NDEJEMBI AAPISHWA RASMI KUWA MAKAMU MPYA WA RAIS NCHINI TANZANIA

 

Deogratius John Ndejembi,ameapishwa rasmi kuwa Makamu mpya wa rais nchini Tanzania, baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Makamu wa Rais Emmanuel Nchimbi.

“Usiwe samaki, mwanetu nenda ukakue, tumekupa majukumu makubwa na ni imani yangu utaweza” alisema Rais Samia Suluhu akimpongeza makamu huyo mpya.

Hafla hiyo ya uapisho imefanyika katika ikulu ya Chamwino, Dodoma.

Ndejembi mwenye umri wa miaka 43, atakuwa Makamu wa rais wa 13 tangu Tanzania ipate uhuru, akiwa miongoni mwa Makamu wa rais vijana zaidi kuwahi kushika nafasi hiyo.

RAIA WAWILI WA NIGERIA WAPELEKWA MAREKANI KUJIBU MASHTAKA YA UHALIFU WA MTANDAONI

 

Wanaume wawili kutoka Nigeria wamesafirishwa hadi nchini Marekani, kujibu mashtaka ya ulaghai wa kingono mtandaoni, katika sakata inayohusisha kifo cha kijana mmoja wa Marekani, kulingana na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).

Mkurugenzi wa FBI, Kash Patel, amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X ,kwamba wanaume hao raia wa Nigeria, walikamatwa baada ya uchunguzi kufanywa.

Shirika la Nigeria la Kupambana na Ufisadi na Uhalifu wa Kifedha (EFCC) liliwataja wanaume hao wawili kuwa Mudashiru Afeez Olawale na Adebola Festus Adekunle.

EFCC ilisema wawili hao walikabidhiwa kwa mamlaka za Marekani kufuatia uchunguzi wa FBI kuhusu madai ya kuwalaghai watoto.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye X, shirika hilo lilisema washukiwa hao wanadaiwa kuwalenga wavulana wenye umri wa kati ya miaka 13 na 17, wakitumia picha zao za uchi kuwalazimisha kutoa pesa kupitia kadi za zawadi, kuwatumia kwa benki na sarafu za kidijitali.

Kwa mujibu wa EFCC, kesi moja ilihusisha mvulana mwenye umri wa miaka 13 ambaye aliwasiliana na wawili hao kwenye mtandao wa Instagram na kubadilishana picha za uchi.

Shirika hilo lilisema baadaye mvulana huyo alitishiwa kuwa picha hizo zitasambazwa kwa watu wake wa karibu iwapo hangewatumia pesa.

“Vitisho hivyo viliendelea hata baada ya kijana huyo kusema kwamba alikuwa na nia ya kujiua,” EFCC ilisema.

Mitandao hiyo ya kuwalaghai watoto kwa kuwatishia kuvujisha picha zao za uchi zilichochea kifo cha mtoto mmoja, na uchunguzi ukapelekea kukamatwa kwa raia hao wawili wa Nigeria.

ZAIDI YA WATU 600 WAMEAGA DUNIA KUTOKANA NA MAFURIKO YALIYOTOKEA NEPAL – TIBET

 

Operesheni ya kuwatafuta manusura wa mafuriko nchini Nepal, imeingia siku ya nne baada ya mafuriko hayo kusababisha maafa katika mpaka wa Nepal na Tibet siku ya Jumatano.

Idadi ya waliofariki nchini Nepal imeongezeka na kufikia watu 626, kwa mujibu wa mamlaka za taifa hilo.

Watu 2,426 wanaripotiwa kutojulikana walipo.

Katika eneo la Tibet, idadi rasmi ya waliofariki imefikia saba, huku watu 554 wakiripotiwa kutojulikana walipo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya China.

Kupata taarifa kutoka Tibet imekuwa vigumu, lakini China sasa imetoa baadhi ya picha za tukio hilo.

Nchini Nepal, angalau raia 517 wa kigeni wameripotiwa kutoweka, wakiwemo mahujaji na watalii waliokuwa wakifanya safari za milimani.

Waziri wa Fedha wa Nepal amekadiria kuwa nchi hiyo itahitaji kati ya dola bilioni 4 au 5, kwa ajili ya kujenga upya taifa hilo baada ya mafuriko hayo makubwa.

“Haya ni makadirio tu. Tathmini ya hasara na uharibifu bado inaendelea,” Swarnim Wagle aliiambia shirika la habari la Reuters.

CWT YATAMBULIWA KUWA MDAU MUHIMU WA JUMUIYA YA WAZAZI.

NA CHAUSIKU SAID

MATUKIO DAIMA, MWANZA

JUMUIYA ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imekitambua Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kuwa miongoni mwa wadau muhimu katika utekelezaji wa majukumu yake, hususani katika maeneo ya elimu, malezi na ustawi wa walimu na wanafunzi.

Hayo yamebainishwa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Wazazi yaliyofanyika kitaifa Mkoani Mwanza, ambapo Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Magesa Protas Magesa, pamoja na viongozi wa CWT Mkoa wa Mwanza, wapoalikwa na kushiriki katika maadhimisho hayo.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, Magesa amesema CWT inafurahia kushirikiana na Jumuiya ya Wazazi, na kueleza  kuwa ushirikiano huo ni muhimu kutokana na majukumu yao yanayogusa kwa karibu masuala ya elimu na malezi ya watoto.

Amesema CWT kwa upande wake inasimamia na kutetea maslahi ya watumishi, hususani walimu, wakati Jumuiya ya Wazazi ikiwa inamiliki shule mbalimbali ambazo zina walimu wanaowakilishwa na CWT.

“Kwa upande wa Chama cha Walimu tunashughulika na maslahi ya watumishi, hususani walimu, lakini Jumuiya ya Wazazi ina shule mbalimbali ambazo zina walimu wetu. Sisi kama Chama cha Walimu tunakuwa walezi wa walimu na wanafunzi, kwa hiyo tunahusika kwa namna moja au nyingine katika masuala ya malezi,” amesema Magesa.

Amesema CWT itaendelea kutoa ushauri na maoni kuhusu namna bora ya kuboresha mazingira ya utumishi, huku ikihakikisha maslahi na ustawi wa walimu vinazingatiwa.

Amesisitiza kuwa ushirikiano huo unalenga pia kuhakikisha walimu wanatekeleza majukumu yao katika mazingira mazuri na kupata motisha ya kuendelea kutoa huduma bora ya elimu kwa wanafunzi.

Aidha, amesema CWT itaendelea kujenga ukaribu na Chama Cha Mapinduzi, akieleza kuwa Serikali iliyopo madarakani inaongozwa na sera na Ilani ya CCM, hivyo ni muhimu kwa chama hicho kufikishiwa maoni na mahitaji ya walimu kupitia njia zinazostahili.

“Tunahakikisha tunakaa karibu na Chama Cha Mapinduzi ili kuwapa maoni ambayo walimu wetu wanataka yafanyike, kuhakikisha huduma na utumishi wa walimu wetu unaenda vizuri na wao wanafurahia utumishi wao kwa miaka yote,” amesema.

Amesema CWT itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu na malezi, ili kuhakikisha masuala yanayowahusu walimu na wanafunzi yanapewa kipaumbele katika jitihada za kuboresha elimu nchini.

Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Mwanza yamewakutanisha viongozi, wanachama na wadau mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya elimu, malezi na maendeleo ya Taifa.

WATU 27 WAFARIKI KATIKA SHAMBULIO LA URUSI MJINI KYIV

 

Takriban watu 27 wameuawa baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani ya Urusi kushambulia ghala moja mjini Kyiv, nchini Ukraine.

Watu wengine 42 wamejeruhiwa, huku zaidi ya 380 wakihamishwa kutoka eneo lililoshambuliwa katika wilaya ya Bucha.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa shambulio hilo dhidi ya ghala lilisababisha mlipuko, huku miundombinu iliyoko karibu ikiharibiwa, ikiwemo majengo ya makazi ya watu na kituo kinachotoa huduma ya uangalizi kwa wazee.

Ndejembi Azungumza na Wanachamwino, Amshukuru Rais Samia, Aahidi Kufanya Kazi – Picha

Global Publishers
August 29, 2026
438 views
0 Comments

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa dhamana ya kuwa msaidizi wake wa kwanza, akiahidi kutekeleza majukumu yake kwa utii, uadilifu, uzalendo na uchapakazi.

Ndejembi ametoa kauli hiyo leo, Agosti 29, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la Chamwino waliojitokeza kwa wingi kumpokea nje ya Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma, muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa Makamu wa Rais.

Amesema atatumia nafasi hiyo kumsaidia Rais Samia kwa uadilifu na kuhakikisha anawatumikia Watanzania wote bila ubaguzi, kwa lengo la kuchangia katika kuharakisha maendeleo ya nchi.

“Nitaendelea kufanya kazi ya kumsaidia Mheshimiwa Rais kwa uadilifu na kuwatumikia Watanzania wote ili kuharakisha maendeleo ya nchi yetu,” amesema Ndejembi.

Aidha, Makamu wa Rais amesema ataendelea kuwa mwakilishi mzuri wa vijana nchini na kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha Tanzania inaendelea kupiga hatua katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Ndejembi ameapishwa leo katika hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino, baada ya kuthibitishwa na Bunge kwa asilimia 100 jana, Agosti 28, 2026.

Kengele Imelia! Pambano la TSh 5M Lafikia Tamati, Usikose Soma Hapa

Global Publishers
August 29, 2026
30 views
0 Comments

Muda unakwenda kwa kasi na mashindano ya Expanse: Big Wins Start Here yanaelekea ukingoni. Ikiwa imesalia takribani wiki moja kabla ya mashindano haya kufungwa rasmi, huu ni wakati wa wachezaji kuingia kazini na kuwania sehemu ya TSh 5,000,000 iliyotengwa kama zawadi. Hapa hakuna nafasi ya kusubiri, kwa sababu kila raundi inaweza kuwa tiketi yako ya kupanda kwenye msimamo na kusogea karibu na zawadi kubwa.

Safari hii inakupa nafasi ya kucheza kwenye michezo 15 ya sloti za Expanse, huku dau la chini likiwa TSh 200 kwa kila mchezo. Kwa hiyo, huhitaji dau kubwa kuanza safari yako. Chagua mchezo unaoupenda, anza kucheza na uone kama bahati itakutupa juu kwenye msimamo. Kila hatua unayopiga inaweza kuwa na umuhimu mkubwa wakati mashindano yakielekea siku ya mwisho.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kumbuka, muda wa mashindano haya unafungwa rasmi Septemba 5, 2026. Hiyo ina maana kuwa siku zilizobaki ni muhimu kwa kila mshiriki anayelenga nafasi za juu. Usiruhusu wengine wakutangulie wakati wewe unaangalia saa ikisogea. Expanse inakupa nafasi ya kuingia kwenye ushindani, kusaka pointi na kuendelea kupambana hadi mwisho kwa matumaini ya kunyakua sehemu ya zawadi nono.

Burudani, ushindani na nafasi ya kushinda vimeunganishwa katika tukio hili maalum linalopatikana Meridianbet pekee. Ukiwa na michezo ya kasino mtandaoni 15 ya Expanse ya kujaribu, kila mchezo unakuwa sehemu ya safari yako.

Sasa ni zamu yako kucheza kwa kuelekea ushindi ulipo. Mashindano yanaelekea mwisho, TSh 5,000,000 zipo mezani na muda unapungua ndani ya Meridianbet. Jiandae, ingia kwenye mashindano na tumia siku hizi za mwisho kufurahia ushindani.

Everton Kutafuta Ushindi wa pili, Bournemouth Yawania Pointi za Kwanza

Leo AFC Bournemouth watawapokea Everton kwenye uwanja wao wa Vitality Stadium, katika mechi ya wiki ya pili ya msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza 2026-27. Timu zote mbili zinatafuta kurekebisha hali baada ya matokeo tofauti wiki iliyopita Bournemouth walipoteza 2-1 dhidi ya Manchester City ugenini, huku Everton wakianza msimu vizuri kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Crystal Palace. Hivyo, Everton wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na kasi zaidi ya kimwili.

Kwa upande wa muundo wa timu, Bournemouth wanakabiliwa na changamoto kubwa ya majeraha. Wamekosa wachezaji kadhaa muhimu akiwemo Julian Araujo, Eli Kroupi, Amine Adli na Veljko Milosavljevic kutokana na majeraha, huku Ryan Christie akiwa nje kwa adhabu ya kufungwa, na wachezaji wengine kama Julio Soler, David Brooks na Alvaro Rodriguez wakiwa katika hali ya mashaka. Hii inamaanisha kocha wa Bournemouth atalazimika kutegemea sana kundi dogo la wachezaji wenye uzoefu wa kutosha kwenye mechi hii nyeti.

Licha ya orodha ndefu ya majeruhi, matumaini makubwa ya Bournemouth yanabaki kwa mshambuliaji wao, anabaki kuwa kiini cha mashambulizi ya Bournemouth, akisaidiwa na mchezaji wa ubunifu Alejandro Jimenez Sanchez.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwa upande wa Everton, hali ni tofauti kabisa kwani ni Timothy Iroegbunam pekee aliye nje kwa jeraha, huku Christian Norgaard akiwa katika hali ya mashaka, hivyo Kiernan Dewsbury-Hall na Iliman Ndiaye wanatarajiwa kuendelea na nafasi zao kutoka mechi ya wiki iliyopita.

Kihistoria, mechi hii imekuwa ikivutia sana kutokana na ushindani wa karibu kati ya timu hizi mbili. Rekodi ya jumla ya michezo kati ya AFC Bournemouth na Everton inaonyesha Bournemouth wakiwa na ushindi 12, Everton ushindi 8, na mechi 2 zikiisha sare.

Hii inaonyesha kuwa Bournemouth wana historia nzuri kidogo dhidi ya Everton wanapocheza nyumbani, jambo litakalowapa kiasi cha matumaini licha ya changamoto za majeraha wanazokabiliana nazo msimu huu.

Kwa mtazamo takwimu za uwezekano zinaonyesha Bournemouth wakiwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda dhidi ya Everton. Ingawa Bournemouth wana faida ya kucheza nyumbani na historia nzuri dhidi ya Everton, orodha yao ndefu ya majeruhi inaweza kuwaathiri sana katika ulinzi na ubunifu wa mashambulizi.

Everton, wakiwa kamili zaidi na mwanzo mzuri wa msimu, wanaweza kuchukua fursa hiyo kupata pointi tatu muhimu Vitality Stadium. Mechi hii inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa, huenda ikaishia kwa sare au ushindi mdogo kwa mwenyeji.