Skip to content
-
Subscribe to our newsletter & never miss our best posts. Subscribe Now!
Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

Habarimpya

Habari Mpya Kilasiku

  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
  • Home
  • Privacy Policy
  • Sample Page
Close

Search

  • https://www.facebook.com/
  • https://twitter.com/
  • https://t.me/
  • https://www.instagram.com/
  • https://youtube.com/
Subscribe
Burudani

MBALI YA DKT NCHIMBI ,WANACHAMA HAWA PIA WALIWAHI KUFUKUZWA CCM

By admin
August 27, 2026 2 Min Read
Comments Off on MBALI YA DKT NCHIMBI ,WANACHAMA HAWA PIA WALIWAHI KUFUKUZWA CCM

NA MATUKIO DAIMA MEDIA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), katika historia yake, kimewahi kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya baadhi ya wanachama na viongozi wake, hatua zilizofikia hadi kuwavua au kuwafukuza uanachama kutokana na sababu mbalimbali za kisiasa na kinidhamu.

Miongoni mwa vigogo wanaotajwa katika historia hiyo ni Seif Sharif Hamad, mwanasiasa mkongwe wa Zanzibar ambaye alifukuzwa CCM mwaka 1988 kufuatia mgogoro wa kisiasa ndani ya chama Zanzibar.

Katika kipindi hicho pia Shaaban Mloo alikumbwa na hatua ya kufukuzwa CCM mwaka 1988, ikiwa ni sehemu ya misukosuko ya kisiasa iliyokuwa ikiendelea Zanzibar.

Mwanasiasa mwingine ni Mansour Yussuf Himid, aliyewahi kuwa Waziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki. Mansour alivuliwa uanachama wa CCM baada ya kuingia katika mgogoro na chama.

Machi 2017, CCM ilifanya maamuzi mengine makubwa ya kinidhamu yaliyowakumba baadhi ya viongozi wake. Miongoni mwao alikuwa aliyewahi kuwa Waziri na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba, ambaye alivuliwa uanachama.

Hata hivyo, Novemba mwaka huo, Sophia alirejeshewa uanachama baada ya kuomba msamaha na chama kuridhia ombi lake.

Wengine waliofukuzwa CCM mwaka 2017 ni Ramadhani Madabida, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam; Jesca Msambatavangu, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa; Erasto Kwilasa, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga; pamoja na Christopher Sanya, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara.

Hatua hizo zilikuwa sehemu ya maamuzi ya chama yaliyolenga kusimamia nidhamu na uwajibikaji miongoni mwa viongozi na wanachama wake.

Mwanasiasa mwingine mkubwa aliyewahi kufukuzwa CCM ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Membe alifukuzwa uanachama Februari 28, 2020 baada ya mvutano wa muda mrefu wa kisiasa ndani ya chama. Baadaye alijiunga na ACT-Wazalendo na kuwa mgombea urais wa chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Katika mjadala wa hatua za kinidhamu ndani ya CCM, jina la Dkt. Emmanuel Nchimbi pia limewahi kujitokeza. Hata hivyo, katika maamuzi ya mwaka 2017, Nchimbi hakufukuzwa wala kuvuliwa uanachama; alipewa onyo kali na kutakiwa kuomba radhi.

Historia hiyo inaonyesha kuwa CCM imewahi kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa ngazi mbalimbali, kuanzia viongozi wa mikoa, mawaziri wa zamani hadi vigogo waliokuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania.

Baadhi ya waliofukuzwa waliendelea na siasa kupitia vyama vingine, huku wengine wakirejeshewa uanachama baada ya kuomba msamaha na kukubaliwa kurejea ndani ya chama.

Author

admin

Follow Me
Other Articles
Previous

AFCON 2027,TANZANIA KUTANGAZA UTAMADUNI WAKE KUPITIA

Next

WAZIRI MKUU DKT NCHEMBA AKIJIBU MASWALI LEO BUNGENI

Recent Posts

  • Watanzania 173 Warejea Nchini kwa Hiari Kutoka Afrika Kusini
  • *WMA WAKAGUA USAHIHI WA VIPIMO KWENYE VIWANDA VYA MABATI MKOANI MWANZA*
  • Shigongo Ahoji Serikali Kuhusu Barabara za Mitaa Nyehunge – Video
  • Dkt. Mwigulu Ampongeza Ndejembi, Aeleza Mikakati ya Serikali Kuhusu Mawasiliano na Usafiri – Vudeo
  • Tanzania yaandaa ziara ujumbe wa ADDI – HabariLeo

Recent Comments

  1. A WordPress Commenter on Hello world!

Archives

  • August 2026

Categories

  • Burudani
  • Habari
  • Magazeti
  • Michezo
  • Siasa
Copyright 2026 — Habarimpya. All rights reserved. Blogsy WordPress Theme