Simba na Yanga Zakutana na Adhabu ya Tsh Milioni 5 Kila Moja

Global Publishers
November 7, 2026
12 views
0 Comments

Klabu za Simba SC na Yanga SC zimepigwa faini ya Shilingi Milioni 5 kila moja na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutokana na matukio tofauti yaliyojitokeza katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC.

Simba imeadhibiwa baada ya watoto wake waokota mipira kuhusishwa na vitendo vilivyoashiria imani za kishirikina wakati wa mchezo dhidi ya Namungo FC, uliomalizika kwa ushindi wa Simba wa mabao 3-2.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi iliyotolewa Novemba 7, 2026, watoto hao walionekana wakimwaga maji nyuma ya lango la Namungo FC, kitendo kilichotajwa kuwa ni ukiukaji wa Kanuni ya 48:1 ya Ligi Kuu inayohusu udhibiti kwa klabu.

Kwa upande mwingine, Yanga imeadhibiwa baada ya mashabiki wake kumrushia chupa za maji Kocha wa Viungo wa TRA United katika mchezo namba 059 wa Ligi Kuu ya NBC uliomalizika kwa sare ya bila kufungana (0-0).

Bodi ya Ligi imeeleza kuwa adhabu hizo zimetolewa kufuatia kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi kilichofanyika Novemba 5, 2026, ambapo ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika michezo ya ligi hiyo.