JAMII YAHIMIZWA KUTUMIA VYAKULA VYA MIMEA ASILI KUIMARISHA KINGA ZA MWILI
Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio Daima Media
JAMII imehimizwa kutumia vyakula vitokanavyo na mimea, mbegu na matunda ya asili ili kuimarisha kinga za mwili na kujikinga na magonjwa sugu.
Mkurugenzi wa HOPECA Products na Amra Gogondi, Dk Manimba Daniel, alisema vyakula vinavyotokana na mimea na mbegu za asili vina vitamini na virutubisho muhimu vinavyosaidia kutunza na kurekebisha mwili.
Alisema jamii inapaswa kubadilisha mtindo wa maisha kwa kutumia vyakula vya asili, kufanya mazoezi mepesi na endelevu kwa ajili ya kuchangamsha mwili, pamoja na kuhakikisha inapata muda wa kutosha wa kupumzika.
Dk Daniel alisema unga wa HOPECA ni tiba lishe unaotokana na mchanganyiko wa aina 20 za mbegu za mimea pamoja na matunda mbalimbali ya asili, hivyo kuwa na virutubisho mbalimbali muhimu mwilini.
“HOPECA ni mchanganyiko wa vitamini C, nyuzinyuzi na madini ambayo yanasaidia kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha homoni na kusaidia kuondoa uchafu mwilini,” alisema Mkurugenzi huyo.
Akizungumza kwenye Tamasha la Utamaduni wa Tanzania lilnalo3nd3lea mkoani Morogoro, Dk Daniel alisema pia unga wa tunda la Amra Gogondi, ambalo ni tundapori, unasaidia kusafisha damu na kuondoa mafuta yasiyofaa mwilini.
“Chai ya Amra inachangamsha mwili, inayeyusha mafuta kwenye damu, inapunguza cholesterol na kusaidia kuondoa uchafu kwenye utumbo unaotokana na mabaki ya vyakula,” alisema Dk Daniel.
Alisema unga wa Amra pia unasaidia kukarabati mwili kwa kuchochea uzalishaji wa chembe hai mpya zinazosaidia mwili kupambana na maradhi.



