamoja na maafisa kutoka mataifa mbalimbali watakaohudhuria mkutano huo.

Kwa mujibu wa taarifa za sasa, ziara hiyo inafanyika wakati ambapo mvutano kati ya Washington na Tehran bado ni mkubwa, huku Mkutano Mkuu wa UN ukiwa moja ya majukwaa muhimu kwa pande mbalimbali kueleza misimamo yao kuhusu masuala ya kimataifa.