Doumbia Bado Anajitafuta! Ashindwa Kutamba Dhidi ya Coastal
Shechambo Chris
August 28, 2026
18 views
0 Comments

Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Doumbia bado anajitafuta kutokana na kushindwa kufungua ukurasa wa mabao katika mechi 4 za ligi zilizochezwa na vinara 2026/27.
Raia huyo wa Mali alianza kikosi cha kwanza Agosti 27,2026 ubao wa Uwanja wa Meja Jen. Isahmuyo uliposoma Simba SC 1-0 Coastal Union, Bao la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Ismail Toure dakika ya 74.
Rekodi zinaonyeshwa kuwa Doumbia alitumia dakika 63 uwanjani baada ya Kocha Mkuu, Steve Barker kumpa nafasi kuanza kupambania nembo ya timu hiyo.
Katika dakika hizo Doumbia alifanya jaribio moja la hatari dakika ya 9 kwa mguu wa kulia. Jaribio hilo liligonga mwamba na kurejea uwanjani.
Majaribio mengine aliyofanya ilikuwa dakika ya 20 kwa pigo la kichwa akitumia pasi ya kona iliyopigwa na Libase Gueye. Dakika ya 24, 27, 36, 57.
Alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 59 kwa kumchezea faulo nyota wa Coastal Union, Alichezewa faulo dakika ya 21.
Licha ya balaa ambalo alionyesha uwanjani, Doumbia hajapata bahati kufunga ndani ya ligi na timu yake inaongoza ligi ikiwa na pointi 12.
Safu ya ushambuliaji ya Simba SC imefunga jumla ya mabao 7, Toure na Clatous Chama kila mmoja amefunga mabao mawilimawili.
Lunyamadzo Mlyuka, DarTU