Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Burudani

‘NCHIMBI SIO CHAWA’ – WARIOBA

By admin
August 28, 2026 2 Min Read
Comments Off on ‘NCHIMBI SIO CHAWA’ – WARIOBA

 

Waziri Mkuu wa zamani na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, Joseph Warioba, amesema aliyekuwa Makamu wa Rais Emmanuel Nchimbi sio “chawa” wa viongozi, akisema misimamo yake ya kisiasa imetokana na kile anachoamini.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Demokrasia Tanzania lililofanyika leo Agosti 28, 2026, makao makuu ya chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), jijini Dar es Salaam, Warioba amesema kwa muda wote ambao amekuwa akimfahamu Nchimbi, hajawahi kumwona akimsifia kiongozi kwa lengo la kujipendekeza, akisema msimamo huo ameendelea nao tangu alipokuwa kijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi, CCM.

“Navyomfahamu Nchimbi, kitu kimoja, Nchimbi si chawa wa aina yoyote. Alipokuwa kwenye chama hakuwa chawa na vijana wenzake na ameendelea hivyo hivyo,” amesema Warioba.

Amesema kauli mbalimbali zilizotolewa na Nchimbi katika nafasi zake za uongozi zilikuwa zikieleza mtazamo wake binafsi kuhusu namna siasa zilivyopaswa kuendeshwa nchini.

Warioba ametaja tukio la kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, akiwemo John Heche, ambapo Nchimbi akiwa Katibu Mkuu wa CCM alitoa wito wa kuachiliwa kwa viongozi hao.

“Kuna wakati kina viongozi wa Chadema walikamatwa, kina Heche. Nchimbi akiwa Katibu Mkuu alisema, waachieni, tushindane kisiasa,” amesema Warioba.

Ameeleza pia kwamba wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024, Nchimbi alizungumza kuhusu hatua alizochukua baada ya kumuona Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Warioba, Nchimbi alitaka kile alichokiita “mambo madogo madogo” yaachwe na vyama vishindane kisiasa.

Kwa mujibu wa Warioba, kauli hizo zilikuwa sehemu ya misimamo ya Nchimbi kuhusu uongozi na ushindani wa kisiasa.

“Ni misimamo alikuwa anaitoa, tofauti ya uongozi,” amesema.

Warioba pia amenukuu kauli ambayo amesema Nchimbi aliwahi kuitoa kuhusu namna ya kukosoa makosa ndani ya CCM, akirejea ahadi ya wana-CCM “Nitasema kweli daima, fitina mwiko, iko kwenye ahadi zetu”, anasema Warioba na kuongeza “lakini siku hizi ukisema ukwlei umeanzisha fitina”.

Nchimbi alitangaza kujiuzulu nafasi ya makamu wa Rais wiki hii, kabla ya kuvuliwa uanachama wa CCM, akisema ameamua kustaafu siasa pia. CCM ilisema imemfukuza kwa sababu za kinidhamu.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI YAANZA UKAGUZI KWA WAKUSANYAJI NA WACHAKATAJI WA TAARIFA HIZO NCHINI.

Next

UN YAITAKA TANZANIA KUSITISHA UHAMISHAJI WA WAMASAI NGORONGORO NA LOLIONDO

Recent Posts

  • BONANZA LA BUNGE KULENGA AFYA NA MSHIKAMANO WA WATUMISHI
  • JAMII YAHIMIZWA KUTUMIA VYAKULA VYA MIMEA ASILI KUIMARISHA KINGA ZA MWILI
  • Doumbia Bado Anajitafuta! Ashindwa Kutamba Dhidi ya Coastal
  • WANANCHI URU KUSINI WACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 200 KUKARABATI SHULE
  • UN YAITAKA TANZANIA KUSITISHA UHAMISHAJI WA WAMASAI NGORONGORO NA LOLIONDO

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme