Maria Nyerere awabariki washiriki wa Vodacom Nyerere Cycling Tour – HabariLeo

Meneja Mauzo na mkakati wa biashara wa kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa Vodacom Tanzania Plc, Caleb Majo akizungumza na waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour wakati wa hafla ya kuwaaga na kupata baraka kutoka kwa Mama Maria Nyerere kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara. Safari hiyo inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kupitia mchezo wa baiskeli na shughuli za maendeleo ya jamii.

Mtoto wa Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Madaraka Nyerere akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour na kutoa salamu za familia ya Mwalimu Nyerere. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya Nyerere Cycling Tour kuelekea Butiama, mkoani Mara, ikiwa na lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere na kuunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii.

Waendesha baiskeli wa msafara wa Nyerere Cycling Tour wakimsikiliza Mama Maria Nyerere akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga na kupata baraka zake kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara. Safari hiyo inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, huku ikiunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii.

Waendesha baiskeli wa msafara wa Nyerere Cycling Tour wakisikiliza wazungumzaji wakati wa kikao cha kuwaaga na kupata baraka kutoka kwa Mama Maria Nyerere kabla ya kuanza mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara. Safari hiyo inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, huku ikiunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Maria Nyerere, Madaraka Nyerere, Meneja Mauzo na Mkakati wa Biashara wa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani wa Vodacom Tanzania Plc Caleb Majo na Mkuu wa kitengo cha tahadhari wa Stanbic Bank, Wilmot Ishengoma, baada ya hafla ya kuwaaga na kupata baraka kwa waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour jijini Dar es Salaam. Safari hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara, inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kupitia mchezo wa baiskeli na shughuli za maendeleo ya jamii.

Mama Maria Nyerere (katikati) akizungumza wakati alipokutana na waendesha baiskeli wa msafara wa Nyerere Cycling Tour ambapo Vodacom Tanzania Plc waliokwenda kumuaga na kupata baraka zake kabla ya kufanya mashindano ya Vodacom Coastal Classic pamoja na Nyerere Cycling Tour.

Safari ya Nyerere Cycling Tour kutoka Dar es Salaam hadi Butiama, mkoani Mara, inalenga kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kuunganisha mchezo wa baiskeli na jitihada za kuleta matokeo chanya katika jamii. Kupitia safari hiyo, waandaaji na washirika wanatarajia kutekeleza shughuli mbalimbali zinazogusa elimu, afya, uhifadhi wa mazingira, elimu ya fedha na maendeleo ya jamii zikiwemo utoaji wa madawati 1,000, ujenzi wa madarasa 10, ukarabati wa madarasa 40 na upandaji miti, huku shughuli hizo zikitarajiwa kuwafikia zaidi ya watu 25,000.

Tukio hilo lilishuhudiwa na Meneja mauzo na mkakati wa biashara wa kanda ya Dar es salaam na Pwani Vodacom Tanzania PLC Caleb Majo(kulia), mtoto wa Mwalimu Nyerere – Madaraka Nyerere (wa pili kushoto) na Wilmot Ishengoma, Mkuu wa Kitengo cha Tahadhari wa Stanbic Bank Tanzania (kushoto) pamoja na wadau wengine wa mchezo wa baiskeli. Tukio hilo lilifanyika wikendi hii, jijini Dar es salaam.

Ni wakati wa utekelezaji fursa zilizopo Afrika – HabariLeo

MISRI:MAKAMU wa Rais wa Tanzania Deogratius Ndejembi, amesema Afrika ina sera, mikakati na makubaliano mazuri ya maendeleo, lakini sasa inapaswa kuongeza kasi ya utekelezaji ili rasilimali na fursa zilizopo barani humo ziweze kuleta manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi.

Amesema hayo leo, Oktoba 3, 2026, akimwakilisha Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwenye Jukwaa la Biashara la Alamein, Afrika linalofanyika katika mji wa New Alamein, Misri.

Akizungumza katika majadiliano ya ngazi ya juu katika mada inayohusu “Makubaliano Mapya ya Ukuaji wa Afrika katika Dunia yenye Misukosuko, Makamu wa Rais amesema katika mazingira ya sasa ya misukosuko ya uchumi na mabadiliko ya kijiografia duniani, Afrika inahitaji kuongeza uzalishaji, kujenga uchumi wenye uwezo wa kustahimili migogoro ya nje na kuhakikisha rasilimali zake zinatumika kuchochea maendeleo yenye manufaa ya moja kwa moja kwa wananchi.

Amesisitiza umuhimu wa uwekezaji katika nishati na miundombinu kama msingi wa ukuaji mpya wa Afrika, akieleza uzoefu wa Tanzania katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 za umeme.

Ameongeza uwekezaji huo ni sehemu ya jitihada za Tanzania za kuongeza upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa wananchi na shughuli za uzalishaji, huku nchi ikiwa na lengo la kufikia upatikanaji wa umeme kwa wote ifikapo mwaka 2050.

Aidha, Makamu wa Rais amesema kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Tanzania imeweka mkazo katika maeneo ya kimkakati yanayolenga kuongeza uzalishaji na kuimarisha sekta ya nishati, ikiwemo matumizi ya gesi asilia na vyanzo vya nishati jadidifu, sambamba na kuboresha miundombinu inayowezesha shughuli za kiuchumi.

Amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi, uwekezaji unaovuka mipaka na kuunganisha uchumi wa nchi za Afrika ili kupunguza utegemezi wa masoko na mitaji kutoka nje ya bara.

“Afrika inahitaji kujenga mazingira yatakayovutia mitaji ya sekta binafsi kuelekezwa katika miradi inayoongeza uzalishaji, ajira na thamani ya rasilimali za bara, sambamba na kuendeleza miradi ya kikanda inayounganisha nchi na masoko,” amesema.

Akitolea mfano Tanzania, Ndejembi amesema nchi imeendelea kushirikiana na mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati katika sekta za reli, mafuta, nishati na bandari, hatua inayochochea biashara na mtangamano wa kiuchumi katika ukanda huo.

Katika mjadala huo, Makamu wa Rais amesisitiza Afrika tayari ina sera, mipango na makubaliano mazuri, hivyo kinachohitajika sasa ni kuyatekeleza kwa vitendo kwa kubadili mitazamo, kuongeza ushirikiano, kuimarisha utashi wa kisiasa na kufanya maamuzi yanayoweka mbele maslahi ya wananchi wa Afrika.

Mkutano huo umefunguliwa na Rais wa Misri,  Abdel Fattah El-Sisi, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Afrika, akiwemo Rais wa Burundi na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Évariste Ndayishimiye, pamoja na viongozi wa taasisi za Afrika, sekta binafsi na taasisi za fedha.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo, Rais wa Burundi na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika,  Évariste Ndayishimiye, amesema Afrika ina utajiri mkubwa wa rasilimali asilia, ardhi ya kilimo, madini, vyanzo vya nishati, idadi kubwa ya vijana na soko kubwa, lakini changamoto iliyopo ni kugeuza rasilimali na fursa hizo kuwa matokeo halisi ya kiuchumi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Dangote Group, Aliko Dangote, amesema misukosuko inayoikabili dunia imeathiri pia uchumi wa Afrika, hivyo bara linapaswa kutumia rasilimali zake kujenga uwezo wa uzalishaji na kuimarisha uchumi wake.

Dangote amesisitiza umuhimu wa Afrika kuharakisha ukuaji wa viwanda na kuongeza thamani ya rasilimali zake ndani ya bara, badala ya kuendelea kuuza malighafi na baadaye kuagiza bidhaa zilizotengenezwa kutokana na malighafi hizo.

Miongoni mwa viongozi wa taasisi wanaoshiriki ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika; Mkurugenzi Mtendaji wa AUDA-NEPAD, na Rais na Mwenyekiti wa Afreximbank.

Jukwaa hilo linalenga kuimarisha biashara, uwekezaji na ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi za Afrika na Sekta Binafsi ili kuchochea mtangamano na maendeleo ya uchumi wa Bara la Afrika.

Jkt Queens Yapoteza Ngao ya Jamii, Simba Queens Yaibuka Mabingwa

Global Publishers
October 3, 2026
0 views
0 Comments

Simba Queens leo Oktoba 3, 2026 wameanza msimu kwa kutwaa Ngao ya Jamii Wanawake 2026 baada ya kuifunga JKT Queens bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa KMC Complex.

Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Aisha Mnunka, ambaye ameipa Simba Queens ushindi na hatimaye kutwaa taji hilo.

Matokeo hayo yanaifanya Simba Queens kuivua JKT Queens ubingwa wa Ngao ya Jamii na kuanza msimu kwa kumbukumbu nzuri baada ya kuondoka na ushindi katika mchezo huo wa fainali.

Chivayo na Mkewe Kuzikwa Bila Kuonyeshwa Miili, Familia Yafunguka

Global Publishers
October 3, 2026
12 views
0 Comments

Familia ya mfanyabiashara wa Zimbabwe, Wicknell Chivayo, imesema hakutakuwa na utaratibu wa kuonyeshwa miili ya marehemu Chivayo na mke wake, Lulu, kabla ya mazishi kutokana na hali ya miili yao baada ya ajali ya helikopta iliyowaua.

Msemaji wa familia, Hebert Chivayo, amesema miili ya wanandoa hao ilipata madhara makubwa katika ajali hiyo, huku sehemu za miili yao zikitawanyika katika eneo la tukio.

Akizungumza na waombolezaji waliokusanyika katika makazi ya marehemu Ijumaa jioni, Hebert amesema hali hiyo imefanya familia kuamua kutokuwa na utaratibu wa kuonyeshwa miili wakati wa mazishi.

Amesema wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi bado wanaendelea na vipimo vya DNA kwa ajili ya kutambua na kutenganisha mabaki ya waathirika, kabla ya familia kuendelea na maandalizi ya mazishi.

Hadi sasa, familia haijatangaza tarehe rasmi ya mazishi.

Chivayo, ambaye baada ya kifo chake alitangazwa kuwa shujaa wa mkoa na Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, alifariki Jumatano pamoja na mke wake na abiria wengine baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika eneo la vijijini la Marondera.

Familia inaendelea kusubiri kukamilika kwa mchakato wa utambuzi wa mabaki kabla ya kutangaza mipango zaidi kuhusu mazishi.

Sekretarieti ya Ajira Yatangaza Nafasi ya Afisa Sheria Mwandamizi

Global Publishers
October 3, 2026
912 views
0 Comments

Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza nafasi moja (1) ya kuhamia ya Afisa Sheria Mwandamizi, kwa Watanzania ambao ni watumishi wa Umma wenye sifa na uwezo.

Majukumu ya nafasi hiyo ni pamoja na kutoa ushauri na msaada wa kisheria kwa Sekretarieti ya Ajira, kutoa mapendekezo ya maboresho katika uandaaji wa miswada ya sheria na sheria ndogo, kufuatilia mashauri yaliyopo mahakamani, pamoja na kusimamia uandaaji na mapitio ya nyaraka mbalimbali za kisheria.

Sifa za mwombaji:
Mwombaji anatakiwa kuwa mtumishi wa Umma mwenye Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) kutoka taasisi inayotambuliwa na Serikali, akiwa na uzoefu wa kazi usiopungua miaka saba katika eneo husika. Pia anatakiwa kuwa amehudhuria na kufaulu mafunzo ya uanasheria kwa vitendo au Shule ya Sheria Tanzania, pamoja na kusajiliwa kama wakili wa Mahakama Kuu.

Aidha, mwombaji anatakiwa kuwa mtumishi wa Umma aliyefanya kazi kwa mwajiri wake wa sasa kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu na awe tayari kugharamia gharama za uhamisho.

Waombaji wanapaswa kuambatisha CV yenye maelezo ya kina, vyeti vya taaluma vilivyothibitishwa, cheti cha kuzaliwa, pamoja na majina ya wadhamini watatu. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa kuhakikisha vyeti vyao vimehakikiwa na mamlaka husika.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 12 Oktoba 2026. Maombi yote yanapaswa kutumwa kupitia Recruitment Portal ya Ajira.

Simba Yapoteza Mechi ya Pili Mfululizo Afrika Kusini

Global Publishers
October 3, 2026
24 views
0 Comments

Klabu ya Simba SC imepoteza mchezo wake wa pili mfululizo wa kirafiki nchini Afrika Kusini, baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Sekhukhune United.

Mchezo huo ulikuwa wa pili kwa Simba katika kambi yao ya siku 10 nchini Afrika Kusini na umehitimisha kambi hiyo, huku timu hiyo ikiendelea na maandalizi ya msimu mpya.

Kipigo hicho kinakuja siku moja baada ya Simba kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Polokwane City, katika mchezo mwingine wa kirafiki nchini humo.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kumaliza kambi ya Afrika Kusini bila kupata ushindi katika michezo yake miwili ya kirafiki, huku benchi la ufundi likitumia michezo hiyo kuwapima wachezaji na kuendelea kujiandaa kwa mechi za msimu ujao.

Simba sasa inaelekeza nguvu kwenye maandalizi ya mechi zake zijazo, ikiwemo Dabi ya Kariakoo dhidi ya Yanga inayotarajiwa kuchezwa Oktoba 10.

Familia ya Chivayo Yataka Watoto Walindiwe Urithi wa Baba Yao

Familia ya mfanyabiashara maarufu nchini Zimbabwe, Wicknell Chivayo, imesema itahakikisha watoto wake wanapata urithi wa mali alizoacha, huku ikimuomba Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, kuingilia kati iwapo kutakuwa na jaribio la kwenda kinyume na matakwa ya marehemu.

Kauli hiyo imetolewa na mjomba wa Chivayo na msemaji wa familia, Herbert Chivayo, wakati Rais Mnangagwa alipofika katika makazi ya marehemu yaliyopo Gletwyn, Harare, kutoa pole kwa familia kufuatia kifo chake.

Chivayo, ambaye alikuwa mfanyabiashara anayefahamika kwa maisha ya kifahari na mahusiano yake na watu mbalimbali mashuhuri, wakiwemo wanasiasa, wasanii na viongozi wa dini, alifariki Jumatano baada ya helikopta aliyokuwa akisafiria kuanguka katika eneo la Kudenga Farm, karibu na Marondera.

Alifariki pamoja na mke wake, Lucy Muteke, rubani Calvin Soda, msaidizi wa rubani Courage Mutavirwa na mlinzi Saneliswe Magagula.

Akizungumza mbele ya Rais Mnangagwa na waombolezaji wengine, Herbert amesema Chivayo aliwahi kueleza mara kadhaa kuwa angependa sehemu kubwa ya mali zake irithiwe na watoto wake iwapo angefariki.

Herbert amesema familia ya Chivayo haina nia ya kugombania mali ya marehemu, akisisitiza kuwa watoto wake ndio warithi halali wa mali alizoacha.

Ameongeza kuwa familia itahakikisha matakwa hayo yanaheshimiwa na kumuomba Rais Mnangagwa kuingilia kati endapo kutatokea mtu atakayejaribu kuichukua au kuiingilia mali ya marehemu kinyume na matakwa yake.

Msiba huo umewakutanisha viongozi wa serikali na siasa, viongozi wa dini, ndugu, marafiki pamoja na maelfu ya waombolezaji waliofika kutoa heshima zao za mwisho.

Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na mwanachama wa Kamati Kuu ya Zanu PF, Kudakwashe Tagwirei, Waziri wa Habari Soda Zhemu, Waziri wa ICT Tatenda Mavetera, kiongozi wa United Family International Church Emmanuel Makandiwa, kiongozi wa dini Walter Magaya pamoja na mshauri maalum wa Rais, Paul Tungwarara.

Maelfu ya waumini wa Johanne Masowe pia walihudhuria msiba huo.

Mke wa zamani wa Chivayo, Sonja Madzikanda, alifika kwenye msiba akiwa pamoja na watoto wao wawili, ambao wameelezwa kuwa ndio watoto pekee walioachwa na marehemu.

Waombolezaji awali walikusanyika katika makazi ya mama mzazi wa Chivayo yaliyopo Borrowdale, kabla ya kuelekea katika makazi yake ya Gletwyn ambako familia ilipokea salamu za pole.

Wakati huo huo, Herbert amesema uchunguzi wa kitaalamu kuhusu miili ya waathirika wa ajali hiyo bado unaendelea.

Amesema kutokana na hali ya miili baada ya ajali, hakutakuwa na utaratibu wa waombolezaji kuuona mwili wa Chivayo kabla ya mazishi.

Familia pia imesema Chivayo anatarajiwa kuzikwa karibu na mke wake, Lucy Muteke, ingawa eneo rasmi la mazishi bado halijatangazwa.

CWT KUWAUNGANISHA WALIMU KUTATUA CHANGAMOTO

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimesema kitaendelea kuwafikia walimu wote nchini na kuwaunganisha pamoja ili kutambua changamoto zinazowakabili na kuzifikisha kwa Serikali kwa ajili ya kupata ufumbuzi.

Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Magesa Protas, alisema hayo wakati akizungumza kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani, ambayo kilele chake kinatarajiwa kufanyika Oktoba 5, 2026.

Magesa alisema CWT itaendelea kushirikiana na walimu katika maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha changamoto zao zinabainishwa, kujadiliwa na kuwasilishwa kwa mamlaka husika kwa wakati.

“Tutahakikisha tunawafikia walimu wote nchini tunaungana na Serikali na walimu wote kuleta unafuu kwa walimu nchini,” amesema.

Amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha mshikamano miongoni mwa walimu na kuongeza ushiriki wao katika kushughulikia masuala yanayohusu maslahi, mazingira ya kazi na maendeleo ya taaluma ya ualimu.

Magesa alisema CWT pia itaendelea na mazungumzo na Serikali kuhusu madai na changamoto mbalimbali za kiutumishi zinazowakabili walimu, huku akisisitiza umuhimu wa masuala hayo kushughulikiwa kwa wakati.

Amesema miongoni mwa masuala yanayohitaji kupewa kipaumbele ni malipo ya fedha za likizo, kupanda madaraja na stahiki nyingine za walimu.

“Tunaiomba Serikali kuendelea kulipa madeni mbalimbali kwa wakati, ikiwemo malipo ya fedha za likizo, kupanda madaraja na stahiki nyingine za walimu,” alisema.

Pamoja na kuwasilisha changamoto hizo, Magesa aliipongeza Serikali kwa hatua zilizochukuliwa katika kutatua baadhi ya kero za walimu, ikiwemo masuala ya madaraja na kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

“Tunaendelea kuipongeza Serikali kwa kuboresha miundombinu tunaomba yale mengine yanayohusu walimu wayafanyie kazi ili mwalimu afanye kazi katika mazingira mazuri,” alisema.

Amesema kumhudumia mwalimu ni sehemu muhimu ya kuwekeza katika elimu na maendeleo ya Taifa kwa kuwa walimu wana jukumu la kuandaa kizazi cha baadaye.

Aidha, CWT imeitaka Serikali kuhakikisha maboresho ya miundombinu yanaendana na mabadiliko yanayofanyika katika mfumo wa elimu, hususan wakati nchi ikiendelea na utekelezaji wa mitaala mipya.

Magesa amesema utekelezaji wa mitaala hiyo unahitaji mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia, hivyo shule zinapaswa kuwa na miundombinu inayokidhi mahitaji ya walimu na wanafunzi.

Amesema CWT itaendelea kusimamia taaluma ya ualimu, kulinda hadhi yake na kuwasilisha kwa Serikali mapendekezo yatakayosaidia kuboresha maslahi na mazingira ya kazi ya walimu.

Awali, Kaimu Mweka Hazina wa CWT, James Asagwile, ameiomba Katibu Mkuu wa chama hicho kushughulikia malalamiko mbalimbali yanayowakabili baadhi ya waajiriwa wa CWT, ikiwemo suala la mishahara.

Asagwile anesema baadhi ya waajiriwa wamekuwa wakilalamikia mishahara yao kubaki katika viwango vya muda mrefu, hivyo kuomba suala hilo liangaliwe upya.

Maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani mwaka huu yanafanyika huku CWT ikisisitiza umuhimu wa Serikali, walimu na wadau wengine wa elimu kushirikiana katika kuboresha mazingira ya kazi, maslahi ya walimu na ubora wa elimu nchini.

‘Benki zisiogope kukopesha wachimbaji madini’ – HabariLeo

GEITA: Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amezitaka benki na taasisi za fedha nchini kuandaa bidhaa na huduma zinazolenga wachimbaji na wadau wengine wa sekta ya madini, akisema hatua hiyo itasaidia kuchochea ukuaji wa sekta hiyo na uchumi kwa ujumla.

Gavana Tutuba ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi, Oktoba 3, 2026, baada ya kutembelea mabanda mbalimbali katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya Dk Samia Suluhu Hassan, mkoani Geita.

Amesema sekta ya madini ina nafasi muhimu katika uchumi wa Tanzania, hivyo taasisi za fedha zinapaswa kuona fursa zilizopo katika sekta hiyo na kuandaa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wachimbaji na wafanyabiashara wa madini.

“Nimepita katika mabanda ya benki mbalimbali katika maonesho haya na nimeona wameanzisha bidhaa zinazowalenga wachimbaji wa madini na wadau wa sekta hii kwa ujumla,”

“Hata hivyo, nitoe rai kwa wale ambao bado hawajaanzisha bidhaa kwa ajili ya wachimbaji kufanya hivyo, kwa sababu sekta hii ni fursa na ina mchango mkubwa katika uchumi wetu,” amesema Tutuba.

Amesema taasisi za fedha hazipaswi kuiona sekta ya madini kwa mtazamo wa vihatarishi pekee, bali zinapaswa kutafuta namna ya kuvirasimisha na kuvitumia fursa zilizopo ili kuongeza tija katika shughuli za uchimbaji.

Halloween Hii Samaki Wamegeuka Kitita Kwenye Big Bass Splash 1000

Global Publishers
October 3, 2026
18 views
0 Comments

Halloween hii, ziwa limebadilika na kuwa uwanja wa kusaka ushindi. Meridianbet inakuletea Big Bass Halloween Splash 1000, mchezo wa kuvua samaki wenye ladha ya Halloween kutoka Pragmatic Play, ambapo kila mzunguko unaweza kukufikisha kwenye bonasi yenye msisimko zaidi.

Mambo yanaweza kubadilika ghafla kwenye mchezo wa kawaida pale Scatter 3 hadi 5 zinapotua. Hapo ndipo bonasi inapoanza kufunguka, huku ukipewa kati ya mizunguko ya bure 10 hadi 20.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Ukiingia kwenye mizunguko ya bure, kila Wild inaweza kuwa kama ndoana yenye nguvu zaidi. Wild inapojitokeza, hukusanya alama za pesa zote zilizo kwenye mchezo, huku thamani ya alama hizo ikifikia hadi mara 1,000. Kwa hiyo, kila mzunguko unakuwa na jambo jipya la kufuatilia huku macho yakielekezwa kwenye Wild na alama za pesa.

Na kama Wild zinaendelea kutua, safari inaweza kuwa tamu zaidi. Kila Wild ya nne inaweza kuanzisha mizunguko ya bure 10 ya ziada pamoja na vizidishi bora vinavyopanda.

Sasa ziwa limefunguliwa kupitia Meridianbet. Ingia kwenye Big Bass Halloween Splash 1000, tupa ndoana yako na uone kama utapata samaki mwenye thamani kubwa kwenye safari hii ya Halloween.