Kamanda Muliro Azungumzia Ulinzi Dar Wakati Hukumu ya Lissu Ikisubiriwa – Video

Global Publishers
November 6, 2026
18 views
0 Comments

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amezungumza na Global TV kuhusu hali ya ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam, wakati Mahakama Kuu ya Tanzania ikitarajia kutoa uamuzi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Muliro ameeleza hatua zinazochukuliwa na Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali ya jiji, katika kipindi hiki ambacho hukumu ya kesi hiyo inafuatiliwa kwa karibu na wananchi na wadau mbalimbali.

Mazungumzo hayo yanakuja wakati ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ambako hukumu ya kesi hiyo imepangwa kutolewa.