Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

UN YAITAKA TANZANIA KUSITISHA UHAMISHAJI WA WAMASAI NGORONGORO NA LOLIONDO

By admin
August 28, 2026 2 Min Read
Comments Off on UN YAITAKA TANZANIA KUSITISHA UHAMISHAJI WA WAMASAI NGORONGORO NA LOLIONDO

 

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi (CERD) imeitaka Tanzania kusitisha mara moja kile ilichokitaja kuwa uhamishaji wa nguvu wa jamii ya Wamasai kutoka makazi ya mababu zao katika Ngorongoro na Loliondo.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Agosti 28, kamati hiyo ilieleza wasiwasi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya jamii hiyo, ikiwemo kufukuzwa na kuhamishwa kwa nguvu, pamoja na vikwazo vya kupata ardhi za mababu, maeneo ya makazi na rasilimali za asili.

CERD pia iliitaka serikali ya Tanzania kuchunguza na kushughulikia madai ya ukiukwaji wa sheria yaliyoripotiwa, yakiwemo kukamatwa holela kwa baadhi ya wakazi na matumizi ya nguvu kupita kiasi na vyombo vya dola.

Kamati hiyo ilisema Tanzania inapaswa kurejesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za msingi katika maeneo husika, zikiwemo elimu, huduma za afya, maji safi na huduma za usafi wa mazingira.

Aidha, ilitoa wito kwa mamlaka za Tanzania kuhakikisha mazingira salama kwa watetezi wa haki za binadamu, mashirika ya kiraia, wanaharakati, wanasheria na waandishi wa habari wanaoshughulikia masuala yanayohusu haki za jamii za wenyeji.

Katika mapendekezo yake, CERD iliitaka Tanzania kutangaza haraka matokeo na mapendekezo ya tume mbili za rais zilizoundwa Februari 2025 kuchunguza sera za matumizi ya ardhi, uhamishaji wa wakazi na uhifadhi ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Kamati hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa kuhakikisha jamii ya Wamasai inashirikishwa kikamilifu katika maamuzi yanayohusu mustakabali wa maeneo wanayoishi na kuyategemea kwa maisha yao.

Serikali ya Tanzania mara kadhaa imekuwa ikisisitiza kuhusu matumizi ya maeneo hayo kwa manufaa ya umma, ikizingatia sheria na masuala ya haki za binadamu.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

‘NCHIMBI SIO CHAWA’ – WARIOBA

Next

WANANCHI URU KUSINI WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 200 KUKARABATI SHULE

Recent Posts

  • BONANZA LA BUNGE KULENGA AFYA NA MSHIKAMANO WA WATUMISHI
  • JAMII YAHIMIZWA KUTUMIA VYAKULA VYA MIMEA ASILI KUIMARISHA KINGA ZA MWILI
  • Doumbia Bado Anajitafuta! Ashindwa Kutamba Dhidi ya Coastal
  • WANANCHI URU KUSINI WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 200 KUKARABATI SHULE
  • UN YAITAKA TANZANIA KUSITISHA UHAMISHAJI WA WAMASAI NGORONGORO NA LOLIONDO

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme