Fahamu Maajabu ya Mapasheni, Tunda Dogo Lenye Faida Kubwa Mwilini

Mapasheni ni miongoni mwa matunda yanayopendwa na watu wengi kutokana na ladha yake ya kipekee, harufu nzuri na uwezo wa kutumika kwa njia mbalimbali. Licha ya kuwa na ukubwa mdogo, tunda hili lina virutubisho muhimu vinavyoweza kuchangia afya njema ya mwili.

Kutokana na kuwa na mchanganyiko wa vitamini, madini, nyuzinyuzi na antioxidants, mapasheni yana nafasi nzuri katika lishe bora.

1. Husaidia kuimarisha kinga ya mwili

Mapasheni yana Vitamin C, kirutubisho kinachohitajika na mwili katika kusaidia mfumo wa kinga kufanya kazi vizuri. Vitamin C pia huchangia katika utengenezaji wa collagen, ambayo ni muhimu kwa ngozi na tishu mbalimbali za mwili.

Collagen ni aina ya protini muhimu sana mwilini inayosaidia kujenga na kuimarisha sehemu mbalimbali za mwili.

Kwa lugha rahisi, unaweza kuufikiria collagen kama “gundi” inayoshikilia na kuipa nguvu baadhi ya tishu za mwili.

Mwili hutumia collagen katika:

  • 🧴 Ngozi – husaidia ngozi kuwa na uimara na unyumbufu.
  • 🦴 Mifupa – huchangia uimara wa mifupa.
  • 💪 Misuli na tendons – husaidia kuunganisha misuli na mifupa.
  • 🦵 Viungo na cartilage – huchangia muundo na uimara wa viungo.
  • 🦷 Meno na fizi – pia huhusika katika tishu zinazozunguka meno.

2. Husaidia mfumo wa chakula

Tunda hili lina nyuzinyuzi (fiber), ambazo ni muhimu kwa afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula. Ulaji wa vyakula vyenye nyuzinyuzi unaweza kusaidia utendaji mzuri wa mfumo wa chakula na kupunguza uwezekano wa kupata choo kigumu.

3. Lina antioxidants

Mapasheni yana antioxidants mbalimbali zinazosaidia kulinda seli za mwili dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na free radicals.

Antioxidants ni sehemu muhimu ya lishe yenye afya na hupatikana pia katika matunda na mboga nyingine nyingi.

Antioxidants ni virutubisho au kemikali zinazosaidia kulinda seli za mwili dhidi ya uharibifu unaoweza kusababishwa na molekuli zisizo imara zinazoitwa free radicals.

Kwa lugha rahisi, unaweza kufikiria antioxidants kama “walinzi” wa seli za mwili.

Husaidia:

  • 🛡️ Kulinda seli dhidi ya uharibifu.
  • ❤️ Kuchangia afya ya moyo na mwili kwa ujumla.
  • 🧬 Kusaidia kulinda tishu za mwili.
  • 🌿 Kusaidia mwili kukabiliana na athari za oxidative stress.

4. Mbegu zake zinaweza kuliwa

Moja ya mambo yanayolitofautisha tunda hili ni kwamba mbegu zake zinaweza kuliwa. Mbegu hizo huja pamoja na nyama laini ya tunda na pia huchangia nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye mapasheni.

5. Hutoa madini muhimu

Mapasheni yana baadhi ya madini muhimu, ikiwemo potassium, ambayo mwili huhitaji kwa ajili ya kazi mbalimbali za kawaida, ikiwemo utendaji wa misuli na mfumo wa fahamu.

6. Linaweza kuwa sehemu ya lishe bora

Mapasheni yanaweza kuliwa kama tunda, kutengeneza juisi au kuongezwa kwenye yoghurt, saladi za matunda na vyakula vingine.

Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa juisi yenye sukari iliyoongezwa si sawa na kula tunda zima, hivyo kwa manufaa ya nyuzinyuzi, kula tunda zima ni chaguo zuri.

Kwa nini ulijumuishe kwenye mlo wako?

Kwa ujumla, mapasheni ni tunda lenye ladha, vitamini, madini, antioxidants na nyuzinyuzi, hivyo linaweza kuwa sehemu ya mlo wenye uwiano.

Pamoja na hayo, hakuna tunda moja linaloweza kutoa virutubisho vyote vinavyohitajika na mwili. Ni muhimu kula aina mbalimbali za matunda, mboga na vyakula vingine vyenye virutubisho ili kupata lishe bora.

TRC Yatangaza Nafasi 24 za Ajira, Waombaji Wapewa Hadi Septemba 10

Dodoma, Agosti 28, 2026 — Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma (PSRS), kwa niaba ya Tanzania Railways Corporation (TRC), imetangaza nafasi 24 za ajira kwa Watanzania wenye sifa, uwezo na uzoefu unaohitajika.

Nafasi hizo zimetangazwa kupitia tangazo lenye Kumb. Na. JA.9/16/01/53 la tarehe 28 Agosti 2026.

Nafasi zilizotangazwa

  1. Instructor II (Civil Engineer) — Nafasi 1
  2. Instructor II (Mechanical Engineer) — Nafasi 1
  3. Artisan II (Auto Electric) — Nafasi 5
  4. Technician II (Automobile) — Nafasi 4
  5. Technician II (Hydraulic Machineries) — Nafasi 2
  6. Engineer II (Signal & Telecommunication) — Nafasi 1
  7. Locomotive Driver II — Nafasi 10

Sifa za jumla kwa baadhi ya nafasi

Instructor II (Civil Engineer):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Uhandisi wa Ujenzi (Civil Engineering) au taaluma inayolingana nayo, yenye kiwango cha NTA Level 8 au sawa, kutoka taasisi inayotambuliwa. Anatakiwa kuwa na GPA isiyopungua 3.5, pamoja na kuwa anastahili kusajiliwa kama mwalimu wa ufundi na kusajiliwa na bodi husika kama Graduate Engineer/Professional.

Instructor II (Mechanical Engineer):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Mechanical Engineering au inayolingana nayo, yenye kiwango cha NTA Level 8 au sawa, kutoka taasisi inayotambuliwa, akiwa na GPA isiyopungua 3.5. Pia anatakiwa kuwa anastahili kusajiliwa kama mwalimu wa ufundi na kusajiliwa na bodi husika kama Graduate Engineer/Professional.

Artisan II (Auto Electric):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne pamoja na CBET Level II/III, Trade Test Grade I/II au NVA II/III katika fani ya Auto Electric au sifa inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambuliwa.

Technician II (Automobile):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne au Sita pamoja na Diploma/NTA Level 6 katika Automobile Engineering, Automotive Mechanics au sifa nyingine inayohusiana na fani hiyo.

Technician II (Hydraulic Machineries):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne au Sita pamoja na Full Technician Certificate (FTC) au Ordinary Diploma in Mechanical Engineering yenye utaalamu wa Hydraulic Machineries au sifa inayolingana nayo.

Engineer II (Signal & Telecommunication):
Mwombaji anatakiwa kuwa na Shahada ya Electrical Engineering, Telecommunication Engineering, Electronics Engineering au inayolingana nayo kutoka taasisi inayotambuliwa na awe amesajiliwa na Engineers Registration Board (ERB) kama Graduate Engineer.

Locomotive Driver II:
Mwombaji anatakiwa kuwa na Cheti cha Kidato cha Nne, Cheti cha Uendeshaji Treni (Locomotive Driving Certificate) cha miaka miwili au Locomotive Shunting Certificate kutoka TIRTEC au taasisi inayotambuliwa, pamoja na leseni ya udereva ya Class F au G.

Masharti muhimu ya maombi

PSRS imesema waombaji wote lazima wawe raia wa Tanzania na kwa ujumla wasizidi umri wa miaka 45.

Waombaji wanatakiwa kuambatanisha nakala zilizothibitishwa za vyeti vyao vya elimu na taaluma, pamoja na transcripts na vyeti vya usajili wa kitaaluma kutoka bodi au mamlaka husika pale inapohitajika.

Aidha, mwombaji anatakiwa kupakia picha ya Passport Size ya hivi karibuni katika mfumo wa maombi.

PSRS imesisitiza kuwa result slips za Form IV na Form VI, testimonials pamoja na partial transcripts hazitakubalika kama nyaraka za maombi.

Waombaji wanapaswa pia kutaja referees watatu wanaotambulika na kutoa mawasiliano yao yanayoaminika.

Kwa waombaji wenye vyeti vya elimu vya nje ya Tanzania, vyeti hivyo vinapaswa kutambuliwa na mamlaka husika, ikiwemo TCU, NECTA au NACTVET, kulingana na aina ya sifa.

Jinsi ya kutuma maombi

Maombi yote yanatakiwa kuwasilishwa mtandaoni kupitia Recruitment Portal ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Waombaji wanaweza kutumia:

portal.ajira.go.tz

Barua ya maombi inapaswa kuandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza, kusainiwa na kuelekezwa kwa:

Secretary,
President’s Office, Public Service Recruitment Secretariat,
P.O. Box 2320,
Mahakama Street, Tambukareli,
Dodoma.

Mwisho wa kutuma maombi

Mwisho wa kutuma maombi ni Septemba 10, 2026.

PSRS imesema maombi yatakayowasilishwa kupitia njia nyingine tofauti na Recruitment Portal hayatazingatiwa.

Aidha, ni waombaji watakaoteuliwa pekee ndio watakaotaarifiwa kuhusu tarehe ya usaili.

Sekretarieti imeonya kuwa mtu atakayewasilisha vyeti vya kughushi au taarifa za uongo atachukuliwa hatua za kisheria.

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA AZINDUA JENGO LA RAMANI LA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 03 Septemba, 2026, amezindua rasmi Jengo la Ramani la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lililopo katika Mji wa Serikali, Mtumba, Jijini Dodoma.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo ambalo ni sehemu ya miundombinu ya kimkakati ya Jeshi, Dkt. Nyansaho amelipongeza JWTZ kwa kukamilisha mradi huo na kupata jengo la kisasa lililowekewa vifaa na teknolojia za kisasa zitakazowezesha utoaji wa huduma kwa ufanisi na weledi zaidi.

Waziri Nyansaho amesema kukamilika kwa mradi huo ni kielelezo cha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendelea kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutekeleza majukumu yake ya msingi ya kulinda uhuru, mamlaka na usalama wa nchi.

 “Kukamilika kwa mradi huu wa kimkakati ni alama ya dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendelea kuliwezesha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kutimiza majukumu yake ya ulinzi na usalama kwa ufanisi,” alisema Dkt. Nyansaho.

Aidha, Waziri Nyansaho amesema ana imani kuwa jengo hilo pamoja na vifaa vilivyowekwa vitatunzwa na kutumika ipasavyo, akieleza kuwa JWTZ limejijengea sifa kubwa katika utunzaji na usimamizi wa mali zake.

Kwa upande wake, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda, amemshukuru Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kulitambua na kulithamini Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na kuliwezesha kutekeleza majukumu yake kwa weledi na ufanisi.

Jenerali Mkunda pia ameishukuru Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa ushirikiano na usimamizi uliowezesha kufanikishwa kwa ujenzi wa jengo hilo, pamoja na kuwezesha wataalamu wa JWTZ kupata mafunzo maalumu kuhusu uendeshaji na matumizi ya mitambo ya kisasa iliyofungwa katika jengo hilo.

Awali, akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuzungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, amesema jengo hilo limejengwa kwa kuzingatia viwango vya juu vya ubora na limewekewa mitambo ya kisasa yenye uwezo wa kutengeneza ramani za kidijitali za 3D, pamoja na ramani za viwango vya juu zaidi kulingana na mahitaji ya kitaalamu.

Dkt. Mnyepe amesema uwepo wa jengo hilo na teknolojia hiyo ya kisasa utaongeza uwezo wa JWTZ katika utengenezaji, uchakataji na matumizi ya taarifa za ramani, hivyo kuchangia katika kuimarisha utekelezaji wa majukumu yake ya kitaalamu na kimkakati.

Uzinduzi wa jengo hilo unaweka msingi muhimu katika kuimarisha uwezo wa kitaalamu na kiteknolojia wa JWTZ, sambamba na juhudi za Serikali za kuendelea kuboresha miundombinu na mazingira ya kazi kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya ulinzi na usalama wa Taifa.

Mwisho

Lucky Loser Yarudisha Matumaini, Ukikosa Zote, Unashinda

Global Publishers
September 3, 2026
48 views
0 Comments

Kwenye mchezo wa Win&Go, kila tiketi inaweza kuwa na simulizi yake, lakini sasa hata pale ambapo namba zako zote zinakataa kuingia, bado kuna sababu ya kutabasamu. Meridianbet imekuja na Lucky Loser, chaguo linaloweza kugeuza tiketi iliyokuwa ikionekana kama imepoteza kila kitu kuwa tiketi ya ushindi. Badala ya kukata tamaa baada ya kukosa namba zote, mchezaji anapata nafasi ya kuona tiketi yake ikigeuka kuwa mshindi.

Kupitia Lucky Loser, kinachovutia zaidi ni kwamba dau la mchezaji linaweza kuzidishwa mara 30. Hii ndiyo sehemu inayoongeza ladha kwenye Win&Go, kwani hata matokeo ambayo mwanzoni yanaonekana kuwa mabaya yanaweza kuleta habari njema. Ni kama dakika za mwisho za mchezo ambapo kila mtu anadhani matokeo yamekwisha, lakini ghafla kinatokea kitu kinachobadilisha kila kitu.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Hata hivyo, ili kunufaika na nafasi hii, mchezaji anatakiwa kuzingatia masharti yaliyowekwa. Lucky Loser inatumika kwa tiketi za Meridianbet zilizowekwa kupitia cash account, huku tiketi husika ikiwa na namba sita ndani ya mchezo wa Win&Go. Kwa hiyo, ni muhimu kuhakikisha tiketi yako inakidhi masharti hayo kabla ya kucheza.

Win&Go sasa unakuja na msisimko mwingine kwa sababu hadithi haiishii tu kwenye kukosa namba. Lucky Loser inaleta nafasi ya tiketi yako kupewa maisha mapya na dau lako kuzidishwa mara 30. Hii ndiyo aina ya kitu ambacho kinaweza kumfanya mchezaji aendelee kuwa na matumaini hadi mwisho.

Kwa mashabiki wa Win&Go wanaotafuta mchezo wenye msisimko wa ziada, Lucky Loser ni sehemu ya kuifahamu. Cheza Win&Go kupitia Meridianbet, kwa sababu hapa hata ukikosa namba zote, bado unaweza kuwa na sababu ya kusherehekea.

Mpigie Kura Godmuya, Kura Yako Ni Ushindi! – Tuzo za Samia Kalamu Awards 2026

Global Publishers
September 3, 2026
18 views
0 Comments

Mtangazaji wa @globaltvonline na @255globalradio, Godfrey Nathan @godmuya ameteuliwa kuwania tuzo za Samia Kalamu Awards 2026.

Sasa Godmuya anaomba support yako, mfuatiliaji wa Global TV, kwa kumpigia kura ili kufanikisha ushindi wake.

🗳️ MPIGIE KURA: GODFREY LUHILABAKE NATHAN
🔢 Kodi: 260246

👉 Piga kura kupitia:
https://samiaawards.tz/mshiriki/260246

📌 Copy link hiyo kisha paste kwenye browser yako ili kumpigia kura.

Kura yako ni mchango mkubwa kwa Godmuya katika safari hii ya tuzo.

🙏 Piga kura, share na mwambie mwingine apige kura!

#SamiaKalamuAwards #VoteForGodmuya #Godmuya #GlobalTVOnline #255GlobalRadio

Hii Ndiyo “Kazi Iendelee” Ya Rais Samia, Mwenye Macho Haambiwi Tazama – Video

Global Publishers
September 3, 2026
42 views
0 Comments

Jiji la Dar es Salaam la leo limebadilika kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka 10 iliyopita, hususan katika sekta ya miundombinu ya barabara, ambapo miradi mbalimbali imeendelea kutekelezwa, kuboreshwa na kupanuliwa.

Baada ya kifo cha ghafla cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, aliyeanzisha na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo nchini, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alichukua dhamana ya kuendeleza miradi hiyo pamoja na kuanzisha mingine mipya.

Hapo ndipo kauli mbiu ya “KAZI IENDELEE” ilipoendelea kushika kasi. Na leo, ukiangalia mabadiliko yanayoendelea kulipamba Jiji la Dar es Salaam, mwenye macho haambiwi tazama! 🔥🇹🇿

Real Sociedad dhidi ya Celta Vigo Vita ya Point tatu La Liga

Global Publishers
September 3, 2026
6 views
0 Comments

Usiku wa leo Septemba 16, Reale Arena itakuwakutanisha wababe wa soka la uhispania Laliga kati ya Real Sociedad na Celta Vigo, mechi itakayoshuhudia matumizi ya mbinu kwa ukubwa na kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi.

Wenyeji wanajulikana kwa mchezo wa kupitisha mpira ardhini kwa uvumilivu, huku wageni wakipendelea mashambulizi ya kasi kupitia mabao ya kupindua mchezo (counter-attacks).

Real Sociedad chini ya usimamizi wa kocha wao wanategemea sana udhibiti wa uwanja wa kati. Hata hivyo, msimu huu wameonesha udhaifu wa wazi katika ulinzi, jambo linaloweza kutumiwa vibaya na washambuliaji wepesi wa Celta.

Kutokuwepo kwa Odriozola upande wa ulinzi kunazidisha wasiwasi huu, hasa endapo Celta watachagua kushambulia kwa kasi kupitia ubavu wa kushoto.

Celta Vigo kwa upande mwingine wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na maandalizi kamili kwani hawana majeruhi wanaotajwa. Timu hii imekuwa ikijenga mtindo wa kucheza kwa mshikamano tangu msimu uliopita na kufuzu kucheza mashindano ya Ulaya (Europa League). Hii inaonyesha kuna kiwango cha kujiamini kwenye kikosi chao.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Takwimu za mechi za hivi karibuni kati ya pande hizi mbili misimu mitano iliyopita zinaonyesha usawa mkubwa ushindi mmoja kwa Real Sociedad, sare tatu, na ushindi mmoja kwa Celta.

Hii inathibitisha kuwa licha ya historia ndefu inayowapendelea wenyeji kwa ujumla, mechi za hivi karibuni zimekuwa na ushindani mkubwa zaidi bila upande mmoja kutawala.

CCWT YAIPA SERIKALI KIJANI, YATOA ONYO KWA WAFUGAJI DODOMA.

 

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma

CHAMA Cha Wafugaji Nchini (CCWT) kimesema kufutwa kwa sheria iliyokuwa ikiruhusu mifugo kutaifishwa baada ya kuingia katika maeneo ya hifadhi ni hatua inayokwenda kuondoa hofu na kero iliyokuwa ikiwakabili wafugaji nchini.

Hata hivyo, chama hicho kimesisitiza kuwa mabadiliko hayo hayatoi ruhusa kwa wafugaji kuingiza mifugo katika maeneo ya hifadhi, kikieleza kuwa wafugaji wanapaswa kutumia nafasi hiyo kuimarisha ufugaji wao na kuzingatia sheria za uhifadhi.

Mwenyekiti wa CCWT, Mrida Mshota, amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari, akieleza kuwa wafugaji wamepokea hatua hiyo kwa matumaini makubwa kutokana na changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo kutokana na utekelezaji wa sheria hiyo.

Amesema pamoja na kuondolewa kwa adhabu ya kutaifishwa mifugo, wafugaji bado wana wajibu wa kuhakikisha shughuli zao zinafanyika katika maeneo yanayotambuliwa kisheria na kuepuka migogoro na maeneo ya hifadhi.

Kwa mujibu wa Mshota, ufugaji wenye tija unahitaji wafugaji kuachana na mifumo ya zamani na kuelekea katika ufugaji wa kisasa unaozingatia matumizi bora ya ardhi, lishe bora ya mifugo na uzalishaji wenye tija.

Amesema hatua hiyo inaweza kusaidia kujenga mazingira mazuri zaidi kati ya wafugaji, Serikali na taasisi zinazohusika na uhifadhi, iwapo wafugaji wataendelea kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Katika hatua nyingine, CCWT imeitaka Serikali kuendelea kuboresha huduma za msingi kwa wafugaji, hasa kuhakikisha chanjo za mifugo zinapatikana na kutolewa kwa wakati katika maeneo mbalimbali nchini.

Mshota pia amesisitiza umuhimu wa kuharakisha utambuzi na usajili wa mifugo, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kuwezesha Serikali kuwa na takwimu sahihi za mifugo na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wafugaji.

Amesema uwepo wa mfumo mzuri wa utambuzi wa mifugo utasaidia pia katika kudhibiti magonjwa, kufuatilia mifugo na kuboresha mipango ya maendeleo katika sekta ya mifugo.

CCWT imesema ushirikiano kati ya Serikali na wafugaji ni muhimu katika kuhakikisha mabadiliko ya sera na sheria yanafikia malengo yaliyokusudiwa, huku wafugaji wakitakiwa kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa.

Marekebisho ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori yaliyofuta utaifishaji wa mifugo inapoingia ndani ya hifadhi yameelezwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuwa utaratibu wa awali ulikuwa ukikiuka misingi ya Katiba.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MIKATABA YA MSAADA WA KIUFUNDI KATIKA SEKTA YA MADINI

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Subira Mgalu (Mb.) imepatiwa mafunzo kuhusu usimamizi wa mikataba ya msaada wa kiufundi katika Sekta ya Madini, ikiwa ni pamoja na masharti ya kisheria yanayohusu umiliki wa leseni ndogo za uchimbaji wa madini.

Akizungumza kupitia mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Madini jijini Dodoma mapema leo Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Madini, Francis Kayichile, kwa Niaba ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini amesisitiza kuwa mtu ambaye si raia wa Tanzania kupewa leseni ndogo ya uchimbaji madini ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Madini, Sura ya 123, kwa kuwa fursa ya kuomba na kumiliki leseni hizo imetengwa kwa Watanzania pekee.

Kayichile amesema Kifungu cha 64 kikisomwa pamoja na kifungu cha 9 (3) cha Sheria ya Madini, Sura ya 123, kinatoa fursa kwa Watanzania pekee kuwasilisha maombi ya leseni ndogo za uchimbaji madini, hivyo mtu asiye raia wa Tanzania hanufaiki na fursa hiyo.

Amesema pamoja na umiliki wa leseni kuwa kwa Watanzania, wamiliki wa leseni ndogo wanaweza kupata msaada wa kiufundi kutoka kwa wawezeshaji kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo.

Aidha ameeleza kuwa kwa mujibu wa kanuni hizo mwenye leseni yenye msaada wa kiufundi amepatiwa  asilimia 30 ya faida baada ya kuondoa tozo zote za Serikali, bila kuzingatia gharama za uendeshaji wa mradi alizobeba mwezeshaji.

Ameongeza kuwa usimamizi wa mgodi, uingizaji wa vifaa na mitambo pamoja na ulinzi wa eneo na mali ni majukumu ya pamoja ya wahusika wa mkataba.

Kayichile amesema mkataba wa msaada wa kiufundi huwa na muda wa awali wa miaka mitatu na unaweza kuhuishwa, lakini kwa jumla muda wake haupaswi kuzidi miaka 12 au uhai wa mgodi unapoisha.

“Mikataba hiyo husajiliwa na Tume ya Madini na wahusika wana haki ya kufanya marekebisho  wakati wowote na pindi kunapofanyika marekebisho ya sheria  yanayoathiri masharti ya mkataba au pale inapobainika uwepo wa madini mapya katika eneo lenye leseni yenye msaada wa kiufundi” amesema.

Amesema Tume ya Madini inaendelea kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mikataba hiyo, huku akisisitiza kuwa ukiukwaji wa masharti unaweza kusababisha hatua kuchukuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 74 cha Sheria ya Madini, Sura ya 123, ikiwemo kusitishwa au kufutwa kwa leseni.

Aidha, Kayichile amesema Serikali imefanya marekebisho ya Kanuni za Haki Madini kwa lengo la kulinda haki za wenye maduara waliopo ndani ya maeneo yenye leseni ndogo za uchimbaji madini.

Amesema kupitia Kanuni za Madini (Msaada wa Kiufundi) za mwaka 2025, hususan Kanuni ya 8(1)(h), mwenye leseni analazimika, kabla ya kuingia mkataba wa msaada wa kiufundi, kufanya makubaliano na wenye maduara au kuwalipa fidia kwa uwekezaji walioufanya katika eneo lenye leseni hiyo.

Kwa mujibu wa Kayichile, hatua hiyo inalenga kuhakikisha haki za Watanzania wanaomiliki leseni na wenye maduara zinalindwa, huku ikiweka mazingira ya ushirikiano katika shughuli za uchimbaji madini yanayozingatia sheria na kuhakikisha rasilimali za madini zinawanufaisha Watanzania wote.

Kikao hicho kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Subira Mgalu (Mb.) kimeshirikisha pia watendaji wa taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini.