Mambo Yalivyokuwa Katika Msiba na Maziko ya Haji Omari Ramadhani Mpili – (Picha + Video)

Global Publishers
September 29, 2026
906 views
0 Comments


Mambo yalivyokuwa katika msiba wa Haji Omari Ramadhani Mpili na maziko yake yaliyofanyika Septemba 28, 2026, katika Makaburi ya Msikiti Mkuu, Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

Maziko hayo yalifanyika majira ya saa 10:00 jioni, kufuatia kifo chake kilichotokea usiku wa Jumapili, Septemba 27, 2026, akiwa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri.

TANAPA Yasitisha Njia Mbili za Kupanda Mlima Kilimanjaro Baada ya Moto

Global Publishers
September 29, 2026
12 views
0 Comments

Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imesitisha kwa muda matumizi ya njia za Lemosho na Londorosi zinazotumiwa na watalii kupanda Mlima Kilimanjaro, kufuatia kuzuka kwa moto mpya wa porini ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa ya TANAPA, moto huo umeibuka katika eneo la Sangarini-Kamwanga na unaelekea upande wa Shira ndani ya hifadhi hiyo.

Kutokana na hali hiyo, watalii waliokuwa wamepanga kutumia njia za Lemosho na Londorosi wataelekezwa kutumia njia nyingine, ambazo ni Machame, Marangu au Rongai, hadi hapo hali ya moto itakapokuwa imedhibitiwa.

TANAPA imesema juhudi za kuuzima moto huo zinaendelea kwa ushirikiano na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori ya Enduimet, vikosi vya akiba, wananchi wa maeneo yanayozunguka hifadhi pamoja na wadau wengine wa utalii.

Moto huo umeibuka wiki chache baada ya moto mwingine kuripotiwa Septemba 3 katika eneo la Kikererwa, karibu na mpaka wa Tanzania na Kenya. Moto huo wa awali ulidhibitiwa kwa zaidi ya asilimia 90 kufikia Septemba 5.

TANAPA imeeleza kuwa usalama wa watumishi, watalii na wadau wengine unaendelea kuwa kipaumbele, huku rasilimali zilizopo zikielekezwa katika juhudi za kudhibiti na kuzima moto huo.

Kesi ya Uhaini ya Lissu: Jamhuri Kuanza Mawasilisho ya Mwisho Leo

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo Septemba 29, 2026, inatarajiwa kuanza kusikiliza mawasilisho ya mwisho ya upande wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu .

Mawasilisho hayo yanatarajiwa kuwasilishwa na Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, baada ya Lissu kukamilisha mawasilisho yake ya mwisho jana, Septemba 28, mbele ya jopo la majaji watatu.

Kesi hiyo, yenye namba 19605/2025, inasikilizwa na jopo linaloongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, likiwa na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Katika mawasilisho yake, Lissu aliiomba Mahakama kuangalia kama upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha kosa linalomkabili kwa kiwango kinachotakiwa katika kesi za jinai, yaani bila kuacha shaka yenye msingi.

Lissu pia alitoa kauli kwamba iwapo majaji wataona kuwa kosa la uhaini limethibitishwa, watoe hukumu kwa mujibu wa sheria, na iwapo hawatabaini kuwa kosa hilo limethibitishwa, wamwachie huru.

Katika hoja zake, Lissu alipinga kwa kina ushahidi wa upande wa Jamhuri, akiwemo ushahidi kuhusu mkutano wa Aprili 3, 2025, tafsiri ya maneno anayodaiwa kuyasema, pamoja na hoja kuhusu kama maneno hayo yanaweza kisheria kuunda kosa la uhaini.

Baada ya upande wa Jamhuri kukamilisha mawasilisho yake, hatua inayofuata itakuwa Mahakama kutathmini hoja na ushahidi uliowasilishwa na pande zote kabla ya kutoa uamuzi kwa mujibu wa sheria.

Usichokijua Kuhusu Mercedes G-Wagon na Aina na Bei Zake

Global Publishers
September 29, 2026
6,804 views
0 Comments

Mercedes-Benz G-Class, inayojulikana zaidi kama G-Wagon, ni moja ya SUV za kifahari zinazoibuka duniani. Gari hili ni mchanganyiko wa nguvu, uimara na kifahari, na ni ikoni inayojulikana kwa muundo wake wa “boxy” na utambulisho wa kipekee barabarani.

Mtengenezaji

G-Wagon inatengenezwa na Mercedes-Benz, kampuni ya Ujerumani inayojulikana kwa magari ya kifahari na teknolojia za kisasa za magari.

Asili na Historia

  • G-Class ilianza mwaka wa 1979 kama gari la kijeshi la Ujerumani, linaloweza kupita milima, matope na barabara ngumu.

  • Muundo wake wa “boxy” haujabadilika kwa zaidi ya miongo 40, jambo ambalo limeiweka ikoni duniani kote.

Uwezo wa Ajabu

  • Off-Road: Mfumo wa 4MATIC (4WD) na differential locks tatu (mbele, kati, nyuma) unaifanya ipite migodi, milima na mito bila shida.

  • Ndani ya Kifalme: Ngozi ya Nappa, ambient lighting, skrini kubwa za MBUX na mfumo wa sauti wa Burmester.

  • Usalama: Lane assist, adaptive cruise control, camera za 360°, airbags nyingi.

Aina Maarufu za G-Wagon

    1. G 500 / G 550

      • Injini ya V8 yenye nguvu ya kutosha

      • Luxury na utulivu kwa matumizi ya kila siku

      • Bei  ya G 500 / G 550 Mpya: TSh 350 – 420 milioni

      • Iliyotumika: TSh 230 – 300 milioni

    2. G 63 AMG

      • Twin-turbo V8 yenye horsepower kubwa (>570 HP)

      • Sauti kali ya injini na muonekano wa kipekee

      • Maarufu kwa mastaa na wapenzi wa magari ya nguvu

      • Bei Mpya: TSh 450 – 550+ milioni

      • Iliyotumika: TSh 300 – 400 milioni

  1. Mercedes-Maybach G-Class

    • Ultra-luxury, vipengele vya kifahari zaidi, viti vya nyuma vya kifalme

    • Limited edition, kwa wapenzi wa hadhi ya juu

    • Bei Mpya: TSh 900 milioni – 1.2+ bilioni

 Sababu ya Umaarufu

  • Hadhi ya kifahari na utambulisho wa kipekee

  • Uwezo mkubwa wa kupita barabara zote, kutoka miji hadi maeneo magumu

  • Muundo wa kijeshi ulio na historia ndefu

  • Kila mmoja anayemiliki anaonekana kama mfanikaji

Mambo Yalivyokuwa Katika Msiba na Maziko ya Haji Omari Ramadhani Mpili – Picha

Global Publishers
September 29, 2026
90 views
0 Comments

Mambo yalivyokuwa katika msiba wa Haji Omari Ramadhani Mpili na maziko yake yaliyofanyika Septemba 28, 2026, katika Makaburi ya Msikiti Mkuu, Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani.

Maziko hayo yalifanyika majira ya saa 10:00 jioni, kufuatia kifo chake kilichotokea usiku wa Jumapili, Septemba 27, 2026, akiwa anapatiwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri.

Sababu 10 za Maumivu ya Tumbo Kwa Wajawazito Wakati wa Miezi Mitatu ya Kwanza

WAJAWAZITO wengi huugua wakati wakiwa na ujauzito. Zipo Sababu zinazofanya kutokea kwa maumivu ya tumbo wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya mimba.

Kuna matatizo mengi ambayo yanahusiana tu na mimba, hata hivyo ni muhimu kukumbuka kwamba hali yoyote ambayo husababisha maumivu kwa mgonjwa asiyekuwa na ujauzito inaweza pia kutokea kwa mama mjamzito.

Tofauti kati ya watu hao wawili hupatikana baada ya uchunguzi. Maumivu ya tumbo kwa mjamzito ni changamoto kwa sababu wengi hupatwa na  kichefuchefu, kutapika na maumivu ya tumbo hujitokeza mara nyingi. Mfuko wa uzazi unapotanuka unaweza kusukuma  viungo vingine kando ndani ya tumbo.

Upungufu wa damu na leukocytosis ni  kawaida katika mimba ya kawaida na si viashiriwa vya upungufu wa damu au maradhi.

Kiinitete kinapojipandikiza katika kuta za ndani za mfuko wa uzazi kinaweza kusababisha maumivu ya tumbo, ambayo huchukua muda wa siku mbili au tatu na kiasi kidogo cha damu ukeni hutoka. Mara nyingi kiasi hiki cha damu huwa ni kidogo na hutokea kati ya siku saba au 12 baada ya tarehe inayohisiwa mimba kutungwa, mara nyingi kipindi hiki hukaribiana na siku ambayo mwanamke alikuwa anatarajiwa kuingia hedhi.

Hivyo, wagonjwa  mara  nyingi hufanya makosa kwa kufikiri kuwa wameingia katika siku zao kama kawaida. Mimba iliyotunga nje ya mfuko Tatizo hili husababisha maumivu kwa akina mama wengi walio na mimba nje ya mfuko wa mimba. Tatizo hili linaweza kubainika kwa kutumia Ultrasounda na kipimo cha homoni cha HCG.

Uzuri ni kwamba tatizo hili linatibiwa kama dharura kwa mama kufanyiwa upasuaji. Kutoka kwa mimba Mimba inaweza kutoka yenyewe au kutolewa kwa makusudi. Tatizo hili huambatana na maumivu pamoja na kuvuja damu. Utoaji wa mimba usiokuwa salama unaongoza kusababisha vifo vya akina mama katika nchi zinazoendelea. Uvimbe kwenye mirija ya mayai (Ovarian cyst) Wakati mwingine uvimbe huu hupasuka au kujizungusha.

Hata hivyo, unaweza kupungua na usipopungua unaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hasa wakati wa muhula wa pili wa ujauzito. Kujizungusha kwa mirija ya mayai (Ovarian torsion) Hii hujitokeza mara chache. Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi pia husababisha maumivu hasa unapokuwa mkubwa. Tatizo hili linaweza kusababisha ujauzito kutoka hasa katika miezi ya awali.

Kidole tumbo (Appendicitis) Kidole tumbo hujitokeza kwa uwiano sawa kama wanawake ambao hawana ujauzito. Matibabu ya ugonjwa huu ni upasuaji. Mara nyingi wanawake wengi hupata uchungu baada ya upasuaji. Mawe kwenye mfuko wa nyonga Lakini pia kutokana na mabadiliko ya homoni wanawake wengi hupata tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo.

Tatizo hii huweza kugunduliwa kwa njia ya kupimwa na kipimo cha Ultrasound na matibabu yake hutegemea na dalili alizonazo mgonjwa. Uvimbe (Inflammation) kwenye mfuko wa nyongo Hili ni tatizo la ghafla linalosababisha maumivu makali ambalo pia hujitokeza wakati mwanamke ana mimba. Tatizo hili mara nyingi husababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo.

Matibabu yake hutumika dawa za kuua bakteria yaani Antibiotics. Wanawake wengi wakati wa hujauzito hupata maambukizi kwenye njia ya mkonjo mara kwa mara. Hii ni kutokana na mabadiliko yanayojitokeza wakati wa mimba. Sababu nyingine ya maumivu husababishwa na Round Ligament.

Ligament hii ndiyo inayoshikilia mfuko wa uzazi. Mfuko wa uzazi unavyozidi kukua, ligament hii huvutika na kusababaisha maumivu.

Dawa za maumivu husaidia kwa tatizo hili. Ultrasound hutumika katika uchunguzi wa maumivu ya tumbo wakati wa ujauzito. Kongosho, mfuko wa nyongo na kidole tumbo vyote huonekana  kwa mama mjamzito. Vipimo vinavyotumia mionzi vitumike tu pale inapohitajika kwa mama mjamzito.

Fahamu Tatizo la Vidonda vya Tumbo kwa Mjamzito

MJAMZITO anaweza kupata vidonda vya tumbo kabla au baada ya ujauzito.  Umakini unahitajika sana katika kumchunguza mama mjamzito ili kuelewa nini kitakuwa ndiyo chanzo cha vidonda vya tumbo kwake. Mwanamke ambaye ulikuwa unaumwa vidonda vya tumbo hata kabla ya kushika ujauzito unaweza kuendelea kutumia baadhi ya dawa rafiki za kutibu au kuzuia dalili za vidonda vya tumbo hata baada ya kuwa umepata ujauzito.

Kwa kawaida, kila dawa huwa na matokeo ya aina mbili yaani matokeo chanya (uponyaji) na matokeo hasi (uharibifu) na matokeo hasi yanapozidi huweza kusababisha hata kifo. Moja ya matokeo hasi ya matumizi mabaya ya dawa za kutibu vidonda vya tumbo kwa kina mama wajawazito ni pamoja na mtoto kuzaliwa kilema, mtoto kufia tumboni na hata kifo kwa mama.

Wakati wa ujauzito, mama mjamzito anaweza kutokewa na kiungulia mara kwa mara na hata kiasi cha asidi kuongezeka mwilini. Ni wakati huu mwanamke anaweza kuanza kutafuta matibabu kwa ajili ya vidonda vya tumbo na ndipo umakini mkubwa unapohitajika. Hivyo, dawa rafiki, yaani dawa ambazo hazina madhara hasi, ndizo zitumike kwa ajili ya mama mjamzito hasa katika kipindi cha majuma 10 ya kwanza ya ujauzito.

Licha ya kwamba dalili za vidonda vya tumbo hutoweka wakati wa ujauzito kwa wanawake wengi, baadhi ya wanawake hulalamika kuwa na maumivu makali. Hii kwa kawaida hutokea kwa wanawake ambao maumivu ya vidonda vya tumbo yalikuwa makali walipokuwa si wajawazito.

Kama nilivyosema hapo juu, kina mama wengi wanaweza kujihisi wamepona kabisa vidonda vya tumbo wakati wanapata ujauzito au wakati wote wa kipindi cha ujauzito, ingawa baadhi yao hutokewa na maumivu makali hata wakati wa ujauzito, na hii inatokea kwa wale ambao hata kabla ya kupata ujauzito walikuwa wakipatwa na maumivu hayo makali.

Hivyo bado nashauri wakati huu wa ujauzito mama apewe dawa rafiki tu hasa zile zitokanazo na vyakula na mimea hadi hapo atakapojifungua. Wakati huohuo kuwa makini kutokutumia vyakula au vinywaji vyenye asidi nyingi.

Kwa kawaida vidonda vya tumbo huzalisha dalili chache pindi tumbo linapokuwa halina kitu, inashauriwa mjamzito asikae muda mrefu bila kula chakula na ale mlo mdogomdogo ili chakula kiendelee kukaa tumboni.

Mjamzito pia aepuke kula kupita kiasi kwa sababu kula kupita kiasi huchochea uzalishwaji wa asidi nyingi tumboni. Kadhalika, chakula kinapokuwa kingi tumboni hulifanya tumbo kujitandaza sana, na hatimaye kuchokoza vidonda.

Mjamzito aepuke kunywa maziwa. Watu wengi hudhani kwa kuwa maziwa hutumika kumpatia mtu mwenye tatizo la sumu mwilini, basi yanaweza pia kudhibiti kiasi cha asidi tumboni hasa yakitumika kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo. Hili si kweli, tafiti za kitaalamu za hivi karibuni zinathibitisha kwamba maziwa yasitumike kwa mtu mwenye tatizo la vidonda vya tumbo.

Muhimu kuliko yote ni kutambua kuwa vidonda vya tumbo vinatibika kabisa, unachohitaji ni kuufahamu hasa ugonjwa wenyewe huletwa na nini hasa mwilini na namna ya kuishi kwa maana ya kula na kunywa na hatimaye uponyaji ufanyike. Dawa peke yake bila kujua nini ule na kunywa hazitasaidia uponyaji wa vidonda vya tumbo.

USHAURI

Kama wewe ni mjamzito una vidonda vya tumbo na una ujauzito ni vema kuwasiliana na wataalamu wa afya ili wakuelekeze utumie dawa gani na nini cha kufanya ili afya yako iwe imara. Usinywe dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu na mtaalamu wa afya kwa sababu kuna dawa hazipaswi kunywewa na wajawazito. Kwa ushauri zaidi wasiliana nami kwa namba hiyo ya simu.

Naibu Mkurugenzi wa FBI Andrew Bailey Ajiuzulu Ghafla

WASHINGTON, Septemba 28, 2026 — Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Andrew Bailey, ametangaza kujiuzulu nafasi yake baada ya kuhudumu katika taasisi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Bailey amesema uamuzi wake wa kuondoka FBI umetokana na sababu za kifamilia, akieleza kuwa anataka kurejea kuwa karibu na familia yake.

Bailey, ambaye ni mshirika wa kisiasa wa Rais wa Marekani Donald Trump, alijiunga na FBI baada ya kuondoka katika nafasi yake ya Mwanasheria Mkuu wa Missouri. Katika kipindi chake FBI, alishiriki katika kusimamia uchunguzi mbalimbali, ukiwemo unaohusiana na masuala ya uchaguzi.

Awali mwaka huu, Bailey alikuwepo wakati mawakala wa FBI walipotekeleza hati ya upekuzi na kuchukua kura za uchaguzi wa mwaka 2020 katika jimbo la Georgia, katika hatua iliyohusishwa na uchunguzi wa masuala ya uchaguzi.

Katika ujumbe wake wa kujiuzulu, Bailey alieleza kuwa ana imani Mkurugenzi wa FBI, Kash Patel, ataendelea na juhudi za kuifanyia mageuzi taasisi hiyo, kupambana na uhalifu wa kutumia nguvu, kulinda usalama wa taifa na kuimarisha uwajibikaji ndani ya shirika.

Nafasi ya Naibu Mkurugenzi wa FBI kwa kawaida imekuwa ikishikiliwa na maafisa wa muda mrefu wa taasisi hiyo, huku majukumu yake yakihusisha kusimamia shughuli za kila siku za utekelezaji wa sheria. Hata hivyo, katika kipindi cha utawala wa Trump, nafasi hiyo imehusishwa zaidi na uteuzi wa watu wenye uhusiano wa kisiasa na utawala.

Bailey awali alihudumu kama mmoja wa Manaibu Wakurugenzi wawili wa FBI pamoja na Dan Bongino, ambaye baadaye aliondoka katika taasisi hiyo. Christopher Raia, afisa mkongwe wa FBI, kwa sasa ni sehemu ya timu ya uongozi pamoja na Bailey na Patel.

Kujiuzulu kwa Bailey kunatokea takribani wiki tano kabla ya uchaguzi wa katikati ya muhula nchini Marekani, ambao utaamua udhibiti wa Bunge la Congress.

Katika kipindi cha uongozi wake, FBI imeendelea kuchunguza masuala mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi katika majimbo kadhaa. Hata hivyo, uchunguzi huo haujaonyesha ushahidi unaothibitisha madai ya Rais Trump kwamba udanganyifu mkubwa wa wapiga kura uliathiri matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

TRA Yabaini Utata wa G-Wagon ya Ommy Dimpoz, G350 Yageuka G63

Global Publishers
September 29, 2026
0 views
0 Comments

Mercedes-Benz G-Class G350

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imebaini tofauti kubwa kati ya taarifa za forodha na hali halisi ya gari aina ya Mercedes-Benz G-Wagon linalohusishwa na msanii Omary Faraji Nyembo, maarufu kama Ommy Dimpoz. Kwa mujibu wa taarifa ya TRA iliyotolewa, Septemba 28, 2026, gari hilo lilikutwa Septemba 26 katika eneo la Palm Beach Casino jijini Dar es Salaam, likiwa halina namba za usajili, wakati operesheni ya mamlaka hiyo ikiendelea kufuatilia ukwepaji wa kodi za magari.

TRA imesema namba ya utambulisho wa gari hilo (VIN) ni WDB4632762X322756, huku nyaraka za awali za forodha zikilitaja kama Mercedes-Benz G-Class G350 ya mwaka 2020. Hata hivyo, mamlaka hiyo imeeleza kuwa baada ya kufanya uhakiki wa kisayansi na uchunguzi wa Forensic, ilibaini kuwa gari hilo ni Mercedes-Benz AMG G63 ya mwaka 2018.

TRA imeongeza kuwa tofauti hiyo inaashiria uwezekano wa taarifa za gari kuwasilishwa kwa namna ambayo ingeweza kupunguza thamani ya gari katika uthamini wa forodha na hivyo kupunguza kiwango cha kodi kilichopaswa kulipwa.