Qwaray atoa maagizo kero za wananchi – HabariLeo

SIMANJIRO. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, amewataka waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuhakikisha changamoto za kiutumishi zinashughulikiwa kwa wakati ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Qwaray ametoa agizo hilo wakati wa kikao kazi cha kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.

Amesema waajiri wanapaswa kuhakikisha stahiki za watumishi, ikiwemo kupandishwa vyeo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara na mafao, zinashughulikiwa kwa wakati kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Aidha, amesisitiza kuwa madai ya watumishi yanapaswa kuhakikiwa na kuwasilishwa yakiwa yameambatanishwa na nyaraka muhimu ili kurahisisha utatuzi wa changamoto hizo.

Qwaray amezitaka Mamlaka za Ajira na Nidhamu kusimamia haki na wajibu wa watumishi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, akisisitiza umuhimu wa kuacha utendaji wa mazoea.

Amesema mambo yaliyo ndani ya uwezo wa waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu yanapaswa kushughulikiwa katika ngazi hizo badala ya kuendelea kuwasilishwa Ofisi ya Rais.

Kuhusu maadili ya utumishi wa umma, Qwaray amewataka watumishi kuyafahamu na kuyatekeleza kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.

“Watumishi wanaokiuka maadili au kutotekeleza majukumu yao ipasavyo wanapaswa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu kwa wakati,” amesema.

Aidha, amewataka waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kushirikiana na Tume ya Utumishi wa Umma katika ukaguzi wa utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi na kuhakikisha mapungufu yatakayobainika yanarekebishwa kwa wakati.

Qwaray atoa maagizo kero za wananchi – HabariLeo

SIMANJIRO. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, amewataka waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuhakikisha changamoto za kiutumishi zinashughulikiwa kwa wakati ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Qwaray ametoa agizo hilo wakati wa kikao kazi cha kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.

Amesema waajiri wanapaswa kuhakikisha stahiki za watumishi, ikiwemo kupandishwa vyeo, uhamisho, malimbikizo ya mishahara na mafao, zinashughulikiwa kwa wakati kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Aidha, amesisitiza kuwa madai ya watumishi yanapaswa kuhakikiwa na kuwasilishwa yakiwa yameambatanishwa na nyaraka muhimu ili kurahisisha utatuzi wa changamoto hizo.

Qwaray amezitaka Mamlaka za Ajira na Nidhamu kusimamia haki na wajibu wa watumishi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, akisisitiza umuhimu wa kuacha utendaji wa mazoea.

Amesema mambo yaliyo ndani ya uwezo wa waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu yanapaswa kushughulikiwa katika ngazi hizo badala ya kuendelea kuwasilishwa Ofisi ya Rais.

Kuhusu maadili ya utumishi wa umma, Qwaray amewataka watumishi kuyafahamu na kuyatekeleza kwa kuzingatia Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.

“Watumishi wanaokiuka maadili au kutotekeleza majukumu yao ipasavyo wanapaswa kuchukuliwa hatua stahiki za kinidhamu kwa wakati,” amesema.

Aidha, amewataka waajiri na Mamlaka za Ajira na Nidhamu kushirikiana na Tume ya Utumishi wa Umma katika ukaguzi wa utekelezaji wa sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi na kuhakikisha mapungufu yatakayobainika yanarekebishwa kwa wakati.

Cheza, Panda Kwenye Msimamo na Ushinde Milioni 5

Global Publishers
September 30, 2026
48 views
0 Comments

Burudani mpya imefika kwa wapenzi wa Kasino Meridianbet. Ni Cash Storm Tournament kutoka Expanse, mashindano yanayokupa wiki mbili za burudani mfululizo za kasino kuanzia Septemba 26 hadi Oktoba 8, 2026. Sasa ni wakati wa kuchagua sloti yako inayoshiriki na kuanza safari ya kuwania nafasi nzuri kwenye msimamo.

Kuanza ni rahisi zaidi kuliko unavyofikiria. Kwa kiasi cha kuanzia Tsh. 500 kwa mzunguko, chagua mchezo unaoupenda na anza kucheza. Kila unaposhiriki, pointi zako zinaendelea kukusanywa na kukusaidia kufuatilia safari yako kwenye msimamo.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Na safari hii ina zawadi kubwa mwisho wake. Jumla ya Tsh. 5,000,000 imetengwa kwa ajili ya wachezaji 20 bora. Hivyo, kila mchezaji ana nafasi ya kufuatilia nafasi yake wakati mashindano yakiendelea na kuona namna anavyosogea kwenye orodha ya washiriki.

Cash Storm imeleta sababu nyingine ya kufurahia sloti kupitia Meridianbet. Ni wiki mbili za mpambano wa kasino, ushindani wa msimamo na nafasi ya kuwania sehemu ya zawadi kubwa. Chagua mchezo wako, ingia kwenye mashindano na uendelee kufuatilia safari yako hadi siku ya mwisho.

Meridianbet ndiyo sehemu ya kuanzia safari ya Cash Storm. Anza kucheza kuanzia Tsh. 500, kusanya pointi zako na fuatilia msimamo hadi Oktoba 8, 2026. Tsh. 5,000,000 inasubiri wachezaji 20 bora, chagua sloti yako na uanze safari leo.

Eritrea Kuikaribisha Afrika Kusini Katika Mchezo Wa Kufuzu Afcon 2027

Hatimaye ile siku ya kutusua imewadia na timu kibao zimejiandaa kwaajili ya kukupatia maokoto ya maana. Je nani unampa nafasi kubwa ya kuondoka na ushindi?. Ingia kwenye akaunti yako na ubeti sasa.

Michuano ya kufuzu AFCON 2027 itaendelea ambapo Eritrea atamleta kwake Afrika Kusini huku timu zote mbili ukiuangalia mchezo huu kwa jicho tofauti sana kwani wote wawili wanahitaji kupata ushindi mnono hapa.

Vijana hao wa Mosimane, Afrika Kusini wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa na pointi 3 baada ya kuifunga Guinea kwa mabao  2-1, huku Eritrea wao walianza kampeni yao i kwa kupata sare ya 1-1 dhidi ya Kenya Nairobi.

Kwa Eritrea, sare dhidi ya Kenya ilikuwa matokeo yaliyowapa nguvu kubwa kisaikolojia. Kenya ililazimika kusubiri hadi dakika ya 87 kusawazisha goli hilo. Hii inaonyesha kwamba Eritrea si timu inayopaswa kuangaliwa kwa ukubwa wa jina pekee. Bashiri hapa.

Mkwanja wa maana upo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Afrika Kusini inaweza kuwa na faida ya kisaikolojia kwa sababu imeanza kampeni kwa ushindi dhidi ya mmoja wa wapinzani wake wakuu wa kundi. Lakini mchezo wa Eritrea utakuwa tofauti. Guinea ilicheza kwa ujasiri na kuilazimisha Bafana Bafana kufanya kazi kwa nguvu, wakati Eritrea inaweza kuwa na mpango wa kujilinda kwa kina zaidi na kusubiri muda sahihi wa kushambulia.

Kwa hiyo, Eritrea haitahitaji kuingia kwenye mchezo wa kushambuliana bila mpangilio. Itahitaji kuwa na subira, kulinda eneo la mbele ya mabeki na kuhakikisha kwamba kila mpira wanaoupata wakati wa kuvunja mashambulizi ya Afrika Kusini unatumiwa kwa ufanisi. Jisajili hapa.

Takwimu zinasema eneo la kiungo linaweza kuwa sehemu muhimu zaidi ya mchezo huu. Afrika Kusini ikifanikiwa kutawala kiungo, kusogeza mpira kwa kasi na kuwafanya wachezaji wa Eritrea kurudi nyuma, inaweza kutumia muda mwingi ikiwa kwenye nusu ya uwanja ya mpinzani.

Pia Eritrea ikifanikiwa kukata njia za pasi na kuzuia Bafana Bafana  kupata nafasi kati ya mistari, mchezo unaweza kuwa wa kusubiri sana. Hapo ndipo Afrika Kusini itahitaji uvumilivu kwa sababu kulazimisha pasi za hatari kunaweza kuipa Eritrea nafasi ya kushambulia kwa kushtukiza.

Je nani anaweza akaondoka na ushindi kwenye mechi hii leo?. Ingia kwenye akaunti yako na usuke jamvi lako hapa.

Sekretarieti ya Ajira Yatangaza Nafasi ya Afisa Sheria Mwandamizi

Global Publishers
September 30, 2026
66 views
0 Comments

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza nafasi moja (1) ya kuhamia ya Afisa Sheria Mwandamizi, kwa Watanzania ambao ni watumishi wa Umma wenye sifa na uwezo.

Majukumu ya nafasi hiyo ni pamoja na kutoa ushauri na msaada wa kisheria kwa Sekretarieti ya Ajira, kutoa mapendekezo ya maboresho katika uandaaji wa miswada ya sheria na sheria ndogo, kufuatilia mashauri yaliyopo mahakamani, pamoja na kusimamia uandaaji na mapitio ya nyaraka mbalimbali za kisheria.

Sifa za mwombaji:
Mwombaji anatakiwa kuwa mtumishi wa Umma mwenye Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) kutoka taasisi inayotambuliwa na Serikali, akiwa na uzoefu wa kazi usiopungua miaka saba katika eneo husika. Pia anatakiwa kuwa amehudhuria na kufaulu mafunzo ya uanasheria kwa vitendo au Shule ya Sheria Tanzania, pamoja na kusajiliwa kama wakili wa Mahakama Kuu.

Aidha, mwombaji anatakiwa kuwa mtumishi wa Umma aliyefanya kazi kwa mwajiri wake wa sasa kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu na awe tayari kugharamia gharama za uhamisho.

Waombaji wanapaswa kuambatisha CV yenye maelezo ya kina, vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa, cheti cha kuzaliwa, pamoja na majina ya wadhamini watatu. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na mamlaka husika.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Oktoba 2026. Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia Recruitment Portal ya Ajira.

Urusi Yashambulia Miundombinu ya Nishati Ukraine, Watu Wanne Wauawa Kyiv

KYIV: Mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani na makombora kutoka Urusi yameua watu wanne katika mji wa Kyiv na maeneo ya jirani, huku miundombinu ya nishati ikiharibiwa na mji huo kufunikwa na moshi.

Kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine, wanawake wawili na mtoto mwenye umri wa miaka 14 waliuawa katika mashambulizi ya usiku yaliyolenga Kyiv na mji mmoja uliopo kaskazini mwa mji huo. Mtu mwingine aliuawa katika shambulio dhidi ya ghala moja jijini Kyiv.

Jeshi la Anga la Ukraine limesema Urusi ilitumia makombora ya balistiki na ya kuzuia meli pamoja na ndege zisizo na rubani 188. Ukraine inadai kuwa ilifanikiwa kuzuia makombora matano na ndege hizo zisizo na rubani 155.

Mashambulizi hayo pia yamelenga miundombinu ya nishati katika eneo la Kyiv, wakati Ukraine ikijiandaa kwa msimu mwingine wa baridi. Kampuni ya nishati ya DTEK imesema wafanyakazi wake wamefanikiwa kurejesha huduma ya umeme kwa kaya 8,000, ingawa haikutoa taarifa kamili kuhusu kiwango cha uharibifu.

Urusi imethibitisha kufanya mashambulizi hayo makubwa ya usiku, ikisema imelenga kituo cha data kinachosaidia majeshi ya Ukraine, mitambo mbalimbali ya kuzalisha umeme katika eneo la Kyiv, kituo cha viwanda katika eneo la Odesa na miundombinu ya bandari ya Izmail.

Huko Kyiv, moshi mzito ulitanda katika maeneo mbalimbali kufuatia mashambulizi hayo, huku huduma za dharura zikiwataka wakazi kufunga madirisha ili kujilinda dhidi ya moshi.

Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko, amesema mabaki ya kifaa kilichotumika katika shambulio yalipatikana katika eneo la ubalozi wa nchi ya Magharibi katikati ya jiji, ingawa hakutaja ubalozi huo ni wa nchi gani.

Mashambulizi hayo pia yameleta taharuki katika nchi jirani. Moldova imesema ndege isiyo na rubani ilivuka anga lake na kulipuka karibu na kijiji cha Hirbovet, huku Romania na Poland zikirusha ndege za kijeshi kufuatilia hali hiyo.

Poland pia ilisimamisha kwa muda safari za ndege katika viwanja vya Lublin na Rzeszow.

Wakati huo huo, Ukraine imeendelea kufanya mashambulizi ndani ya Urusi, yakilenga miongoni mwa mengine mitambo ya kusafisha mafuta na maeneo yanayohusishwa na shughuli za kiuchumi za Moscow.

Maafisa wa Urusi wamesema mtu mmoja aliuawa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika eneo la Bryansk, linalopakana na Ukraine. Mashambulizi mengine ya Ukraine katika eneo la Samara, linalozalisha mafuta, yaliripotiwa kusababisha uharibifu katika baadhi ya nyumba.

England Yaichapa Czechia, Yamal Aongoza Hispania Kuifunga Croatia

Global Publishers
September 30, 2026
456 views
0 Comments

England na Hispania zimeendelea kuonyesha uwezo katika UEFA Nations League baada ya kupata ushindi dhidi ya Czechia na Croatia mtawalia.

England iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Czechia, huku Anthony Gordon na nahodha Harry Kane wakiwa miongoni mwa wachezaji walioipa timu hiyo matokeo hayo.

Gordon alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 47, kabla ya Kane kuongeza bao la pili dakika ya 69 na kuipa England ushindi wa 2-0.

Ushindi huo umeendelea kuonyesha kiwango kizuri cha Kane, ambaye kwa mujibu wa takwimu zilizotajwa amefikisha mabao manane katika michezo saba iliyopita.

Gordon naye ameendelea kufanya vizuri baada ya kufunga katika michezo miwili mfululizo akiwa na timu ya taifa ya England.

Katika mchezo huo, Trent Alexander-Arnold alirejea kwenye kikosi cha kwanza na kutoa assist iliyomaliziwa kwa bao la Gordon.

Kwa upande wa Hispania, Lamine Yamal alikuwa nyota wa mchezo baada ya kuhusika moja kwa moja katika mabao matatu wakati timu hiyo ikiichapa Croatia kwa mabao 4-1.

Yamal alifungua akaunti dakika ya pili, kabla ya Marc Pubill kuongeza bao la pili dakika ya 31. Croatia ilipata bao la kufutia machozi kupitia Dion Drena Beljo dakika ya 28.

Kipindi cha pili, Yamal alifunga bao lake la pili dakika ya 63 na kukamilisha brace, kabla ya Nico Williams kufunga bao la nne dakika ya 89 na kuhitimisha ushindi wa Hispania.

Mbali na mabao yake mawili, Yamal pia alitoa assist kwa bao la Pubill, hivyo kuhusika moja kwa moja katika mabao matatu ya Hispania.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotajwa, Yamal amefikisha michango 18 ya mabao (G/A) katika michezo yake nane iliyopita, huku akiendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wanaoangaziwa zaidi katika kikosi cha Hispania.

Stori na Didas Didas | GPL -TUDACO

TANZANIA ITAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA UWEKEZAJI KUKUZA BIASHARA NA OMAN— LONDO

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesisitiza utayari wa kuendelea kuweka mazingira bora na rafiki ya uwekezaji ili kukuza sekta ya biashara na kuleta manufaa ya kiuchumi kwa wananchi wa Tanzania na Usultani wa Oman. 

Hayo  yameelezwa Septemba 29, 2026 na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb.), alipotembelea ofisi za Wekeza Oman na kuzungumza na Naibu Waziri wa  Biashara, Viwanda na Kukuza Uwekezaji (MoCIIP) anayeshughulikia Biashara na Viwanda Mhandisi Ghalib Al Maamari, mjini Muscat.

Mhe. Londo alieleza kuwa ingawa takwimu za biashara kati ya nchi hizo mbili zimekua kutoka Dola za Marekani Milioni 18 mwaka 2017 hadi kufikia Dola Milioni 160.8 mwaka 2025, Tanzania imejipanga kuondoa vikwazo vya kiuwekezaji na kutumia nafasi yake ya kimkakati kijiografia kufungua masoko mapya.

Akiwasilisha fursa zilizopo Tanzania, Mhe. Londo alibainisha kuwa Tanzania inatoa lango kuu la kibiashara linaloiunganisha Oman na soko kubwa la zaidi ya watu Milioni 700 katika Ukanda wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Afrika (SADC). 

“Tunawakaribisha kuwekeza katika Sekta mbali mbali ikiwemo machinjio ya kisasa, uchakataji wa nyama na mazao ya baharini,  pamoja na kilimo cha biashara ili kuimarisha salama  wa chakula na kuongeza kiasi cha bidhaa za Tanzania zinazouzwa katika soko la Oman na Nchi za Ghuba” Alisema Mhe. Londo

Kwa Upande wake Mhandisi Al Maamari ameelezea nia ya Oman kuendelea kuwekeza Tanzania katika Sekta mbalimbali za Kimkakati kwa manufaaa ya mataifa yote mawili.

Mbali na Mazungumzo hayo, Mhe. Londo ametembelea ofisi za Mamlaka ya Uwekezaji Oman (OIA) na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Idara hiyo Mhe. Mulham bin Basheer Al Jarf. Mazungumzo Yao yalijikita katika kubadili uhusiano baina ya Tanzania na Oman kutoka undugu wa kihistoria pekee na kuwa ushirika wa kiuchumi wenye manufaa kwa pande zote mbili kupitia kuanzisha miradi ya ushirikiano wa pamoja.

 

Hukumu ya Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu Kusomwa Novemba 6, 2026

Global Publishers
September 30, 2026
0 views
0 Comments

DAR ES SALAAM: Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imepanga kusoma hukumu ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, Novemba 6, 2026 saa 3:00 asubuhi.

Uamuzi huo umetangazwa Jumanne, Septemba 29, na Jaji Dunstan Ndunguru, anayeongoza jopo la majaji watatu linalosikiliza shauri hilo lenye namba 19605/2025. Majaji wengine ni James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Jaji Ndunguru amesema jopo hilo linahitaji muda wa kupitia kwa kina ushahidi uliowasilishwa na pande zote pamoja na hoja zao za mwisho kabla ya kutoa uamuzi.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa Jamhuri kukamilisha mawasilisho yake ya mwisho. Katika hoja zake, upande wa mashtaka uliliambia Mahakama kuwa unaamini umeweza kuthibitisha shtaka dhidi ya Lissu kwa kiwango kinachotakiwa katika kesi ya jinai.

Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Kanuni ya Adhabu, likihusishwa na kauli anazodaiwa kutoa Aprili 3, 2025 kuhusu kuzuia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Upande wa utetezi umepinga tafsiri ya mashtaka hayo na umehoji iwapo kauli zinazodaiwa kutolewa zinaweza kisheria kuthibitisha kosa la uhaini.

Awali, Agosti 21, 2026, Mahakama Kuu iliamua kwamba Lissu ana kesi ya kujibu, hatua iliyomruhusu kuanza kutoa utetezi wake. amp.dw.com+1

Baada ya kukamilika kwa ushahidi na mawasilisho ya mwisho ya pande zote mbili, sasa macho yanaelekezwa Novemba 6, siku ambayo jopo la majaji linatarajiwa kutoa hukumu katika shauri hilo.

Miaka 17 ya Manchester City Yafika Kwenye Kivumbi cha Mashtaka 115

Historia ya mafanikio ya Manchester City katika zaidi ya muongo mmoja imeambatana na mjadala mkubwa kuhusu namna klabu hiyo ilivyofadhili ukuaji wake tangu iliponunuliwa na Abu Dhabi United Group mwaka 2008.

Sasa, klabu hiyo inakabiliwa na kesi kubwa zaidi ya kinidhamu katika historia ya Premier League, baada ya kushutumiwa kwa jumla ya makosa 115 ya kanuni za kifedha yanayohusishwa na kipindi cha mwaka 2009 hadi 2018.

Kesi hiyo imechukua miaka kadhaa, huku Manchester City ikikanusha madai hayo na kusisitiza kuwa ushahidi wake utaonyesha kuwa haikukiuka kanuni hizo.

Mwanzo wa enzi mpya

Mabadiliko makubwa Manchester City yalianza Septemba 2008, wakati Abu Dhabi United Group iliponunua klabu hiyo kutoka kwa Thaksin Shinawatra.

Usajili wa Mbrazil Robinho kwa ada iliyokuwa rekodi nchini England siku hiyo ulikuwa ishara ya kwanza ya uwezo mkubwa wa kifedha wa wamiliki wapya.

Msimu uliofuata City iliendelea kutumia fedha nyingi katika usajili, ikiwemo kumsajili Carlos Tevez kutoka Manchester United, Emmanuel Adebayor kutoka Arsenal na wachezaji wengine.

Wakati huo huo, UEFA ilikuwa inaanzisha mfumo wa Financial Fair Play (FFP) uliolenga kuhakikisha klabu hazitumii fedha zaidi ya mapato zinazozalisha.

Mafanikio yakaanza kuja

Chini ya Roberto Mancini, Manchester City ilianza kubadilisha nguvu yake ya kifedha kuwa mafanikio uwanjani.

Mwaka 2011, City ilishinda FA Cup, ikiwa ni taji lake kubwa la kwanza baada ya miaka 35.

Mwaka mmoja baadaye, ilikuja moja ya siku maarufu zaidi katika historia ya Premier League.

City ilihitaji ushindi dhidi ya Queens Park Rangers ili kutwaa ubingwa, lakini ilikuwa nyuma hadi dakika za nyongeza. Edin Dzeko na Sergio Aguero walifunga katika dakika za mwisho na kuipa City ushindi wa 3-2 na ubingwa wake wa kwanza wa England tangu mwaka 1968.

Maswali kuhusu fedha

Kadiri mafanikio yalivyoongezeka, ndivyo maswali kuhusu matumizi na vyanzo vya fedha yalivyozidi.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni mikataba ya udhamini iliyohusisha kampuni kutoka Abu Dhabi, ikiwemo Etihad Airways.

Baadaye, nyaraka zilizochapishwa na Der Spiegel kupitia Football Leaks ziliibua madai kuhusu namna baadhi ya mikataba hiyo ilivyofadhiliwa.

Manchester City ilikanusha madai hayo, ikisema taarifa zilizotolewa zilitokana na udukuzi wa barua pepe na uchapishaji wa nyaraka nje ya muktadha.

UEFA nayo ikaingia

Mwaka 2014, UEFA iliichukulia City hatua kwa kukiuka kanuni za Financial Fair Play, baada ya klabu hiyo kuripoti hasara kubwa.

City ilifungiwa baadhi ya matumizi na kutozwa faini, huku idadi ya wachezaji wake katika mashindano ya Champions League ikipunguzwa.

Mwaka 2020, UEFA ilichukua hatua kubwa zaidi baada ya kuamua kuifungia City kushiriki mashindano ya Ulaya kwa miaka miwili.

Hata hivyo, Manchester City ilikata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), ambayo iliondoa adhabu ya kufungiwa na kupunguza faini.

Guardiola na enzi ya mafanikio makubwa

Kufikia kipindi hicho, City ilikuwa tayari imekuwa moja ya timu kubwa zaidi England.

Kuwasili kwa Pep Guardiola mwaka 2016 kuliongeza kasi ya mafanikio.

City ilitwaa mataji mengi ya Premier League, FA Cup na League Cup, huku mwaka 2023 ikifikia kilele kwa kushinda UEFA Champions League na kukamilisha treble baada ya kutwaa pia Premier League na FA Cup.

Erling Haaland naye aliingia katika historia kwa kuvunja rekodi nyingi za ufungaji tangu alipowasili mwaka 2022.

Mashtaka 115

Mnamo Februari 2023, Premier League iliishtaki Manchester City kwa madai ya kukiuka kanuni za kifedha mara 115 katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2018.

Mashtaka hayo yalihusisha madai mbalimbali kuhusu taarifa za kifedha, mapato ya udhamini, malipo ya mameneja na wachezaji pamoja na wajibu wa klabu kushirikiana na uchunguzi.

City ilikanusha mashtaka hayo na kusema ilikuwa na imani kuwa ushahidi wake ungeonyesha kuwa madai hayo hayakuwa na msingi.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwaka 2024 mbele ya jopo huru.

Uamuzi wa jopo

Mnamo Septemba 25, 2026, iliripotiwa kuwa jopo huru lililokuwa likisikiliza kesi hiyo limefikia uamuzi.

Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, Manchester City imepatikana na hatia katika idadi kubwa ya mashtaka hayo 115, ingawa maelezo kamili kuhusu ni mashtaka gani yamekubaliwa na yapi yamekataliwa bado hayajawekwa wazi.

City haijatoa maelezo ya kina kuhusu uamuzi huo, huku mchakato wa kisheria ukiendelea na klabu ikiwa na uwezekano wa kukata rufaa.

Adhabu bado haijajulikana

Kwa sasa, hatua inayofuata ni kusubiri mchakato wa kuamua adhabu.

Miongoni mwa adhabu zinazoweza kujadiliwa ni faini, kupunguzwa pointi au hatua nyingine kali zaidi kwa mujibu wa kanuni husika. Pia kumekuwa na mjadala kuhusu uwezekano wa mataji kuathiriwa iwapo ukiukaji uliothibitishwa utahusishwa na misimu husika.

Hata hivyo, hakuna adhabu ya mwisho iliyotangazwa bado, na mchakato wa rufaa unaweza kubadilisha matokeo ya sasa.

Kesi yenye athari kubwa

Kesi hii imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu kwa sababu inaweza kuwa na athari kubwa kwa Manchester City na historia ya Premier League.

Kwa zaidi ya miaka 17, City imebadilika kutoka klabu iliyokuwa ikipambana kupata mafanikio hadi kuwa moja ya timu zilizotawala soka la England na Ulaya.

Lakini sasa mafanikio hayo yameingia katika kipindi cha kusubiri majibu ya mwisho ya mchakato wa kisheria.

Kinachobaki ni kujua ni mashtaka gani hasa yamebaki, adhabu itakayowekwa na kama Manchester City itaweza kubadilisha matokeo hayo kupitia rufaa.

Hivyo, baada ya miaka mingi ya uchunguzi, kesi ya “Manchester City 115” bado haijafikia mwisho wake.