Mwandaaji wa Miss Grand Tanzania Afungiwa na BASATA, Atozwa Faini

Global Publishers
September 24, 2026
894 views
0 Comments

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limechukua hatua dhidi ya mwandaaji wa shindano la Miss Grand Tanzania kwa tuhuma za kuendesha shindano hilo bila kuwa na kibali cha tukio kinachotakiwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za uendeshaji wa matukio ya sanaa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, mwandaaji huyo alipewa notisi ya kosa hilo tarehe 12 Agosti 2026 na kutakiwa kuwasilisha utetezi wake ndani ya siku 21.

Hata hivyo, BASATA imeeleza kuwa mwandaaji huyo hakutekeleza matakwa ya notisi hiyo ndani ya muda uliowekwa.

Kwa kuzingatia Kanuni ya 45 ya Kanuni za Baraza, BASATA imeamua kumtoza mwandaaji huyo faini ya Shilingi milioni tatu (TSh 3,000,000), ambayo anatakiwa kuilipa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.

Aidha, BASATA imeamuru mwandaaji huyo kutokujishughulisha na kazi za sanaa kuanzia tarehe ya uamuzi hadi pale atakapotekeleza maamuzi yaliyotolewa.

Hatua hiyo imekuja katika mazingira ambayo waandaaji wa matukio ya sanaa wanatakiwa kuzingatia taratibu na kupata vibali vinavyohitajika kabla ya kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa masharti ya mamlaka husika.

 

Mpigie Kura Godmuya, Kura Yako Ni Ushindi! – Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026

Global Publishers
September 24, 2026
3,156 views
0 Comments

Mtangazaji wa @globaltvonline na @255globalradio, Godfrey Nathan @godmuya ameteuliwa kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards 2026.

Sasa Godmuya anaomba support yako, mfuatiliaji wa Global TV, kwa kumpigia kura ili kufanikisha ushindi wake.

🗳️ MPIGIE KURA: GODFREY LUHILABAKE NATHAN
🔢 Kodi: 260246

Kura yako ni mchango mkubwa kwa Godmuya katika safari hii ya tuzo.

🙏 Piga kura, share na mwambie mwingine apige kura!

Trump Alivyompokea Xi Marekani Biashara, Taiwan na Iran Kutawala Mazungumzo

WASHINGTON, Septemba 23, 2026 — Rais wa Marekani Donald Trump amempokea Rais wa China Xi Jinping mjini Washington, katika ziara ya siku tatu inayotarajiwa kujikita katika masuala ya biashara, teknolojia, Taiwan na Iran, huku mataifa hayo mawili yakiendelea kukabiliana na mvutano wa muda mrefu wa kiuchumi na kimkakati.

Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Xi Jinping nchini Marekani katika kipindi cha takribani miaka mitatu na inafanyika wakati uhusiano kati ya Washington na Beijing ukiendelea kuwa na changamoto katika maeneo mbalimbali.

Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, amesema Marekani na China zimekubaliana kuongeza muda wa makubaliano ya kusitisha vita vya kibiashara hadi Januari 10, 2027. Makubaliano hayo yalitarajiwa kumalizika Novemba 10.

Trump mwenyewe alimkaribisha Xi katika kituo cha kijeshi cha Joint Base Andrews, Maryland, muda mfupi baada ya kiongozi huyo wa China kuwasili nchini Marekani.

Katika hafla hiyo, viongozi hao pamoja na wake zao walionekana wakipeana mikono na kuzungumza kwa muda mfupi kabla ya kupigwa picha. Hafla hiyo iliambatana na muziki wa bendi ya kijeshi, mizinga na ndege ya kijeshi ya B-1 iliyopita angani.

Xi, kupitia taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa China mjini Washington, amesema China na Marekani zinapaswa kuwa washirika badala ya wapinzani.

Hata hivyo, pamoja na ishara hizo za kidiplomasia, tofauti kubwa bado zipo kati ya mataifa hayo mawili.

Masuala yanayotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na udhibiti wa usafirishaji wa madini adimu na teknolojia za kompyuta, uhusiano wa China na Iran, pamoja na sera ya Marekani kuhusu Taiwan.

Mazungumzo hayo pia yanaweza kujadili ushirikiano katika kukabiliana na biashara ya dawa za kulevya, kuongeza mawasiliano kati ya majeshi ya nchi hizo mbili na kuendeleza mazungumzo kuhusu teknolojia ya akili bandia (AI).

Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wanaofahamu mipango ya mazungumzo hayo, Trump pia anatarajiwa kujadili suala la baadhi ya raia wa Marekani na watu wengine wanaoshikiliwa nchini China.

Ziara ya Xi inatarajiwa kuendelea na ratiba yenye hafla mbalimbali, ikiwemo chakula cha jioni cha kitaifa kitakachowakutanisha viongozi wa kampuni kubwa za teknolojia kama Apple, Nvidia na OpenAI.

Licha ya kuwepo kwa tofauti kuhusu biashara, teknolojia na masuala ya kimataifa, Marekani na China zimeendelea na mkutano huo huku zikisisitiza umuhimu wa kudumisha utulivu katika uhusiano kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani.

Zijue Athari za Kula Chipsi, Moja Kati ya Chakula Pendwa Zaidi Duniani

Global Publishers
September 24, 2026
7,792 views

Chipsi ni moja kati ya chakula kinanchopendwa zaidi duniani

KIUKWELI katika vyakula vitamu duniani na vinavyopendwa haswaa na watu duniani usiposema chipsi utakuwa mtu waajabu sana. Chipsi haziliki bongo tu ata ughaibuni chips zinalika sana na zinapendwa haswaa, chipsi zinaenda na vitu vingi kama chipsi yai, chipsi kuku na kadharika.

Hizi ndio athari za ulaji wa chipsi.

  • Husababisha magonjwa ya moyo

Kwa kuzingatia ukweli kwamba zimekaangwa sana katika mafuta ya hidrojeni, chipsi huja na kiasi kikubwa cha mafuta, ambayo huongeza cholesterol yako mbaya na kupunguza cholesterol yako nzuri. Athari kubwa ya hii ni kwamba utaongeza hatari ya ugonjwa wa moyo.

Ulaji wa chipsi husababisha magonjwa ya moyo

Kulingana na utafiti uliochapishwa katika jarida la Current Opinion in Clinical Nutrition & Metabolic Care, kula chakula chenye mafuta mengi na vyakula vyakukaanga vingi unaweza kuwa unaharibu utumbo wako kwa kuongeza bakteria wasio na afya na kupunguza bakteria wa afya ya mwili wako. Kwa kuzingatia jukumu la utumbo katika kusaidia kufahamisha mfumo wa kinga ya mwili wako, unaweza kuwa unaweka mwili wako hatarini kupata magonjwa.

Vyakula vya kukaangwa katika mafuta, huwa mabomu ya kalori, na kusababisha kupata uzito. Utafiti uliochapishwa katika jarida la The American Journal of Clinical Nutrition uligundua kuwa kula vyakula vya kukaanga kunahusishwa moja kwa moja na unene kupita kiasi.

Chipsi huongeza uzito wa mwili

 

UDOM Yatangaza Nafasi Mpya za Kazi 15, Maombi Septemba 28, 2026

Global Publishers
September 24, 2026
888 views
0 Comments

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimetangaza nafasi mbalimbali za ajira kwa Watanzania wenye sifa zinazohitajika, kwa ajili ya kujaza nafasi za kitaaluma. Tangazo hilo limetolewa Septemba 15, 2026.

Nafasi zilizotangazwa

  1. Tutorial Assistant – Fine Arts and Design – Nafasi 1
  2. Tutorial Assistant – International Relations – Nafasi 1
  3. Tutorial Assistant – History – Nafasi 1
  4. Tutorial Assistant – Chinese Language – Nafasi 1
  5. Tutorial Assistant – Biotechnology and Bioinformatics – Nafasi 1
  6. Tutorial Assistant – Applied Entomology – Nafasi 1
  7. Tutorial Assistant – Biomedical Engineering – Nafasi 1
  8. Tutorial Assistant – Psychiatry and Mental Health – Nafasi 1
  9. Tutorial Assistant – Pathology – Nafasi 1
  10. Tutorial Assistant – Physics Teaching Methods – Nafasi 1
  11. Tutorial Assistant – Biology Teaching Methods – Nafasi 2
  12. Tutorial Assistant – Nursing Nephrology – Nafasi 2
  13. Tutorial Assistant – Health Information Science – Nafasi 1

Kwa nafasi nyingi za Tutorial Assistant, mwombaji anatakiwa kuwa na shahada husika yenye GPA ya angalau 3.8 kati ya 5, ingawa sifa zinatofautiana kulingana na nafasi.

Masharti muhimu

Waombaji wote wanapaswa kuwa raia wa Tanzania na wasiwe na umri zaidi ya miaka 45. Pia wanatakiwa kuambatanisha CV yenye mawasiliano sahihi pamoja na nakala zilizothibitishwa za vyeti vya elimu, transcripts, vyeti vya Form IV na Form VI, vyeti vya usajili wa kitaaluma pale inapohitajika, pamoja na cheti cha kuzaliwa.

Waombaji walio katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi, kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa kwenye tangazo.

Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 28, 2026. Maombi yote yanatakiwa kutumwa kupitia Recruitment Portal ya Ajira iliyoainishwa kwenye tangazo.

Furahia Habari za Michezo Ndani ya Meridianbet Sports Portal Leo

Global Publishers
September 23, 2026
60 views
0 Comments

Meridianbet Sport Portal ni jukwaa la kisasa linalolenga kuwahudumia wapenzi wa michezo na kwa kuwapa taarifa sahihi, burudani. Kupitia mfumo wake rahisi na wa kuaminika, mashabiki wa michezo hupata matokeo ya papo kwa papo, takwimu za wachezaji nakadhalika.

Katika harakati za kuendelea kujitangaza zaidi na kuwarahisishia wateja wake, Meridianbet waliona ni vyema kuja na Meridianbet Sport Portal ambapo hapa wateja watapata taarifa sahihi kabisa za michezo.

Pia Meridianbet Sport Portal utakuta taarifa nyingi zaidi za promosheni mbalimbali kimichezo ambazo zinaweza kukunufaisha kwa namna moja au nyingine.

Mashabiki wengine kupitia habari tunazoziandika kupitia Portal hiyo ya Meridianbet wanajua ni namna gani ya kuangalia habari za wachezaji ambao wana majeraha, msimamo wa ligi mbalimbali, mikutana yao nakadhalika.

Kupitia Sport Portal ya Meridianbet unaweza ukaangalia pia mechi za (Live) yaani zinazoendelea kwani kwenye jukwaa hilo huwa zinaandikwa mechi ambazo zipo mapumziko ili kuweza kumjuza shabiki moja kwa moja kuhusu timu ambazo zinaendelea uwanjani na matokeo yake.

Vilevile ni rahisi sana wewe kupata habari zote za kimichezo ambazo sio za mpira pekee, bali hata michezo mingine ikiwemo Masumbwi, Mpira wa Kikapu, Tenisi na mingine mingi. Ingia kwenye akaunti yako moja kwa moja na uazne kujua nini kinaendelea kimichezo zaidi.

Lissu Atoa Hoja Kuhusu Mkutano wa Aprili 3 Na Waandishi wa Habari

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antiphas Lissu, leo Septemba 23, 2026 ameendelea na mawasilisho yake ya mwisho katika Mahakama Kuu ya Tanzania, akieleza hoja mbalimbali za kisheria na kiushahidi anazoomba mahakama izingatie katika uamuzi wa kesi ya uhaini inayomkabili.

Katika mawasilisho hayo, Lissu amesisitiza kuwa hakatai kwamba aliwahi kutoa maneno yanayodaiwa kuwa sehemu ya shtaka, akisema hoja yake ya msingi ni iwapo maneno hayo yanatosha kisheria kuunda kosa la uhaini au kosa lingine la jinai. Amesema kauli hizo zilitolewa katika nyakati na maeneo mbalimbali nchini na hazikuwa siri.

Lissu amesema kesi hiyo ni ya tatu ya uhaini kufunguliwa nchini Tanzania, lakini ametofautisha kesi hiyo na kesi mbili zilizotangulia mwaka 1970 na 1983, akisema kesi hizo zilihusu madai ya jaribio la kupindua Serikali na kumuua Rais. Kwa mujibu wa mawasilisho yake, kesi yake inahusu madai ya kutishia Serikali, hivyo uamuzi wa mahakama unaweza kuweka msingi wa kisheria kuhusu tafsiri na matumizi ya kosa hilo katika siku zijazo.

Akifafanua kifungu cha sheria kinachotumika katika mashtaka yake, Lissu amesema kuna masharti kadhaa ambayo upande wa mashtaka unapaswa kuyathibitisha, ikiwemo kuwepo kwa nia ya kutenda kosa la uhaini, nia ya kuchochea mtu au kikundi cha watu, pamoja na kuoneshwa kwa nia hiyo kupitia uchapishaji au njia nyingine inayotambuliwa na sheria. Pia ameeleza kuwa, kwa tafsiri yake ya sheria, matokeo yaliyolengwa na nia hiyo yanapaswa kuoneshwa.

Lissu pia amerejea kanuni za kisheria zinazohusu uhaini, akisema moja ya masharti muhimu ni kuthibitishwa kwa kitendo cha wazi na si kutegemea maneno pekee. Ameeleza kuwa katika mazingira fulani maneno hayawezi kuchukuliwa kuwa kitendo cha wazi cha uhaini isipokuwa yawe yanaelezea matendo yanayohusiana na kosa hilo.

Katika hoja nyingine, Lissu amepinga madai kwamba ndiye aliyeitisha mkutano wa CHADEMA wa Aprili 3, 2025, akisema hakuna hata mmoja kati ya mashahidi 17 wa upande wa mashtaka aliyetoa ushahidi wa namna mkutano huo ulivyoitishwa. Ameirejea pia hoja ya mashahidi wa utetezi, akiwemo John Mnyika, ambao walieleza kuwa mkutano uliandaliwa na Sekretarieti ya CHADEMA na kwamba Lissu pamoja na John Heche walikuwa miongoni mwa walioalikwa.

Kuhusu madai kwamba aliwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano huo, Lissu ameyapinga akirejea ushahidi wa upande wa utetezi kwamba waandishi walialikwa na Brenda Rupia. Amesema ushahidi huo uliungwa mkono na mashahidi wengine wa utetezi na kwamba haukuhojiwa na upande wa mashtaka.

Hoja nyingine aliyoiwasilisha ni kuhusu matumizi ya neno “umma” katika shtaka. Lissu amesema kifungu cha sheria kinachotumika kinataja kuchochea mtu au kikundi cha watu kuitishia Serikali, wakati hati ya mashtaka inamtuhumu kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Kwa msingi huo, amehoji uhalali wa shtaka hilo na kudai kuwa sheria haijaweka kosa la “kuchochea umma” kama linavyoelezwa katika mashtaka yake.

Lissu pia amerejea Ibara ya 13(6)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayohusu kutoadhibiwa kwa kitendo ambacho hakikuwa kosa chini ya sheria wakati kilipofanyika. Amesema kwa kuzingatia msingi huo, anaamini mahakama inapaswa kuangalia kwa umakini kama kitendo anachotuhumiwa nacho kimeainishwa wazi kuwa ni kosa katika sheria.

Mawasilisho hayo yanaendelea katika hatua ya mwisho ya kesi, huku Lissu akiomba majaji kuzingatia hoja zake za kisheria pamoja na ushahidi uliotolewa na pande zote kabla ya kutoa uamuzi.

Lissu: Waheshimiwa majaji, kifungu cha 39(2)(d) cha sheria iliyotumika kunishtaki kinasema: “Mtu yeyote anayechochea mtu au kikundi cha watu…”

Shtaka dhidi yangu linasema nimechochea umma. Kwenye kifungu hicho cha 39(2) hakuna umma, kuna mtu au kikundi cha watu.

Sasa umma ni nini? Hiki kitu kinachoitwa umma ni kitu gani?

Kanuni ya Adhabu imetoa tafsiri ya neno umma. Tafsiri ya umma kwa mujibu wa sheria hii ina maana ya watu wote wa Tanzania Bara bila kujali uraia wao. Kila mtu aliyeko ndani ya mipaka ya Tanzania Bara, pamoja na watu wanaokaa mahali popote au wanaotumia sehemu yoyote, mfano baa, gesti au vilabu. Ni idadi yoyote ya watu, hata watu ambao hata ufanyeje huwezi kuwajua.

Huo ndio umma ambao ninatuhumiwa kuuchochea ili uzuie uchaguzi.

Sheria niliyoshitakiwa nayo inasema unachochea mtu au kikundi cha watu. Mtu anajulikana. Lakini kikundi cha watu ni nini hasa?

Natumia Oxford Advanced Learner’s Dictionary. Kikundi ni idadi ya watu au vitu ambavyo vipo pamoja katika sehemu moja au vinaunganishwa kwa namna fulani.

Hiyo ndiyo maana ya kikundi.

Si watu wote. Watu wote hawawezi kuwa kikundi. Kikundi ni sehemu ya watu wote.

Nimeshtakiwa kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria.

Lissu: Waheshimiwa majaji, hili kosa lilivyoletwa, hizi taarifa zilivyoletwa, haziwezi kujibika.

Hakuna mtu anayeweza kujitetea kwa hati kama hii, kuambiwa umechochea watu wote, waliopo uwanja wa ndege na waliopo majumbani kwao.

Hilo halipo kwenye kifungu cha sheria ya Kanuni ya Adhabu niliyoshitakiwa nayo.

Waheshimiwa majaji, kwa sababu ya upana wa hilo neno umma, upande wa mashtaka ulikuwa na wajibu wa kisheria kueleza huo umma ni upi katika hati yao ya mashtaka ili kumwezesha mshtakiwa kuandaa utetezi wake.

Upande wa mashtaka ulitakiwa kueleza huo umma unaodaiwa kuchochewa.

Wameleta kitu ambacho hakipo kwenye sheria.

Basi turudi kwenye misingi.

Nilisema kitu kinachoitwa kosa la jinai ni kile kilichokatazwa na sheria. Ni kitendo.

Kifungu cha 39(2) kimetengeneza kosa la uhaini kwa mtu yeyote anayechochea mtu au kikundi cha watu kuitishia serikali.

Sheria haijatengeneza kosa la mtu kuchochea watu wote, yaani umma.

Hakuna sheria ya namna hiyo.

Hakuna sheria inayosema ukichochea watu wote ni kosa.

Sheria inasema ukichochea mtu au kikundi cha watu.

Nimeshtakiwa. Nipo gerezani kwa mwaka mmoja na nusu sasa kwa kitu ambacho hakipo kwenye sheria za nchi hii.

Ibara ya 13(6)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema:

“Ni marufuku kwa mtu kuadhibiwa kwa kitendo chochote ambacho alipokifanya hakikuwa kosa chini ya sheria.”

Nimeshtakiwa kwa kuchochea umma.

Hakuna sheria inayoitwa kuchochea umma.

Kuna sheria inayosema kuchochea mtu au kikundi cha watu.

Nimeshtakiwa kwa kitendo ambacho wala si kosa.

Lissu: Hoja yangu ni kwamba, kwa sababu migongano hiyo inahusu jambo kubwa linalohusu ushahidi wa kwamba mshtakiwa aliwaalika au hakuwalika waandishi wa habari, inaonesha kwamba ushahidi huo hauna thamani yoyote.

Vipi kuhusu ushahidi wa utetezi kwenye hoja hii? Unasemaje?

Ushahidi wa utetezi umefuta shaka yoyote kuhusu mshtakiwa kuwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.

Kama kulikuwa na shaka kwamba mshtakiwa aliwaalika waandishi wa habari, imeondolewa yote na ushahidi wa utetezi.

Sisi tunasema kwamba waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025 walialikwa na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia, bila shaka yoyote. Wote wamesema hivyo.

Ushahidi huu upo katika ukurasa wa 592. Ushahidi wa DW2 upo katika ukurasa wa 621 hadi 622. Ushahidi wa DW3 upo katika ukurasa wa 693. Ushahidi wa DW4 upo katika ukurasa wa 800.

Mashahidi hao wote wanne wamesema kwamba aliyewaalika waandishi wa habari ni DW4, Brenda Rupia.

Waheshimiwa majaji, ushahidi huo haukuhojiwa hata mara moja.

Sasa, nini maana ya kutokuhojiwa kwa ushahidi huu?

Lissu: Kwa sababu hizi, jibu la swali la pili, je, mshtakiwa aliwaalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025, jibu lake ni hapana.

Hiyo ni kusema kwamba mshtakiwa hakuwalika waandishi wa habari kwenye mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025.

Swali la tatu ni hili: Je, mshtakiwa alitengeneza nia ya kuchochea mtu yeyote au kikundi cha watu kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Kwa kesi hii, hili ni suala la kufa au kupona, kwa sababu ni moja ya mambo muhimu zaidi katika kesi nzima dhidi yangu.

Taarifa iliyopo mahakamani inayonishtaki inanituhumu kwamba nilitengeneza nia ya kuhamasisha umma na kuchochea umma kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa lengo la kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwandaaji Miss Grand Tanzania Afungiwa Shughuli za Sanaa, Atozwa Tsh Milioni 3

Global Publishers
September 24, 2026
12 views
0 Comments

Mwandaaji wa shindano la Miss Grand Tanzania alitenda kosa la kuendesha shindano husika bila kuwa na KIBALI CHA TUKIO kutoka BASATA Kinyume na Kanuni na taratibu za uendeshaji wa matukio ya Sanaa hapa nchini. Alipewa Notisi ya kosa hilo tarehe 12/08/2026 na kutakiwa kuwasilisha utetezi wake ndani ya siku 21 na hakutekeleza, Kwa mujibu wa Kanuni ya 45 ya Kanuni za Baraza, imeamuliwa:-

• Kulipa faini ya Shilingi Milioni Tatu (Tsh 3,000,000/=) ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.

• Kutokujishughulisha na kazi za Sanaa kuanzia tarehe ya uamuzi huu hadi atakapotekeleza maamuzi yaliyotolewa.​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​​

Basata Yawatoza Faini Harmonize, Sanga, Nandy na Waandaaji

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya wasanii na waandaaji wa shughuli za sanaa baada ya kubainika kuwa wamekiuka maadili na taratibu zinazohusiana na shughuli za sanaa nchini.

1. HARMONIZE AADHIBIWA KWA VIDEO YA “KUDOS”

Msanii Rajab Abdulkahali maarufu Harmonize ameadhibiwa kwa kutenda kosa la kimaadili la kusambaza video ya wimbo unaoitwa “Kudos”, ambayo kwa mujibu wa BASATA haizingatii kabisa maadili ya Kitanzania na inavunja heshima ya misikilizaji au mtazamaji.

BASATA imesema kosa hilo ni kinyume na Kanuni ya 20(a) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, Tangazo la Serikali Na. 137 la tarehe 22 Mei 2026.

Hadi wakati wa kutolewa kwa taarifa hiyo, BASATA haikupokea utetezi wala maelezo mbadala kutoka kwa Harmonize.

Kwa kuzingatia Kanuni ya 45 ya Kanuni za Baraza, Harmonize amepewa adhabu zifuatazo:

  • Kusitisha video ya wimbo “Kudos” kwenye mitandao yake ya kijamii.
  • Kulipa faini ya Shilingi milioni tano (TSh 5,000,000) ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.
  • Kutokujishughulisha na kazi za sanaa kwa namna yoyote kuanzia tarehe ya uamuzi hadi atakapotekeleza maamuzi yaliyotolewa.

2. KENNEDY DAVID SANGA

Mwongoza video ya wimbo “Kudos”, Kennedy David Sanga, pia ameadhibiwa baada ya kubainika kuwa alitenda kosa la kimaadili linalokiuka heshima ya misikilizaji au mtazamaji.

Kwa mujibu wa BASATA, Sanga alikiuka Kanuni ya 20(a) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, Tangazo la Serikali Na. 137 la tarehe 22 Mei 2026, kwa kuongoza video hiyo iliyokuwa na maadili yasiyozingatia maadili ya Mtanzania.

Baada ya kusikilizwa, ilibainika kuwa alitenda kosa hilo na kupewa adhabu zifuatazo:

  • Kusitisha video ya wimbo “Kudos” kwenye mitandao yake ya kijamii.
  • Kulipa faini ya Shilingi milioni tano (TSh 5,000,000) ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.
  • Kutokujishughulisha na kazi za sanaa kwa namna yoyote kuanzia tarehe ya uamuzi hadi atakapotekeleza maamuzi yaliyotolewa.

3. AVIL CONTRACTORS COMPANY LTD

Avil Contractors Company Ltd, mwandaaji wa shindano la Miss Grand Tanzania, ameadhibiwa kwa kutenda kosa la kuendesha shindano hilo bila kuwa na KIBALI CHA TUKIO kutoka BASATA.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kampuni hiyo ilikiuka Kanuni na taratibu za uendeshaji wa matukio ya sanaa hapa nchini.

BASATA ilisema kampuni hiyo ilipewa notisi ya kosa hilo tarehe 12 Agosti 2026 na kutakiwa kuwasilisha utetezi ndani ya siku 21, lakini haikutekeleza.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 45 ya Kanuni za Baraza, kampuni hiyo imeamriwa:

  • Kulipa faini ya Shilingi milioni tatu (TSh 3,000,000) ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.
  • Kutokujishughulisha na kazi za sanaa kuanzia tarehe ya uamuzi hadi itakapotekeleza maamuzi yaliyotolewa.

4. NANDY AADHIBIWA KWA VIDEO YA KIMAAADILI

Msanii Faustina Charles Mfinanga maarufu Nandy ameadhibiwa na BASATA baada ya kutenda kosa la kimaadili la kuvaa nguo isiyokuwa na staha inayovunja heshima ya mtazamaji.

BASATA imesema kosa hilo lilitokea wakati Nandy akitumbuiza katika fainali ya shindano la Miss Universe 2026, lililofanyika katika ukumbi wa Haddypo, kinyume na Kanuni ya 20(a) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, Tangazo la Serikali Na. 137 la tarehe 22 Mei 2026.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Nandy amekiri kosa, ameshusha video hiyo isiyozingatia maadili ya Mtanzania kwenye mitandao yake ya kijamii na amelipa faini ya Shilingi milioni tatu (TSh 3,000,000).

Hata hivyo, msanii huyo ameruhusiwa kuendelea na shughuli zake za sanaa chini ya uangalizi.

5. MILLEN PRIVE & CO. LIFESTYLE LIMITED

Millen Prive & Co. Lifestyle Limited, mwandaaji wa shindano la Miss Universe Tanzania, ameadhibiwa kwa kosa la kimaadili lililohusisha msanii Faustina Charles Mfinanga maarufu Nandy.

Kwa mujibu wa BASATA, kampuni hiyo ilitenda kosa la kuvaa nguo ambayo haina staha inayovunja heshima ya mtazamaji, wakati Nandy akitumbuiza kwenye fainali ya Miss Universe Tanzania 2026 iliyofanyika katika ukumbi wa Haddypo, Dar es Salaam.

BASATA imesema kosa hilo ni kinyume na Kanuni ya 20(2)(a) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa, Tangazo la Serikali Na. 137 la tarehe 22 Mei 2026.

Baada ya kusikilizwa, ilibainika kuwa kampuni hiyo ilitenda kosa la kimaadili na imepewa adhabu zifuatazo:

  • Kulipa faini ya Shilingi milioni tatu (TSh 3,000,000) ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.
  • Kupewa onyo kali na kutakiwa kuwa makini wakati wa kutekeleza kazi zake za sanaa.

BASATA imetoa rai kwa wasanii na wadau wa sanaa kuhakikisha wanazingatia Sheria, Kanuni, Miiongozo na Maadili ya Mtanzania wanapotekeleza kazi zao za sanaa.

MAWAZIRI WATATU USO KWA USO NA WANANCHI WA ZINGIZIWA KUTAFUTA SULUHU YA MGOGORO WA MIPAKA

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Profesa Riziki Shemdoe akiwa amembatana na Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt Leonard Akwilapo pamoja,na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Stanslaus Nyongo amefanya mkutano na wananchi wa kata ya zingiziwa eneo la Chanika Wilayani Ilala kwa lengo la kushughulikia mgogoro wa siku nyingi wa mipaka kwenye eneo hilo.

Mkutano huo ni kufuatia utekelezaji wa maagizo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Deogratias Ndejembi alipofanya ziara ya kutembelea dampo la Pugu Jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka viongozi hao kushughulikia mgogoro wa mipaka ya kiutawala kati ya Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani kwenye kata ya Zingiziwa pamoja na mgogoro wa mpaka kati ya wananchi wa kata hiyo na hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi.

Akizungumza mara baada ya kusikiliza hoja na malalamiko ya wananchi Profesa Shemdoe ametoa muda wa wiki mbili kuanzia leo Sept 23,2026 kwa wataalamu kutoka TAMISEEMI,Wizara ya ardhi pamoja na wataalamu kutoka wizara ya Maliasili na Utalii kwenda kufuatilia vipimo vya mipaka ili kupata ufumbuzi na watafika tena katika eneo hilo baada ya wiki mbili huku akiwaahidi kumaliza migogoro hiyo ndani ya muda wa mwezi mmoja hadi miwili

Kwa upande wa Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt Leonard Akwilapo amesisitiza kuwa wizara yake inaitambua migogoro hiyo hivyo wanakwenda kushughulikia huku Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Hamad Chande akisisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita ni sikivu hivyo suluhu ya migogoro hiyo itapatikana mapema iwezekanavyo.

Sanjari na hilo Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewahakikishia wananchi wa maeneo hayo kuwa katika kipindi chote ambacho migogoro hiyo inashughulikiwa hakutakia na vitendo vya uvunjifu wa amani huku akiwataka wananchi kuwa wastahamilivu

Awali wananchi wa eneo hilo walipata wasaa wa kueleza namna migogoro hiyo imekuwa ni changamoto kwenye maisha yao huku Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo akiahidi kuendelea kushuhjulikia migogoro ya ardhi ili kumaliza maumivu waliyonayo wananchi kwenye ardhi