SERIKALI YAWEKA MKAKATI MAALUM KWA WATU WENYE ULEMAVU WAKATI WA EL NIÑO

 

Na Matukio DaimaMedia 

Serikali imeweka mkakati maalum wa kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata taarifa kwa wakati kuhusu mvua za El Niño pamoja na hatua za kuchukua kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza, ikiwamo kuhakikisha taarifa hizo zinawafikia kulingana na mahitaji yao.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Watu Wenye Ulemavu), Profesa Palamagamba Kabudi, amesema mbinu na nyenzo maalum tayari zimeandaliwa kwa ajili ya kutoa taarifa kwa makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu, yakiwamo watu wenye uoni hafifu, viziwi na wenye ulemavu wa aina nyingine.

Profesa Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika Jukwaa la Uratibu na Utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Haki na Ustawi wa Watu Wenye Ualbino Bandiliko wa mwaka 2024–2029, lililowakutanisha wadau mbalimbali kujadili utekelezaji wa mpango huo.

Amesema maandalizi hayo ni sehemu ya kuhakikisha makundi yenye mahitaji maalum hayaachwi nyuma wakati wa utoaji wa taarifa za tahadhari, hasa katika kipindi ambacho Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa taarifa kuhusu uwezekano wa mvua za El Niño.

Akizungumzia hali ya ulinzi na haki za watu wenye ualbino bandiliko, Profesa Kabudi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na changamoto zinazolikabili kundi hilo, ikiwamo unyanyapaa, ubaguzi, mauaji na vitendo vya ukatili.

Kwa upande wao, wawakilishi wa Chama cha Watu Wenye Ualbino Tanzania (TAS) wameipongeza Serikali kwa juhudi zinazochukuliwa katika kupambana na mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino, wakisema utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa unatoa matumaini ya kuboresha zaidi maisha yao.

Wamesema utekelezaji wa mpango huo unatarajiwa kuendelea kufungua fursa sawa kwa watu wenye ualbino katika maeneo muhimu kama elimu, ajira na huduma za afya, huku ukisaidia kuimarisha ulinzi wa haki zao na kuongeza ushiriki wao katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Serikali imesema itaendelea kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Huduma na Maendeleo ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 ili iendane na mabadiliko ya teknolojia na mahitaji ya sasa ya kijamii na kiuchumi, hatua inayolenga kuboresha huduma na mazingira ya watu wenye ulemavu nchini.

Jukwaa hilo limewakutanisha wawakilishi wa Serikali, taasisi za kimataifa, asasi za kiraia pamoja na vyama vya watu wenye ulemavu, kwa lengo la kuimarisha uratibu wa hatua zinazolenga kulinda haki, usalama na ustawi wa watu wenye ulemavu nchini

.

SUSAN MUWONGE KUANDIKA HISTORIA SERENGETI RALLY

 

Na Lilian Kasenene,Morogoro

Matukio Daima Media 

MWANAMKE kutoka Uganda, Susan Muwonge, anatarajiwa kuandika historia katika mashindano ya Serengeti Rally of Tanzania, yatakayofanyika Oktoba 1 hadi 4, 2026, baada ya kujitosa kushiriki kama dereva katika mashindano hayo.

Muwonge anakuwa miongoni mwa wanawake wanaoshiriki mashindano ya mbio za magari barani Afrika, huku akiwa dereva rasmi wa gari aina ya Subaru Impreza, akisaidiwa na Musa Nsubuga kama dereva msaidizi (co-driver).

Mashindano hayo ya awamu ya nne na ya mwisho kwa mwaka 2026 yatafanyika katika Shamba la Miti la Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), eneo la Makundi, mkoani Morogoro.

Akizungumza kuhusu maandalizi ya mashindano hayo, Msimamizi Mkuu wa mashindano, Dk. Mosi Makau, alisema ushiriki wa Muwonge unatarajiwa kuongeza mvuto wa mashindano hayo na kutoa hamasa kwa wanawake zaidi kushiriki katika mchezo wa mbio za magari.

“Mashindano haya yatahusisha magari nane. Kwa Tanzania madereva wawili tu ndio watashiriki, huku wengine wakitoka Kenya, Zambia, India na Uganda,” alisema Dk. Makau.

Alisema kinachowapa fahari ni ushiriki wa Muwonge kama dereva, akieleza kuwa wanawake waliowahi kushiriki katika mashindano hayo walikuwa wakifanya kazi ya udereva msaidizi, tofauti na safari hii ambapo Muwonge ataendesha gari mwenyewe.

Kwa mujibu wa Dk. Makau, mashindano hayo yatahusisha jumla ya magari 23, ambapo magari nane yatashindania ubingwa wa African Rally Championship, huku magari 15 yakishiriki National Rally Championship.

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mkwawa Group of Companies, ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo, Richard Sinamtwa, alisema mashindano hayo ni hatua muhimu katika kukuza mchezo wa magari na kuwaunganisha wadau wa mchezo huo kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Sinamtwa alisema kupitia mashindano hayo Tanzania itaendelea kunufaika katika kukuza utalii na uchumi wa jamii, ikizingatiwa kuwa mchezo huo unawakutanisha washiriki na mashabiki kutoka mataifa mbalimbali.

“Kupitia mashindano haya tuweze kutunza taswira ya Tanzania, kupitia michezo tuendelee kuhamasisha utalii, uhifadhi pamoja na kuhakikisha tunasimamia maendeleo ya jamii zetu,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mbio za Magari Tanzania, Satinder Singh Bardi, aliwataka wakazi wa Morogoro na mashabiki wa mchezo huo kuzingatia usalama wao wakati wote wa mashindano.

Alisisitiza umuhimu wa wananchi kufuata maelekezo ya vyombo vya usalama na kukaa katika maeneo yaliyotengwa kwa watazamaji ili kuepusha ajali na madhara.

Aidha, aliwahakikishia mashabiki kuwa maandalizi ya usalama yamezingatiwa ili mashindano hayo yafanyike kwa utaratibu na usalama.

MAGAZETINI LEO JUMANNE SEPT 29/2026:SARUJI KITENDAWILI,WANANCHI IRINGA WAELEZA KUHUSU UDUMAVU..

 

KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS HAPA
 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

KUPIGA KURA KWA MATUKIO DAIMA TUZO ZA SAMIA KALAMU AWARDS HAPA

 

 

MATUKIO DAIMA IMETEULIWA KUSHIRIKI TUZO ZA UMAHIRI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANAHABARI TANZANIA TUZO HIZI ZIMETOLEWA NA TCRA NA TAMWA 

 MAARUFU KWA JINA LA SAMIA KALAMU AWARDS (SKA2026)⬇️⬇️⬇️

1:TUZO YA CHOMBO CHA HABARI -MATUKIO DAIMA MEDIA 

PIGA KURA YA CHOMBO MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

2:TUZO YA JINSIA ,WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM 

PIGA KURA YA PILI YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

3:TUZO YA AFYA

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

4:TUZO YA MPIGA PICHA 

PIGA KURA YA TATU YA MATUKIO DAIMA BONYEZA HAPA

AHSANTE KWA KUPIGIA KWA KUENDELEA KUTUPIGIA KURA MATUKIO DAIMA MEDIA ENDELEA KUTUPIGIA KURA KILA BAADA YA SAA 24 HADI SEPT 30 KASI YAKO YA KUPIGA KURA NDIO USHINDI .

PROF. SHEMDOE ASHIRIKI MAFUNZO YA UONGOZI HARVARD KUIMARISHA UWEZO WA UONGOZI, UTEKELEZAJI WA SERA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, anashiriki  mafunzo maalum ya uongozi kwa Mawaziri wa Kisekta yanayofanyika katika Chuo Kikuu cha Harvard, jijini Boston, Marekani.

Mafunzo hayo ya siku nne yameanza Septemba 26, 2026 na yanatarajiwa kukamilika Septemba 30, 2026, yakilenga kuwawezesha Mawaziri wa Kisekta kutoka nchi mbalimbali za Afrika na maeneo mengine kubadilishana uzoefu na maarifa katika uongozi, usimamizi na utekelezaji wa majukumu ya wizara za kisekta.

Mafunzo hayo yanahudhuriwa na Mawaziri wa Kisekta kutoka Tanzania, Kenya, Nigeria, Namibia, Chile, Dominican Republic, Malawi, Benin, Côte d’Ivoire, Gabon, Ghana, Guinea, Mauritius, Mauritania, Msumbiji, Sierra Leone na Togo.

Kupitia mafunzo hayo, Mawaziri hao wanapata fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu mbinu mbalimbali za uongozi wa kisekta, usimamizi wa taasisi za umma, ufanyaji wa maamuzi na namna ya kuimarisha utekelezaji wa sera na mipango ya Serikali kwa manufaa ya wananchi.

Aidha, mafunzo hayo yanawapa washiriki fursa ya kujifunza kutoka kwa viongozi wenye uzoefu mkubwa, wakiwemo Mawaziri wa zamani na Marais wastaafu, pamoja na kushirikishana uzoefu kuhusu changamoto na fursa zinazojitokeza katika uongozi wa sekta za umma.

Miongoni mwa wakufunzi katika mafunzo hayo ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na Rais wa Tano wa Botswana, Mhe. Mokgweetsi Masisi.

Ushiriki wa Prof. Shemdoe katika mafunzo hayo unatoa fursa ya Tanzania kushiriki katika jukwaa la kimataifa la kubadilishana uzoefu wa uongozi na usimamizi wa sekta za umma, hususan katika maeneo yanayohusu Serikali za Mitaa na utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa wananchi.

Maarifa na uzoefu unaopatikana kupitia mafunzo ni nyenzo muhimu katika kuendelea kuimarisha uongozi, usimamizi na utoaji wa huduma za Serikali kwa ufanisi, pamoja na kuongeza ujuzi wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa majukumu ya kisekta pamoja na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kozi hiyo  imeandaliwa na T.H. Chan School of Public Health, Harvard Graduate School of Education na Harvard Kennedy School, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwawezesha viongozi wa kisekta kujenga uwezo na kubadilishana uzoefu katika uongozi wa umma.

TANZANIA NA OMAN ZAFUNGUA UKURASA MPYA WA USHIRIKIANO KWENYE SEKTA ZA KIMKAKATI

Ukurasa mpya wa kimkakati na wa kihistoria umefunguliwa rasmi katika uhusiano wa diplomasia na uchumi kati ya Jamhuri ya Muunganio wa Tanzania na Usultani wa Oman, kufuatia kufanyika kwa Mkutano wa Kwanza wa Uwili Kati  ya Nchi hizo tangu kusainiwa kwa Mkataba wa Mashauriano ya Kisiasa mwaka 2009.

Mkutano huo uliofanyika Septemba 28, 2026 jijini Muscat, Oman ambao umeongozwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya nje wa Oman Mhe. Sheikh Khalifa Al-Harthy, pande hizo mbili zimekubaliana kuimarisha uhusiano wao wa kihistoria; kidugu na kirafiki kwa kutumia nafasi ya kijiografia ya nchi hizo  kuwa madaraja na vituo muhimu vya biashara na uwekezaji kati ya Afrika na Ghuba. 

Akizungumza wakati wa Mkutano huo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb.) amebainisha kuwa mkutano huo ni hatua kubwa ya kimfumo inayolenga kubadilisha nia njema kuwa matokeo yanayoonekana.  

Mhe. Londo ameishukuru Oman kwa kuendelea kuwekeza Tanzania Katika Sekta mbalimbali huku akiwakaribisha wawekezaji kupitia Mfuko wa Uwekezaji wa Oman (OIA) kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji, gesi asilia, na madini. OIA imeonesha nia ya kuwekeza nchini kupitia ubia wa kibiashara na miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP).

Kupitia mkutano huo Tanzania na Oman zimejadiliana kwa kina kuhusu umuhimu wa kuimarisha ziara za viongozi na wataalamu katika ngazi mbalimbali, kwa lengo la kuongeza fursa za kubadilishana uzoefu, maarifa na utaalamu, pamoja na kuimarisha utekelezaji wa makubaliano baina ya nchi hizo.

Aidha, wamejadili Ushirikiano Katika Sekta Muhimu na za Kimkakati ikiwemo Biashara na Uwekezaji, kilimo, afya, elimu, Uchumi wa buluu na Fursa za Kazi na ajira rasmi  pamoja na utalii na malikale ambazo zitasaidia kutekeleza kwa ufanisi Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 na Dira ya Maendeleo Oman 2040.

Mkutano huo unaiweka diplomasia ya nchi hizo mbili kwenye mwelekeo mpya unaotoka kwenye utamaduni na undugu wa kale, na sasa kujikita kwenye ushirikiano thabiti wa biashara, uwekezaji wa kimkakati, na fursa za kiuchumi zitakazonufaisha wananchi wa mataifa hayo mawili.

 

MAKAMU WA RAIS AAGIZA MILANGO IFUNGULIWE KWA VIJANA 10,000

ARUSHA, Agosti 28, 2026

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi ametoa wiki mbili kwa Wizara ya Mipango na Uwekezaji, Fedha na Kilimo kuandaa mpango wa mafunzo kwa Vitendo ambao utaanza kuchukua walau  vijana 10,000 kupata uzoefu katika Taasisi, Mashirika ya Umma na Sekta binafsi ili kuandaa vijana watakaokuwa na uzoefu wa kujiajiri na kuajiriwa kama sehemu muhimu ya kutekeleza nguzo ya pili ya Dira ya Taifa 2050 na kusaidia maendeleo ya Nchi.

 

Makamu wa Rais ametoa maelekezo hayo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma, kinachofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).

 

Amewataka Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Umma kubadili namna taasisi hizo zinavyofanya kazi na kuwa injini ya mageuzi ya uchumi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, huku akielekeza kuanzishwa kwa mkakati huo utakaowapatia angalau wahitimu 10,000 nafasi za mafunzo kwa vitendo na kuwapatia fedha za kujikimu katika mashirika ya umma na wengine wasiopungua 20,000 katika sekta binafsi.

 

” Kila mwaka kwa takribani vijana 62,570 wanahitimu elimu ya juu na hii ni takwimu ya mwaka Jana 2025 toka TCU, idadi hiyo haihusishi wale wanaomaliza VETA na Vyuo vya Kati. Ukiangalia TAESA takwimu zao zinaonesha vijana  3,200 pekee walikuwa wamepitia programu za mafunzo internship, idadi hii ni ndogo sana kwa kulinganishwa na wahitimu  62,570 kutoka vyuo mbalimbali nchini. Mlitazame hili kama uwekezaji wa kimkakati katika nguvu kazi ya Taifa kwa kubana matumizi ya kawaida, na hapa mtakuwa mmetekeza kwa Vitendo nguzo ya pili ya Dira 2050″ alisisitiza

 

Mhe. Ndejembi, amesema dhamana ya Watendaji, Wakuu wa Mashirika na Wenyeviti wa Bodi ni kubwa, na hivyo wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa ustadi na umakini mkubwa na kwa wakati sahihi katika kujenga uchumi, kuibua fursa mpya na kuinua maisha ya watanzania.

 

“Mashirika ya Umma yana nafasi ya kipekee katika kufikia malengo ya Dira 2050 kutokana na dhamana yake ya kusimamia mali za umma, kuendesha miundombinu ya kimkakati, kutoa huduma muhimu za nishati, usafirishaji, mawasiliano, fedha, afya, maji, na nyingine zinazobeba uchumi wetu. Kutokana na hilo, lazima tuyaangalie mashirika hayo kama injini ya mageuzi makubwa ya kiuchumi tunayoyalenga katika Dira 2050.” alisisitiza Ndejembi.

 

Sambamba na ajira na ujuzi kwa vijana, Makamu wa Rais amezitaka Taasisi na Mashirika ya Umma ukiangalia   namna ya kupunguza matumizi yasiyo na tija na utegemezi kwa Serikali, huku zikibuni vyanzo endelevu vya mapato na kuhakikisha kila shilingi ya umma inaleta thamani inayostahili.  

 

Ili kuhakikisha maelekezo hayo yanatafsiriwa kuwa matokeo, Ndejembi ameitaka Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha mfumo wa tathmini ya utendaji wa mashirika ya umma, na kutambua kwenye tuzo za mwaka ujao Taasisi zitakazotekeleza agizo la kuchukua vijana na kuwapa mafunzo.

 

Amehitimisha kwa kuzitaka Taasisi na Mashirika   kujiandaa mapema kukabiliana na athari za mvua za El Niño ili kulinda miundombinu na uwekezaji wa umma na kuhakikisha huduma muhimu kwa wananchi haziathiriki.

 

Kikao hicho cha C-CEOs Forum 2026 kimewakutanisha jijini Arusha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali, pamoja na Mawaziri, Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, Makatibu Wakuu na viongozi wengine wa Serikali.  

 

Kikao hicho cha siku tatu   kimeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa lengo la kutoa mwelekeo wa kimkakati kuhusu mustakabali wa Mashirika ya Umma, kutathmini yalipotoka na kujadili hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuongeza mchango wake katika uchumi na maendeleo ya Taifa, hususan wakati Tanzania imeanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

 

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

28 Septemba 2026

Arusha.

DKT. MWIGULU AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA QATAR

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumatatu, Septemba 28, 2026, amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani, katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Qatar, jijini Doha.

Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar.

Dkt. Mwigulu na ujumbe wake wamepokelewa katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Qatar, ikiwa ni sehemu ya ratiba ya ziara yake ya kikazi nchini Qatar.

Ziara hiyo inaendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano wa Tanzania na Qatar, pamoja na kufungua fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya maendeleo na uwekezaji.

 

MAGEREZA YAIPIGISHA KWATA POLISI BAMMATA 2026

Na Ssgt Mawazo Mtondo – MWANZA

Timu ya mpira wa pete ya Jeshi la Magereza imeendeleza kiwango chake kizuri katika Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026, baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 63–36 dhidi ya timu ya Polisi Tanzania katika mchezo uliochezwa leo, Septemba 28, 2026, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, timu ya Magereza ilionyesha uwezo mzuri katika kujenga mashambulizi na kutumia vyema nafasi ilizopata, hali iliyoiwezesha kufunga magoli 63 na kuibuka na ushindi wa kishindo dhidi ya Polisi.

Ushindi huo unaendeleza mwendelezo mzuri wa Kanda ya Magereza katika mashindano hayo, baada ya awali kuifunga Kanda ya JKT Tanzania kwa magoli 46–43.

 

ENG. SAMAMBA ATOA MAELEKEZO KWA WAMILIKI WA MIGODI NA MAAFISA MADINI WAKAZI WA MIKOA

🔶Aagiza maboresho ya taratibu za migodi, ukaguzi wa maduara, mabwawa ya tope sumu na maandalizi ya dharura

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eng. Yahya I. Samamba, amewaelekeza wachimbaji wadogo, wamiliki, mameneja na wakaguzi wa migodi nchini kuchukua hatua za haraka kujiandaa na kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu, ikiwemo kuongeza kasi ya ukaguzi wa maeneo ya uchimbaji (maduara), mabwawa ya kuhifadhia tope sumu na kuimarisha mipango ya dharura.

Eng. Samamba ametoa maelekezo hayo leo, Septemba 28, 2026, wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakati akifungua mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua hizo, akisema tahadhari hiyo inazingatia taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu uwezekano wa mvua kubwa kuliko wastani katika kipindi hicho.

Amesema mvua hizo zinaweza kuathiri shughuli za uchimbaji na kusababisha madhara kwa watu, mazingira, miundombinu na uzalishaji iwapo hatua stahiki za tahadhari hazitachukuliwa mapema.

“Wamiliki, mameneja na wakaguzi wa migodi wanapaswa kuboresha taratibu za usalama ili ziakisi hali ya mvua kubwa, kuongeza ukaguzi wa maduara na mabwawa ya kuhifadhia tope sumu, pamoja na kuhakikisha kila mgodi una mpango wa dharura unaoeleweka na kutekelezeka,” amesema.

Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wachimbaji wadogo katika maendeleo ya sekta ya madini na uchumi wa Taifa, hivyo maandalizi hayo ni muhimu ili shughuli za uchimbaji ziendelee kwa usalama na tija.

Eng. Samamba amesema miongoni mwa hatari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua kubwa ni kuporomoka kwa maduara na kuta za migodi kutokana na miamba kulainika na kupoteza uimara, mafuriko ndani ya migodi, kudhoofika kwa mihimili inayoshikilia miamba, pamoja na kufurika au kudhoofika kwa mabwawa ya kuhifadhia tope sumu.

Amesema pia mazingira yasiyo safi na maji yaliyotuama yanaweza kuongeza hatari za kiafya kwa wachimbaji na jamii zinazozunguka maeneo ya migodi.

 

Kwa mujibu wa Eng. Samamba, wamiliki, mameneja na wakaguzi wa migodi wanapaswa kuhakikisha hakuna mchimbaji anayeingia au kuendelea kufanya kazi chini ya ardhi wakati wa mvua kubwa au mara baada ya mvua kukatika iwapo hali ya eneo husika si salama.

 

Aidha, amewaagiza kuhakikisha maduara yanakaguliwa kila siku kabla ya kazi kuanza na sehemu zote dhaifu kuimarishwa kwa kutumia mihimili imara ya miti au chuma kulingana na mahitaji ya kiusalama.

 

Amesema mifereji inayozunguka midomo ya maduara na maeneo ya kazi inapaswa kujengwa na kusafishwa mara kwa mara, huku matuta, kingo, mawe na vifusi vikitumika katika maeneo yanayohitaji ulinzi ili kuzuia maji ya juu ya ardhi kuingia kwenye migodi.

 

“Kila mgodi unapaswa kuwa na pampu za kuvuta maji pamoja na mafuta ya kutosha ili kuwezesha kuchukua hatua za haraka endapo maji yatajaa kwenye mashimo,” amesema.

 

Kuhusu mabwawa ya kuhifadhia tope sumu (TSF), Eng. Samamba amewataka waendeshaji wa migodi kuhakikisha mabwawa hayo yana nafasi na uimara wa kutosha kupokea ongezeko la maji wakati wa mvua, huku ukaguzi wa kingo, mifereji, kiwango cha maji, dalili za kuvuja na mmomonyoko ukifanyika kwa wakati.

 

Amesema hatua hizo ni muhimu katika kuzuia madhara kwa binadamu, wanyama, mimea na mazingira.

 

Eng. Samamba pia amesisitiza kuzingatiwa kwa taratibu za usalama wakati wa ulipuaji, akielekeza kuhakikisha watu wote wanatoka katika eneo la tukio na kufika umbali salama kabla ya ulipuaji, na kurejea baada ya muda uliowekwa kwa mujibu wa taratibu za usalama.

 

Amesema zamu za wachimbaji zinapaswa kusimamiwa kwa kuzingatia uwezo wa watendaji ili kuzuia uchovu unaoweza kuongeza uwezekano wa kutokea kwa ajali.

 

Aidha, amewaelekeza Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo pamoja na Kanuni za Madini (Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira) za mwaka 2010, na kuchukua hatua stahiki pale ukiukwaji unapobainika.

Amesema ukaguzi wa mabwawa ya kuhifadhia tope sumu, maeneo ya kuhifadhi miamba taka na miundombinu mingine ya migodi unapaswa kuongezwa kabla na wakati wa mvua, huku kasoro zinazoweza kuhatarisha usalama zikishughulikiwa mara moja.

 

Amesisitiza kuwa kila mgodi unapaswa kuwa na mpango wa dharura unaoeleweka kwa watendaji, unaoainisha namna ya kutoa taarifa, kuokoa watu, kusimamisha shughuli pale inapobidi na kuwasiliana na mamlaka husika.

 

Aidha, amewataka viongozi wa vyama vya wachimbaji wa madini kutumia mitandao yao kutoa elimu kwa wanachama na kuwataka wachimbaji kufuatilia taarifa rasmi za hali ya hewa na kuzitumia katika kupanga shughuli zao za kila siku.

 

“Kaeni na wachimbaji, wasikilizeni hoja zao na mzitatue kwa kushirikiana. Tusifanye kazi kwa maelekezo pekee, bali kwa ushirikiano,” amesema.

 

Amesema usalama haupaswi kuchukuliwa kuwa gharama inayopunguza uzalishaji, kwa kuwa ajali inaweza kusababisha kusimama kwa shughuli za uchimbaji, kuharibu miundombinu, kuathiri mazingira na jamii na kusababisha kupoteza maisha.

 

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakaguzi wa Migodi Tanzania, Shija Mussa, amesema wachimbaji wadogo wanakabiliwa na changamoto ya maji kujaa kwenye mashimo wakati wa uchimbaji na kuiomba Serikali kusaidia upatikanaji wa mitambo mikubwa ya kunyonya maji (heavy-duty pumps) pamoja na vifaa vingine vya dharura.

 

Amesema mitambo hiyo inapaswa kuwekwa katika maeneo ya kimkakati ili iweze kutumika kwa haraka wakati wa dharura.

 

Awali, Mkurugenzi wa Leseni kutoka Tume ya Madini, Eng. Aziza Swedi, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Eng. Ramadhani Lwamo, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwapa wachimbaji wadogo

 elimu na uzoefu kuhusu namna ya kuchukua tahadhari dhidi ya athari za mvua kubwa.

 

Amesema Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Tume ya Madini imeamua kuchukua hatua mapema baada ya kutolewa kwa tahadhari ya mvua, ambapo wataalamu wanawasilisha mada kuhusu usalama wa migodi, mabwawa ya kuhifadhia tope sumu, maeneo ya kuhifadhi miamba taka, udhibiti wa mafuriko na mipango ya dharura.

 

Eng. Swedi amesema mafanikio ya mafunzo hayo yataonekana kupitia utekelezaji wa vitendo katika maeneo ya uchimbaji, akiwataka washiriki kurejea katika maeneo yao ya kazi, kufanya tathmini, kubaini maeneo hatarishi na kurekebisha kasoro kabla ya madhara kutokea.