Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MEYA wa maanispaa ya Kigoma Ujiji Mussa Maulid ametoa wito kwa viongozi wa dini mkoani Kigoma katika malezi ya watoto wao na jamii kwa ujumla ili kukabiliana na wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili linaloukabili mkoa huo ikiwemo kukithiri kwa vitendo vya ushoga.
Meya Maulid alisema hayo wakati wa Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika kwenye msikiti wa Mujahidina Ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji na kubainisha kuwa mmomonyoko wa maadili unapoteza sifa na taswira ya Ustaarab ya mkoa huo hasa ya mji wa Ujiji.
Alisema kuwa mji wa Ujiji kwa miaka mingi ulikuwa unafahamika kama mji wa ustaarab kutokana na idadi kubwa ya watu wake kuishi kwa kufuata misingi ya dini na kuzingatia maadili mema ya jamii lakini la kushangaza kwa sasa Ujiji ndiyo imekuwa ikiongoza kwa mmomonyoko wa maadili ikiwemo kuandaa karamu za ushoga na kualika watu kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania na nje ya Tanzania kuhudhuria karamu hiyo.
“Ujiji imetoa wanazuoni wakubwa wa dini ya kiislam na Mashekhe na wahubiri wengi wa kiislam wamesoma Ujiji, lakini pia lipo kanisa katoliki lililoanzishwa karne ya 13 hayo yalifanya eneo hilo kuwa na ustaarabu na maadili mema lakini yote yameondokana na Ujiji imekuwa mfano mbaya kwa maisha ya vijana wa sasa,”Alisema Meya huyo wa manispaa ya Kigoma Ujiji.
Kwa upande wake Kadhi wa mkoa Kigoma,Abdul Muhsin Kitumba alisema kuwa ni lazima waumin wa kiislam mkoani Kigoma waishi kwenye maadili kama ambavyo wanasherehekea maisha ya Mtume Muhammad (SAW) ambaayee anaapigiwa mfano kuwa binadamu aliyeishi katika maadili ya haali ya juu.
Kitumba alisema kuwa inashangaza kuona mambo machafu yanafanywa na vijana na kufurahiwa ikiwemo kutukana viongozi huku baadhi ya wanaofanya hivyo wanatoka kwenye familia za viongozi wa dini na kwamba hilo halikubaliki ni lazima jambo hilo likemewe na kuachwa mara moja.
mwisho




