KILOSA: WAFUGAJI WATAKIWA KUJITENGENEZEA UHAKIKA WA MALISHO

Upatikanaji wa malisho ya mifugo ni miongoni mwa masuala yanayohitaji mipango endelevu katika sekta ya ufugaji, huku wafugaji wilayani Kilosa wakihimizwa kuwa na mashamba yao ya malisho ili kuepusha migogoro na wakulima.

Akizungumza na wafugaji wa jamii ya Kisukuma katika Kijiji cha Mbamba, Kata ya Kilangali, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, amesema matumizi ya maeneo yaliyotengwa kwa ufugaji yanaweza kusaidia kupunguza migogoro inayotokana na mifugo kuingia katika mashamba ya mazao.

Amesema Serikali inaendelea kusimamia matumizi sahihi ya ardhi na kwamba hatua za kuwaondoa wafugaji wanaovamia maeneo yasiyoruhusiwa zitaendelea, akiwataka wafugaji kupanga shughuli zao kwa kuzingatia maeneo yaliyotengwa kwa ajili hiyo.

Wafugaji katika kijiji hicho wameiomba Serikali kuwakumbuka kwa kuwajengea Majosho na visima kwaajili ya Maji ya mifugo ili wapunguze  changamoto kwa wafugaji kwenda kutafuta huduma hizo na kulazimika kupita kwenye mashamba na kusababisha sintofahamu.

Mwisho

Mwisho