Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Habari

WANANCHI URU KUSINI WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 200 KUKARABATI SHULE

By admin
August 28, 2026 2 Min Read
Comments Off on WANANCHI URU KUSINI WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 200 KUKARABATI SHULE

 

Na Matukio Daima Media, Moshi

WANANCHI wa Kata ya Uru Kusini, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameonyesha nguvu ya ushirikiano kwa kuchangisha zaidi ya shilingi milioni 200 na kuzitumia kukarabati Shule ya Msingi Kimanganuni iliyokuwa na baadhi ya majengo chakavu.

Ukarabati huo umehusisha kubomoa baadhi ya majengo yaliyokuwa katika hali mbaya na kujenga miundombinu mipya ikiwemo vyumba vya madarasa, vyoo, maji, umeme pamoja na kuweka majiko yanayotumia nishati safi kupikia.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ukarabati wa shule hiyo, Leonard Kisarika, amesema fedha hizo zimetokana na michango ya wananchi pamoja na wanafunzi wa zamani waliosoma shuleni hapo tangu mwaka 1965.

Kisarika amesema hatua hiyo imeonyesha kuwa wananchi wanaweza kushirikiana katika kutatua changamoto za maendeleo ya jamii badala ya kusubiri kila jambo lifanywe na Serikali.

Kwa upande wake, Wakili Octavian Kiwale, ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo, amesema wahitimu wameona umuhimu wa kurudisha kwa jamii walichopata kupitia shule hiyo kwa kushiriki katika ukarabati wake.

Kiwale amesema shule hiyo ina historia kubwa kwa jamii ya Uru Kusini na kwamba kuboresha mazingira yake ni uwekezaji katika elimu ya watoto wa kizazi cha sasa.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ukarabati,Gaudens Anizeth Mushi, amesema ushiriki wa wananchi na wahitimu katika kuboresha shule hiyo ni mfano wa namna jamii inavyoweza kuunganisha nguvu zake katika kuharakisha maendeleo.

Akizungumzia hali ya shule hiyo, Mkuu wa Shule ya Msingi Kimanganuni, Hadija Mfinanga, amesema ukarabati huo umebadilisha mazingira ya shule na kuwapa wanafunzi mazingira bora zaidi ya kujifunzia.

Mfinanga amesema pamoja na maboresho hayo, bado shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa madawati zaidi ya 50.

Amesema maboresho hayo yana umuhimu mkubwa kwa wanafunzi na walimu, kwa kuwa mazingira bora ya shule yana mchango katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji.

Hata hivyo, viongozi wa shule na wadau hao wameendelea kuomba ushirikiano wa jamii katika kukamilisha mahitaji yaliyobaki, hususan upatikanaji wa madawati.

Mwisho

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

UN YAITAKA TANZANIA KUSITISHA UHAMISHAJI WA WAMASAI NGORONGORO NA LOLIONDO

Next

Doumbia Bado Anajitafuta! Ashindwa Kutamba Dhidi ya Coastal

Recent Posts

  • BONANZA LA BUNGE KULENGA AFYA NA MSHIKAMANO WA WATUMISHI
  • JAMII YAHIMIZWA KUTUMIA VYAKULA VYA MIMEA ASILI KUIMARISHA KINGA ZA MWILI
  • Doumbia Bado Anajitafuta! Ashindwa Kutamba Dhidi ya Coastal
  • WANANCHI URU KUSINI WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 200 KUKARABATI SHULE
  • UN YAITAKA TANZANIA KUSITISHA UHAMISHAJI WA WAMASAI NGORONGORO NA LOLIONDO

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme